ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 21, 2023

MBOWE ASIMULIA ALIVYOKAMATWA, KUPEWA KESI YA UGAIDI.

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amewasimulia wakazi wa Mkoa wa Mwanza na mikoa jirani waliohudhuria ufunguzi wa mikutano ya hadhara ya chama hicho uliofanyika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza namna alivyochulkuliwa ‘kinyemela’, kutoka Mwanza hadi kufikishwa Dar es Salaam kisha kufunguliwa mashtaka ya ugaidi.

Akiwaadhithia wananchi hao Mbowe amesema akiwa msibani kwa kaka yake Kilimanjaro Julai, 2021 alisikia Dk Azaveli Lwaitama na Mzee Sylivester Masinde mmoja kati ya waasisi wa chama hicho kuwa wameshikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mwanza na kulazimika kuondoka msibani (Kilimanjaro) na kuja hadi Mwanza kwaajili ya kuwatoa mahabusu.

“Nilivyotua Mwanza kuwatoa rumande, siku ya kwanza, siku ya pili nikakamatwa mimi nikafungwa vitambaa machoni, nikafungwa pingu miguuni, nikafungwa pingu mikononi, nikasafirishwa mazingira nisiyoyajua napelekwa wapi? (alijiuliza), nikapelekwa Dar es Salam na ndio kesi yangu ya ugaidi ikaanzia hapo,”amesimulia.

“Ndugu zangu wa Mwanza nazungumza mambo haya mnaweza kuyaona kama mambo mepesi lakini mimi kama Mwenyekiti wenu kesi ile ikapelekwa miezi nane, asanteni ndugu zangu wa Mwanza na dunia inasikiliza kwa sababu wote mlisikiliza na mkasimama mkasema ‘Mbowe sio gaidi’,”amesema

Hatahivyo, Mbowe na wenzake watatu walifutiwa mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakabili katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Machi 4, 2022 baada ya upande wa Jamuhuri kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo.





PAMBALU ALIZA MKUTANO WA CHADEMA MWANZA AKUMBUSHIA KUKAMATWA KWA MBOWE

 

 

NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Viongozi na makada wengine wa Chadema waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Katibu Mkuu, John Mnyika na wajumbe wa Kamati Kuu wakiwemo wabunge wa zamani Joseph Mbilinyi maarufu Sugu, Mchungaji Peter Msigwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa chama hicho (Bawacha), Sharifa Suleiman, katibu wake, Catherine Ruge, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee (Bazecha), Hashim Issa Juma na wabunge wa zamani Suzan Kiwanga na Suzan Lyimo.

'SUGU MOTO CHINI' HECHE, MSIGWA, RUGE 'CHADEMA TULIKUWA KIFUNGONI'

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Viongozi na makada wengine wa Chadema waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Katibu Mkuu, John Mnyika na wajumbe wa Kamati Kuu wakiwemo wabunge wa zamani Joseph Mbilinyi maarufu Sugu, Mchungaji Peter Msigwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa chama hicho (Bawacha), Sharifa Suleiman, katibu wake, Catherine Ruge, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee (Bazecha), Hashim Issa Juma na wabunge wa zamani Suzan Kiwanga na Suzan Lyimo.

HII NDIYO TAFSIRI YA RANGI KWENYE BENDERA YA CHADEMA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Akihutubia mbele ya umati uliofurika kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza ikiwa ni ufunguzi wa mikutano ya hadhara iliyozuiwa kwa takribani miaka 7, huku cha hicho kikiadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake, John Mnyika ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)......

MASHINE ZA KAZI YANGA KAMILI KWA RUVU

 

AZIZ Ki kiungo wa Yanga ni miongoni mwa mastaa ambao wameanza mazoezi kwa ajili ya mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumatatu, Uwanja wa Mkapa Januari 23,2023.

Yanga ni vinara wa ligi wakiwa wameweka kibindoni pointi 53 kwenye mechi 20 ambazo wamecheza wamepoteza mchezo mmoja pekee.

Mbali na Aziz KI pia Yannick Bangala, Kennedy Musonda, Dickosn Job, Clement Mzize ni miongoni mwa waliokuwa kwenye mazoezi hayo.

Ofisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema kuwa wanawaheshimu wapinzani wao watapambana kupata matokeo.

Friday, January 20, 2023

VIDEO - RONALDO, MESSI WAONESHANA UBABE.

 PSG Vs All Nassr And Elhilal 5-4 | All Goals & Highlights 2023 HD

Lionel Messi na wachezaji wenzake wa PSG wamewashinda nyota wa Saudia akiwemo Cristiano Ronaldo katika mchezo wa kusisimua wa mabao tisa.


Mchezo huo ulijaa vituko na vivutio lukuki, ulishuhudia Messi, Ronaldo na Kylian Mbappe wakifunga bao.

Ikicheza na wachezaji 10 mara baada ya mmoja wa wachezaji wa PSG kulamba umeme, katika dakika ya 39 na Neymar akakosa penalti lakini bado waliweza kushinda mechi ya kirafiki ya Alhamisi huko Saudi Arabia.

Mbele ya umati wa watu uliookuwa ukishangilia mwanzo mwisho hivyo kutengeneza muonekano wa tamasha kubwa ulishuhudia Messi, Mbappe na Ronaldo wakiwa miongoni mwa wafungaji waliopasia nyavu kiufundi na kwa style tofauti.

CCM KUIRUDISHA TANGA YA VIWANDA

 

MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman akizungumza na wazee wa Mkoa wa Tanga
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman akizungumza na wazee wa Mkoa wa Tanga
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman akizungumza na wazee wa Mkoa wa Tanga
Sehemu ya Wazee wa Mkoa wa Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali

Na Oscar Assenga, TANGA.

MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman amesema wamejipanga ndani ya miaka mitano ya uongozi wao kuhakikisha wanaurudisha mkoa huu kwenye hadhi yake ya viwanda kwa kuvutia wawekezaji wapya.

Mkakati huo ulitangazwa na Mwenyekiti huyo wakati wa kikao chake na Wazee wa Mkoa wa Tanga kilichofanyika kwenye ukumbi wa CCM Mkoa wa Tanga ambapo alisema watakachofanya ni kuanisha viwanda vilivyopo kuona changamoto zao na kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi.

Rajabu alisema pamoja na hayo ni kuona namna bora ya kuwavutia wawekezaji wapya kwenda kuwekeza kwenye mkoa Tanga ambao una fursa nyingi za kiuchumi ambazo zitawawezesha kuendesha shughuli zao bila vikwazo.

“Kama Mkoa wa Pwani wameweza kufanya vizuri kwenye viwanda kwanini Tanga ambako ndio kwenye asili ya viwanda nyie wazee wetu ndio mnaijua hii vizuri tuiteni mtueeleza kwamba tunakosea wapi moja mbili tatu wazee wetu mnafahamu ”Alisema

“Bandari ya Tanga ilifanya kazi ipasavyo,Reli na tukawa na viwanda vya kutosha ajira za kumwaga na tukachangia kwa kiasi kikubwa pato la uchumi wa Taifa letu lakini niwaambie kwamba kwa sasa tumedhamiria kuirudisha Tanga kwenye hadhi yake tena kwa haraka sana ”Alisema Mwenyekiti huyo

Hata hivyo alisema kwamba uchumi wa Tanga ukiinuka hata vilabu vya Coastal Union na African Sports navyo vitainuka kwa sababu watu wataweze kuvichangia vilabu vyao.

Kuhusu Migogoro ya Ardhi

Mwenyekiti huyo alisema kwamba wamejipanga vema kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba kukaa chini kutafutaka namna bora na nzuri ya kuweza kuondoa migogoro ya ardhi kwenye mkoa huo.

Rajabu alisema unaweza usione athari ya migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji mpaka pale utakapopigiwa simu kwamba ndugu yao ameuwawa kutokana na migogoro ya ardhi kwenye maeneo yao.

“Tumeenda wenyewe kwenye baadhi ya maeneo hatukutaka kusimuliwa watu imefika wakati wakulima na wafujaji wanauana wanachomea mali zao ukikaa mjini yanayoendelea vijijini huwezi kuyajua na mimi niliomba Uenyekiti kuja kusaidia chama changu,wananchi wa Tanga tumeenda kujioneka na baadhi ya maeneo hali sio shwari lakini kwa kufika CCM katika maeneo hayo hali nzuri imerejea na shwari watu wanaishi kwa Amani hivyo tuitake jamii iendelee kuienzi Amani iliyopo”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba wanajua serikali inadhamira njema na mkoa wa Tanga na Rais Samia kwa hatua kubwa anayoendelea kuichukua kuimarisha Tanga kiasiasa na kiuchumi hivyo aliwataka waendelee kumpa muda Rais ikiwemo kumuombea na kumuunga mkono yeye na Makamu wa Rais Philip Mpango,Waziri Mkuu Kasim Majaliwa.

Kauli yake kwa viongozi wa dini.

Mwenyekiti huyo aliwataka viongozi wa dini na wazee wa mkoa huu waisaidie Serikali katika suala la mmomonyoko wa maadili ambalo limekuwa ni tatizo .

“Hivyo tukirudi kwenye maadili mazuri nchi yetu itaendelea kuwa salama na lawama kwa serikali itaondoka na kupungua kwa asilimia kubwa hivyo suala hilo ni muhimu mkubwa kwenu kuhimiza maadili mema “Alisema

Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Suleiman Mzee alisema Mwenyekti baada ya kuchaguliwa alianza kazi za dharura ikiwemo ya maeneo yalikuwa migogoro ya ardhi mikubwa baina ya wakulima na wafugaji nako kumeanza kutulia. Alisema sasa wanataka kuanza rasmi kazi za Chama wakaona sio vema kuanza bila kukutana na wazee wa mkoa huo wafanye kikao hicho kwa ajili ya Baraka kwa ajili ya ratiba zao mbalimbali za kichama.

Thursday, January 19, 2023

MELI MPYA ZINAJENGWA LAKINI MAKEPTENI NA MAINJINIA WETU WATAWEZA KUZIENDESHA - MAKUBALIANO YASAINIWA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Kampuni ya huduma za meli nchini (MSCL) pamoja na wakala wa uwezeshaji wa usafiri wa ushoroba wa kati (CCTTFA) zimetiliana saini makubaliano ya ushirikiano yanayolenga kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa kampuni hiyo. Makubaliano hayo yatawezesha kampuni ya MSCL kupokea shilingi millioni 165.6 kutoka kwa wakala huo zitakazotumika kugharamia shughuli za utafiti wa masoko katika ziwa victoria na ziwa tanganyika pamoja na kutoa mafunzo kwa mabaharia. Makubaliano ya ushirikiano baina ya kampuni ya MSCL pamoja na wakala wa CCTTFA yamesainiwa Jijini mwanza na yatadumu kwa muda wa miaka mitatu.

WANAWAKE WAWILI WAUAWA GEITA MMOJA AKATWA SEHEMU ZA SIRI.

 


 Wanawake wawili wameuawa kwa kukatwa mapanga wilayani Nyang’wale mkoani Geita huku mmoja wao akiondolewa sehemu za siri na wauaji kuondoka nazo.

 Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Jamhuri Wiliam amesema tukio la kwanza limetokea Kijiji cha Nyabulanda alfajiri ya Januari 16 wakati mama huyo akiwa shambani kwake.


Mkuu huyo wa wilaya amemtaja aliyeuawa na sehemu za siri kuondolewa kuwa ni Bigile Mweshemi (53) na kusema chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa kuwa ni mgogoro wa kifamilia na imani za kishirikina.

“Aliondoka na kwenda shambani alfajiri kwa hiyo hao wakata mapanga walimvamia na kumkata na mbaya zaidi wakaondoka na sehemu za siri mambo mengine yanatisha ndugu zetu hawa wana mambo magumu sana,” amesema.


Amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi na hadi sasa watu watatu wanashikiliwa.


 “Mmoja anayeshukiwa ambaye ni ndugu wa karibu waliyekuwa na mgogoro wa shamba kwa sasa ametoweka na wanaendelea kumsaka huyu ndiye anaedaiwa kuwatuma wakata mapanga,” amesema William.


Tukio jingine ni kikongwe aliyetambulika kwa jina la Melesiana Shija (70) mkazi wa Kijiji cha Nyugwa aliyeuawa kwa kukatwa mapanga na wauaji kutokomea.


Mmoja wa wananchi Serafine Richard amesema mshukiwa aliyetoroka anadaiwa kuondoka kwa mganga  wa kienyeji saa 10 alfajiri na baada ya hapo tukio hilo likatokea na hadi sasa hajulikani aliko.

Wednesday, January 18, 2023

ASILIMIA 53 YA KIDATO CHA KWANZA WARIPOTI SHULE, DC MASSALA AONYA MICHANGO.

 


Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Massala amekataza michango ya aina yeyote itakayosababisha wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2023 washindwe kuripoti shuleni.

Ambapo jumla ya wanafunzi 12,507 Wilaya ya Ilemela waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka mpya wa masomo wa 2023 ambao walipaswa kuripoti shuleni walikopangiwa tangu shule zilipofunguliwa Januari 9 mwaka huu.

Kati ya hao mpaka sasa jumla ya wanafunzi 6367 pekee ndio waliokwisha ripoti shuleni sawa na asilimia 53 ya wanafunzi wote huku wanafunzi 6140 wakiwa hawajaripoti.

Massala ametoa agizo hilo jana wakati wa ziara yake kwa shule za msingi na sekondari zilizopo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela yenye lengo la kufuatilia mahudhurio ya kidato cha kwanza, awali na darasa la kwanza.

Pamoja na kusikiliza changamoto za walimu na kuhamasisha ufaulu ambapo amewataka Wakuu wa shule, Maofisa Elimu na viongozi wa mitaa na kata kuhakikisha watoto wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wanaripoti shuleni na hakuna kuzuia mtoto yeyote kuingia darasani.

“Kuna wazazi mnawazuia eti sababu hawajajaza fomu za kujiunga na shule kwenye kile kipengele cha daktari, wengine kwa kukosa sare, wengine sijui hawana jembe,nasema marufuku kuzuia watoto kwasababu ya michango yeyote,”ameeleza Massala.

Mbali na hayo pia ametaka hatua zichukuliwe kwa wazazi watakaoshindwa kupeleka watoto shuleni pamoja na watendaji watakaokwamisha zoezi la wanafunzi kuripoti shuleni.

Diwani wa Kata ya Mecco Godlisten Kisanga amewaasa viongozi wa mitaa kushirikiana ili kuhakikisha watoto wote wanaripoti shuleni.Huku akiahidi ufuatiliaji wa nyumba kwa nyumba ili kubaini watoto waliochaguliwa na hawajaripoti shuleni.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Ofisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mwl.Alex Mkusa amewapongeza walimu kwa kazi kubwa wanayoifanya kuhakikisha Halmashauri hiyo inaendelea kushika nafasi nzuri kitaifa huku akiwataka kuongeza juhudi katika ufundishaji ili ufaulu kwa nafasi na daraja la ufaulu viende sambamba (GPA).

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza Hassan Massala akizungumza na wanafunzi wa moja ya shule za sekondari zilizopo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela wakati wa ziara yake ya kutembelea shule za msingi na sekondari kwa ajili ya kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi wa kidato cha kwanza,awali na darasa la kwanza wilayani humo.

MBARAWA AKEMEA HUJUMA UJENZI MIUNDOMBINU YA DARAJA LA MAGUFULI NA MV MWANZA HAPA KAZI TU

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amekemea vitendo vya hujuma katika mradi wa ujenzi wa daraja la Kigongo – Busisi, maarufu kama daraja la John Pombe Magufuli unaotekelezwa na serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 700.

Katika ziara hiyo pia Waziri amefanya ukaguzi wa maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa mkoani Mwanza, ukiwemo wa ujenzi wa meli ya Mv. Mwanza Hapa Kazi Tu unaogharimu shilingi bilioni 107.



SAO HILL WAGAWA MICHE YA MITI MILIONI MOJA WILAYANI MUFINDI.

 

Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego akiwa na viongozi mbalimbali wakigawa miche ya miti kwa taasisi ya jeshi la JKT lililopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego akiwa na viongozi mbalimbali wakigawa miche ya miti kwenye moja ya shule zilizopo wilaya ya Mufindi inayolizunguka shamba la miti la Sao Hill.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego wa pili kushoto akiwa kwenye picha na viongozi mbalimbali wakati wa zoezi la ugawaji wa Miche ya miti kwa wananchi, wadau na taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi.

Na Fredy Mgunda/ Iringa.

WAKALA wa huduma za misitu Tanzania (TFS )kupitia shamba la miti la Sao hill Mkoani Iringa limefanikiwa kugawa zaidi ya miche ya miti milioni moja kwa wadau na wananchi mbalimbali wa wilaya ya Mufindi kwa lengo la kuendelea kulinda mazingira ya misitu na kuhifadhi vyanzo vya maji kwa faida ya Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari Mhifadhi mkuu wa Shamba la Miti la Serikali Sao Hill,Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Sao Hill Ignas Lupala  alisema kuwa shamba hutenga miche zaidi  ya milioni moja kwa ajili ya kuigawa kwa jamii na Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi zilizopo Wilayani Mufindi na maeneo jirani ili ipandwe katika maeneo yao kwa ajili ya kuhifadhi mazingira pamoja na kutumika kama chanzo cha kipato baada ya kuivuna na kuuza hata hivyo miche hiyo inayogawiwa kila mwaka  ina thamani ya takribani TZS 300,000,000/=.

Lupala alisema kuwa Jamii ,Taasisi mbalimbali na mashirika ya Umma
yamesisitizwa kuendelea kuthamini na kutunza mazingira kutokana na umuhimu wake kwenye maisha ya binadamu.

Alisema ni jukumu la kila mmoja kuendelea kuyatunza mazingira na hasa juu ya ulinzi wa Bayoanuai zilizopo ambazo zimekuwa na manufaa makubwa kwa viumbe hai wote wakiwamo Binaadam huku
akitaja za kutoweka kwa bayoanuai

Lupala alieleza namna ambavyo Shamba la Miti Sao Hill linavyohamasisha jamii kuendelea kuyatunza mazingira kwa kuihusisha katika shughuli rafiki za uhifadhi wa masitu ikiwamo ajira na ufugaji wa nyuki.

Alisema kuwa misiti imekuwa na faida mbalimbali kwa viumbe vyote duniani ikiwepo kuwa makazi ya wadudu,wanyama,ndege na eneo sahihi kujipatia chakula,ikolojia ya misitu ya Sao Hill imechangia sana upatikanaji wa maji ya mto Ruaha Mkuu na Ruaha Mdogo ambavyo hupeleka maji katika vituo vya kuzalishia umeme.

“Umeme unazalishwa katika vituo vya Mtera,Kihansi na mwalimu Nyerere wanategemea maji kutoka katoka hifadhi ya misitu ya Sao Hill kutokana na utunzaji bora wa ikolojia yake”alisema

Lupala alisema kuwa upandaji wa miti unasaidia upatikanaji wa dawa mbalimbali za asili ambazo zimekuwa zinasaidia katika maisha ya binadam hivyo misiti inaumuhimu mkubwa sana kwa wananchi kote ulimwenguni.

Aidha lupala alisema kuwa shamba la miti la Sao Hill limekuwa lanachangia kukuza uchumi katika sekta mbalimbali kama viwanda,miundombinu na sekta ya ujenzi.

Kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego aliwapongeza TFS kupitia Shamba la Miti SaoHill kwa zoezi la ugawaji wa miche kwa wananchi wanaolizunguka shamba kwa kufanya hivyo kunasidia kujenga uhusiano mzuri baina ya Shamba na wananchi.

Dendego alisema kuwa shamba la miti la Sao Hill lina umuhimu mkubwa kwa kuwa asilimia 15 ya maji yanayoingia katika bwawa la Mwalimu Nyerere yanatoka katika vyanzo vya maji vinavyopatikana katika Shamba hilo la Miti SaoHill hivyo aliwaomba  wanachi kuendelea kupanda miti katika maeneo yao na kutunza vyanzo vya maji

"Nawapongeza sana TFS kupitia Shamba la  SaoHill kwa zoezi hili mnalolifanya la kuwapatia wananchi miche na nawaomba msiishie hapa kwani miti inachangia katika ukuaji wa uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla hivyo msisitishe zoezi hili" alisema Dendego

Dendego alisema kuwa Shamba hilo linachangia kwa kiasi kikubwa mapato ya nchi yetu na hayo ndiyo yanayotumika katika kutatua changamoto nyingi za wananchi hivyo wananchi wanatakiwa kuendelea kushirikiana na uongozi wa Shamba ili  kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji kwa faida ya Taifa kwa ujumla.

Alisema kuwa misitu iliyopo katika Mkoa wa Iringa imekua na  faida kwa wananchi na taifa kwani inasaidia katika upatikanaji wa malighafi za viwanda na mapato kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Saad Mtambule alisema kuwa  wilaya inashirikiana vyema na uongozi wa Shamba la Miti SaoHill wanajua na kutambua mchango wa Shamba hilo katika Halmashauri zilizopo Wilayani Mufindi na Taifa kwa ujumla.

"Shamba la Miti Sao Hill limekua na mchango mkubwa katika wilaya yetu kwani linasaidia upatikanaji wa malighafi za viwandani na kusaidia katika utunzaji wa mazingira yetu hivyo zoezi hili la ugawaji miche kwa wananchi  linasaidia katika kujenga uhusiano bora baina ya wananchi na shamba"alisema Mtambule

Nao wadau wa mazingira kutoka Shamba la Miti Sao hill wameeleza namna wanavyonufaika na uwepo wa shamba hilo la Serikali huku wakipongeza hatua zinazochukuliwa hasa juu ya ulinzi wa mazingira.

“kuchukua hatua za ulinzi wa misitu na uhifadhi wa mazingira ili kuendelea kunufaika na rasilimali zitokanazo na uhifadhi” walisema wadau

MARY CHATANDA APIGA MARUFUKU WABUNGE NA MADIWANI VITI MAALUM KUFANYA VIKAO NA WAJUMBE TU

 

Na Mwandishi Wetu,Dar, 

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzana (UWT) Mary Chatanda amepiga marufuku Wabunge na Madiwani wa Viti Maalum kuandaa na kufanya vikao na Wajumbe wa Baraza huku akiwaonya atakayekiuka marufuku hiyo atahukuliwaa hatua kali


Amesema miongoni mwa hatua atakazochukuliwa Mbunge au Diwani wa Viti Maalum akibainika kukiuka marufuku hiyo ni pamoja na kuchukuliwa hatua za kufikishwa kwenye vikao kuonywa na akikaidi zaidi atafikishwa Kamati ya Maadili kwa ajili ya hatua zaidi.


Chatanda aliyasema hayo wakati akizungumza na Viongozi na Wanachama wa UWT katika Mkutano wa Mapokezi uliofanyika katika Ukumbi wa Kiramuu, Mbezi Beach, Kata ya Kawe,ikiwa ni sehemu ya mapokezi rasmi yaliyofanywa na UWT mkoa wa Dar es Salaam, kufuatia kuwasili kwake mkoani hapa kwa mara ya kwanza tangu ashike wadhifa huo. 


Hata hiyo Mwenyekiti huyo aliwaasa madiwani na wabunge kuacha utaratibu wa kupita kuwatafuta wagombea na kuzungumza nao sio wakati muafaka badala yake wazungumze na wanawake wote na sio wale ambao wamewapigia kura.


Alisema maana kuna utamaduni umejengeka kwamba wanaporudi wilayani au mkoani wanawachukua mjumbe wa baraza tu huyo sio sawa na haipo badala yake waende kukutana na wanawake wote kwenye maeneo yao.


"Na ni marufuku kufanya vitendo hivyo wale watakaobainika wataitwa kwenye vikao na wakionekana wamekaidi watapelekwa kwenye vikao vya maadili lengo ni kukomesha vitendo vya namna hii ndani ya umoja huu"Alisema Mwenyekiti Chatanda. 

Tuesday, January 17, 2023

MWANAJESHI APIGWA RISASI KWA KUMUULIZA JAMAA MBONA ALIKUWA AKIVUTA BANGI.


Mwanajeshi mmoja anauguza jeraha hospitalini baada ya kupigwa risasi mkononi na mwanamume anayeshukiwa kuwa jambazi kuwa kumuuliza kwa nini alikuwa akivuta bangi hadharani. 

Mwanajeshi huyo alipigwa risasi kwa kumuuliza mwanamume huyo mbona alikuwa akivuta bangi hadharani. 

Timothy Mwangi alikuwa kwenye likizo katika kijiji chake cha Kihoni katika kaunti ya Murang'a kisa hicho kilipotokea Jumapili mchana. 

Kwa mujibu wa Mwangi, alikuwa njiani akitembea kijijini kwao alipokutana na pikipiki iliyokuwa na mwendeshaji pamoja na abiria mmoja. "Abira alikuwa anavuta bangi hali ambayo ilinifanya kumuuliza kwa nini alikuwa anavuta bangi hiyo," Mwangi amenukuliwa na gazeti la the Star. 

Mwanajeshi huyo anasema kuwa mwendeshaji pikipiki alipunguza kasi, abira huyo kushuka na kutembea hadi alipokuwa. 

Abiria huyo alichomoa bastola na kuilekeza kwa mwanajeshi huyo ambaye aliinua mikono yake juu ishara ya kusalimu amri. 

Mwangi anasimulia kuwa abiria huyo alichukua mkono wake wa kushoto kwa fujo na kumpiga risasi kwenye kiganja. 

Risasi ilitokea upande wa pili na Mwangi kwenda chini kwa uchungu huku akibubujikwa na damu. 

Kwa mujibu wa mwanajeshi huyo, wawili hao walirukia pikipiki yao na kuondoka eneo hilo bila kumwibia chochote. 

Mwangi alikimbizwa katika Hospitali ya Kandara Level Four na baadate kuhamishiwa Thika Level Five ambako amelazwa, kwa mujibu wa polisi. 

Hakuna mshukiwa aliyekamatwa kuhusiana na kisa hicho lakini juhusi za kulinasa genge hilo zinaendelea huku polisi wakiamini kuwa washukiwa walikuwa kwenye oparesheni ya ujambazi.

MABONDIA ZAIDI YA 20 KUPANDA ULINGONI JANUARI 18 NA 28 JIJINI TANGA KUONYESHANA UMWAMBA,IBRAHIM CLASSIC,MATUMLA WAMO

 

 


MASHABIKI wa ngumi mkoa wa Tanga wanatarajiwa kushuhudia pambano la ngumi la kufungua mwaka 2023 wakati w mabondia Mustafa Doto kutoka Dar es Salaam atakapopambana na Said Mundi kutoka Tanga katika mnyukano wa round 10 kesho Januari 18, 2023. 


Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini hapa leo, Promota maarufu  nchini, Ali Mwazoa na ambaye pia mtayarishaji wa pambano hilo alieleza kutakuwa na mengine ya utangulizi  9.


Mapambano hayo yatakuwa kati ya Jay Jay atakayepambana na Peter Julius wakati Jonas Mtafya atapigana na Patrick Kimweri.  Wengne ni Hamis Mwambashi dhdi ya Haji Juma, wote kutoka Tanga.


Mtoto wa bondia mkongwe nchini, Rashid Matumla, Snake Junior atapambana na Ali Reli wote kutoka  Tanga..


Haya ni mapambano ya utangulizi kwa ajili ya mabondia chipukizi kuelekea pambano kubwa la aina yake mkoani na nchini Tanzania kati ya mabondia wawili wanaogopwa, Ibrahim Classic atakayemkabili bondia mwenye mikwara na ngumi nzito, Ndondande Harmer, wa nchini Zimbabwe. Pambano hilo litakuwa la round 10.


Promota Mwazoa alitoa wito kwa mashabiki wa jijini Tanga na nje ya  mkoa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mabambano hayo mawili yatakayofanyika 18 na 28 Januari ambayo yatautangaza mkoa katika fursa za biashara na ajira.


Pia Mwazoa aliahidi kuandaa mapambano mengine ya ngumi ambayo yatatoa zaidi fursa kwa vijana wanaochipukia katika ulingo wa michezo ya ngumi nchini.

MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI MKOA WA PWANI AWAFUNDA WANACHAMA KUFUATILIA UTEKELEZAJI WA MIRADI.


Na Victor Masangu,Pwani


MWENYEKITI Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani Jackson Kituka amesema ni jukumu la wanachama wa chama hicho kujiandaa kuelezea wananchi kwenye mikutano ya hadhara kuhusiana na utekelezaji wa miradi mbalimbali uliofanywa na Serikali. 


Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza katika  Baraza la Jumuiya hiyo lililofanyika Kibaha ambapo alisema baada ya kuruhusiwa mikutano ya hadhara yapo mambo mengi yatasemwa na vyama vingine hivyo chama tawala kinatakiwa kujiandaa kujibu kwa vielelezo.


"Inabidi kufika kwenye ofisi za Wakuu wa Wilaya mkapate taarifa za miradi iliyotekelezwa na Serikali ambayo imetatua kero za wananchi, msinyamaze kimya Serikali ikishambuliwa" alisema.


Aidha alisema viongozi waliochaguliwa hivi karibuni wanatakiwa kufanya kazi  kwa ushirikiano na kuepuka migogoro itakayosababisha baadhi ya majukumu kutofanyika kwa ufanisi.


" Sitaki kuwa mwenyekiti wa migogoro kaeni mfanye kazi vizuri jiandaeni kujibu yale yatakayokuwa yanasemwa vibaya kwenye mikutano ya hadhara mkiwa na takwimu ya kila eneo nini kimefanyika na fedha zilizotumika mkajibu pale mnapoona kuna upotoshaji" alisema 

Awali Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Pwani Elisante Msuya  akizungumza kwenye Baraza hilo alisema wajumbe kutoka katika wilaya za mkoa huo wameshiriki katika baraza hilo la siku mbili ambalo liliambatana na kuchagua wajumbe kamati ya Utekelezaji.


Msuya alisema wajumbe wa Baraza walipata fursa ya kupatiwa semina ya Mazingira, changamoto za mazingira zinazoukabili mkoa wa Pwani, Sera ya elimu, Sera ya Malezi na changamoto za kimalezi kwa mkoa huo.


Alieleza kuwa baada ya Baraza hilo wajumbe watakwenda kusimamia yale waliyojifunza kwa kuhakikisha utunzaji mazingira unaimarika pamoja na malezi ya watoto ikiambatana na kuhamasisha jamii ya mkoa huo kujenga tabia ya kuwa karibu na watoto wao kusimamia maadili yao na kuipa elimu kipaumbele.


Katika Baraza hilo Selina Koka alichaguliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Pwani pamoja na Judith Muluge, Hemed Salim na Dk. Michael Benedict.

"VIJANA MKIPATA MIKOPO YA SERIKALI KWA VIKUNDI HUU HAPA UWEKEZAJI WENYE UHAKIKA"

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

WATANZANIA wametakiwa kuanza kilimo cha Vannila kwani zao hilo lina soko na bei kubwa katika mataifa yenye uchumi mkubwa duniani hivyo lina uwezo wa kumwinua mkulima haraka na husistawi kwa muda mfupi.

Wito huo umetolewa Jijini Mwanza na Mkurugenzi Mtendaji wa Vanilla International Ltd Simon Mnkondya katika semina za kufungua fursa zitokanazo na kilimo hicho katika Kanda ya ziwa.

Amesema licha ya zao hilo kuwa na maslahi makubwa ya kumwezesha mkulima kujikomboa kimaisha vilevile ni rafiki wa mazingira hata hivyo mpaka sasa Kanda ya ziwa ni wakaazi asilimia 0.02 ndo wanalima zao hilo.

Mnkondya ameongeza kuwa zao hilo huchukua mwaka mmoja tangia kupandwa hadi kuvunwa huku kilo moja inauzwa sh 1,000,000/= na inatumika katika kutengenezea pafumu nzuri, vipodozi,hutumika kutengenezea juisi, pipi, soda na kutibu magonjwa kama kansa.

Mpaka sasa bado watanzania wengi hawajazichangamkia fursa za uwekezaji wenye tija kwa kulima zao la vanilla hali inayopekelea kuwa na maeneo machache yaliyolimwa zao hilo, mikoa na maeneo kama 
Zanzibar, Kwimba, Arusha, Kilimanjaro,Singida, Daressalaam,Bagamoyo, Kibaha na Ubungo.


Mkaazi wa Jiji la Mwanza Dolla Ng’wandu ameiomba serikali kuangalia fedha zinazotolewa kwa makundi ya vijana toka kwenye halmashauri zao watumie kwa kilimo cha vanilla kutokana na kuwa na bei kubwa kwenye soko ili waweze kupata manufaa.

Amesema mikopo hiyo kwa vijana ambayo imekuwa ikitolewa na halmashauri zao mara kwa mara haina tija ya kuwainua kiuchumi ambapo pia hupotea kutokana na mzunguko kuwa mgumu hivyo ameshauri kutokana na ujio wa fursa kwa zao la vanilla hakuna budi kusaidiwa vijana waendeshe kilimo hicho kwa sasa.

Mkulima kutoka Mkoani Simiyu, Bayege Mbugani ambaye alikuwa ni mfugaji wa ng’ombe na kwa muda amekuwa akihamahama kutafuta marisho hadi kufika mikoa ya Kusini lakini baada ya kupata kufahamu fursa ya zao la vanilla ameachana na ufugaji wa namna hiyo.

“Naomba serikali isaidie wakulima kupata urahisi wa kupata utaalam wa kilimo hicho ili walime kwa mafanikio makubwa tofauti na ilivyo kwa sasa” alisema Mbugani.

Amesema kuwa mpaka sasa anamiezi saba tangu awekeze kwenye zao hilo na faida ambayo ameipata ikiwemo kuuza matawi ya vanilla futi 2 kwa kiasi cha shilingi 20,000, kwa muda

Monday, January 16, 2023

USHINDI WA MANDONGA WANUSURU UBUNGE WA JALANG'O

 NA ALBET G. SENGO

Mbunge wa Lang'ata Mheshimiwa Jalang'o kabla ya pambano la Mandonga dhidi ya Wanyonyi lililofanyika nchini Kenya, aliahidi kwamba kama Madonga angepigwa basi yeye angelazimika kutoka nchini Kenya na kuhamia Tanzania, "Wanyonyi Anyonywe Kabisa " alimalizia kusema mbunge huyo.

DKT MWINYI ATETA NA VIONGOZI WA UWT TAIFA LEO WAMPONGEZA

 

Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg Mary Chatanda akikabidhi Tuzo ya Pongezi kwa Mhe Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar na Kutekeleza Ilani ya CCM ya Uchaguzi 2020-2025. #UWTImara #JeshiLaMama #KaziIendelee

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi akiteta jambo na ujumbe waViongozi wa Umoja  wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Ikulu Zanzibar mapema leo


Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi akiteta jambo na ujumbe waViongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Ikulu Zanzibar mapema leo
Ndg Mary Chatanda, Mwenyekiti wa UWT Taifa akiwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi mara baada ya mazungumzo


Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Zainab Shomari mara baada ya kuteta na Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Ikulu Zanzibar mapema leoujumbe ambao uliongozwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Mary Chatanda.
Ndg Riziki Kingwande, Naibu Katibu Mkuu UWT - Bara





Mbunge Neema Lugangira: Mbunge Neema Lugangira akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi leo Jumatatu   




Na Mwandishi WetuZanzibar.

Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi leo Jumatatu Januari 16,2023 amekutana na Viongozi wa Umoja  wa Wanawake Tanzania (UWT) Ikulu Zanzibar.

Uongozi wa Jumuiya hiyo uliongozwa  na Mwenyekiti wa  UWT Taifa Ndugu Mary Chatanda ,Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa aliyeambatana na  Makamu Mwenyekiti UWT Zanzibar Ndugu Zainab Shomari ,viongozi mbalimbali wa  kitaifa wa Jumuiya hiyo kwa nia ya kujitambulisha baada ya kuchaguliwa .

 Pia wamempongeza Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa kuchaguliwa  kuwa Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar na Kutekeleza Ilani ya CCM ya Utekelezaji 2020-2025 .