MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amewasimulia wakazi wa Mkoa wa Mwanza na mikoa jirani waliohudhuria ufunguzi wa mikutano ya hadhara ya chama hicho uliofanyika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza namna alivyochulkuliwa ‘kinyemela’, kutoka Mwanza hadi kufikishwa Dar es Salaam kisha kufunguliwa mashtaka ya ugaidi.
Akiwaadhithia wananchi hao Mbowe amesema akiwa msibani kwa kaka yake Kilimanjaro Julai, 2021 alisikia Dk Azaveli Lwaitama na Mzee Sylivester Masinde mmoja kati ya waasisi wa chama hicho kuwa wameshikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mwanza na kulazimika kuondoka msibani (Kilimanjaro) na kuja hadi Mwanza kwaajili ya kuwatoa mahabusu.
“Nilivyotua Mwanza kuwatoa rumande, siku ya kwanza, siku ya pili nikakamatwa mimi nikafungwa vitambaa machoni, nikafungwa pingu miguuni, nikafungwa pingu mikononi, nikasafirishwa mazingira nisiyoyajua napelekwa wapi? (alijiuliza), nikapelekwa Dar es Salam na ndio kesi yangu ya ugaidi ikaanzia hapo,”amesimulia.
“Ndugu zangu wa Mwanza nazungumza mambo haya mnaweza kuyaona kama mambo mepesi lakini mimi kama Mwenyekiti wenu kesi ile ikapelekwa miezi nane, asanteni ndugu zangu wa Mwanza na dunia inasikiliza kwa sababu wote mlisikiliza na mkasimama mkasema ‘Mbowe sio gaidi’,”amesema
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.