ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 13, 2014

SHINYANGA WALIVYO SAMBAZA UPENDO NA SERENGETI FIESTA

Pichani kati msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Rachael akiwa na madansa wake wakilishambulia jukwaa kwa namna ya kipekee usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga.
Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,atambulikae kwa jina la kisanii Ommy Dimpo akiwaimbisha mashabiki huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa na wakazi wa mji huo usiku katika tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage
Mmoja wa wasanii wa Bongofleva anaefanya vyema katika muziki huo atambulikae kwa jina la Young Killer a.k.a Msodoki akiimba jukwaani kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga

Pichani juu na chini ni umati wa wakazi wa mji wa Shinyanga waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage,usiku wa kuamkia leo.
Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Ney Wa Mitego (pichani kulia) na Stamina wakilishambulia jukwaa kwa wimbo wao wa Huko Kwenu vipi,huku makele ya shangwe yakiwa yametawala kila kona ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga usiku.
Sehemu ya mashabiki wa Fiesta wakishangilia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la Fiesta 2014 ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga.
Mwanadada Linah akionesha umahiri wake wa kucheza wimbo wake wa Ole Temba juu ya jukwaa la Fiesta 2014 usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage.
Ukipenda muite Mr Blue,msanii wa muziki wa kizazi kipya juu ya jukwaa la Fiesta 2014 ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga.
Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,atambulikae kwa jina la kisanii Ommy Dimpo akiimba mbele ya mashabiki wimbo wake wa ani kama mama katika tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage
Wanajiita Wakata Mkaa kutoka kundi la Wanaume TMK,Chege na Temba kwa pamoja wakilishambulia jukwa la fiesta mbele ya umati wa watu (hawapo pichani) ndani ya tamasha la Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja mdodogo wa Kambarage mjini Shinyanga.
Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Khadija anaetamba na wimbo wake wa maumivu akiwa sambamba na mwanadada Rachael anaetamba na wimbo wake wa Ole temba,kwa pamoja wakilishambulia jukwaa la Fiesta usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,atambulikae kwa jina la kisanii Ommy Dimpo akiwaimbisha mashabiki wimbo wake wa nani kama mamaa, kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage
Sehemu ya umati wa watu wakishangweka na Fiesta .
Mmoja wa wakali wa kukamua mangona kutoka Clouds FM,Dj Zero akikamua  ngoma jukwaani mbele ya umati wa wakazi wa Shinyanga kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage
Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Shinyanga wakiwa ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage,wakishuhudia tamasha la Fiesta 2014 likifanyika.
Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Shinyanga wakiwa ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage,wakishuhudia tamasha la Fiesta 2014 likifanyika.
PICHA ZOTE NA MICHUZIJR.

MSANII MPYA WA DANCE HALL KUTOKA MWANZA SADAM PIDDE A.K.A RAIS WA MWANZA

RAP CITY NATION ENT Presents Sadam Pidde "Rais Wa Mwanza"
Track: Hello Lady (Nakuita)
Studio: MPJ Records/ Produced By T Joh Touchez
#RAPCITYNATION ENT 2014

Friday, September 12, 2014

PEPSI KOMBE LA MEYA ROBO FAINALI YA PILI IMECHEZWA LEO JIJINI MWANZA

Wachezaji wa timu ya soka ya Mkolani Fc wakishangilia goli la pili la ushindi dhidi ya Igoma Fc katika mchezo wa robo fainali michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014 uliochezwa leo katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. Hadi mwisho wa mchezo Mkolani Fc 2-1Igoma 
Na ALBERT G. SENGO, MWANZA.
MICHUANO ya kombe la Pepsi Meya 2014 inayoratibiwa na My Way Entertainment ikiwa chini ya Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula sasa imeingia hatua ya robo fainali ambapo timu nane zimeanza kuchuana kupata timu nne za kucheza nusu fainali Septemba 17 na 18 mwaka huu katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Timu zilizoingia robo fainali na tarehe zake za kushuka dimbani ni pamoja na :-
11th sept- Sokoni vs Mbugani 3-2
12th sept- Mkolani vs Igoma 2-1
13th sept- Wanahabari vs Mirongo Fc  (....)
14th sept- Mnadani vs Magazeti           (....) 

Kwa matokeo zaidi BOFYA PLAY KUSIKILIZA YALIYOJIRI..

UFUNGUZI WA SAFARI POOL TAIFA MOSHI KILIMANJARO

Katibu Tawala wa Wilaya ya Moshi mjini, Remida Ibrahim (wa pili kulia) akicheza kuashilia uzinduzi wa fainali za mashindano ya Pool Taifa yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014” yanayo fanyika katika Ukumbi wa Kuringe Mkoani Kilimanjaro. Kutoka kushoto ni Katibu wa chama cha Pool Taifa(TAPA), Amos Kafwinga, Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na Makamu Mwenyekiti wa TAPA, Fred Mushi.
Baadhi ya Wachezaji wa Pool wakiwa na zawadi mbalimbali wakielekea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi kutoa kwa wagonjwa ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii kile wanacho fadhiliwa wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakati wa ufungunguzi wa mashindano ya Pool Kitaifa yanayofanyika Mkoani humo yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014”.
Baadhi ya wachezaji wa Pool wakitoa zawadi za vitumbalimbali kwa wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii kile wanachofadhiliwa wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakati wa ufungunguzi wa mashindano ya Pool Kitaifa yanayofanyika Mkoani humo yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014”.
Baadhi ya wachezaji wa Pool wakitoa zawadi za vitumbalimbali kwa wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii kile wanachofadhiliwa wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakati wa ufungunguzi wa mashindano ya Pool Kitaifa yanayofanyika Mkoani humo yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014”.
Na Mwandishiwetu,Moshi
WACHEZAJI wa mchezo wa pool nchini wametakiwa kutumia mchezo huo kama sehemu ya ajira kwao na pia sehemu ya kukukutana na kupeana mawazo ya kuinuana kimaisha.

Hayo yamesemwa jana na Katiba Tawala wa Wilaya ya Moshi mjini, Remida Ibrahim wakati alipokuwa mgeni rasmi kwaniaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Ibrahim Msengi katika ufunguzi wa fainali za taifa za mashindano ya ‘Safari Lager National Pool Championship 2014’, zinazofanyikia kwenye ukumbi wa Kuringe mkoani hapa. 

Ibrahim alisema mchezo huo kwa sasa ni ajira kwa wanaoucheza, hivyo ni vema wachezaji wakautumia vizuri kwaajili ya kuwainua kimaisha badala ya kuutumia kwa masuala ambayo hayana faida katika maisha yao.

“Nitumie nafasi hii kuwashukuru wadhamini wa mchezo huu bia ya Safari lager kutokana na kwamba umeongeza ajira kwa vijana, hivyo wachezaji niwasihi tumieni mchezo wa pool kuweza kuinua maisha yenu na pia mnapokutana katika mashindano kama hayo tumieni nafasi hii kushauriana masuala ya msingi ya kuwainua kimaisha,”alisema Ibrahim.

Naye menaja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo aliwataka wachezaji wa timu zote zinazoshiriki fainali hizo kucheza kwa utulivu hadi mwisho wafainali hizo.

Shelukindo alisema haitakuwa jambo la busara endapo fainali hizo zitamalizika huku wakiacha gumzo la vitendo ambavyo si vyakiungwana.

“Kwanza niwape pole kwa uchovu wa safari ndefu mlikotoka kwenye mikoa yenu kwa ajili ya kufika hapa kushiriki fainali hizi lakini ni wombe tucheze kwa amani bila ya kufanya jambo lolote la kuashiria vurugu na tukitoka hapa tuache simulizi nzuri mkoani hapa,”alisema Shelukindo.

Kabla ya fainali hizo kufunguliwa rasmi wachezaji na viongozi wachama cha mchezo huo taifa (TAPA) pamoja na meneja wa bia ya Safari Lager, Osacr Shaelukindo walitembelea wagonjwa katika hospitali ya Rufaa ya Mawenzi na kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo unga, juice, sabuni , biscut, mafuta ya kupaka na pesa taslim.

Timu zinazoshiriki fainali hizo na mikoa yao ikiwa kwenye mabano ni Blue Leaf (Lindi), Bilele (Kagera), Mpo Afrika (Temeke), Mashujaa (Ilala), Topland (Kinondoni), Ya kwetu (Pwani), Billiard (Mwanza) na New Stend (Shinyanga).


Nyingine ni Delux (Dodoma), Black Point (Mbeya), Ngarenaro (Arusha), Nginja Master (Iringa), Corner Kasara (Manyara), Absom (Tanga), Anatory (Morogoro), Tiptop (Tabora) na wenyeji Mboya (Kilimanjaro).

MBUNGE WA VITENDO ALIVYODHAMILIA KUOKOA MAISHA YA WANANCHI WAKE KWA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA AFYA JIMBONI RORYA.

Mkimbiza mwenge wa uhuru kitaifa, Hashim Mahamod, akimpatia mmoja mama mjamzito chandalua kati ya 50 waliopatiwa baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la wodi ya wazazi na watoto la Kituo cha Afya Utegi linalojengwa kwa ufadhili wa Mbunge wa jimbo la Rorya Mhe. Lameck Airo hivi karibuni wakati wa ziara ya mwenge wa uhuru wilayani Rorya mkoani Mara. 
Kazi ya Mbunge wa Jimbo la Rorya, Mhe. Lameck Airo inayoonekana, kushoto ni jengo la utawala na kulia ni jengo la wodi ya wazazi na watoto kushoto kabisa ni jengo la kuhifadhia maiti la kituo cha Afya Utegi
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Kituo cha Afya Utegi Dk Judith Manonga akisoma taarifa fupi ya ujenzi wa kituo cha Afya Utegi kwa wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Mkoa wa Mara na Wilaya ya Rorya hivi karibuni na kueleza kuwa Mbunge Airo ametumia nguvu zake kiasi cha Sh milioni 472.5 kwa ujenzi hadi kukamilika kwa kushirikisha wazaliwa wa Rorya walio nje ya Rorya na kuwa si msemaji bali mtu wa vitendo tunampongeza kwa jitihada za kusaidia wananchi kupata huduma bora za afya. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA


Shehemu ya jengo la wodi ya wazazi na utabibu kama linavyoonekana.
Sehemu ya wananchi wa Utegi waliofika kushuhudia Mwenge wa Uhuru lipofika katika Kituo cha Afya Utegi kuweka jiwe la msingi jengo la wodi wa watoto .
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Rorya (OCD) kulia na kushoto ni Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya Jinai (RCO) Kanda Maalumu ya Tarime Rorya wakiwa timamu kikazi.
Mwonekano wa nje wa Kituo cha Ugani cha kuratibu na Uhifadhi chakula Wilaya ya Rorya kilichojengwa na Halmashauri ya Rorya.
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa katikati akikata utepe katika uzinduzi wa jengo la ofisi ya Ugani, Uratibu na Uhifadhi chakula lililojengwa kijiji na Kata ya Ryagoro wilayani humo, Mkuu wa Wilaya ya Rorya Elias Goroi (wa nne kutoka kushoto) akishiliki tukio hilo. 
Ndani ya Ofisi za  jengo la Ugani na kuratibu Hifadhi ya chakula katika Wilaya ya Rorya ililozinduliwa wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru hivi karibuni.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA UONGOZI WA NEC-JAPAN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Rais wa Shirika la NEC Corporation la Japan, Dkt. Nobuhiro Endo, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 12, 2014 akiwa ameongozana na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Uongozi wa Shirika la NEC Corporation la Japan, wakiongozwa na Rais wao Dkt. Nobuhiro Endo, wakati walipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 12, 2014 kwa ajili ya mazungumzo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Uongozi wa Shirika la NEC Corporation la Japan, wakiongozwa na Rais wao Dkt. Nobuhiro Endo, wakati walipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 12, 2014 kwa ajili ya mazungumzo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwakatika picha ya pamoja na Rais wa Shirika la NEC Corporation la Japan, Dkt. Nobuhiro Endo (kushoto) na Balozi wa Japan Nchini Tanzania, Masaki Okada, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 12, 2014. Picha na OMR
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA UONGOZI WA NEC-JAPAN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo amekutana na Uongozi wa Kampuni ya NEC yenye makao yake makuu jijini Tokyo nchini Japan. Ujumbe wa NEC-Japan umeongozwa na Rais wa Kampuni hiyo inayojishughulisha na masuala ya Mawasiliano na Teknolojia, Dkt. Nobuhiro Endo.

Ujio wa Kampuni hii nchini Tanzania unatokana na mwaliko wa Tanzania kwa makampuni ya Japan kufuatia ziara ya kikazi aliyoifanya Mheshimiwa Makamu wa Rais nchini Japan, mwezi wa Mei mwaka huu. Mheshimiwa Makamu wa Rais alitembelea Makao Makuu ya Kampuni hiyo wakati za ziara hiyo.

Katika mazungumzo na uongozi wa NEC Mheshimiwa Makamu wa Rais aliwaeleza wageni wake nia ya Tanzania kuona inatanua mawasiliano na teknolojia nchini ili kuinua uchumi na akafafanua kuwa teknolojia yoyote kutoka NEC inakaribishwa hapa nchini ili kusaidia Tanzania kupiga hatua.
Uongozi wa NEC nao ulimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa, NEC inaushirikiano wa karibu na Shirika la Simu Tanzania (TTCL) na kwamba wanatarajia kukutana na uongozi wa wizara ya Mambo ya Ndani kwa lengo la kutazama fursa za kusaidia teknolojia katika ulinzi.
Imetolewa na:              Ofisi ya Makamu wa Rais
Ikulu Dar es Salaam Septemba 12, 2014

MASHABIKI WA SKYLIGHT BAND KUSHEHEREKEA BIRTHDAY YA MR. JACK’S HUKU WA WAKIKARIBISHWA NA SHOT'S ZA JACK DANIEL

IMG-20140911-WA0023
Mpango mzima unahisika kwa usiku wa leo pale Thai Village.
DSC_0159
Vijana watanashati wa Skylight Band wakimsindikiza Sam Mapenzi (wa pili kuhsoto) kutoa burudani ya Live Music kwa mashabiki wa bendi hiyo Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam, huku usiku wa leo wataungana na mashabiki wake kusheherekea Birthday Mr. Jack's huku mlangoni wakipata SHOT za Jack Daniel's kusindikiza usiku huo.
DSC_0036
Divas wa Skylight Band wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mary Lucos, igna Mbepera na Meneja wa Band Aneth Kushaba AK47 wakiwajibika.
DSC_0134
Sony Masamba wa Skylight Band akitoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo huku akicheza "style" mpya ya bendi hiyo inayoitwa "FUNGA ZIPU" sambamba na Mary Lucos na Aneth Kushaba AK47.
DSC_0192
Sehemu ya mashabiki wakisakata sebene la Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0139
Mutu muzima Joniko Flower akipiga vocal na kupewa sapoti na Mary Lucos, Sony Masamba na Digna Mbepera.
DSC_0195
Zipopo zilikunyumba.......ni moja ya Swaga za Skylight Band huku mashabiki nao hawakukubali kushindwa.
DSC_0206
Ni raha iliyoje unapoanzisha kitu na mashabiki wako wakipenda kujifunza na kukicheza kama wewe....Skylight Band #Balsaaaa# ndio habari ya mujini.
DSC_0203
Mpiga kinanda wa Skylight Band ambaye anahusika sana kunogesha muziki wa Live wa Skylight Band.
DSC_0206
DSC_0105
Huku burudani ikiendelea #WANAMANYOYA wakipata Ukodak kutoka kulia ni Joshua Ndege, The Big Boss Sebastiana Ndege, Rais wa Wanamanyoya Justine Ndege, Magaua pamoja na Eddievied.
DSC_0038
Aneth Kushaba AK47 a.k.a Komando kipensi akipiga vocal za uhakika kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye uwanja wao wa nyumbani Thai Village ambapo leo patakuwa hapatoshi baada ya kukusanya mashabiki wapya kwenye NYAMA CHOMA FESTIVAL 2014 wikiendi iliyopita.
DSC_0046
Hashimu Donode a.k.a Mzee wa Kiduku akiwajibika jukwaani na hisia kabisa.
Kwa picha zaidi ingia humu

OG WALAWALA CUP YAZINDULIWA RASMI WILAYANI MUHEZA.

Ikiwa ni sehemu ya kuendeleza michezo nchini na kukuza vipaji vya vijana na michezo ajira mpambanaji Omary Muhando toka wilayani Muheza mkoani Tanga ameanzisha ligi yake inayojulikana kama OG Walawala Cup, ligi ambayo imeanza kutimua vumbi tangu jumanne ya tarehe 12 mwezi uliopita wa nne mwaka huu 2014 katika uwanja wa Jitegemee. 
Timu 18 shiriki za michuano hiyo zikiwa katika paredi la utambulisho kabla ya mchezo wa ufunguzi kwa ligi hiyo, inayoshirikisha timu za vijana toka kata mbalimbali wilayani Muheza mkoani Tanga.
Michezo ni urafiki michezo ni udugu na udugu ni kufahamiana kunakodumisha uzalendo.
Mkuu wa wilaya ya Muhaza mkoani Tanga Mhe. Subira Mgalu ndiye alikuwa mgeni rasmi wa mchezo wa ufunguzi wa ligi ya OG Walawala Cup kati Lusanga v/s Muheza uliochezwa tarehe 12/08/2014 ambapo matokeo Muheza waliibuka washindi bao 2 dhidi 1 la Lusanga.