WACHEZAJI
wa mchezo wa pool
nchini wametakiwa kutumia mchezo huo kama sehemu ya ajira kwao na pia sehemu ya kukukutana na kupeana mawazo ya kuinuana kimaisha.
Hayo yamesemwa jana na Katiba Tawala wa Wilaya ya
Moshi mjini, Remida Ibrahim wakati alipokuwa mgeni rasmi kwaniaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo,
Ibrahim Msengi katika ufunguzi wa fainali za taifa za mashindano ya ‘Safari Lager
National Pool Championship 2014’, zinazofanyikia kwenye ukumbi wa Kuringe mkoani hapa.
Ibrahim
alisema mchezo huo kwa sasa ni ajira kwa wanaoucheza, hivyo ni vema wachezaji wakautumia vizuri kwaajili ya kuwainua kimaisha badala ya kuutumia kwa masuala ambayo hayana faida katika maisha yao.
“Nitumie nafasi hii kuwashukuru wadhamini wa mchezo huu bia ya
Safari lager kutokana na kwamba umeongeza ajira kwa vijana,
hivyo wachezaji niwasihi tumieni mchezo wa pool kuweza kuinua maisha yenu na pia mnapokutana katika mashindano kama hayo tumieni nafasi hii kushauriana masuala ya msingi ya kuwainua kimaisha,”alisema
Ibrahim.
Naye menaja wa bia ya
Safari Lager, Oscar
Shelukindo aliwataka wachezaji wa timu zote zinazoshiriki fainali hizo kucheza kwa utulivu hadi mwisho wafainali hizo.
Shelukindo alisema haitakuwa jambo la busara endapo fainali hizo zitamalizika huku wakiacha gumzo
la vitendo ambavyo si vyakiungwana.
“Kwanza
niwape pole kwa uchovu wa safari
ndefu mlikotoka kwenye mikoa yenu kwa ajili ya kufika hapa kushiriki fainali hizi lakini ni wombe tucheze kwa amani bila ya kufanya jambo lolote
la kuashiria vurugu na tukitoka hapa tuache simulizi nzuri mkoani hapa,”alisema Shelukindo.
Kabla ya fainali hizo kufunguliwa rasmi wachezaji na viongozi wachama
cha mchezo huo taifa (TAPA) pamoja na meneja wa bia ya Safari Lager, Osacr Shaelukindo walitembelea wagonjwa katika hospitali ya Rufaa ya Mawenzi na kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo unga,
juice, sabuni , biscut, mafuta ya kupaka na pesa taslim.
Timu zinazoshiriki fainali hizo na mikoa yao ikiwa kwenye mabano ni
Blue Leaf (Lindi), Bilele (Kagera), Mpo Afrika (Temeke), Mashujaa (Ilala),
Topland (Kinondoni), Ya kwetu (Pwani), Billiard (Mwanza) na New Stend (Shinyanga).
Nyingine ni Delux
(Dodoma), Black Point (Mbeya), Ngarenaro (Arusha), Nginja Master (Iringa),
Corner Kasara (Manyara), Absom (Tanga), Anatory (Morogoro), Tiptop (Tabora)
na wenyeji Mboya (Kilimanjaro).
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.