ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 12, 2014

MBUNGE WA VITENDO ALIVYODHAMILIA KUOKOA MAISHA YA WANANCHI WAKE KWA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA AFYA JIMBONI RORYA.

Mkimbiza mwenge wa uhuru kitaifa, Hashim Mahamod, akimpatia mmoja mama mjamzito chandalua kati ya 50 waliopatiwa baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la wodi ya wazazi na watoto la Kituo cha Afya Utegi linalojengwa kwa ufadhili wa Mbunge wa jimbo la Rorya Mhe. Lameck Airo hivi karibuni wakati wa ziara ya mwenge wa uhuru wilayani Rorya mkoani Mara. 
Kazi ya Mbunge wa Jimbo la Rorya, Mhe. Lameck Airo inayoonekana, kushoto ni jengo la utawala na kulia ni jengo la wodi ya wazazi na watoto kushoto kabisa ni jengo la kuhifadhia maiti la kituo cha Afya Utegi
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Kituo cha Afya Utegi Dk Judith Manonga akisoma taarifa fupi ya ujenzi wa kituo cha Afya Utegi kwa wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Mkoa wa Mara na Wilaya ya Rorya hivi karibuni na kueleza kuwa Mbunge Airo ametumia nguvu zake kiasi cha Sh milioni 472.5 kwa ujenzi hadi kukamilika kwa kushirikisha wazaliwa wa Rorya walio nje ya Rorya na kuwa si msemaji bali mtu wa vitendo tunampongeza kwa jitihada za kusaidia wananchi kupata huduma bora za afya. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA


Shehemu ya jengo la wodi ya wazazi na utabibu kama linavyoonekana.
Sehemu ya wananchi wa Utegi waliofika kushuhudia Mwenge wa Uhuru lipofika katika Kituo cha Afya Utegi kuweka jiwe la msingi jengo la wodi wa watoto .
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Rorya (OCD) kulia na kushoto ni Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya Jinai (RCO) Kanda Maalumu ya Tarime Rorya wakiwa timamu kikazi.
Mwonekano wa nje wa Kituo cha Ugani cha kuratibu na Uhifadhi chakula Wilaya ya Rorya kilichojengwa na Halmashauri ya Rorya.
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa katikati akikata utepe katika uzinduzi wa jengo la ofisi ya Ugani, Uratibu na Uhifadhi chakula lililojengwa kijiji na Kata ya Ryagoro wilayani humo, Mkuu wa Wilaya ya Rorya Elias Goroi (wa nne kutoka kushoto) akishiliki tukio hilo. 
Ndani ya Ofisi za  jengo la Ugani na kuratibu Hifadhi ya chakula katika Wilaya ya Rorya ililozinduliwa wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru hivi karibuni.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.