ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 20, 2013

MKUU WA MKOA WA MWANZA KUWA MGENI RASMI FAINALI ZA BALIMI NGOMA FESTIVAL ZITAKAZO FANYIKA KESHO UWANJA WA POLISI MABATINI

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager leo imetangaza kuwa fainali za mashindano ya Ngoma za asili kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa inayojumuisha Tabora, Shinyanga, Kagera, Mara na Mwanza zitafanyika kesho katika uwanja wa Polisi Mabatini jijini Mwanza. Pichani Msimamisi wa Mashindano mbalimbali ya TBL Michael Machela akitoa utambulisho wa wadau watakao shiriki bega kwa bega kuhakikisha fainali inafanyika kwa matokeo stahili.


Meneja wa Matukio wa TBL Kanda ya Ziwa, Erick Mwayella (katikati) amesema fainali za kesho zitahusisha mabingwa wa mikoa waliopatikana katika michakato ya awali iliyofanyika hivi karibuni na kushirikisha vikundi vingi toka mikoa ya Tabora, Shinyanga, Kagera, Mwanza na Musoma. Wengine katika picha kushoto ni Chief Judge wa mashindano hayo ya Ngoma asili Kilonzo Musa na kulia ni Mratibu wa Mashindano Peter Zacharia. Zaidi Bofya play kusikiliza....
Washindani wa wawakilishi Mabingwa wa mikoa ni kama ifuatavyo:-
Tabora - kikundi cha Mwenge
Shinyanga - kikundi cha Mwanajilunguja
Kagera - kikundi cha Ruau
Mwanza - kikundi cha Utandawazi
Mara - kikundi cha Egumba


Mratibu wa Mashindano hayo Peter Zacharia (kulia) amezitaja zawadi:-
Mshindi wa kwanza - 1100,000/= Kombe na Medali
Nafasi ya pili - 850,000/=
Nafasi ya tatu - 600,000/=
Nafasi ya nne - 500,000/=
Nafasi ya tano - 250,000/=


Mashindano haya yamekuja yakiwa na lengo la kuenzi na kulinda tamaduni asili zisipotee, yakihusisha pia tukio la kukutanisha watu mbalimbali kufahamiana na kufurahi pamoja katika suala zima la kudumisha amani na upendo baina yetu.


Na kwa upande wake Chief Judge wa Fainali za Balimi Ngoma Festival, Kilonzo Musa  amesema kuwa kamati yake ya maamuzi haitopendelea bali itatumia kanuni zilizopitishwa na kutambulika kitaifa akiwa na matumaini kuwa wananchi watakao hudhuria hiyo kesho fainali hizo wataridhika na matokeo pindi mshindi atakapo tangazwa.

Mgeni rasmi wa Fainali hizo anatarajiwakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza injinia Evarist Ndikilo ambaye pia atakabidhi zawadi kwa washindi watakao ibuka kwenye shindano hilo.

WANAFUNZI BWIRU WASHIRIKI MCHAKATO WA KUFANYA TATHIMINI YA MAPOKEO YA KAMPENI YA MALARIA HAIKUBALIKI JIJINI MWANZA

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari wavulana Bwiru wakiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa zoezi la Mchakato wa kufanya tathinimi ya jinsi kampeni ya Malaria  Haikubaliki imeleta mabadiliko gani kwa wakazi wa mkoa wa Mwanza kabla ya kelekea mitaani kuzungumza nawananchi.


Wanafunzi wa Shule ya Sekondari wavulana Bwiru wakiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa zoezi la Mchakato wa kufanya tathinimi ya jinsi kampeni ya Malaria  Haikubaliki imeleta mabadiliko gani kwa wakazi wa mkoa wa Mwanza kabla ya kelekea mitaani kuzungumza na wananchi.

Hili ni zoezi litakalodumu kwa siku kumi kwa wadau hawa kupita kaya kwa kaya kulingana na vigezo vyao kwa mategemeo kuwa mwisho wasiku watakuja na majibu ya tathimini.


Waratibu wa zoezi la Mchakato wa kufanya tathinimi ya jinsi kampeni ya Malaria  Haikubaliki imeleta mabadiliko gani nchini, Aunty Sadaka (kulia) na Dada wakijadiliana mambo ya msingi kabla ya kuelekea kwenye kaya mbalimbali na sehemu za mikusanyiko.


Wafanya tathimini wakielekea zoezini.


Kila la kheri kwa Tathimini Team twajua mwisho wasiku mtakuja na majibu yakinifu.


Big up pia kwa Chata la Skonga hii... 

SUPER D ATOA DVD NYINGINE TATU MPYA, TYSON VS HOLYFIELD NDANI


DVD hizi kwa sasa zinapatikana katika makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani wasiliana na kocha kwa simu 0713406938 ili uweze kupata dvd hizo kwa ajili ya kujifunza zaidi mchezo huo

DVD zina mabondia wakari wanaotamba Duniani kama vile Mike Tyson, Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali 
na wengine wengi 

Super D aliongeza pia anakaribisha vijana kuja kujiunga katika mchezo huo kwani mbali ya kukujengea uwezo wa kujiamini pia unajijenga ki Afya na Kimwili


DVD YA MPAMBANO MKALI ULIOWAKUTANISHA BONDIA FELIX TRINIDAD VS ROY JONES JR MPAMBANO HUU UTANGALIA URUDIA NA KURUDIA TENA KWA WAPENZI WA MCHEZO HUU KWANI WOTE WAMEKUTANA MAFUNDI WA UJUZI WA MCHEZO WA MASUMBWI
Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akitoa maelekezo kwa mashabiki wa ngumi jinsi DVD zake zilizo na mafunzo ya mchezo huo kwa mashabiki kujua sheria na kanuni za mchezo huo 
ZAIDI TEMBELEA BLOG YA  
SUPER D

Friday, July 19, 2013

MAAJABU: PAMOJA NA KUPATA MZINGA WA KUTISHA WAKUTWA WAKIWA HAI

Mwananamke mmoja pamoja na dereva wamenusurika kifo kufuatia tukio la ajali mbaya ya kutisha mara baada ya kugonga nyuma ya roli lililokuwa likiendeshwa mbele yao.

Dereva pamoja na mwanamke huyo ambao walikuwa wakisafiria gari ndogo huku wakiwa katika mwendo wa kasi bila kuzingatia distance ya gari na gari wakiwa katika mji wa Guizhou nchini China walijikuta gari lao likibamiza nyuma ya roli lililokuwa mbele yao, mara baada ya roli hilo kupunguza mwendo.
Mwanamke huyo ambaye wakati wa tukio alikutwa amezirai, amelowa damu chepechepe huku akiwa hajavaa mkanda safarini wakati wa ajali alichomoka toka kwenye kiti chake na kichwa chake kubamiza kwenye kioo na kukivaa kama blauzi hali iliyomwonyesha kama kipande cha kichwa cha sanamu kilicho pachikwa kwenye kioo cha ajali ya gari.
Zima moto (waokoaji) waliwahi eneo la tukio na kutoa msaada, hatua ya kwanza ikiwa ni kwa uangalifu walianza kumchomoa dreva ambaye alikuwa katika upande rahisi kutoka kisha kwa mwendo wa kasi yenye umakini na uangalifu wa hali ya juu walianza kuvitoa vioo vilivyokuwa vimemzonga shingoni abiria huyo mwanamke ili wapate kumtoa kiurahisi bila madhara.

Kwa mujibu wa madaktari wa hospitali waliyolazwa jamaa hao ambapo wanapata matibabu taarifa zinasema kuwa hali zao zinaendelea kuimarika siku baada ya siku tofauti na hali waliyokuwa nayo siku ya Jumatano wiki hii walipopata ajali.

DIRECTOR "JOHN KALLAGHE" ALIFANYA KWA TID, JAY DEE, MATONYA NA SASA KWA "AMA G"?

Director John Kalage.

Ama G.
Muandaaji wa video wa kampuni ya Kalla pics amejikuta akikataa au kuzungusha kukabidhi video mpya ya msanii AMA G ambaye alifanya poa kupitia video ya NENDA SALAMA siku za hivi karibuni, kichupa hicho kipya cha AMA G kilifanyika miezi kadhaa (5) iliyopita chini ya kampuni ya KALLAPICS na kutokana na sababu ambazo hadi sasa hazijafahamika kichupa hicho hakijatoka.

Wadau wengi wamekuwa wakihoji, kwa nini kila siku iwe Kallage? 

Msanii Ama G amesema kuwa hatopenda kulizungumzia kwa kina suala hilo kwani tayari amekwisha lifikisha mbele ya vyombo vya dola na kukabidhiwa RB, hivyo kinachofuata ni kumnasa director huyo na kumfikisha panapostahili ili aweze kurudisha gharama zote likiwemo suala la kupotezewa muda!

Ama G. amesema kuwa mara baada ya kushauriana na wadau wake siku si nyingi atauweka wazi mkasa mzima wa tukio na kipi kilichojiri.

Taarifa hii imewasilishwa na DJ Sauti.

Thursday, July 18, 2013

WADHAMINI TBL WASHIRIKI CHAKULA CHA PAMOJA NA TAIFA STARS USIKU HUU HOTEL LAKAIRO MWANZA

"Maneno ya mashabiki huwa matamu sana hasa pale ushindi unapoonekana..Leo umecheza vizuri basi kesho itakuwa neema kwako kama uko peponi kesho umepoteza mchezo watakuona hufai kabisa wala hustahili kuitwa timu ya taifa" "Hao ni wapenzi wa mpira lakini sisi ambao tunakaa na mpira tunasema kwamba matokeo ya uwanjani hayatuvunji  moyo hata siku moja bali yanatujenga kupata nafasi ya kujua matukio mengi zaidi"

" Wanasema kuwa tumejikita zaidi katika majukumu ya Uchaguzi tukaisahau timu, hilo siyo kweli Stars inamipango na ina watu na kila mmoja analijua jukumu lake, kwa mwaka mzima hatuwezi kufanya jambo moja tu! ile hali tuna ratiba na tunamgawanyo wa madaraka"

"Namshukuru Mwalimu aliomba timu ije Mwanza kupitia takwimu zake za kisaikolojia na kijiografia, hivyo tunaamini kuwa tunakila sababu ya kufanya vizuri hiyo siku ya tarehe 27 mjini Kampala"


Benchi la ufundi likisikiliza kwa makini mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea ndani ya hafla iliyoandaliwa na TBL katika Hotel Lakairo jijini Mwanza. 


Meza waliyoketi magolikipa wa timu ya Taifa.


Pamoja tutashinda.


Kutoka kushoto ni Kocha mkuu wa timu ya Taifa Kim Poulsen akitfuatiwa na Meneja kuuu wa timu ya Taifa Leopard Tasso, Kocha wa makipa Juma Pondamali na Kocha msaidizi Slyvester Mash wakijadiliana masuala makuu ya hapa na pale kwenye hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na TBL Mkoa wa Mwanza katika Hotel Lakairo usiku huu. 


Canavaro akiwa na Kiemba.


Dole.....!!!


Peace....!


Kwa upande wake kocha mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen, anasema kuwa anaifuatilia kwa karibu sana hali ya hewa ya nchini Uganda na kila kinachojiri mjini Kampala, kuanzia mazingira watakayofikia, hali ya ya hewa ambayo kila siku najaribu kupata data za vipimo vya majiji yote mawili Kampala na Mwanza walipopiga kambi, vipimo vikionyesha kuwa na hali joto sawa, hivyo hawatokuwa wageni pindi watakapotua Uganda.


Hapa palikuwa patamu sana wakati kila mchezaji kuitwa na kusalimiana na Wadhamini, mwendesha tukio alikuwa Juma Kaseja, eti naye alitaka wachezaji wenzake wamsalimu, inshu ilikuwa ni maneno ya chini chini yaliyokuwa yakizungumzwa na wachezaji wenzake aliokuwa akisalimiana nao... majina ya aka duh ni viroja (Siunaona wadhamini  wakicheka...) 


Wakisalimiana ni Amri Kiemba na Meneja wa TBL Mkoa wa Shinyanga Mr. Robert, huku Kaseja akichombeza kwa utani jina la Kiemba kwa style ya Kocha Kim Poulsen awaitavyo wakati wa kutangaza timu ya Taifa!!


Kelvin Yondani na Juma Kaseja.


Salaaaam...


Picha ya pamoja Stars na Wadhamini wao TBL.


Picha ya pamoja benchi la ufundi na Wadhamini TBL.


Ni flash kwa G. Sengo Blog.
Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Taifa Stars

WAFANYAKAZI WOTE WA AIRTEL DAR WAINGIA MITAANI KUTOA SOMO JINSI YA KUJIUNGA NA AIRTEL YATOSHA NA SHINDA NYUMBA LEO

Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Bi, Adriana Lyamba akijipanga na mmoja wa afisa mauzo wa Airtel wa Dar es salaam Bi, Violet Kajubili muda mfupi kabla ya wafanyakazi wote  kuelekea katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar esa salaam kuonana na wateja ili kutoa huduma mbalimbali ikiwemo  kuwaelimisha wateja wao jinsi ya kutumia huduma ya Airtel yatosha na promosheni ya shinda nyumba 3.

Meneja Uhusioano wa Airtel jackson mmbando akibadilishana mawazo na Maafisa mauzo wa Airtel  wa mkoa wa Dar es Salaam leo wakati wafanyakazi hao wakijipanga kuingia mtaaani kukutana na wateja wao na kuwaelekeza jinsi ya kujiunga na huduma ya Airtel Yatosha SHINDA NYUMBA 3

Baadhi ya maofisa na viongozi wa Timu Airtel Yatosha  wakiendelea kupeana maelekezo jinsi ya kwend a kuingia sokoni kwenye kila mtaa jijini Dar es salaam ili kuwapa somo la AIRTEL YATOSHA shinda nyumba tatu

Usafiri maridadi umeandaliwa ili kuhakikisha kazi na mizunguko ya Airtel yatosha tour inakamilika bila zengwe

Meneja wa Masoko na Chapa wa Airtel Bi, Upendo Nkini nae anawakilisha Timu Yatosha kwenda mtaani sasa.AIRTEL YATOSHA NA BADOOOO!

Leo Airtel imefanya zoezi  la kuingia mtaani jijini dar es salaam na wafanyakazi wao wote wa ofisi kuu jijini Dar es salaam kwa lengo ka kuhakikisha kuwa kila mteja anafaham jinsi ya kufaidika na huduma zao zote ikiwemo ya Airtel Yatosha ambapo mteja hujiunga kwa kupiga *149*99# Kisha kuchagua kifurushi nafuu cha  SIKU WIKI AU MWEZI ili kuongea kwa gharama nafuu kwenda mtandao wowote nchini Tanzania


ECOBANK YAFUNGULIWA RASMI TAWI LAKE JIJINI MWANZA

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akikata pazia la jiwe la msingi kuashiria ufunguzi rasmi wa Ecobank Tawi la Mwanza katika shughuli iliyofanyika jana jioni kwenye jengo la benki hiyo lililopo barabara ya Karuta likitizamana na stesheni ya reli jijini Mwanza.

Hili ndilo jiwe la msingi.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akisoma kwa umakini maelezo ya jiwe la msingi la ufunguzi aliloweka kwa tawi jipya la Ecobank litakalo hudumia wakazi wa pande zote Kanda ya ziwa pamoja na wageni waingiao na kutoka mkoani hapa.

Injinia Ndikiloakisalimiana na Afisa Masoko wa Ecobank mkoa wa Mwanza Manfred Kayala kabla ya kuingia ndani ya benki hiyo kukagua shughuli mbalimbali tawini hapo.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Ndikilo akisaini kitabu cha wageni kwenye tawi jipya la Ecobank Mkoa wa Mwanza huku akishuhudiwa na mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (kulia) ambapo ndipo tawi hilo lilipo.

Ndani ya Ecobank tawi jipya jijini Mwanza. 

Mara baada ya uzinduzi huo hafla fupi ilifuata ndani ya hotel JB Belmont Mwanza ikihudhuriwa na viongozi wa serikali, wafanyabiashara, wajasiliamali wadogo kwa wakubwa hali kadhalika wandishi wa habari.

Mkurugenzi wa Ecobank Tanzania Enock Osei Safo anaimani kuwa benki yake italeta mapinduzi makubwa katika sekta za biashara ndogo kwa kubwa sambamba na kuimarisha soko la zao tegemeo la samaki. 

Injinia Ndikilo amesema kuwa kutokana na Benki hiyo kufungua tawi lake Mkoani Mwanza itawasaidia wafanyabiashara na wajasiliamali kupata huduma kwa ubora wa kiushindani hasa ikizingatiwa Mwanza ni kitovu cha nchi za Maziwa makuu na Jiji la pili kwa shughuli za kibiashara kubwa na linalokuwa kwa kasi zaidi nchini kwa uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo za kibenki. 

Safu ya wafanyakazi wa Ecobank tawi la Mwanza.

Safu ya wafanyakazi wa Ecobank tawi la Mwanza.

Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nyamagana Raphael Shilatu, mkuu wa wilaya ya Magu Jaqueline Rianna, mkuu wa wilaya ya Sengerema na mkuu wa wilaya ya Ilemela Amina Masenza

Meneja wa TRA mkoa wa Mwanza idara ya mapato Mr. Shawiwa (katikati) akiwa na mkewe pamoja na mmoja wa wafanyabiashara maarufu ambaye ni mmiliki wa MSETI Investiment.

Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka mkoa wa Mwanza (WAUWASA) Antony Sanga, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga Patrick Kalangwa pamoja na mmoja wa wadau muhimu wa Ecobank. 

Wakuu mbalimbali.

Meza hii ya wadau iliongozwa na Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu (aliyeketi wa kwanza kulia).

Ni wafanyakazi wa Ecobank wakiwa na zawadi kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, kutoka kushoto ni Ziada Lymo na Anachurine Mushi

Philomena Jacob ambaye ni meneja wa Ecobank tawi la Mwanza (kushoto) akimkabidhi zawadi mkuu wa mkoa wa Mwanza injinia Ndikilo kama kumbukumbu ya ufunguzi wa tawi la benki hiyo.

Kwa mujibu wa Bi. Philomena picha iliyochorwa ya farasi huyu akimbiaye ni mfano wa taswira ya Ecobank katika kuyafukuzia mafanikio kwa wananchi hivyo wategemee kasi katika ukuzwaji kiuchumi kupitia Ecobank.

Naye Mkurugenzi wa Ecobank Mr.Enock alipata fursa ya kumtunukia zawadi mkuu wa mkoa wa Mwanza kwenye hafla hiyo.

Wadau walipata fursa ya kupata chakula cha pamoja na kuabadilishana mawazo.

Wadau namba moja.

'Tuko sawa, karibu ufaidi huduma zetu'

Ecobank Mwanza Crew.

Wafanyakazi wa Ecobank na wakuu wa idara mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na safu ya meza kuu kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya Nyamagana Baraka Konisaga, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo, Mkurugenzi wa Ecobank Enock Osei Safo, Mstahiki meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula na Meneja wa tawi Ecobank Mwanza Bi. Philomena Jacob.

Meneja wa tawi Ecobank Mwanza Bi. Philomena Jacob akizungumza na waandishi wa habari.

Mjengo wa Ecobank tawi la Mwanza.
"Ecobank, pamoja na huduma za kibenki pia ina kampeni yake ya Ecobank Inakuwezesha inayonuia kuwawezesha watanzania kutambua nafasi mabalimbali za kiuchumi kwa kutoa ujuzi, maarifa na elimu  ili kupiga hatua zaidi katika kuzishika zile nafasi na kuboresha maisha ya wananchi. Nawaomba wananchi kutambua nafasi hizi na kuzipokea kila zinapotokea kwani tutafaidi sana kwa kupata maarifa kutokana na uzoefu wa benki hii katika nchi mbalimbali Afrika na kujifunza kutokana na changamoto za nchi nyingine ili kutusaidia sisi kuepuka matatizo madogo madogo katika mada yetu ya maendeleo". alisema Injinia Ndikilo.