ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 20, 2013

MKUU WA MKOA WA MWANZA KUWA MGENI RASMI FAINALI ZA BALIMI NGOMA FESTIVAL ZITAKAZO FANYIKA KESHO UWANJA WA POLISI MABATINI

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager leo imetangaza kuwa fainali za mashindano ya Ngoma za asili kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa inayojumuisha Tabora, Shinyanga, Kagera, Mara na Mwanza zitafanyika kesho katika uwanja wa Polisi Mabatini jijini Mwanza. Pichani Msimamisi wa Mashindano mbalimbali ya TBL Michael Machela akitoa utambulisho wa wadau watakao shiriki bega kwa bega kuhakikisha fainali inafanyika kwa matokeo stahili.


Meneja wa Matukio wa TBL Kanda ya Ziwa, Erick Mwayella (katikati) amesema fainali za kesho zitahusisha mabingwa wa mikoa waliopatikana katika michakato ya awali iliyofanyika hivi karibuni na kushirikisha vikundi vingi toka mikoa ya Tabora, Shinyanga, Kagera, Mwanza na Musoma. Wengine katika picha kushoto ni Chief Judge wa mashindano hayo ya Ngoma asili Kilonzo Musa na kulia ni Mratibu wa Mashindano Peter Zacharia. 



Zaidi Bofya play kusikiliza....
Washindani wa wawakilishi Mabingwa wa mikoa ni kama ifuatavyo:-
Tabora - kikundi cha Mwenge
Shinyanga - kikundi cha Mwanajilunguja
Kagera - kikundi cha Ruau
Mwanza - kikundi cha Utandawazi
Mara - kikundi cha Egumba


Mratibu wa Mashindano hayo Peter Zacharia (kulia) amezitaja zawadi:-
Mshindi wa kwanza - 1100,000/= Kombe na Medali
Nafasi ya pili - 850,000/=
Nafasi ya tatu - 600,000/=
Nafasi ya nne - 500,000/=
Nafasi ya tano - 250,000/=


Mashindano haya yamekuja yakiwa na lengo la kuenzi na kulinda tamaduni asili zisipotee, yakihusisha pia tukio la kukutanisha watu mbalimbali kufahamiana na kufurahi pamoja katika suala zima la kudumisha amani na upendo baina yetu.


Na kwa upande wake Chief Judge wa Fainali za Balimi Ngoma Festival, Kilonzo Musa  amesema kuwa kamati yake ya maamuzi haitopendelea bali itatumia kanuni zilizopitishwa na kutambulika kitaifa akiwa na matumaini kuwa wananchi watakao hudhuria hiyo kesho fainali hizo wataridhika na matokeo pindi mshindi atakapo tangazwa.

Mgeni rasmi wa Fainali hizo anatarajiwakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza injinia Evarist Ndikilo ambaye pia atakabidhi zawadi kwa washindi watakao ibuka kwenye shindano hilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.