ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 16, 2017

DC MCHEMBE AZINDUA KAMPENI YA KUPANDA MITI WILAYA YA GAIRO KATA KWA KATA

 Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe akizungumza machache na wananchi waliofika katika uzinduzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe akipanda miti kuashiria uzinduzi wa kampeni hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe akielekea eneo la tukio na wananchi eneo la tukio.

Na Mwandishi wetu.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe amezindua kampeni ya kupanda miti Kata kwa Kata. 

 Akizungumza jana wakati akizindua kampeni hiyo iliyofanyika katika tarafa la Nongwe kata ya Chanjale, alisema kuwa wananchi ni lazima waheshimu kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti na si kuikata ovyo. 

 Katika kampeni hiyo Mhe. Siriel aliambatana na Meneja wa Misitu Wilaya Bw. David Maiba waliweza kuwahamasisha wananchi kupenda mazingira maana ndiyo yamekuwa yakisababisha wao kupata nvua. "Nawaomba wananchi mpende kuhifadhi mazingira maana ndiyo uhai wetu ambao unasababisdha hata mvua kupatikana, sehemu ikiwa jangwa hamuwezi pata hata maji, niwaombe sana mtunze mazingira kwa ukaribu sana," alisema mhe. Siriel. Kampeni hiyo imeanzia Tarafa ya Nongwe Kata ya Chanjale.

Tarafa hii ipo uwanda wa juu ambapo mvua tayari zimeanza. Viongozi wengine ambao aliambatana nao ni Diwani wa Chanjale Mhe. Maswaga Malima, Mtendaji Kata Bi. Stella Ngomano, Wenyeviti wa Vijiji, Watendaji wa Kata, Wazee Maarufu, Viingozi wa Dini na wananchi kwa ujumla.

Kata ya Chanjale ina Misitu ya Hifadhi yenye ukubwa wa ekari 3,000. Aliongeza kuwa upandaji wa miti utakuwa ni zoezi endelevu na ameshaagiza kila kijiji kiwe na kitalu cha kuzalisha miti japo changamoto inayowakabili ni viriba, ambapo wanahitaji viriba zaidi ya milioni moja kwa Wilaya yote ya Gairo.

WALIOACHIA MAENEO KUPISHA MGODI WATAKIWA KULIPWA FIDIA

 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mang'onyi, Kata ya Mang'onyi, wilayani Ikungi waliosimamisha msafara wake (hawapo pichani)

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mang'onyi, Kata ya Mang'onyi, wilayani Ikungi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani).

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (mbele katikati) akiwa nyumbani kwa Mzee Bastan Mtundwi (mbele kulia) na mkewe Esta Mtundwi ambao walijengewa Nyumba na Kampuni ya Shanta ikiwa ni fidia ya kupisha eneo.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mang'onyi, Kata ya Mang'onyi, wilayani Ikungi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani).

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) akimsikiliza  Meneja wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Shanta Mining Limited, Mhandisi Philbert Rweyamamu (aliyesimama) akielezea shughuli na mkakati wa kampuni yake.


Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza na Wafanyakazi wa Kampuni ya Shanta Mining Limited (hawapo pichani) alipotembelea eneo linalomilikiwa na kampuni hiyo.

SHANTA MINING YATAKIWA KUKAMILISHA ULIPAJI FIDIA

Serikali imeiagiza Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Shanta Mining Limited inayofanya shughuli zake Mkoani Singida kuharakisha ulipaji fidia kwa wananchi waliopisha maeneo yao ili shughuli za uchimbaji zianze mara moja.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alitoa agizo hilo Desemba 12, 2017 wakati wa ziara yake ya kutembelea migodi ya dhahabu katika wilaya za Ikungi na Manyoni ili kujionea shughuli zinazoendelea pamoja na kuzungumza na wachimbaji wa madini.

“Mchakato wa fidia ufanyike haraka na mgodi uanze shughuli zake za uchimbaji mapema,” aliagiza Naibu Waziri Nyongo.

Akiwa njiani kuelekea kwenye Mgodi wa Dhahabu wa Elizabeth Shango uliopo katika Kijiji cha Sambaru, msafara wake ulisimamishwa na wananchi katika Kijiji cha Mang'onyi, Kata ya Mang'onyi, wilayani Ikungi ambao walilalamika kuzuiwa kuendeleza maeneo yao na kampuni hiyo na huku wakicheleweshewa kulipwa fidia.

Walisema kuwa tayari wameachia maeneo waliyokuwa wakimiliki kwa kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo kilimo na uchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu ili kupisha shughuli za uchimbaji mkubwa lakini Kampuni hiyo ya Shanta bado haijakamilisha ulipaji wa fidia.

Wananchi hao vilevile walimuomba Naibu Waziri Nyongo kuiagiza kampuni hiyo kuwapatia maeneo yaliyo wazi ili wafanye shughuli za uchimbaji.

Kufuatia malalamiko hayo, Naibu Waziri Nyongo aliiagiza kampuni hiyo kuhakikisha inakamilisha taratibu za ulipaji wa fidia bila kuchelewa ili shughuli za uchimbaji zianze mapema iwezekanavyo.

“Wananchi wanayo hoja ya msingi na inapasa wasikilizwe, ili taratibu zifanyike bila kuwepo migongano isiyokuwa ya lazima,” alisema.

Aliiagiza kampuni hiyo kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo pamoja na Uongozi wa Vijiji  kujenga mahusiano bora baina yao na wananchi.

Nyongo alisema ili kupunguza migogoro baina ya kampuni na wananchi ni busara wakapatiwa maeneo ili wafanye shughuli za uchimbaji.

“Wapeni na wao maeneo wachimbe, busara itumike kuwapatia maeneo mazuri ili kujenga mahusiano mazuri,” aliagiza Naibu Waziri Nyongo.

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni hiyo, Mhandisi Philbert Rweyamamu alisema kuchelewa kwa mchakato wa ulipaji fidia kumetokana na migongano ya kijamii.

Alisema kutokana na wananchi kutokuwa na elimu sahihi ya faida ya mradi wamekuwa wakileta vikwazo katika hatua mbalimbali za mchakato wa fidia.

Friday, December 15, 2017

LIBYA KUWAADHIBU WANAOHUSIKA NA BIASHARA YA UTUMWA.

Libya kuwaadhibu wanaohusika na biashara ya utumwa
Serikali ya Libya imesema itawaadhibu wale wote watakaopatikana na hatia ya kuhusika na biashara ya utumwa na udhalilishaji wa wahajiri wa Kiafrika
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Mkuu wa Libya Bw. Ahmad M'etig, ambaye ameongeza kuwa, yeyote anayehusiana na ukiukaji wa haki za wahamiaji haramu nchini Libya ataadhibiwa na serikali.
Hivi karibuni kulienea ripoti kuhusu minada katika sehemu mbalimbali nchini Libya ambapo wahamiaji wa Afrika waliuzwa kama watumwa kwa dola 400 za Kimarekani.
Bw. Metig amesema, tume ya kuchunguza matukio hayo imeundwa nchini Libya. Pia amesisitiza kuwa mateso na uuzaji wa binadamu ni vitu vilivyopigwa marufuku nchini Libya na katika nchi za Kiislamu.

Watumwa wakishikiliwa nchini Libya
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, mnada huo wa kuwauza Waafrika kama watumwa nchini Libya ni uhalifu dhidi ya binadamu
Libya ilitumbukia kwenye machafuko tangu mwaka 2011 baada ya madola ya Magharibi yakiongozwa na Marekani kuingia kijeshi huko Libya katika kampeni ya kumng'oa madarakani Kanali Muammar Gaddafi. Tangu mwaka huo hadi hivi sasa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika haijawahi kushuhudia usalama na utulivu hata mara moja.

HABARI KWA HISANI YA  parstoday Shwahili.

POLISI TAZARA WATOA ONYO KWA WAHALIFU.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi Patrick Byatao akimkabidhi cheti cha utendaji bora WP Nina Dachi wa kikosi hicho baada ya kufanya vizuri katika kazi zake ambapo alifanikisha kuzuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA hivi karibuni. (Picha na Jeshi la Polisi)


Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi Patrick Byatao akimkabidhi cheti cha utendaji bora mmoja wa askari wa  kikosi hicho baada ya kufanya vizuri katika kazi zake ambapo alifanikisha kuzuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA hivi karibuni. (Picha na Jeshi la Polisi)
Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi Patrick Byatao akimkabidhi zawadi ya jiko la gesi mmoja wa askari wa  kikosi hicho baada ya kufanya vizuri katika kazi zake ambapo alifanikisha kuzuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA hivi karibuni. (Picha na Jeshi la Polisi)
Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi Patrick Byatao akikagua gwaride wakati wa hafla fupi ya kuwatunuku askari waliofanya vizuri kwa mwaka 2017 katika kikosi hicho ambapo kwa kiasi kikubwa wamezuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA(Picha na Jeshi la Polisi)

Na. Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi nchini limewaonya badhi ya watumishi wasio waaminifu wanaofanya kazi katika Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA)  ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya wizi wa mafuta na miundombinu mbalimbali ya shirika hilo kuacha mara moja.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi, Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi Mwandamizi PATRICK BYATAO wakati wa hafla fupi ya kuwatunukia zawadi baadhi ya Askari waliofanya vizuri katika kuhakikisha usalama wa miundombinu ya shirika hilo ambapo baadhi yao walifanikiwa kuwakamata watumishi wa shirika hilo wakiiba mafuta.

Amesema katika siku za karibuni kumekuwa na matukio kadhaa ya watumishi wa shirika hilo wasio waaminifu ambapo wamekuwa wakilitia hasara shirika hilo jambo ambalo amesema wanaendelea kuimarisha usalama ili kuhakikisha kuwa wanawadhibiti.

BYATAO amesema Kikosi hicho kitaendelea kufanya operesheni za mara kwa mara ili kuhakikisha wanakomesha tabia hiyo ambayo imekuwa ikidhoofisha utendaji wa TAZARA pamoja na kuitia hasara Serikali.

Akizungumzia utoaji wa Zawadi hizo BYATAO amesema askari hao kumi wamefanya vizuri kwa kujituma katika kipindi cha mwaka 2017 hivyo kwa mujibu wa taratibu za Jeshi la Polisi ni vyema kuwazawadia ili kuongeza morali yao ya kazi na kuwafanya wengine kuendelea kujituma zaidi.

Kwa upande wake mmoja wa Askari waliopata zawadi baada ya kufanya vizuri WP NINA DACHI amewaasa askari wenzanke kuendelea kufanya kazi kwa umakini ili kuhakikisha kuwa miundominu ya shirika hilo inakuwa salama wakati wote.

MWANASHERIA WA GGM MBARONI KWA KUMNYIMA NYARAKA NAIBU WAZIRI

Mwanasheria Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) David Nzarigo akipandishwa kwenye gari ya Polisi Baada ya agizo la  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola akipokea taarifa ya shughuli zinazofanywa na Mgodi huo.

Mganga Mkuu wa Mgodi ambaye pia anasimamia kitengo cha mazingira Mgodini wa Dhahabu wa Geita(GGM)akitoa taarifa ya namna ambavyo mgodi umekuwa ukihifadhi mazingira.

Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akitazama baadhi ya nyaraka wakati ambapo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola.

Mwanasheria Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) David Nzarigo akipelekwa kwenye gari la polisi na askali baada ya agizo la Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola.

Moja kati ya Nyumba ambayo hipo ndani ya eneo la Mgodi.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola akikagua madarasa ambayo yanaonekana kuharibiwa na mipasuko.


 Na Joel Maduka,Geita
Mwanasheria Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) David Nzarigo amekamatwa na serikali baada ya kukutwa na nyaraka za serikali .
                                                                                                                                   
Mwanasheria huyo amekamatwa kwa  amri ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola alipotembelea Mgodi huo ambapo pamoja na mambo mengine amebaini mgodi huo kuwa unaendesha shughuli zake bila kufuata sheria ya mazingira .

Mhe. Lugola akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili  Wilayani Geita ameagiza kukamatwa kwa mwanasheria  Mkuu  wa Mgodi wa dhahabu wa  Geita (GGM) David Nzogila baada ya kukutwa na nyaraka za serikali ambazo hazijawa rasmi kutumika kutoka taasisi  ya wakala wa utafiti wa jiolojia Tanzania(GST).

 Hata hivyo katika hali hisiyo ya kawaida na  bila kutarajia mwanasheria huyo aliyekuwa akiukingia kifua mgodi huo  ili usikumbane na rungu la fidia ya uharibifu wa kimazingira kama sheria inavyotamka alijikuta akimweleza Naibu Waziri kuwa anayo ripoti ya GST aliyodai haijaeleza iwapo mgodi huo unahusika moja kwa moja kwenye uharibifu hivyo mgodi huo usibebeshwe mzigo huo.

Kutokana na hali hiyo,Naibu Waziri Lugola aliomba apatiwe riporti hiyo ili ajiridhishe lakini mwanasheria huyo akijibu kwa kujiamnini alimtaka kiongozi huyo wa juu   kutumia mbinu zake kuipata Serikalini lakini yeye  hawezi kutoa nyaraka ya serikali, jambo  lililomkasirisha Naibu Waziri  wa Muungano na Mazingira na kutoa agizo la kukamatwa mara moja.

Diwani wa kata ya mtakuja Constatine Morandi ameelezea kuwa wananchi wamekuwa wakisumbuliwa muda mrefu na mgodi bila ya kupatiwa fidia  na kwamba kutokana na wao kuwa ndani ya bikoni kumesababisha kutokupatiwa huduma mbali mbali za kijamii  hivyo ni vyema kwa serikali wakaweka nguvu kuwasaidia wananchi hao.

Bw Abdallah Omary-Mkazi Nyamalembo alimweleza Naibu waziri  kwamba wamekuwa wakiishi maisha ya mashaka kutokana na hali ilivyo ya maeneo hayo ya mgodini na kwamba mgodi ulikwisha wai kuwapatia fidia ya shilingi elfu ishirini jambo ambalo limeonekana kuwa ni udhalilishaji kwani pesa hiyo ni ndogo.


 Kwa upande wake Makamu wa Rais wa mgodi huo Saimon Shayo,alisema kuwa  eneo ambalo wananchi wamekuwa wakilalamika kuhusu suala la fidia hadi sasa kuna nyumba mbili na kwamba fidia ya kwanza walilipa kiasi cha sh,Bilion Moja na waliipatia serikali iweze kuwafidia wananchi.

HII NDIYO FIMBO YA UHALIFU KWA BODABOBA SENGEREMA



MKUU WA USALAMA BARABARANI MKOA WA MWANZA (RTO)KAMISHNA MSAIDIZI WA JESHI LA POLISI MAKADAM HAMIS MAKADAM  AMEWATAKA WAENDESHA BOBADOBA  WILAYNI SENGEREMA KUFUATA NA KUZINGATIA SHERIA YA USALAMA BARABARANI NA KUACHA KUJIINGIZA KATIKA MATUKIO YA UWALIFU


Akizungumza na waendesha bodaboda hao katika kikao kilichofanyika katika shule ya wavulana Sengerema Sekondari RTO MAKADAM amesema  dhumuni la kikao hicho ni kuwa karibu ili kuelimishana juu ya matumizi ya barabara ikiwemo kufuata sheria na kwayeyeto atakaye kaidi atachukuliwa hatua  za kisheria.

Thursday, December 14, 2017

WALE WAOKAJI WA MIKATE NA KEKI TAMU, ROYAL OVEN SASA WAMEKUSOGEZEA HUDUMA ROCK CITY MALL MWANZA

Carolyne ni meneja wa Royal Oven Mwanza hapa anakuonjesha kwa macho moja ya mikate inayozalisha na Royal Oven, katika duka lake la utoaji huduma lililoko ndani ya Rock City Mall jijini Mwanza. Duka hili limefunguliwa mwezi Disemba 2017 kama sehemu ya juhudi ya kusogeza huduma kwa wananchi hususani wa Jimbo la Ilemela.
Chapati za kumimina.
Half Hot .......
Keki tamu tamu ziko hapa ...
Kwa sendoff, harusi, kitchen party, birthday na dhifa mbalmbali Royal Oven ndiyo jibu.
Birthday cake.
Buns.....
Donut.
Birthday cake.
Stylish.....
Cake za style mbalimbali.
Watoto wanakila sababu ya kupenda wazazi wao.
Ushindwe mwenyewe.
Njoo tukuhudumie.
Mikate kila aina.
Hii utaipenda.
Sun Star, visheti, biscuit na vitafunwa aina zote utavikuta hapa.
Mikate.
Mikate.
Mikate.
Hapa ushinde mwenyewe.
Jiografia ya eneo la kati.
Muonekano toka nje.

JPM: WANAOSEMA VYUMA VIMEKAZA WAWEKE GRISI LA SIVYO VITAVUNJIKA.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli leo amefanya mazungumzo na walimu mjini Dodoma ambapo mbali namambo mengine, wamemueleza changamoto mbalimbalai zinazowakabili ambapo naye ameahidi kuzishughulikia, huku akitoa kiwango cha shilingi milioni kumi kwa ajili ya kuwachangia walimu. Katika mazungumzo yake hayo Rais Magufuli, amewajibu watu wanaotumia msemo wa 'Vyuma Vimekaza' wakimaanisha kwamba maisha ni magumu, ambapo amewashauri vikizidi kukaza sana waweke Grisi la sivyo vitavunjika.

KHERI APOKELEWA KWA KISHINDO MKOANI DODOMA.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg:Kheri D James (katikati) akiwasili Ofisi za Makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa kushoto kwake ni Ndg Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Shaka Hamdu Shaka.
Ndg:Rodrick Mpogolo Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi akimpokea Mwenyekit wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi alipowasili Makao makuu ya chama cha mapinduzi.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana mkoa wa Dodoma akiwasilisha salamu za vijana wa mkoa wake kwa mwenyekiti wa umoja wa vijana Taifa.
Kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ndg:Shaka Hamdu Shaka akizungumza.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha mapinduzi ndg:Thabia Mwita akizungumza na vijana wa Umoja wa Vijana wa chama cha mapinduzi katika viwanja vya makao makuu ya ccm dodoma.
Kikundi cha chipukizi kikitoa burudani
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ndg:Kheri D James akipokea wanachama wapya 200 toka vyama mbalimbali vya upinzani pichani ni alie kuwa katibu wa chama cha ACT WAZALENDO mkoa wa Mwanza ndg:gwanchele.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ndg:Kheri D James akizungumza na Vijana wa mkoa wa dodoma katika hafla ya kumkaribisha iliofanyika makao makuu ya CCM DODOMA.

 Meza kuu 
Vijana wakisikiliza kwa umakini hotuba ya mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ndg:Kheri D James.
PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI