ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 4, 2015

MTU ALIYEBADILI MAUMBILE AONGOZA KWENYE ORODHA YA WANAWAKE 10 WENYE USHAWISHI DUNIANI.

Caitlyn Jenner. 

CHANZO BBC SWAHILI.
Mtu aliyejibadilisha maumbile na kuwa mwanamke Caitlyn Jenner ameorodheshwa miongoni mwa wanawake 10 mashuhuri wenye ushawishi mkubwa pamoja na Angelina Jolie, Singer Sia na Anna Wintour.
Orodha hiyo iliyoongozwa na waziri wa kwanza wa Uskochi Nicola Sturgeon inawatambua wanawake ambao wamekuwa wakiathiri uma pakubwa.
null
Kardashians Jenner 
Nyota wa kipindi cha Keeping up with the Kardashians Jenner aliyejulikana kama Bruce ameorodheshwa katika nafasi ya saba.
Alibadilisha maumbile yake na kujiita Caitlyn katika jarida la Vanity Fair mwezi uliopita.
null
Nicola Sturgeon
Mwanariadha huyo wa zamani ambaye wanawe ni pamoja na mwana wa kambo Kim Kardashian na Kendall Jenner ametunukiwa heshima ya kuonyesha maumbile yake mapya kwa uma.

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MH. MECK SADICK AONGOZA ZOEZI LA KUOSHA MAGARI KUPAMBANA NA KANSA.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Meck Sadick akizindua zoezi la kuosha Magari katika viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya kuchangia Fedha kwa waandishi wa Habari ambao wanamatatizo ya Kiafya ikiwemo Saratani 
 Mkuu wa Wilaya ya Kinomdoni Paul Makonda Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuongea na Waandishi wa Habari pamoja na wadau 
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Meck Sadick akiongea na waandishi wa Habari pamoja na Wadau mbalimbali waliofika kuosha Magari yao kwa ajili ya kuwachangia waandishi wa Habari wenye Matatizo ya Saratani
 Wakielekea kuosha Magari
Mkurugenzi Mkuu wa Habari Maelezo(wa kwanza kushoto)  Athur Mwambene Akiosha Gari
 Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe akiosha Gari wakati wa  Shughuli hiyo maalum kwa ajili ya Kuchangia waandishi wenye udhoofu wa afya zao.
Mzee wa Father Kidevu Blog  Ambaye pia ni mwana TBN  akiendelea na yake....
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akiosha Pikipiki wakati wa shughuli hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akiendelea Kuosha moja ya Magari yaliyofika kuoshwa katika Media Car Wash for Cancer. Ikiwa ni kuchangia waandishi wa habari wenye magonjwa mbalimbali ikiwemo Saratani.
Ankali Issa Michuzi wa Libeneke la Michuzi Blog na Michuzi Media Group na Mwana TBN  akiwa Bizeee... Anaosha Moja ya Magari kwa ajili ya kuchangie waandishi wa habari ambao wanamaradhi ya Saratani
 Watu wanazidi kuchangia .....
Hapa ni zaidi ya Tsh 1,600,000 zimechangishwa na kukabidhiwa 
Chezea Changizo wewe
 Waandishi wakichukua kwa Makini Tukio zima
Picha ya pamoja ya waandishi wa Habari pamoja na Baadhi ya Viongozi 

Unaweza Changia pia kupitia M-Pesa 0766 970240
au
Tigo Pesa 0653 155 808

(Picha zote na Fredy Tony Njeje wa Blogs za Mikoa.)

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA MASHINDANO YA TANO YA KUHIFADHI QUR-AN TUKUFU YALIYOANDALIWA NA TAASISI YA ISTIQAAMA, JIJINI DAR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa hafla fupi ya Utoaji wa Tuzo na Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama,  iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaam, Ilala jijini Dar es Salaam jana usiku. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheki ya Sh. Milioni 3, mshindi wa kwanza wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu, Said Nassor Said, aliyehifadhi Juzuu 30, wakati wa hafla fupi ya Utoaji wa Tuzo na Kuwakirimu washindi hao wa mashindano yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama Ilala jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mehdi Aghajafari, wakati akiondoka kwenye Msikiti wa Istiqaama jana usiku baada ya kushiriki swala ya Talaweh na kukabidhi Tuzo za Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu  wakati akiondoka kwenye Msikiti wa Istiqaama jana usiku baada ya kushiriki swala ya Talaweh na kukabidhi Tuzo za Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu  wakati akiondoka kwenye Msikiti wa Istiqaama jana usiku baada ya kushiriki swala ya Talaweh na kukabidhi Tuzo za Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu  wakati akiondoka kwenye Msikiti wa Istiqaama jana usiku baada ya kushiriki swala ya Talaweh na kukabidhi Tuzo za Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu  wakati akiondoka kwenye Msikiti wa Istiqaama jana usiku baada ya kushiriki swala ya Talaweh na kukabidhi Tuzo za Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama. Picha na OMR

Friday, July 3, 2015

"NATAMANI KUPATA VIPAJI VYA KIKE TOKA JIJINI MWANZA" ASEMA MADAM RITHA WA BSS.

Mkurugenzi wa Benchmark Production, Rita Paulsen aka Madam Rita akizungumza na Jembe Fm 93.7 Mwanza.

Ile team ya Majaji ya jukwaa la kusaka vipaji nchini Tanzania kupitia BSS (Bongo Star Search 2015) tayari imekwisha wasili jijini Mwanza kwaajili ya kufanya usaili kwa washiriki mbalimbali. 

Jembe Fm Mwanza imepata kuzungumza na moja kati ya majaji Madam Ritha BOFYA PLAY MSIKILIZE
'PAMOJA SANA' Mkurugenzi wa Jembe Media Dr. Sebastian Ndege (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Benchmark Production, Rita Paulsen aka Madam Rita ndani ya studio za Jembe Fm 93.7 Mwanza.
Mtayarishaji wa muziki nchini ambaye ni mmoja wa majaji wa BSS Master J (katikati) akifanya mahojiano na Jembe Fm Mwanza.
Mwakilishi wa Salama Condom ambao ni moja kati ya wadhamini wa BSS 2015.
Crew.
Kutoka kushoto ni Dj K-Flip, producer wa Jembe Fm, Oxy na Master J.
Picha ya pamoja.
Jaji Salama Jabir akizungumza na 93.7 Jembe Fm. 
"Hapana siyo mimi labda Salama" Master J na salama walikuwa na jambo hapa....
The area...
Walipotua tu.....

BANK BUDHA Ft_VESTINA - THIS WEEKEND


BOFYA PLAY KUSIKILIZA

AIRTEL YATANGAZA OFA KABAMBE 'NUNUA AIRTEL HOME Wi-Fi NA UPATE NYINGINE BURE.

Ofisa uhusiano na Matukio  wa Airtel, Bi Dangio Kaniki akionyesha kifaa cha HOME Wi-Fi wakati wa kutangaza ofa kabambe ya Sabasaba itakayo wawezesha watanzania kupata kifaa cha bure cha ziada pindi watapokinunua katika viwanja vya maonyesho ya Sabasaba. Pichani, Afisa Masoko wa Airtel ,Ndevonaeli Eliakimu
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza ofa kabambe katika viwanja vya Sabasaba itakayomwezesha mteja kununua kifaa cha HOME Wi-Fi, chenye uwezo wa kuunganisha zaidi ya vifaa 32 kupata huduma ya internet kwa kutumia kifurushi kimoja kwa gharama nafuu zaidi na kuunganishwa kwenye kifurushi cha internet cha 40GB Bure.

 Ofa hiyo itamwezesha mteja kununua HOME Wi-Fi, kwa shilingi 195,000/- na kujipatia Home Wi-Fi ya bure pamoja na kifurushi cha internet cha 40GB cha bure .

Ofa hii inapatikana kwenye banda la Airtel katika viwanja vya maonyesho ya Sabasaba kwa muda wa kipindi hiki cha maonyesho. Akiongea wakati wa kutangaza ofa hii Ofisa uhusiano na Matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki alisema " Tumeona ni vyema kuwazawadia wateja wetu kwa kuwapatia ofa hii ya kifaa kitakachowawezesha kuunganishwa kwenye huduma ya internet kwani mahitaji ya huduma ya internet yanazidi kuongezeka kwa kasi. Airtel HOME WiFi inaweza kuunganisha vifaa zaidi ya 32 kwenye huduma ya intenet ya kasi bila kuhitaji simcard yoyote ya ziada".

"Sambamba na hilo, Airtel HOME Wi-Fi vilevile itaunganisha hadi simu 4 za mkononi zilizoko kokote nchini kwenye akaunti moja na kuwapatia internet ya kasi ya 3.75G.

Kwa sasa wanafamilia na watumiaji wa intenet Tanzania hawana haja ya kununua vifurushi vya intaneti kwa kila simu , kompyuta, Television au vifaa vyovyote vinavyoweza kuunganishwa na internet na badala yake watakachotakiwa kufanya ni kununua kifurushi kwenye kifaa hiki cha HOME Wi-Fi na kuwawezesha wote waliounganishwa na kifaa hicho kupata huduma ya intaneti popote walipo Tanzania na watatumia kifurushi kimoja walichonunua"

"Natoa wito kwa wateja wetu na watanzania kutembelea Banda letu na kujipatia Home Wi-Fi na kuungalisha kweny internet wakati wote". Aliongeza Kaniki

AIRTEL YAKABIDHI FUTARI KWA WATOTO YATIMA KATIKA VITUO VITATU MKOANI DAR ES SALAAM.

Meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia) akiongea na wawakilishi wa vituo vitatu vya watoto yatima baada ya kukakabidhi msaada wa vyakula mbalimbali vya mfungo wa Ramadhani kwa wawakilishi wa vituo vya kulelea watoto waliokatika mazingira magumu. 
 Vituo vilivyopata msaada huo ni pamoja na Almadina cha Tandale, Dogodogo cha Kigogo na Hisani cha Mbaga .wakishuhudiwa na baadhi ya watoto waishio katika vituo hivyo, katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Airtel kupitia mpango wake wa huduma kwa jamii imeanza kutoa futari kwa vituo mbali mbali hapa nchini. 
Meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia) akimkabidhi bibi Kurudhumu Yusuph Juma mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Al- Madina (wa pili Kulia) msaada wa vyakula mbalimbali kwa ajili ya mfungo wa Ramadhani wakishuhudiwa na walezi wa vituo vingine vya Dogodogo kilichopo Kigogo bw, Ditufu Ally (tatu Kulia) na Kituo cha Hisani kilichopo Mbaga bw. Twaha Kambaya (kushoto) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. 
Airtel kupitia mpango wake wa huduma kwa jamii imeanza kutoa futari kwa vituo mbali mbali hapa nchini. 
Meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia) akimkabidhi bw. Twaha Kambaya (kushoto) mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Hisani kilichopo Mbagala msaada wa vyakula mbalimbali kwa ajili ya mfungo huu wa Ramadhani wakishuhudiwa na baadhi ya watoto wa vituo hivyo na mlezi wa kituo cha Al- Madina bi Kurudhumu Yusuph Juma (kati) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana
Meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel, Hawa Bayumi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto waishio katika vituo vya kulelea watoto walio katika mazingira magumu wakati wa hafla ya kuwakabithi msaada wa vyakula kwaajili ya mfungo wa Ramadhani iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, vituo vilivyopata msaada ni pamoja na Almadina cha Tandale, Dogodogo cha Kigogo na Hisani cha Mbagala Dar es salaam.

Thursday, July 2, 2015

NI MSIBA TENA JAMBO CONCEPTS (T) LTD, WACHAPISHAJI WA GAZETI LA JAMBO LEONa Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Jambo Concepts (T) Ltd, inayochapisha magazeti ya Jambo Leo, Staa Spoti na Jarida la Jambo Brand, limempoteza mfanyakazi wake mwingine wa idara ya masoko, Kinai Mtinda (pichani), baada ya kufariki dunia saa 7 usiku wa kuamukia leo katika Hospitali ya Sinza Palestina jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Msiba na mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa kaka yake Mbezi Beach na taratibu zingine kuhusiana na msiba huo zitatolewa baadae.

Marehemu Kinai ameacha watoto wawili.

Kifo cha Mtinda kinakuja ikiwa ni siku chache tangu afariki dunia Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, Ramadhani Kibanike mwishoni mwa mwezi uliopita. Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake libarikiwe Amina.

AIRTEL SMARTFONIKA YAMFIKIA MTANGAZAJI EPHRAIM KIBONDE WA CLOUDS TV

Ofisa Mauzo wa Airtel, Salma Juma akimuelekeza jambo Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Clouds, Ephraim Kibonde kabla ya kumsmartfonika simu ya kisasa mapema wiki hii katika duka la  wazi la Airtel lililopo Game Mlimani City jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga.
Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga (kulia), akimsmartfonika simu Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Clouds, Ephraim Kibonde.
Ofisa Mauzo wa Airtel, Rehema Hoza (katikati), akimkabidhi Kibonde kifaa cha kutunzia umeme 'Powerbank'. Kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Aneth Muga.
Meneja Mawasiliano wa Airtel, Jackoson Mmbando, akimuelekeza jambo, Kibonde baada ya kusmartfonika simu hiyo ya kisasa.
 Ofisa Mauzo wa Airtel, Eveline Amos (kushoto), akiwaelekeza jambo, Kibonde na mteja mwingine waliofika katika duka la wazi lililopo Game Mlimani City.
 Maofisa Mauzo wa Airtel wakiwahudumia wateja katika duka hilo la wazi.
Maofisa mauzo wa Airtel wakiwa katika duka la wazi Game Mlimani City.
Wateja wakihudumiwa katika duka la Airtel Mlimani City.
 Wateja wakihudumiwa katika duka la Airtel Mlimani City.
Wateja wakiwa duka la wazi Game Mlimani City.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Simu ya Airtel imeendelea kuwa smartfonika watu maarufu kwa kuwapatia zawadi za simu kwa awamu tofauti kama walivyojiwekea utaratibu huo.

Akizungumza na mtandao wa www. habari za jamii.com Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema kwa wiki hii mpango huo wa smartfonika umemdondokea Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Clouds, Ephrahim Kibonde ambapo amepata zawadi ya simu ya kisasa yenye uwezo mkubwa.

"Tumejipanga vizuri katika mpango huu wa kuwasmartfonika watu maarufu wakiwemo wa sanii na wadau mbalimbali katika wakati tuliopanga" alisema Mmbando.

Mmbando alisema pamoja na kuendelea kuwasmartfonika walengwa hao sasa mpango mzima utakuwa kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara yaliyoanza mapema wiki hii katika viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Mmbando ametumia fursa hiyo kuwataka wateja wa Airtel kutembelea banda lao lililopo katika viwanja hivyo ili kupata huduma mbalimbali pamoja na kujipatia simu za aina mbalimbali kwa bei nafuu. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)