ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 10, 2025

MWENDELEZO WA KESI YA TUNDU LISSU - MAHAKAMA KUU KUSIKILIZA UAMUZI MDOGO WA KESI HIYO YA UHAINI Oktoba 13

 

MAHAKAMA Kuu, Masijala Ndogo ya Dar es Salaam, inatarajiwa Oktoba 13, mwaka huu kutoa uamuzi mdogo kuhusu pingamizi lililowasilishwa na upande wa Jamhuri, juu ya maelezo ya shahidi ambayo upande wa utetezi uliomba yapokelewe na mahakama ili mshitakiwa ayatumie katika maswali ya dodoso.


Mshitakiwa katika shauri hilo ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, anayekabiliwa na kesi ya uhaini ambayo ipo katika hatua ya usikilizwaji.

Hatua hiyo imefikiwa Leo Oktoba 10,2025 mbele ya jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akisaidiana na Majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.

Awali, Lissu alianza kumhoji Mkaguzi wa Polisi kutoka Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Mtandao, PF 22863 John Kaaya (45), ambaye alikuwa ametoa ushahidi wake wa msingi hapo jana.

Katika maswali yake ya awali, Lissu alimuuliza shahidi huyo ikiwa anauelewa kuhusu tume mbalimbali zilizowahi kuundwa kwa ajili ya mabadiliko ya Katiba, zikiwemo zile zilizokuwa chini ya majaji Francis Nyalali, Robert Kisanga, Mark Bomani na Joseph Warioba, katika vipindi tofauti vya uongozi.

Akijibu, Kaaya alisema hakumbuki tume nyingine kwa kuwa nyingi ziliundwa miaka mingi iliyopita wakati yeye bado yuko shule, lakini alikiri kuifahamu Tume ya Warioba, ambayo iliundwa wakati wa Awamu ya Nne ya Uongozi na rasimu yake kujadiliwa bungeni kwa muda wa miezi sita.

Baada ya maswali hayo, Lissu alimuuliza Kaaya kama aliwahi kuandika maelezo yoyote kabla ya kutoa ushahidi wake mahakamani, na shahidi akajibu kwamba alifanya hivyo na angeweza kuyatambua akiyaona.

Lissu alichukua nakala ya maelezo hayo, akaisoma na kisha kudai kwamba alibaini vipengele 47 vilivyokuwa vinakinzana kati ya ushahidi aliotoa mahakamani na maelezo aliyoyatoa awali. Alidai kuwa kabla ya kuendelea na maswali ya dodoso, mahakama inapaswa kupokea maelezo hayo kama kielelezo.

Akirejea uamuzi wa Mahakama ya Rufani katika kesi ya Lilian Jesus Fotes ya Septemba 2, 2020, Lissu alisema msingi wa hoja yake unatokana na kanuni kwamba shahidi hawezi kuulizwa maswali ya dodoso kabla ya maelezo yake kupokelewa rasmi.

Baada ya maombi hayo, upande wa Jamhuri ulipinga vikali hoja hizo.

Wakili wa Serikali Mkuu, Ajuaye Zegeli, aliibua pingamizi akidai kuwa Lissu hajafuata utaratibu unaotakiwa kisheria, akibainisha kuwa lengo la maelezo ya shahidi ni kuonyesha mkinzano wa kile alichokisema mahakamani na alichokiandika, si kuonyesha mambo aliyoyaacha.

Naye Wakili wa Serikali Mkuu, Ignus Mwiinuka, alidai mshtakiwa hakuzingatia ipasavyo kanuni za msingi za kumhoji shahidi kuhusu uaminifu wake. Alisema upande wa Jamhuri hauna tatizo na Lissu kusoma maelezo kwa shahidi, lakini taratibu nyingine hazikuzingatiwa.

“Anayepaswa kutoa maelezo haya kuwa kielelezo ni shahidi, si mshtakiwa. Hatujasikia mshtakiwa akimuuliza shahidi kama anataka kuyatoa. Badala yake, mshtakiwa mwenyewe ndiye ameomba mahakama yapokee,” alisisitiza Mwiinuka.

Akijibu hoja hizo, Lissu alisisitiza kuwa msimamo wa Mahakama ya Rufani ni wazi kwamba huwezi kumdodosa shahidi kabla ya maelezo yake kupokewa kama kielelezo, akieleza kuwa amefuata utaratibu sahihi.

“Waheshimiwa majaji, nimefuata utaratibu. Wameniletea rejeo la uamuzi. Siku ile nilikosea kwa kuwa sikuwa na rejeo hilo, lakini leo nimezingatia kila hatua. Naombeni msikubali pingamizi hili,” alisema Lissu.

Hata hivyo, Wakili Mwiinuka na Zegeli walisema kuwa baada ya kusikiliza hoja za mshtakiwa, bado msimamo wao ni kwamba utaratibu haukuzingatiwa ipasavyo.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, mahakama iliahirisha shauri hilo hadi Oktoba 13, mwaka huu saa 3:00 asubuhi, kwa ajili ya kutolewa kwa uamuzi mdogo kuhusu pingamizi hilo.

DK.SAMIA AFUNGUKA UMUHIMU KUKAMILISHA MCHAKATO KATIBA MPYA AKIMUELEZEA NYERERE KWA WANANCHI WA BUTIAMA

 

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema Chama hicho kinatambua umuhimu wa kuimarisha zaidi mshikamano wa Watanzania kwa kukamilisha mchakato wa Katiba mpya kama ilivyoelekezwa kwenye Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030.


Akizungumza leo mbele ya wananchi wa Wilaya ya Butiama mkoani Mara ambako ameendelea na mikutano ya kampeni kuomba kura kuelekea Oktoba 29 mwaka huu, Dk.Samia ametumia nafasi hiyo kuelezea mchango wa Baba wa Taifa Mwalimu Julisu Nyerere sambamba na kuelezea miradi iliyokuwa ndogo za Nyerere kwa Watanzania.

Kuhusu Katiba Mpya amesisitiza Chama Chq Mapinduzi (CCM)kinatambua umuhimu wa kuimarisha zaidi mshikamano wa Watanzania kwa kukamilisha mchakato wa Katiba mpya kama ilivyoelekezwa kwenye Ilani ya Uchaguzi Mkuu.


"Haya ni matakwa ya makundi mbalimbali ya Watanzania kwa nyakati tofauti. Tulijaribu wakati wa awamu ya nne mchakato haukukamilika, awamu ya sita tunakwenda kuendeleza mchakato huo.

"Kama walivyofanya waasisi wa taifa na chama chetu, nasi tutaendelea kulinda chama cha mapinduzi katika kusimamia yote hayo kwa maslahi mapana ya Watanzania kwani Baba wa Taifa letu alisema bila CCM madhubuti nchi yetu itayumba," amesema na kusisitiza hatakubali nchi yetu iyumbe kwa kisingizio chochote kile.

Akimueleza zaidi Mwalimu Nyerere Mgombea Urais Dk.Samia amesema Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere ni vigumu kumtenganisha na misingi ya falsafa aliyoijenga nchini ikibebwa na dhana ya uhuru na umoja, uhuru na kujitegemea, uhuru na kazi, uhuru na wajibu na dhana zingine muhimu za kiitikadi.

Dk.Samia amesema kwamba dhana hizo alizianzisha kwa lengo la kuleta umoja na mshikamano nchini kwa lengo la kujenga taifa imara lenye kutegemea na kujali maendeleo ya watu.

"Alisisitiza kuwa maendeleo yote yenye maana hayana budi kuwalenga watu ndiyo maana dira na mipango yetu ya maendeleo pamoja na ilani za Chama Cha Mapinduzi zinajielekeza kujenga taifa linalojitegemea lenye uchumi jumuishi na ustawi wa watu.


"Yaani maendeleo ya jamii, uwezeshaji wa kiuchumi na kukuza uchumi mkubwa wa taifa letu," amesema Dk.Samia amesema Serikali imeweza kutekeleza miradi mikubwa ya utawala bora inayotoa msukumo kwenye sekta za uzalishaji ambayo ni sehemu ya ndoto ya Mwalimu Nyerere.

Ameitaja miradi hiyo ni utekelezaji mpango wa kuhamisha makao makuu ya nchi Dodoma."Tuliamua miaka ile kwamba makao makuu ya nchi yetu yatakuwa Dodoma, tumechelewa kidogo lakini kuanzia awamu ya tano na hii ya sita tumekamilisha uhamiaji wa serikali na kuifanya makao makuu iwe Dodoma.

Aliongeza: "Mihimili yote mitatu ya serikali tayari ipo Dodoma, Bunge lilitangulia, serikali tukafuata na Mahakama mwaka 2024 imehamia Dodoma."

Mgombea Urais Dk.Samia amesema jambo lingine ambalo lilikuwa ndoto ya Mwalimu Nyerere ni ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Julius Nyerere.

Amefafanua kwamba bwawa hilo alitaka lijengwe kipindi chake lakini hali haikuruhusu hata hivyo kwa sasa serikali imeshakamilisha ujenzi wa bwawa hilo.

“Mradi mwingine alioutaja ni mradi wa maji Same - Mwanga ambako alijenga bwawa la Nyumba ya Mungu lakini hakuweza kuuendeleza mradi huo.”

Amesema serikali imeundeleza na kuukamilisha mradi huo ambapo sasa wananchi wa Same, Mwanga na Korogwe wanafaidika na mradi huo.

Aliyataja mabwawa mengine ambayo Hayati Mwalimu Nyerere alitaka yajengwe ni bwawa la Mkomazi lililopo Korogwe ambalo limefikia asilimia 50 na bwawa la Kidunda ambalo lingesaidia maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani na sehemu ya Morogoro.

Ameongeza bwawa hilo ujenzi wake upo asilimia 50."Zile ndoto za Mwalimu za utawala bora, sekta za uwezeshaji wananchi kiuchumi, maendeleo ya jamii ndiyo haya ambayo tunaendelea kutekeleza.

"Baba wa Taifa alituachia misingi mizuri kifalsafa, kisera na kisiasa. Kazi yetu ni kutafsiri misingi ile na fikra zile katika mazingira ya sasa," amesema na kuongeza Serikali itaendelea kudumisha tunu za amani, umoja, mshikamano wa taifa na muungano.







Thursday, October 9, 2025

SALUM MWALIMU AJA NA MAMBO MATATU YA KUMALIZA TATIZO LA AJIRA NCHINI

Salumu Mwalimu
Mgombea urais wa Chama Cha Ukombozi wa Umma(CHAUMMA), Salum Mwalimu,

Mgombea urais wa Chama Cha Ukombozi wa Umma(CHAUMMA), Salum Mwalimu, ametaja mambo matatu ambayo atayafanya kumaliza tatizo la ajira nchini.

Mojawapo amesema ni kuboreshe sekta ya kilimo kwa kuifungamanisha na viwanda.

Amesema kilimo kisichofungamanishwa na viwanda ni kilimo mfu na hakiwezi kuwa na faida kwa nchi.

Mwalimu ametoa kauli hiyo Kigamboni, wakati akiendelea na kampeni zake za kuomba ridhaa ya kuaminiwa kuwa rais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu mwezi huu.

Amesema ili nchi itatue tatizo la ajira ni lazima itengeneze fursa ambazo zinaigharimu kidogo lakini zenye faida kubwa.

"Duniani kote, nchi zinafungamanisha kilimo na viwanda kwa sababu kilimo msingi wake ni kuzalisha malighafi za viwandani.

"Kwa hiyo, Tanzania tusipoheshimu kilimo, hatuwezi kuondokana na tatizo la ajira hata tufanyeje,"amesema Mwalimu.

Jambo la pili ambalo amesema serikali yake italitumia kutengeneza fursa za ajira ni kuboresha mfumo wa elimu ambao utawaandaa Watanzania kupambana na fursa za ajira ndani na nje ya Tanzania.

"Vijana kutoka nchi nyingine, wanakuja Tanzania wanaingia kwenye makampuni yetu na kuchukua ajira zetu kwa sababu vijana wetu uwezo wao wa kufanya kazi katika makampuni hayo ni mdogo kwa sababu elimu yetu haikuwaandaa vizuri.

"Tutaboresha elimu yetu ili kuwaandaa vijana kuziona fursa za ajira na kuwa na uwezo nazo ndani na nje ya Tanzania,"amesema Mwalimu.

Jambo la tatu, amesema serikali yake itahakikisha inazilinda biashara zinazoanzishwa na wananchi wake kuanzia mdogo, za kati na kubwa.

Wednesday, October 8, 2025

MIRADI INAYOTEKELEZWA AWAMU YA DKT. SAMIA MWANZA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Asha- Rose Migiro akiamsha amsha alipowasili kwenye Mkutano wa kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza asubuhi hii Oktoba 8, 2025.

Mkoa wa Mwanza ni Kati ya Mikoa ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amewapendelea sana Kwa kuimiminia miradi lukuki tena ya mabilioni Kwa mabilioni.

‎Miradi hiyo imegawanyika katika mafungu makuu 3 ambayo ni:-

‎a)Miradi ya Urithi kutoka awamu ya 5,iliyokamilika na inayoendelea.


‎b)Miradi mipya iliyoanza awamu ya 6 iliyokamilika na inayoendelea.


‎c)Na miradi ambayo iko mbioni kuanza wakati wowote .


Mwanza yahamia viwanja vya  Nyamagana kumsikiliza Samia

Ifuatavyo ni miradi ambayo inatekelezwa na Rais Samia Mkoani Mwanza kwa kila kundi. 

(a)MIRADI MIPYA

‎1.Ujenzi wa Barabara za lami mitaani mradi wa TACTIC Mwanza CC na Ilemela MC km 32 eg Buhongwa-Igoma


‎2.Ujenzi wa Soko La Kirumba na Soko la Samaki Mkuyuni Bilioni 25.


‎3.Ujenzi wa Kampasi ya TIA Usagara-Mwanza ,Bilioni 8


‎4.Ujenzi wa Soko Kuu la Jiji la Mwanza


‎5.Ujenzi wa Hospitali ya Jiji gorofa 6


‎6.Ujenzi wa Majengo Mapya ya Gorofa Chuo Cha Ufundi na Maendeleo Misungwi.


‎7.Ujenzi wa Jengo jipya la Mwanza Airport na kukarabati wa uwanja kuwa wa Kimataifa


‎8.Ujenzi wa Jengo la Kitega Uchumi la TBA Ghana Kota gorofa 7


‎10.Ujenzi wa Tawi la Chuo Kikuu Cha Ardhi Mwanza (Sengerema)


‎11.Ujenzi wa Barabara za Mitaani chini ya TARURA eg Kisesa-Bujora,kiyungi road nk


‎12.Ujenzi wa shule Mpya za msingi na sekondari zikiwemo za gorofa eg Mwanza girls High School(Magu) only for science ,Nyanza P/School etc.


‎13.Ujenzi wa Hospital za Wilaya eg Sengerema ,Ujenzi wa Vituo vya Afya na ununuzi wa vifaa tiba Wilaya zote za Mwanza.


‎14.Mradi wa Maji Ukiriguru-Sumve Wilayani Misungwi Bilioni 32.


‎15.Ujenzi wa Barabara ya Hungumalwa-Ngudu-Magu km 71


‎16.Ujenzi wa Hospitali Mpya ya Rufaa Ukerewe


‎17.Upanuzi wa Bandari za Mwanza South sanjali na ujenzi wa vivuko vipya.


‎18.Ujenzi wa Chuo Cha Michezo Malya (Malya Sports Complex and Training Centre).Zaidi ya Bilioni 40.


‎19.Ujenzi wa Barabara ya Mabuki-Jojiro-Ngudu


‎20.Ujenzi wa Barabara ya Mwanza Airport -Kayenze-Nyanguge


‎21.Ujenzi wa Barabara ya Nansio-Rugezi


‎22.Ujenzi wa Barabara ya Mwanangwa-Misasi-Salawe-Solwa-Kahama km 150.


‎23.Ujenzi wa Barabara ya Bukokwa-Nyakalilo


‎24.Ujenzi wa Barabara ya Ilalila-Shibula


‎25.Ujenzi wa Barabara ya Sengerema -Nyehunge km 54.4 (Bilioni 73).


‎26.Ujenzi wa Daraja Kubwa la Simiyu lenye mita 150 pamoja na Barabara Unganishi.


‎27.Ujenzi wa Daraja Kubwa la Sukuma lenye urefu wa mita 70 na barabara Unganishi km 4.


‎28.Ujenzi wa Kituo Cha Kanda Cha Uokoaji Ziwa Viktoria


‎29.Majengo ya Utawala ya Halmashauri eg Kwimba,Magu, Sengerema DC nk.


‎30.Ujenzi wa Uwanja Mpya wa Michezo "Tabasam" Sengerema pamoja na Kukarabati wa viwanja vya CCM kirumba na Nyamagana.


‎31.Mradi wa Maji Kisesa bln 49


‎(b)Miradi ya Urithi


‎1.Ujenzi wa daraja la JPM. Umekamilika.


‎2.Ujenzi wa Sgr ya Mwanza-Isaka


‎3.Ukamilishaji wa Stendi za


‎Nyegezi na Nyamhongolo


‎4.Ukamilishaji wa mradi wa Maji Butimba


‎5.Ukamilishaji wa Jengo la OPD Sekou Toure gorofa 6


‎6.Ukarabati wa Meli kubwa ya MV Mwanza Hapa kazi tuu. Umekamilika.


‎7.Ukamilishaji wa Chuo Cha Ufundi na Teknolojia DIT Mwanza Campus


‎8.Ukamiloshji wa Tawi la Chuo Cha Mipango Vijijini Mwanza Centre


‎(c)Miradi ambayo Iko Mbioni kuanza ni


‎-Upanuzi wa Barabara ya njia 4 kutoka Mwanza CBD Hadi JPM bridge (lot 1 km 25),CBD-Usagara Jnct km 25.


‎-Ujenzi wa mgodi mkubwa wa Madini ya Dhahabu Nyanzaga


‎-Upanuzi wa Barabara kuu ya Musoma kuwa njia 4


‎-Upanuzi wa Barabara kuwa njia 4 kutoka Usagara-Shinyanga Border


‎-Kamanga-Katunguru-Sengerema km 3.


‎-Upanuzi kuwa njia 4 wa Barabara ya Mwanza-Nyanguge km 35.


‎-Mwanza Airport-Igombe-Kayenze-Nyanguge km 46


‎-Mkuyuni-Mahina-Nyakato km 10


‎-Nyakato(VETA)-Buswelu-Mhonze km 18.