ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 11, 2012

INAHUUU!

Nikikosa matatizo nikibapa tabu kweli Riziki mwanzo wa chuki.

'RED IN LADY' RELOADED 2012 YAKWEA CHATI

Mwandaaji wa onyesho la mavazi la 'Lady in Red' Reloaded 2012 Mama wa mitindo Asia Idarous Khamsin akiwakaribisha wageni katika onyesho hilo lililofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Katika onyesho hilo palichangishwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walioathirika na madawa ya Kulevya nchini Tanzania ambacho kitakachojengwa huko Kikale, Rufiji mkoani Pwani.

Jokate Mwegelo ambaye alikuwa ni mc wa onyesho la mavazi la 'Lady in Red' Reloaded 2012, katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Katika onyesho hilo pamlichangishwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walioathirika na madawa ya Kulevya nchini Tanzania ambacho kitakachojengwa huko Kikale, Rufiji mkoani Pwani.

Mambo hayooooo, mwanadada ambaye alipanda katika ufunguzi.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Chiddy Benzi akiwasha moto.

Chiddy Benzi on the stage.

Mwandaaji wa onyesho la mavazi la 'Lady in Red' Reloaded 2012 (wa kwanza kulia) Mama wa mtindo Asia Idarous Khamsin akiwa na mumewe Mzee Khamsin katika onyesho hilo lililofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Katika onyesho hilo pamlichangishwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walioathirika na madawa ya Kulevya nchini Tanzania ambacho kitakachojengwa huko Kikale, Rufiji mkoani Pwani.

Ehe! umeona mbao hayo...

Safi, (kulia) mbunifu wa mavazi akiwa na mwanamitindo wake.

Mbunifu chipukizi akiwa na mwanamitindo wake.

Haya sasa, unalo la kusema...'Lady In Lady' Reloaded 2012.

Mambo ya harusi... mpo...

'Lady in Red' Reloaded 2012 liliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

Wabunifu wachanga walionyesha mambo yao.

Ehe! mambo ya kizamani... kitu cha kaptula

Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

Friday, February 10, 2012

DALADALAaaaaa MWANZA MPOoooooo!!

Daladala katika mitaa ya Mwanza.
Kile kipindi cha Daladala kinachorushwa kila siku kupitia ITV kikifanyika ndani ya Daladala ambamo humo abiria hujadiliana masuala mbalimbali yanayozunguka katika harakati za maisha yao ya kila siku, sasa ni zamu ya mkoa wa Mwanza hivyo basi ukikutana na Daladala maeneo ya Nyegezi, Kilimahewa, Pansiasi, Igombe, Igoma, Mabatini, Magu na kwingineko kote panda kisha husika....

Mtangazaji wa kipindi cha Daladala kinachorushwa kupitia ITV Daniel Kijo akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Mwanza Erenest Ndikilo, pindi crew ya kipindi hicho ilipodhuru ofisini kwa mkuu huyo jijini Mwanza leo tayari kuanza shughuli zake rasmi kuanzia wiki ijayo siku ya jumatatu.

Jenerali Ulimwengu akizungumzia mdahalo wa Uhuru wa vyombo vya habari uliofanyika leo katika chuo cha SAUTI Mwanza.
Mdahalo umelenga kuainisha maeneo yanayohusiana na uhuru wa vyombo vya habari ni changamoto zipi, matatizo yapi, wapi kunahatarisha uhuru wa tasnia ya habari, ni namna gani ya kuikwepa hali hiyo na kila mtu anamajukumu yake iwe ni Mwandishi wa habari, wahariri wao, wamiliki wa vyombo vya habari, jamii kwa ujumla vyama vya siasa, serikali na nk kila mtu majukumu yake yameainishwa yote ni kwaajili ya kuboresha maisha yao kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

Umma uliohudhuria mdahalo uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano Chuo Kikuu Cha Sauti jijini Mwanza.

Sahihi kwa kitabu cha mada kilichozinduliwa.

Mwanafunzi kutoka SAUT akizungumza na kipindi cha Daladala.
Nashukuru sana vijana wenzangu kuonyesha uvumilivu wa hali ya juu katika mdahalo wa leo kwani katika mijadala mingi ya miaka ya sasa tumezoea kuona watu wakizomeana, kukatishana kabla mtu hajamaliza kuzungumza na mambo kama hayo...

Kijana ukimpa nafasi na siyo kumwezesha tu, atasema kitu na hiyo nafasi itatumika na ninandoto kuwa siku moja uhuru wa vyombo vya utakuwepo kwani serikali itakuwa ikitenda kazi kwa wananchi na siyo serikari iliyo bosi kwa wananchi.

ZE SAMPO YA KIPINDI KIDEONI MADA:-Ulevi na unyanyasaji wa kijinsia nchini Tanzania

KAZI YA MIKONO YETU SISI WENYEWE.....!!!

Siyo kila kitu unachotumia ni lazima kiwe kimetoka kwa mzungu, angalia ubunifu huu wa Pull!

Thursday, February 9, 2012

FARAJ KATALAMBULA KUZIKWA MKOANI TABORA

Aliyekuwa mtunzi mahiri wa vitabu vya hadithi na riwaya nchini marehemu Faraj Katalambula (kulia) anatazamiwa kuzikwa kesho Isevya mkoani Tabora majira ya saa kumi jioni.

Faraj Katalambula alifariki juzi saa kumi na mbili jioni katika hospitali ya rufaa Muhimbili. Faraj Katalambula ambaye ni mmoja wa watunzi wa vitabu mahiri kupata kutokea atakumbukwa zaidi kwa utunzi wake wa kitabu kilichosomwa sana cha ' Simu ya Kifo'. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa John Katalambula mwanae marehemu.

Ewe Mwenyezi Mungu ilaze Mahali Pema Peponi roho ya marehemu, Amen.

HATIMAYE MGOMO WA MADAKTARI WAMALIZIKA

Maandamano ya jana wakati Mama Kijo-Bisimba akiwa front.
Ule mgomo wa madaktari uliodumu kwa kipindi kirefu hata kuhatarisha maisha ya watanzania katika sekta ya Afya hatimae umefikia mwisho asubuhi ya leo baada ya waziri mkuu Mizengo Pinda kukaa meza moja na madktari hao na kukubaliana yafuatayo.

Kwanza Pinda aliingia mkutanoni hapo Muhimbili saa 9:54 asubuhi kwenye ukumbi wa CPL (Central Pathology Laboratory) na cha kushangaza alipigiwa makofi na madaktari kitu mbacho hakikutegemewa na wengi kutokana na hasira walizokuwa nazo madaktari hao.

Pinda ametangaza Blandina Nyoni amesimamishwa kazi mara moja kama Katibu Mkuu na Deo Mutasiwa amesimamishwa kama Mganga Mkuu wa serikali kama sehemu ya kujibu hoja za madaktari waliogoma wakati uchunguzi ukiendelea..huku interns (Madaktari wa mafunzo) wakirudi kuendelea na kazi Muhimbili.

Pia ametangaza kuwa serikali imekubali kuongeza on call allowance toka Sh10,000 mpaka elfu 25,000 kwa specialists na 20,000 kwa madaktari wa kawaida katika kipindi cha mpito na kwenye bajeti mpya masuala ya mafao ya madaktari yataangaliwa upya.. pia amesema Madaktari wapewe nyumba na Green cards lakini mpaka anaondoka hajaelezea kivipi!

Pinda pia amesema Waziri wa Afya Haji Mponda na Naibu wale Dk. Lucy Nkya watawajibishwa na Mheshimiwa Rais.

EPI BAZIDEI YA KUZALIWA

Anaitwa Snake Fey huyu ni mtaalam wa mitandao, blogu hii inapenda kumtakia kheri katika siku yake muhimu ya kuzaliwa:- "A simple celebration, a gathering of friends; here is wishing you great happiness, a joy that never ends.
HAPPY BIRTHDAY MWANA"

Wednesday, February 8, 2012

MGOMO BUGANDO SASA NI LIVE MEMO ZABANDIKWA UONGOZI WAMTUPIA MKUU WA MKOA KUTOA KAULI

Baba wa Edina Julis (10) akiwa amembeba mtoto wake mwenye maumivu makali ya mguu wakirundi nyumbani baada ya kukosa huduma leo katika hospitali ya Bugando...hata hivyo baadhi ya wauguzi wa kliniki ya mifupa wamemshauri baba huyo kumpeleka mtoto wake katika hospitali binafsi baada ya kuhisi huenda tatizo la mtoto huyo kuwa kubwa kama atakaa bila yaa kupata huduma.

Yaliyojiri leo Hospitali ya rufaa Bugando jijini Mwanza mgomo upo tena unafukuta chini kwa chini na memo tayari zimebandikwa kwenye baadhi ya milango ya vyumba vya mikutano ya wanataaluma wa utibabu tangu jana, Uongozi unakigugumizi kulizungumzia hili na kuweka bayana.

Tangazo linasema:-Kuanzia leo tarehe 7/2/2012 siku ya jumanne saa sita mchana tunataarifu kuwa tunasitisha huduma zote zikiwemo zile za dharula hadi hapo serikali itakapotimiza madai yote yanayosimamiwa na kamati kuu ya madaktari Tanzania. Imetolewa na jumuiya ya Madaktari bugando (Residents, Registrers,Interns)

Huku akipinga kauli iliyoripotiwa na baadhi ya Vyombo vya habari kuhusu yeye kuagiza wagonjwa kuja toka mikoa mbalimbali nchini kuja kupata huduma hospitalini hapa, Kaimu mkurugenzi wa Hospitali ya Bugando Dr.Japhet Giliyoma hakuwa tayari kuelezea bayana hali halisi akisisitiza kuwa mkuu wa mkoa ndiye atakayetoa taarifa rasmi kwani tayari wamekwisha mpatia hali halisi.

Mapokezi wagonjwa wengi wamelalamikia suala la kupigwa tarehe kurejea wiki kadhaa zijazo...

"Naitwa Rehema Wasongwa tareha 25 nilikuja wakanipa tarehe ya leo, leo nimekuja wamenipiga tarehe wiki mbili kurudi tena mimi masikini nitafanyaje na ninasafiri kutoka Musoma hadi Mwanza kuitafuta huduma?"

Julius Lutabi baba wa mtoto Edna aliyegongwa na gari toka jumamosi iliyopita, yuko hapa tangu asubuhi jibu limetoka akipigwa tarehe mpaka.... ameiomba serikali kusitisha mijadala mingine na kuigeukia wizara ya afya.

Mwendo ni kupigwa karenda tuu wengi wamekosa huduma...

Jamani hata kitengo cha ULTRASOUND kama zipo vile...

Shughuli nyingine zinaendelea kama kawa lakini matibabu mmmh!...

Wadau wa habari na sehemu ya wafanyakazi wa hospitali wakipata taarifa toka kwa kaimu mkurugenzi.

Tuesday, February 7, 2012

SHEREHE ZA CCM KILA MDAU ANASEMA LAKE

Ze Videoz'Mambo matamu live.
Basiz' zilizopaki viwanja vya Furahisha nje ya CCM kirumba.
@Kwa tunaoijua vizuri Mwanza, tumefurahi kuona idadi kubwa ya watu waliojazana uwanja wa Kirumba jana wakiwa ni wana vijiji waliosombwa kwa malori, mabasi, na usafiri mwingine kuja Mwanza kucheza ngoma za sungusungu, kugawiwa t-shirt, kanaga na kofia, kula wali nyama, kuona jiji la Mwanza, kuuonekana kwenye luniga, na kisha kupatiwa shilingi 2000 kila mmoja. Safi sana! Wengi walitoka wilaya za vijijini; Magu, Kwimba, Misungwi, na wachache toka wilaya zenye miji kama Sengerema na Geita. Wajanja wenyewe wa Mwanza mjini hawakujisumbua. Na bila kusomba watu toka vijijini - yaani wale maskini wasioweza kupata hata sh 1000 kwa mwezi, CCM itapata wapi watu kwenye mikutano yao? Mchezo wa kizamaaaaaaaani. Kama mnabisha, subiri kilio cha CCM mkoa wa Mwanza uchaguzi mkuu 2015. Hivi hamuwajui wasukuma? Wakisema "twalemaga" ndo "twalemaga" kweli! Unaweza kucheka nao, ukawapa pesa wakachukua, ukawapo wali wakala, na kibano bado unapata. Kamuulize .....!
Nyomiz' ndani ya CCM Kirumba
@Wengine wengi tu leo wamerudishwa makwao, kogongo ferry kulikuwa na coaster moja, bus la mohamed trans na hiance nguo zile zile za jana wanatia huruma wako hoi midomo mikavu!
Fusoz' uwanja wa Furahisha nje ya dimba la CCM Kirumba.
@Mh hivi kweli watu mko serious au ni chuki tu. Nani kasema Watanzania hawana uhuru wa kusafiri kokote nchini? Mnashangaa nini watu kuchukuliwa na mabasi kukutana Kirumba CCM? Si ndiko ilikuwa RV yao kwa ajili ya maadhimisho? Mlitaka wakanyage kwa mguu kutoka Kisesa, Kigongo, Ukiriguru na kwingineko kuja mjini Mwanza? Acheni hizo!

@Watu wanazidi miminika uwanjani hapa, ukweli ni watu ni wengi kutokana kuletwa na Mabasi Makubwa. Uwanja wa ndani ile pich ya kuchezea kandanda imefurika vikundi takribani 50 hivi vya ngoma wakiongozwa na TOT.

Mbonjiz'katikati ya sherehe.
@Jamani kila raia ana haki ya kusema chochote ilimradi asivunje Sheria za Nchi. Tatizo ni kwamba tunapenda kusikia habari za aina fulani tu. Wacha watu wajimwaage wawe wamenunuliwa ama lah kila mmoja anasaka ugali wa familia. Wenye mabasi nao wanatafuta ugali kama Kirumba ndiko kunalipa hata mimi ningekuwa dereva ama utingo ningepeleka gari huko.

@Nimeingia Mwanza leo asubuhi, kitu kilicho nishangaza ni kuonaMabasi yalikuwa yakizunguka mji mzima leo yakibeba watu kuelekea kilumba! Inashangaza kuona kwanini ccm wanatumia nguvu kubwa hivyo kukusanya watu? Hii inaashiria nini?
Paul Masatu,

Monday, February 6, 2012

MKOMBOZI BANK YAZINDUA TAWI MWANZA

Utepe ukikatwa kama ishara ya uzinduzi wa tawi la pili la Benki ya Mkombozi, ulizinduliwa rasmi leo asubuhi na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Catholic la Mwanza, Thadues Ruwaaiich.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Edwina Lupembe amesema kuwa tawi hilo la benki lililofunguliwa jijini Mwanza ambalo ni la pili nchini, limeanzishwa kwa lengo la kutoa huduma za kibenki sanjari na kushughulika na matatizo ya kiuchumi kwa jamii katika nyanja mbalimbali.

Mr M. A Kashonda moja kati ya Board Member
“Hasa benki yetu imewalenga watu wenye kipato cha chini kwa kutoa huduma hizo zikiwemo za akiba, mikopo na kutuma fedha na walengwa wakuu ni wananchi wote na hasa wale wenye vipato vya chini ikiwa ni pamoja na kuwaendeleza katika kilimo kwanza”,

Katika kipindi cha miaka miwili na nusu tangu benki hiyo ianzishwe tangu ilipofungua milango yake hadi Desemba 31mwaka huu, raslimali za benki hiyo zimekua hadi kutoka shilingi bilioni 7 Septemba 2009 hadi kufikia shilingi bilioni 33.49.

Sehemu ya mahudhurio ya ufunguzi huo uliofanyika barabara ya Nyerere jijini Mwanza.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Catholic la Mwanza, Thadues Ruwaaiich akifungua akaunti katika benki hiyo.

Mazungumzo ya hapa na pale na mkurugenzi.

Askofu Paul Lunzoka kutoka Tabora ambaye aliungana na wana Mwanza kwaajili ya tukio la uzinduzi naye akifungua akaunti katika benki hiyo.

Ni mafanikio makubwa kwani ni siku ya kwanza tu lakini wengi wamejitokeza kufungua akaunti katika benki hii.

Mdau wa Mkombozi benki akitoa maelezo kwa wateja.

Baadhi ya wafanyakazi Mkombozi Bank wakipata flash.

Picha ya pamoja na mama Mkurugenzi.

Baba Askofu pamoja na Board Members.

Baba Askofu pamoja na Wafanyakazi.

Benki hii imeanzishwa kama ilivyo kwa huduma nyingine zinazotolewa na Kanisa Katoliki kama vile shule na hospitali huku walengwa wakuu wakiwa ni wananchi wenye kipato cha chini pamoja na kuendeleza kilimo.