Ule mgomo wa madaktari uliodumu kwa kipindi kirefu hata kuhatarisha maisha ya watanzania katika sekta ya Afya hatimae umefikia mwisho asubuhi ya leo baada ya waziri mkuu Mizengo Pinda kukaa meza moja na madktari hao na kukubaliana yafuatayo.
Kwanza Pinda aliingia mkutanoni hapo Muhimbili saa 9:54 asubuhi kwenye ukumbi wa CPL (Central Pathology Laboratory) na cha kushangaza alipigiwa makofi na madaktari kitu mbacho hakikutegemewa na wengi kutokana na hasira walizokuwa nazo madaktari hao.
Pinda ametangaza Blandina Nyoni amesimamishwa kazi mara moja kama Katibu Mkuu na Deo Mutasiwa amesimamishwa kama Mganga Mkuu wa serikali kama sehemu ya kujibu hoja za madaktari waliogoma wakati uchunguzi ukiendelea..huku interns (Madaktari wa mafunzo) wakirudi kuendelea na kazi Muhimbili.
Pia ametangaza kuwa serikali imekubali kuongeza on call allowance toka Sh10,000 mpaka elfu 25,000 kwa specialists na 20,000 kwa madaktari wa kawaida katika kipindi cha mpito na kwenye bajeti mpya masuala ya mafao ya madaktari yataangaliwa upya.. pia amesema Madaktari wapewe nyumba na Green cards lakini mpaka anaondoka hajaelezea kivipi!
Pinda pia amesema Waziri wa Afya Haji Mponda na Naibu wale Dk. Lucy Nkya watawajibishwa na Mheshimiwa Rais.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.