Kamanda mpya wa jeshi la polisi mkoani Mwanza, Simon Sir leo amekabidhiwa rasmi ofisi na kuanza kutekeleza majukumu yake kufuatana na majukumu aliyopangiwa na jeshi hilo.
Kamanda Siro anaanza rasmi kazi hiyo mkoani Mwanza kuongoza jeshi la polisi baada ya aliyekuwa kamanda wa polisi wa mkoani Mwanza Bw. Jamal Rwambow kuhamishiwa makao makuu ya jeshi hilo kitengo cha upelelezi, katika mabadiliko yaliyofanywa na inspekta Jenerali wa polisi Saidi Mwema hivi karibuni.
Wakazi wa jiji hili Tunasema karibu Mkoani petu ambako kuna changamoto kubwa ambazo zinalikabili jeshi lako kiutendaji kutokana na mambo kadhaa ambayo kamanda Siro unapaswa kuyazingatia wakati ukiwa ofisini kwako.
Mkoa ya mwanza ni mojawapo ya mikoa Mikubwa hapa nchini yenye utajiri mkubwa wa biashara ya samaki, pamba, madini ya dhahabu na kiasi kidogo cha dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogowadogo.
Pengine kutokana na mkoa wa Mwanza kuwa na wafanyabiashara wakubwa wasije wakakuletea vishawishi ambavyo vinalenga kupindisha sheria na baadae ukaweza kuingia matatani bili ya wewe kujua kuwa uko ktk mstari usionyooka.
Aidha ndani ya jeshi lako la polisi wapo askari ambao ni watiifu na wanafanya kazi kwa kujituma na kwa moyo mkunjufu wa kuwatumikia wananchi kufuatana na taratibu za jeshi la polisi.
Pia miongoni mwa askari hao watiifu wapo pia baadhi ya askari katika jeshi hilo ambao si waaminifu ni wana mtandao wa uhalifu tangu kipindi cha mwaka 2004 hadi 2009 ambao mara nyingi kutokana na kujiweka safi, hupenda kuwa karibu na makamanda wapya kwa kuwaelekeza au kutoa ushauri, wakajifanya marafiki lakini mwisho wa siku huja na vishawishi ili waweze kukuingiza katika mitego kwa faida zao binafsi.
Tunasema hivyo kwa sababu tunayo mifano mingi ambapo baadhi ya askari polisi wasio zingatia maadili ya kazi hudiriki kuvaa magwanda hata kama hawako zamu, kukaa barabarani na kusimamisha magari na kufanya upekuzi usio halali na wengine kufanya uporaji mchana kweupee, wakishirikiana na askari wa kikosi cha usalama Barabarani ambao hutanda barabarani kukagua makosa ambayo hayapo.
Tunasema karibu kamanda Siro, ila zingatia maoni yetu, hatuna budi kuwa nawe hadi 2020. Mungu ibariki kazi ya mikono yako na mawazo yako.
CHURA MAPOZI YAKE KIBAO USHAYATIA MACHONI, HILI JE?
SANAMU HII YA BABA WA TAIFA MWL. JULIUS KAMBARAGE NYERERE IPO PALE MATANDANI KATIKA KIJIJI CHA MALAMPAKA KILICHOPO WILAYANI MASWA MKOANI SHINYANGA. ILIZINDULIWA KIPINDI CHA MBIO ZA MWENGE 2009 NA KAMA UIONAVYO SANAMU HII MKONONI IMEBEBA MWENGE HIVYO IKIFIKA USIKU MWENGE UNAWAKA.
Tuesday, March 09, 2010
MWANZA
SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYOKUWA YAKIENDELEA JANA KATIKA VIWANJA VYA GAND HALL MWANZA. MAADHIMISHO HAYO YAMEKUJA HUKU YAKIWA YAMEKUSANYA TAARIFA NYINGI KUHUSU HALI YA WANAWAKE DUNIANI.
KTK TOP TEN YA NCHI ZINAZOONGOZA KTK MASUALA MABAYA ZAIDI BARANI AFRIKA KWA WANAWAKE AMBAYO NI UKEKETAJI, UBAKAJI WA WANAWAKE NA WATOTO, GHASIA NA UKATILI, ELIMU DUNI, MAAMBUKIZI YA UKIMWI NA UBAGUZI NA UKANDAMIZAJI, AFRIGHANISTANI NDIYO NCHI YA KWANZA DUNIANI KWA UKANDAMIZAJI WA WANAWAKE.
HATA HIVYO BADO BARA LA AFRIKA LINA HALI YA KUTISHA KWANI KTK HIZO TOP TEN LINA NCHI SABA. SOMALIA IKIWA INAONGOZA KWA DHULUMA NA UKATILI KWA WANAWAKE(YA PILI KWA UBAYA DUNIANI KOTE) WASICHANA WADOGO HUOZWA NA UKEKETAJI HUWAKUMBA ASILIMIA 98 YA WANAWAKE WOTE KISOMALI.