Friday, October 4, 2024
Simba SC 2-2 Coastal Union | Highlights | NBC Premier League 04/10/2024
Coastal Union imelazimisha sare ya 2-2 dhidi ya Simba katika mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa kwenye Dimba KMC Complex, Dar es Salaam.
Simba wametangulia kwa magoli mawili kipindi cha kwanza kutoka kwa Mohamed Hussein Zimbwe Jr. na Lionel Ateba kwa penati , lakini Coastal wakacharuka kipindi cha pili na kupata magoli mawili kupitia kwa Abdallah Hassan na Hernest Malonga....Thursday, October 3, 2024
VIJIJI VYOTE MTWARA VIMEFIKISHIWA UMEME SASA NI ZAMU YA VITONGOJI
📌BILIONI 16.7 KUSAMBAZA UMEME VITONGOJI 150
UWT KIBAHA MJI WACHARUKA WALAANI VIKALI VITENDO VYA KUCHOMA PICHA ZA RAIS SAMIA
NA MWANDISHI WETU, KIBAHA
Jumuiya ya umoja wa wanawake wa Chama cha mapinduzi (UWT) Wilaya ya Kibaha mjini imeungana na Mwenyekiti wao wa Taifa Mary Chatanda kupinga na kulaani vikali kwa baadhi ya wanawake wanaodaiwa kuwa ni wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema (BAWACHA) kuchoma vitenge ambavyo vilikuwa na picha ya Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hasssan kitendo ambacho sio cha uzalendo katika Taifa la Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutoa tamko juu ya tukio hilo Mwenyekiti wa (UWT) Wilaya ya Kibaha mjini Elina Mgonja amesema kwamba wanawake wote kwa umoja wao wamesikitishwa sana kuona vitenge vyenye picha ya Rais vinachomwa hadharani na picha zake kusambaza katika baadhi ya mitandao kitendo ambacho sio cha kiungwana hata kidogo.
Mgonja alibainisha kwamba kitendo hicho ni utovu mkubwa wa nidhamu kwani kufanya hivyo ni ukosefu wa maadili ya nchi na kwamba kundi la wanawake hao wameamua kuvunja heshima baada ya kusema maneno ya uwongo ambayo yanaweza kuleta uchonganishi mkubwa baina ya wananchi pamoja na Rais Samia.
Mwenyekiti huyo alifafanua kwamba Rais wa waamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweza kufanya mambo makubwa katika miradi mbali mbali ya maendeleo na hivyo maneno ambayo yamesemwa na baadhi ya wanawake hao hayana ukweli kabisa hata kidogo hivyo amewaomba watanzania wote kuwa na uzalendo na nchi yao na kuachana kabisa na maneo ya kashfa kwa Rais Samia.
"Sisi kama Jumuiya ya wanawake wa umoja (UWT) Wilaya ya Kibaha mjini tunapinga vikali kabisa na kulaani kitendo hicho kilichofanywa hivi karibuni na baadhi ya wanawake wanaodaiwa kuwa wa (Bavicha) kuchoma vitenge vyenye picha ya Rais Samia huu ni ukosefu mkubwa wa utovu wa nidhamu na maadili kwa hivyo jambo hili limetuumiza sana na alipaswi kufumbiwa macho hata kidogo,"alisema Mwenyekiti Mgonja.
Katika hatua nyingine aliviomba vyombo vya dola ambavyo vinahusika na usalama kuwakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wanawake wote ambao wamehusika kwa makusudi kuchoma kitenge chenye picha ya Rais Samia Suluhu Hassan na kwamba wangekuwa wazalendo na nchi yao wasingefanya tukio kama hilo ambalo wao kama wanawake hawawezi kulifumbia macho hata kidogo.
Kadhalika alisema kitendo walichokifanya ni uchochezi na ni uvunjifu wa amani hivyo wanapaswa kukamatwa kwani wameshindwa kuheshimu mamlaka na madaraka aliyonayo Rais Samia Suluhu Hassan na kwamba wameahidi kuendelea kumlinda na kumtetea kwa hali na mali kwani amefanya mambo makubwa kwa wananchi wa Tanzania katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja naa ili mikubwa ya kimkakati.
Wednesday, October 2, 2024
RC PWANI AUNGURUMA AAHIDI NEEMA KWA WAZEE WA KIBAHA MJI
VICTOR MASANGU, KIBAHA
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge amewahimiza wazee kuhakikisha kwamba wanaweka misingi mizuri na imara kwa ajili ya kuweza kumsapoti Rais wa awamu wa sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumlinda, kumtunza na kumtetea katika shughuli mbali mbali anazozifanya ikiwemo kuwatumikia wananchi wa Tanzania sambamba na kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta tofauti .
Kunenge ameyasema hayo wakati wa kilele cha maadhimisho wa siku ya wazee Duniani ambayo katika ngazi ya Wilaya yamefanyika katika Halmashauri ya Kibaha mji na kuhudhuliwa na wazee mbali mbali kutokana kata zote 14 za Kibaha mji pamoja na viongozi wa serikali, viongozi wa dini pamoja na viongozi wa vyama vya siasa.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani amesema kwamba anatambua mchango mkubwa uliofanywa na wazee wa Mkoa wa Pwani hivyo ana imani wanaweza kumsemea mazuri Rais Samia kwa mambo mazuri ambayo ameyafanya kwa weledi mkubwa katika kuboresha sekta mbali mbali ikiwemo kuifanya Pwani kuwa na miradi mingi ya kimikakati ambayo itakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi.
"Mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Pwani nimefarijika sana kukukutana katika siku hii muhimu ya maadhimisho ya wazee lakini kitu kikubwa ninachowaomba tumpe ushirikiano wa kutosha Rais wetu na kuhakikisha kwambaa tunamlinda na kumtetea kwa yale yote mazuri ambayo amekuwa akiyafanya katika nchi hii kwani ameweza kutenga fedha nyingi ambazo zimeweza kuleta matokeo chanya katika Mkoa wetu wa Pwani ikiwemo kuongoza kwa viwanda nchi nzima,"Kunenge.
Kunenge pia alisema lengo la serikali ya awamu ya nne ni kuweka mikakati madhubuti ya kuendelea kuboresha huduma ya afya hususan kwa wazee ikiwa pamoja na kuwapatia vitambulisho maalumu ambayo vitaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika suala zima la kutambulika pindi wanapokwenda kupatiwa matibabu na huduma nyingine za msingi wanazostahili.
Kadhalika alifafanua kwamba wazee wa Mkoa wa Pwani wana busara nyingi hivyo wanapaswa kama wazazi na walezi kuweza kumpa amani na faraja Rais wao ili aweze kuendelea kuwatumikia wananchi wa Tanzania ikiwa pamoja na kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuboresha huduma mbali mbali kwa wananchi na kuwaahidi kuwatembeza katika mirida ya kimikakati ili waweze kujionea na kujifunza mambo makubwa aliyoyafanya Rais Samia.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa Halmashauri ya Kibaha mji Catherine Saguti amesema kuwa kwa sasa kuna jumla ya wazee wapatao 12,724 na kwamba wameweka mipango ya kuhakikisha wazee wote wanatambuliwa kwa lengo la kuweza kuwabaini ili kuweza kuwabaini na kuwapatia mahitaji yao ya msingi ikiwemo kuwapa kipaumbele zaidi katika mahitaji yao muhimu.
Dkt. Catherine aliongeza kwamba wanaendelea kutekeleza sera ya wazee ya mwaka 2003 ya kuwawezesha wazee wenye umri wa miaka 60 na kuendelea kupatiwa fursa ya huduma ya matibabu pasipokuwa na vikwazo vyovyo vile hususan kwa wale wasiokuwa na uwezo wa kumudu ya kuchangia gharama mbali mbali za matibabu.
Pia alifafanua kwamba Halmashauri ya mji Kibaha katika kuwajali wazee hao imeendelea kutengeneza vitambulisho kwa ajili ya msamaha wa kuweza kupata matibabu bila malipo ambapo wameweza kuwafikia jumla ya wazee wapatao 8,540 ambao tayari wameshatengenezewa vitambulisho hivyo na kukabidhiwa.
Naye Afisa maendeleo ya jamii Halmashaauri ya Kibaha mji Rea Lwanji akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha amebainisha kuwa siku ya wazee dunianiaa inalenga kuleta mabadiliko makubwa katika suala zima la uboreshaji wa maisha pamoja na kuwapatiaa huduma stahiki kwa ustawi wao wa siku za baadae.
Alisema kwamba serikali ya Wilaya ya Kibaha itakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba inaboresha zaidi huduma kwa wazee wote na kwa kuzingatia utekelezaji wa sera ya mwaka 2003 ya kuwapatia wazee hao vitambulisho vya msamaha wa matibabu lengo ikiwa waweze kupatia huduma ya matibabu bila ya vigwazo vyovyote na kuwaweka katika mazingira ambayo ni rafiki katika maisha yao.
Nao baadhi ya wazee hao akiwwemo Rose Lwanda ambaye ni katibu wa baraza la wazee katika Halmashauri ya Kibaha mji ameishukuru serikali japo bado wanakabiliwa na changamoto ya kutoingizwa kwenye mfumo wa Tasaf hivyo wameiomba serikali kuliangalia jambo hilo kwa jicho la tatu ili kuweza kuwasaidia waweze kupata fursa hiyo.
Kadhalika wameiomba serikakali kupitia Halmashauri ya Kibaha mji kuwawekea mfumo mzuri wazee hao kuwaingia katika vikundi ili waweze kupata fursa ya kukopesheka kwa urahisi zaidi lengo ikiwa ni kuweza kujikwamua kiuchumi na kujiendeleza kimaisha ikiwa pamoja na kuomba kushirikishwa katika vikao mbali mbali vya kimaendeleo.
Tuesday, October 1, 2024
SAO HILL YAKABIDHI VIFAA VYA UJENZI KILOSA MUFINDI
VIONGOZI WA DINI NACHINGWEA KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI UCHAGUZI
MAMA KOKA ATEKELEZA AHADI KWA VITENDO YA VITI NA MEZA SHULE YA BOKO TIMIZA
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
BENKI YA NMB YACHANGIA VIFAA VYENYE THAMANI YA MILIONI 60 KWA SHULE TANO ZA MSINGI WILAYA YA MUHEZA
BENKI ya NMB nchini imetoa imechangia vifaa vyenye thamani ya Milioni 60 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya elimu kwa shule tano za Msingi katika wilaya ya Muheza mkoani Tanga ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali
Msaada huo ulikabidhiwa kwa Naibu Waziri Mkuu Dkt Doto Biteko na Afisa Mkuu wa Udhibiti wa Benki ya NMB Doreen Joseph katika Halfa iliyofanyika kwenye uwanja wa Jitegemee wilayanu humo katika wakati Juma la Elimu uliokwenda sambamba na uzinduzi wa Kampeni ya Mtoto wa leo Samia wa Kesho.
Alivitaja vifaa hivyo ambavyo benki hiyo imechangia kuwa ni Madawati 200 kwa shule ya Msingi Kwemkamba ,Magusuru,Mdote,Ngomeni na Mwembeni ambapo kila shule itapata madawati 50 ,vifaa yengine ni vitanda 40 vya double deka na magodoro 80 kwa ajili ya shule ya Msingi Ngomeni .
Alisema pia wamekabidhi vitanda 32 na magodoro 64 kwa ajili ya msingi Masuguru ambayo vitakuwa chachu katika kuhakikisha wanatatua changamoto ambazo zilikuwepo awali katika shule hizo.
“Nikushukuru Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Dotto Biteko pamoja na Serikali kwa kazi kubwa inayofanywa kuendelea kuleta maendeleo nchini na sisi Benki ya NMB tupo tayari kushirikiana na Serikali katika kuendeleza maendeleo”Alisema .
Aidha alisema kwamba utoaji wa vifaa hivyo ni sera ya Benki hiyo kuendelea kurudisha kwa jamii ambayo ni sehemu ya faida wanayoipata kama benki inatoka kwa wadau na jamii hivyo hiyo sehemu yao wanatakiwa kurudisha kwa jamii.
“Benki ya NMB inatambua juhudi za serikali katika kusimamia elimu kwa nguvu zote zilizowekwa ili kuboresha utoaji wa mijini na vijiji ikiwemo utoaji wa elimu bure tunaipongeza Serikali kwa hilo sisi kama wadau furaha yetu ni kuunga mkono juhudi hizo za maendeleo kuisaidia jamii yetu”Alisema
Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo Naibu Waziri Mkuu Dkt Dotto Biteko alisema kampeni hiyo ya Mtoto wa leo ni Samia wa kesho muhimu ambayo inaonyesha walivyoamua kuwekeza kwenye msingi wa muhimu wa watoto kujiamini na hatimaye kuweza kutimiza ndoto ya kuwa viongozi bora wa baadae.
Naibu Waziri Mkuu huyo aliwataka pia wazazi na walimu kushirikiana kuwaandaa wanafunzi wao kuwa viongozi na wazazi bora kwa siku zijazo huku akieleza kwamba Serikali imewekeza katika sekta ya elimu ili kupata matokeo na maendeleo yanayoendana na uwekezaji huo.
Naye kwa upande wake Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Zainabu Katimba alisema Serikali imejipanga kuwaandaa viongozi bora wa kesho kwa kuwekeza zaidi katika sekta ya elimu na miundombinu mbalimballi ikiwemo mazingira bora ya kujifunzia.
Monday, September 30, 2024
TUKAJIANDIKISHE KWENYE DAFTARI LA MKAZI ILI TUPIGE KURA
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la Mkazi ambalo linatarajiwa kufanyika Oktoba 11 hadi 20, 2024 na upigaji wa kura 27, Novemba 2024 kuchagua viongozi wa serikali za Mitaa.
"Niwaombe vijana wote, niwaombe akina mama, akina Baba tuende tukajiandikishe kwenye daftari la mkazi ili tukaweze kupiga kura "
Wito huo ameutoa leo katika viwanja vya Kilwa Kivinje ambako kivinje Jogging klabu wameandaa bonanza lakualika klabu mbalimbali kutoka maeneo mikoa mbalimbali kama vile Dodoma, Mtwara, Pwani na Dar Es Salaam lenye lengo la kudumisha afya, ushirikiano, upendo, umoja na hamasa ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Novemba 27, 2024.
Mhe. Zainabu Telack ametoa angalizo kwa wananchi ambao hawana taarifa sahihi kuhusu vitambulisho walivbyo navyo na zoezi la kujiandikisha katika daftari la mkazi.
"Wapo wenzetu ambao wanasema tayari wanavitambulisho vya kupiga kura vitambulisho kwahiyo hawaoni sababu ya kujiandikisha tena , vile vitambulisho ni kwa ajili ya uchaguzi wa Mwaka kesho lakini kwa uchaguzi huu wa serikali za mitaa, serikali zamitaa ,vijiji na vitongoji tunakwenda kujiandikisha kwenye daftari la mkazi "
Aidha, amewasihii siku ya kupiga kura wajitokeze mapema kwa ajili ya kutimiza wajibu nahaki ya kupiga kura mapema.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary amesema kilammojaazishike tarehe hizo muhimu ambazo tarehe 11 hadi 20 Oktoba , 2024 kwa ajili ya kujiandikisha na tarehe 27 siku ya kupiga kura.