ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 3, 2024

UWT KIBAHA MJI WACHARUKA WALAANI VIKALI VITENDO VYA KUCHOMA PICHA ZA RAIS SAMIA

 


NA MWANDISHI WETU, KIBAHA

 
Jumuiya ya umoja wa  wanawake wa Chama cha mapinduzi (UWT) Wilaya ya Kibaha mjini imeungana na Mwenyekiti wao wa Taifa Mary Chatanda kupinga na kulaani vikali kwa baadhi ya wanawake  wanaodaiwa kuwa ni wa chama cha demokrasia na maendeleo  Chadema (BAWACHA) kuchoma vitenge ambavyo vilikuwa na picha ya  Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hasssan kitendo ambacho sio cha uzalendo katika Taifa la Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari  wakati wa kutoa tamko juu ya tukio hilo Mwenyekiti wa (UWT) Wilaya ya Kibaha mjini Elina Mgonja  amesema kwamba  wanawake wote kwa umoja wao wamesikitishwa sana kuona vitenge vyenye picha ya Rais vinachomwa hadharani na picha zake kusambaza katika  baadhi ya mitandao kitendo ambacho sio cha kiungwana hata kidogo.

Mgonja alibainisha kwamba kitendo hicho ni  utovu mkubwa wa nidhamu  kwani kufanya hivyo ni ukosefu wa maadili ya nchi  na  kwamba kundi la wanawake hao  wameamua kuvunja heshima  baada ya  kusema maneno ya  uwongo  ambayo yanaweza kuleta  uchonganishi mkubwa  baina ya wananchi pamoja na  Rais Samia.

Mwenyekiti huyo alifafanua kwamba Rais wa waamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweza kufanya mambo  makubwa katika miradi mbali mbali ya maendeleo na hivyo maneno ambayo yamesemwa na baadhi ya wanawake hao hayana ukweli kabisa hata kidogo hivyo amewaomba watanzania wote kuwa na uzalendo na nchi yao na kuachana kabisa na maneo ya kashfa kwa Rais Samia.

"Sisi kama Jumuiya ya wanawake wa umoja (UWT) Wilaya ya Kibaha mjini tunapinga vikali kabisa na kulaani kitendo hicho kilichofanywa hivi karibuni na  baadhi ya wanawake wanaodaiwa kuwa wa (Bavicha) kuchoma vitenge vyenye picha ya Rais Samia huu ni ukosefu mkubwa wa utovu wa nidhamu na maadili kwa hivyo jambo hili limetuumiza sana na alipaswi kufumbiwa macho hata kidogo,"alisema  Mwenyekiti  Mgonja.

Katika hatua nyingine aliviomba vyombo vya dola ambavyo vinahusika na usalama kuwakamata na  kuwachukulia hatua kali za kisheria wale  wanawake wote ambao wamehusika kwa makusudi kuchoma kitenge chenye picha ya Rais  Samia Suluhu Hassan na kwamba wangekuwa wazalendo na nchi  yao wasingefanya tukio kama hilo ambalo wao kama wanawake hawawezi kulifumbia macho hata kidogo.

Kadhalika alisema kitendo walichokifanya ni uchochezi na ni uvunjifu wa amani hivyo wanapaswa kukamatwa kwani wameshindwa kuheshimu mamlaka na madaraka aliyonayo Rais  Samia Suluhu Hassan  na kwamba wameahidi kuendelea kumlinda na kumtetea kwa hali na mali kwani amefanya mambo makubwa kwa wananchi wa Tanzania katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja naa ili mikubwa ya kimkakati.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.