ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 5, 2019

SHIRIKA LA RELI TANZANIA LAKANUSHA TAARIFA ZA AJIRA ZAIDI YA 200

Shirika la Reli Tanzania limekanusha taarifa zinazosambaa atika mitandao ya kijamii kuhusu fursa za ajira zaidi ya 200 zilizotangazwa na Shirika la Reli Tanzania - TRC.

ZIARA YA RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI MKOANI SONGWE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli anafanya ziara ya siku tatu Mkoani Songwe ambapo anafungua na kukagua miradi ya Maendeleo pamoja na kuzungumza na Wananchi wa Maeneo mbalimbali ya Songwe na Wilaya zake

BODABODA WAFUNGUKA SAKATA LA KUTAJWA KUWAPIGA MIMBA WANAFUNZI



Tabia mbaya za malezi na makuzi, vishawishi na changamoto za mazingira kama vile umbali kutoka majumbani hadi shuleni ni moja ya sababu zinazotajwa kuchangia ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaopata mimba wakiwa mashuleni.

Ingawa ni vigumu kupata takwimu sahihi kujua kundi gani la wanaume linaloongoza kutajwa katika mimba hizo lakini wengi wanawanyooshea vidole madreva wa pikipiki al-maarufu 'bodaboda'. 

Kutoka kata ya Lumiji wilayani Magu mkoani Mwanza Bodaboda wamefunguka haya katika kongamano la Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wilayani humo.

Thursday, October 3, 2019

TAIFA STARS DIMBANI MECHI YA KIRAFIKI DHIDI YA RWANDA.

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) October 14, 2019 pambano ambalo litakuwa kwenye tarehe za kalenda ya FIFA litapigwa nchini Rwanda.


'WAKURUGENZI MSIINGIE MTEGONI" JAFO

 Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, akizungumza wakati wa kikaokazi kilichokwenda sambamba na zoezi la kula kiapo cha maadili kwa kwa Wakurugenzi wapya jijini Dodoma (Picha zote na Atley Kuni-TAMISEMI)
 Kaimu Katibu Mkuu akizungumza katika kikaokazi cha Wakurugenzi wapya.
 Zoezi la kiapo cha uadilifu likiendelea.
 Picha ya pamoja mara baada ya Hotuba ya Mhe. Waziri wakati wakikaokazi hicho.
 Kiapo kikiendelea.

 ‘Wakurugenzi Msiingie Mtegoni’ – Jafo

Na. Atley Kuni- TAMISEMI.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Seleman Jafo amewatahadharisha wakurugenzi wapya walioteuliwa hivi karibuni kukwepa mtego uliowanasa wenzao waliondolewa madarakani na badala yake wakajenge mshikamano na umoja kwa watumishi watakao wakuta kwenye vituo vyao vipya vya kazi.

Akizungumza katika kikaokazi cha Wakurugenzi hao kilichokwenda sambamba na zoezi la kula kiapo cha Maadili kwa viongozi wa umma, Jafo amewatahadharisha viongozi hao dhidi ya baadhi ya watumishi watakao wapelekea majungu kwakujipendekeza na kutaka kuchonganisha watendaji na kuvuruga utendaji wa Halmashauri.

“Ajenda kuu ya Serikali hivi sasa ni ukusanyaji wa mapato, lakini pia usimamizi wa Miradi ya maendeleo ikiwepo fedha za vituo vya afya ambazo baadhi walishindwa kuzisimamia hivyo ili muweze kufanikiwa katika hili lazima mkatengeneze mahusiano   na morali miongoni mwa watumishi ili   msikwame na watu wachape kazi kwa hamasa kubwa” alisema Waziri Jafo.

Awali akitoa maneno ya utangulizi, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mathias Kabunduguru, aliwataka wakurugenzi hao watambue huu ni mwaka wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivyo wakasimamie ipasavyo zoezi la kuandikisha wapiga kura litakalo anza tarehe 08 Oktoba, 2019.

“Idadi kubwa mlioteuliwa mlikuwa watumishi katika ngazi ya mamlaka ya Serikali za Mitaa, hivyo haitakuwa kazi sana, lakini yapo yale ambayo yalikuwa yanakukera ukiwa kama Afisa Tarafa unapoagizwa na Mkurugenzi, sasa hayo usiende kuwafanyia waliochini yako bali mkafanye kazi kwa ushirikiano” Alisema Kabunduguru.

Bw. Mohamed Mavura ni miongoni mwa Wakurugenzi wapya aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani, amesema kuwa anakwenda Kibiti akiwa anajua kabisa ipo Miradi ya Maendeleo, suala la mapato, lakini pia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu wa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 hivyo ameahidi kufanya kazi kwa umoja na mshikamano kama Waziri alivyowaasa.

Wakurugenzi waliokula kiapo hicho mbele ya Afisa Mfawidhi wa Sekretarieti ya Maadili ni pamoja na Bw. Ndaki Stephano Muhuli, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, Bi. Rehema Said Bwasi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Bi. Sheillah Edward Lukuba, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro mkoani Morogoro, Bw. Mohamed Mavura Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani.

Wengine ni  Bw. Ezekiel Henrick Magehema, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, Bi. Diana Sono Zacharia, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama mkoani Mara, Bi. Hanji Godigodi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Bw. Said H. Magaro Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Bi. Hawa Lumuli Mposi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro, na Bw. Godwin Justin Chacha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro.

AZAKI MKOA WA MWANZA ZAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO ZA KISEKTA


Asasi za kiraia zaidi ya 80 za Mkoa wa Mwanza zimekutana leo hii kujadili fursa na changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

Lengo kuu la kukutana kwa Asasi hizi ilikuwa ni kukutana kwa pamoja na kujadili baadhi ya masuala muhimu ya kisekta yanayohitaji mjadala mpana ili kuboresha ushirikiano miongoni mwa asasi za kiraia za Mkoa wa Mwanza.

Akifungua mkutano huo wa jukwaa la asisi za Mkoa wa Mwanza, Dr Philmon Sengati alisema kuwa, tamaduni za asasi za kiraia kukutana na kujadili mambo ya kisekta ni jambo jema sana kwani linaleta afya njema ndani ya sekta.

Naye Mwezeshaji Bwana Israel Ilunde alisema kuwa, lengo la kuwa na jukwaa na Kimkoa ni kupaza sauti kwa pamoja na kujua namna ya kusonga mbele licha ya kukabiliana na vikwazo vya kiutendaji.

Naye Mkurugenzi wa shirika la Wote Sawa Angela Bemedikto alisema kuwa, jukwaa la Asasi za Mwanza ni jukwaa huru hivyo lina wajibu wa kukutana na kujadili changamoto za kisekta.

Kabla ya mkutano kamati ya maandalizi ya Jukwaa la Asasi za Kiraia Mkoa wa Mwanza ilikuwa na mkutano na waandishi wa habari, ambapo walieleza mchango wa Asasi za Kiraia kwenye Maendeleo ya Taifa.

Pia walisema Jukwaa hilo lipo tayari kufanya kazi na Serikali ya Mkoa wa Mwanza kwenye kuchakata maendeleo ya kimkoa.

Asasi za Mkoa wa Mwanza zimeishukuru Foundation for Civil Society kwa ufadhili wa mkutano huo.

Edwin Soko
Mwanza

DC Misungwi kuratibu zoezi la kufufua kiwanda cha Pamba Manawa

Naibu Waziri wa Kilimo, Husseis Bashe (wa pili kulia) akiwa pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya Misungwi mkoani Mwanza, Juma Sweda (kulia) kukagua sehemu ya mitambo ya kiwanda cha kuchakata pamba Manawa kilichopo Kata ya Misasi wilayani Misungwi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Septemba 27, 2019 Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alitembelea kiwanda hiki 
 Mwonekano wa baadhi ya mitambo katika kiwanda cha kuchakata pamba Manawa kilichopo wilayani Misungwi ambacho tangu mwaka 2014 kilisitisha shughuli zake.
Tazama BMG Online TV hapa chini

MKUU WA WILAYA ATANGAZA VITA DHIDI YA MAFATAKI


MKUU wa Wilaya ya Magu, Phellimon  Sengati ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo kuwakamata na kuwashughulikia watu wote wanaoendelea kufanya vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto ili kusaidia kukomesha vitendo hivyo.

Amesema vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo vinapaswa kuchukua hatua stahiki kwa wale wote wanaofanya vitendo hivyo, kwa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani bila kumuonea mtu yeyote.
Kauli hiyo ameitoa juzi wakati wa uzinduzi wa mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na watoto katika wilaya ya Magu iliyofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba Magu mjini.

 Bernadina Kahabuka ni Kaimu Afisa Elimu Sekondari wilayani Magu Jeh takwimu za mimba tangu 2016 hadi 2019 HALI INATISHA ........

Nao baadhi ya wanafunzi wasichana changamoto gani wanazopitia kwenye mapito yao ya kuisaka elimu. ......... 

JOSEPH PASTOR NI MMOJA WA DEREVA WA BODABODA YEYE HAKUMUMUNYA MANENO ZAID YA KUFUNGUKA AKIKIRI KWAMBA BAADHI YAO WAMEKUWA CHANZO.....

 Waimbaji wa kwaya ya AICT Magu wakiwasilisha ujumbe kupitia nyimbo zao.
Safu ya mbele ya ma-sololist wa kwaya ya AICT Magu ambao wametunga wimbo maalum kuiasa jamii kusimamia haki sawa.