Asasi za kiraia zaidi ya 80 za Mkoa wa Mwanza zimekutana leo hii kujadili fursa na changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
Lengo kuu la kukutana kwa Asasi hizi ilikuwa ni kukutana kwa pamoja na kujadili baadhi ya masuala muhimu ya kisekta yanayohitaji mjadala mpana ili kuboresha ushirikiano miongoni mwa asasi za kiraia za Mkoa wa Mwanza.
Akifungua mkutano huo wa jukwaa la asisi za Mkoa wa Mwanza, Dr Philmon Sengati alisema kuwa, tamaduni za asasi za kiraia kukutana na kujadili mambo ya kisekta ni jambo jema sana kwani linaleta afya njema ndani ya sekta.
Naye Mwezeshaji Bwana Israel Ilunde alisema kuwa, lengo la kuwa na jukwaa na Kimkoa ni kupaza sauti kwa pamoja na kujua namna ya kusonga mbele licha ya kukabiliana na vikwazo vya kiutendaji.
Naye Mkurugenzi wa shirika la Wote Sawa Angela Bemedikto alisema kuwa, jukwaa la Asasi za Mwanza ni jukwaa huru hivyo lina wajibu wa kukutana na kujadili changamoto za kisekta.
Kabla ya mkutano kamati ya maandalizi ya Jukwaa la Asasi za Kiraia Mkoa wa Mwanza ilikuwa na mkutano na waandishi wa habari, ambapo walieleza mchango wa Asasi za Kiraia kwenye Maendeleo ya Taifa.
Pia walisema Jukwaa hilo lipo tayari kufanya kazi na Serikali ya Mkoa wa Mwanza kwenye kuchakata maendeleo ya kimkoa.
Asasi za Mkoa wa Mwanza zimeishukuru Foundation for Civil Society kwa ufadhili wa mkutano huo.
Edwin Soko
Mwanza
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.