ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 9, 2022

WAZIRI GWAJIMA AZINDUA KITUO CHA WATOTO SOKO LA MIRONGO MWANZA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima Mapema ya leo Februari 09, 2022 akikata utepe kama ishira ya kuzindua Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto Mirongo kilichopo katika soko la wajasiriamali Mirongo jijini Mwanza.
Ujenzi wa Kituo hicho umeenda sambamba na uboreshaji wa miundombinu ya Soko la Mirongo ambayo ni pamoja na vyoo, mitaro na paa katika eneo la kuuzia bidhaa na hivyo kuondoa adha kwa wajasiriamali katika soko hilo la mbogamboga na matunda ambalo asilimia kubwa wauzaji ni wanawake.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima (wa kwanza kushoto) akiwasaidia watoto kuburudika na mchezo wa bembea. 
Kusanyiko la uzinduzi.
Baadhi ya wafanyabishara wadogowadogo wa soko la Mirongo wakimsikiliza Waziri Gwajima.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama Wamachinga wa mirongo jijini Mwanza.
Hii ni Wizara ya kuwabadilisha fikra za jamii.
Maboresho hayo yaliyofanywa na shirika la kutetea haki za wanawake na watoto KIVULINI kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo I4IF, UKAid, IrishAid pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yamegharimu kiasi cha shilingi Milioni 88.

Miundombinu bora katika soko la Mirongo itasaidia wajasiriamali kufanya biashara zao katika mazingira salama na kukuza biashara zao huku Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto kikisaidia kuimarisha usalama wa watoto pindi wazazi wao wanapokuwa kwenye biashara huku pia akina mama wanaonyonyesha wakiwa na eneo maalum la kunyonyeshea.