ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 28, 2015

ILIVYOKUWA PARTY BIRTHDAY YA MTANGAZAJI WA METRO FM MWANZA

Ze ugali wa kidhungu....
February 26 Miaka kadhaa iliyopita Mtoto George Binagi-GB Pazzo alizaliwa. Karibu uweze kutazama picha za BIRTH DAY PARTY yake iliyofanyika juzi Lake Hotel Jijini Mwanza kwa mwaka huu 2015. 

"Zaidi ya yote nawashukuru sana Wazazi wangu The late Mzee Daniel Marwa Binagi pamoja na my dear Mama Leah Daniel Binagi kwa malezi yenu bora." Alisema GB

"Ndugu zangu leo naadhimisha miaka kadhaa ya Kuzaliwa. Hakika nimekuwa mpya siku ya leo huku nikiwa ndani ya Kristo. Ninaloweza kusema ni kwamba ya kale yote yamepita. Mabaya tusameheane na mazuri tuyaendeleze...Maneno yangu zaidi nimeyatoa katika kitabu cha 2 Wakorintho 5:17 naombeni mkayasome nanyi. Mungu awabariki na Karibuni sana".
Baba Jutibeibi alisimamia vyema shughuli kama mc.
Alphonce Tonny Kapela hapa alikuwa akimwaga nasaha zake kama meneja wa Metro Fm kwa mtotomzaliwa George Binagi ambaye wanafanya kazi naye kituo kimoja.
Kata keki tule
Kata keki tuleeeee
Kata keki tule woteEEEEeee
Kata keki tuleeeeee.....
To Tommy.
To Juliet.
To Sefroza.
To Loyce na wakati huo huo mamamarazi (kulia)  wakiwa bize kuchukuwa matukio...
To Okeleky.
To Mariam Juma.
To my dada ake Binagi
To Mahmood.
To sister Doric.
Wawoooo na mapozi hata wakati wa kula....
To Kipara aka CHADEMA naye alifurahia utamu wake.
G. Sengo toka 88.1 Clouds Fm Mwanza akilishwa keki na GB
Kutoka kushoto ni Oxs Okeleky ambaye ni Producer @Jembe Fm na Sound Engeneer wa JJ Band akifuatiwa na Sefroza Joseph na Alphonce Tonny Kapela wote kutoka Metro Fm Mwanza.

NAMNA YANGA ILIVYOING'OA BDF XI MICHUANO YA SHIRIKISHO

bdf
Na. Richard Bakana, Dar es salaam

Wawakirishi wa Tanzania bara katika michuano ya Kombe la Shirikishi barani Afrika, Dar es salaam Young Africans  wamefanikiwa kusonga mbele licha ya kuambulia kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa wenyeji wao BDF XI ya Botswana.
Dakika ya 3 Mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngassa anakosa bao la wazi baada ya kubaki nna kipa lakini anapiga mpira ambao unatoka nje licha yakuwa Kipa na mabeki wa BDF XI kuwa chini.
Dakika ya 13 Simon Msuva anapiga kona lakini inakuwa haina matunda
BDF XI wanapata kupiga shuti kali ambalo linatoka nje na kuwa halina madhara kwa Yanga ikiwa ni dakika ya 14,
Dan Mrwanda anapata nafasi ambapo anapiga shuti kali ambalo linakuwa halina faida kwa Yanga kwani linatoka juu ikiwa ni dakika ya 15.
Simon Msuva anafanyiwa madhambi baada ya kuganyagwa mguuni na Mchezaji wa BDF XI kunako dakika ya 21, Muamuzi wa mchezo huo akaamua kutoa adhabu ya kadi Nyekundu kwa Mbotswana huyo.
Dakika ya 26 BDF wanapata faulo ya kwanza nje kidogo ya 18 ya Yanga ambapo inapigwa lakini inakuwa haina macho baada ya mabeki wa Yanga kuwa makini na kuondoa hatari hiyo.
Dan Mrwanda anapewa kadi ya Njano baada ya kumfanyia madhambi mchezaji wa BDF XI
Ngassa anaifungia Yanga bao la kichwa kufatia Simon Msuva ku chonga krosi ambayo inawabaatiza mabeki wa BDF na kumkuta Ngassa ambaye anapiga kichwa cha kuogelea.
Dakika ya 38 Kipa wa Yanga Aly Mustafa anagumbana na dhahama baada ya kuganyagwa mguuni na mshambuliaji wa BDF XI aliporudishiwa mpira ndio akagongana na mshambuliaji huyo katika mguu wa kulia.
Simon Msuva kwa mara nyingine anamimina kroi safi kutoka winga ya kulia ambayo inamkuta moja kwa moja kipa wa BDF XI ambaye anaidaka na kusaidia timu yake isizidi kuzama.
Dakika ya 45+2 kipindi cha kwanza Amis Tambwe anakosa bao baada ya kupiga kichwa ambapo mpira unagonga mwamba wa juu na kutoka baada ya Dan Mrwanda kuchonga krosi akitokea winga ya kushoto.
Hadi Mwamuzi wa mchezo huo kutoka Afrika KUsini anapuliza kipenga kuashiria kipindi cha kwanza kimemalizika Yanga walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0 kutoka kwa Ngassa.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa timu zote zikisaka mabao ndipo wenyeji hao BDF wakafanikiwa kusawazisha na kufanya kuwa 1-1.
Dakika ya 72 Dan Mranda anapewa kadi nyekundu kufatia kupewa kadi ya pili ya njano baada ya kumfanyia madhambi mchezaji wa BDF XI.
Dakika ya 75 BDF wanakosa bao baada ya gonga gonga lakini zinaishia kwa Aly Mustafa baada ya kudaka mpira wa kichwa cha mshambuliaji wa BDF XI.
Oscar Jushua anapewa kadi ya njano katika dakika ya 83 baada ya kuchelewesha muda kwa kuchelewa kurusha.
BDF XI wanapata bao la pili kupitia kwa Madziba katika dakika ya 85 Baada ya mchezaji huyo kupiga kichwa ambacho kinagonga mwamba na kurudi ndani na kumkuta tena naambapo anaupiga kwa mguu na kutumbukia kimiani.
Hadi mwamuzi wa mtanange huo anamaliza mchezo Yanga walikuwa nyuma kwa bao 2-1 lakini wanakuwa wamevuka katika hatua hiyo kwa jumla ya goli 3-2.

MSHITUKO: KAPTENI JOHN KOMBA AFARIKI DUNIA

Mara zote aliimba kwa hisia.... enzi za uhai wake Kapteni John Komba.

Habari zilizotufikia muda mchache uliopita, zinasema kuwa aliyekuwa Mkurugenzi wa TOT na Mbunge wa Mbinga Magharibi (CCM) Kapteni John Komba amefariki dunia katika Hospitali ya TMJ.

Hivi sasa juhudi zinafanyika kuhamisha mwili wa marehemu kutoka TMJ kwenda Hospitali ya Lugalo.

Aidha imeelezwa kuwa KOmba amefariki baada ya kufikishwa Hospitalini hapo akisumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari ambapo ilikuwa imepanda hadi kufikia 30 majuzi na kufanikiwa kupunguza hadi kufikia 9 jana.


Pia ikumbukwe kuwa marehemu Komba ameacha kazi kubwa aliyokuwa tayari ameianza ya kutunga na kurekodi nyimbo za kampeni akishirikiana na baadhi ya wanamuziki wake wa zamani kama Thabiti Abdul, Jerry Juma na wengineo.

Taarifa zaidi tutazidi kupashana kupitia hapa GSENGO blog.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

WANAFUNZI ZAIDI YA 450 WILAYA YA KIBAHA KWA SASA WANASOMA CHINI YA MITI KUFUATIA MADARASA KUBOMOKA

Na Victor Masangu, Pwani
 
WANAFUNZI wa shule ya msingi ya mailimoja iliyopo Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani kwa sasa baadhi yao wamelazimika kusomea chini ya miti kutokana na madarasa ambayo walikuwa wanayatumia kuezuliwa mabati na kubomoko kutoka na mvua na upepo mkali uliotokea hivi karibuni.
 
 Hali hiyo imebainika baada ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini  Silvester Koka alipofanya ziara maalumu ya kwenda kuitembelea shule ili na kujionea uharibifu mkubwa  wa madarasa ambao umejitokeza.
 
Akizungumza kuhusiana na maafa waliyoyapata Mkuu msaidizi wa Shule hiyo Theresia Mtoni amesema kwamba kwa sasa wapo katika wakati mgumu kutokana na madarasa 11 kuharika hivyo kuwalazimu wanafunzi zaidi ya 450 kusomea chini ya miti hali ambayo ni hatari kwa usalama wao kwani mazingira wanayosomea  sio rafiki.
 
Mkuu huyo aliongeza kuwa wameamua kutokana na hali hiyo wanafunzi wanasoma kwa zamu ambapo baadhi yao wakiwa wanasoma madarasani wengine wanakuwa wanasomea nje chini ya miti.
 
“Kwa kweli ndugu mwandishi nadhani wewe mwenyewe umeweza kushuudia hali yenyewe ilivyo tupo katika wakati mgumu sana, kwani vyumba vya madarasa vimeharibika sana nah ii kutokana na upepo mkali uliokuja hivyo kuharibu miundombinu ya madarasa kwa ali halisi ndio hiyo,” alisema Mkuu huyo.
 
Aidha Mwalimu huyo alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvester Koka  kwa kuweza kuonyesha ushirikiana  wake wa dhati na kuwasaidia msaada wa mabai 50 pamoja na mifuko ya simenti.
 
Kwa upande wao wanafunzi wanaosoma katika  shule hiyo iliyokumbwa na maafa hayo akiwemo  Diana Mbowe, pamoja na Upendo Chilale walisema kwamba kitendo hicho cha kusomea chini ya miti kinawapa shida kubwa sana kwani hawawezi kusoma kwa uhuru kama ilivyokuwa hapo awali.
 
Walisema kuwa mbali na kuwepo kwa changamoto hiyo ya kuharibika kwa madarasa pia wanakabiliwa na changamoto nyingine ya kutokuwa na matundu ya vyoo vya kutosha ukilinganisha na idadi ya wanafuzni waliopo na kwamba vilivyopo vipo  katika hali ambayo sio nzuri kwani miundombinu yake ni mibovu.
 
Naye Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvester Koka ambaye alikwenda kutembelea shule hiyo na kuchangia msaada wa mifuko 50 ya simenti pamoja na mabati 50,alisema kwamba atahakikisha kwamba anafanya jitihada za hali na mali ili kuweza kuhakikisha wanafunzi hao wanarejea madarasani na kuendelea na masomo kama kawaida.
 
Pia Mbunge huyo aliwaomba wazazi kuwa mstari wa mbele katika kuchangia kitu chochote ili kuweza kukarabati miundombinu hiyo ya madarasa lengo ikiwa ni kuunga juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu katika halmashauri ya mji wa Kibaha na wanafunzi waweze kusoma katika mazingira mazuri.   
 
SHULE ya msingi ya maili moja Wilayani Kibaha ambayo ina wanafunzi  963 kwa sasa inakabiliwa na ubovu mkubwa wa majengo yake ambayo miundombinu yake imeharikika kutokana na upepo ulioambatana na mvua hali ambayo imesababisha wanafunzi kusoma wakiwa chini ya miti.

WAFANYAKAZI AIRTEL WACHANGIA KUBORESHA MAZINGIRA YA SHULE YA MSINGI USHINDI

Wafanyakazi wa Airtel Tanzania, Kitengo cha Biashara za Mashirika, wakishiriki kupaka rangi darasa la Chekechea linalokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam. 
Wafanyakazi wa Airtel Tanzania, Kitengo cha Biashara za Mashirika, wakishiriki kupaka rangi darasa la Chekechea linalokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam. 
Wafanyakazi wa Airtel Tanzania, Kitengo cha Biashara za Mashirika, wakigawa zawadi kwa watoto wa chekechea baada ya kushiriki kupaka rangi darasa la Chekechea linalokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Airtel Tanzania, Kitengo cha Biashara za Mashirika, wakiupamba ukuta kwa viganya vya mikono vilivyopakwa rangi nyekundu wakati waliposhiriki kupaka rangi darasa la Chekechea linalokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam. 

Wafanyakazi wa Airtel wachangia kuboresha mazingara ya shule ya msingi Ushindi
KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa “AirtelTunakujali” wakishirikiana na wafanyakazi wa kitengo cha Airtel Biashara za Mashirika wameendeleza dhamira ya kusaidia jamii kwa kukarabati darasa la chekechea katika shule ya msingi Ushindi iliyopo jijini Dar Es Salaam.

 Airtel imeendelea kushirikiana na wafanya kazi wake kutoa mchango kwa jamii kwa kuhakikisha shule zinakuwa na miundombinu na mazingira bora ya kujifunza hali itakayochochea wanafunzi kupenda shule.

 Uchakavu wa miundombinu ya shule hasa za msingi nchini ikiwemo vyumba vya madarasa ni moja ya chanzo kikuu kinachodhoofisha mahudhurio ya wanafunzi na hivyo kusababisha matokeo yasiyoridhisha.

 Mwishoni mwa wiki wafanyakazi wa kitengo hicho walishiriki ukarabati wa darasa hilo la chekechea katika shule ya msingi Ushindi lenye kuhitaji marekebisho makubwa ambayo yanatazamiwa kuongeza hamasa ya watoto kuhudhuria shuleni.

 Akizungumza katika tukio hilo mwalimu Mkuu wa Shule ya hiyo Bw Iddi Kaminja alisema, "tumekuwa na changamoto kubwa mahudhurio kutokana na wanafunzi kutokufurahia kuja shuleni na hii inasababishwa na shule kuwa na miundombinu chakavu isiyowapa ari ya kusoma."

 "Tangu mpango huu wa ukarabati ulipotangazwa wanafunzi wamekuwa na shauku kubwa ya kutaka zoezi hili liweze kuisha na kuanza kutumia darasa hili. Hali hii limekuwa faraja kwetu hivyo ni wazi kwamba itatusaidia kuongeza kiwango cha mahudhurio shuleni na hatimaye kuongeza kiwango cha elimu hapa shuleni."

Aliongeza Mwalimu Kaminja Aidha Mwalimu Kaminja ametumia fursa hiyo kuwapongeza wafanayakazi wa Airtel kwa moyo wao wa kujitolea kwa hali na mali kuinua kiwango cha elimu ya awali na kutoa rai kwa makampuni mengine kuona umuhimu wa kuborosha madarasa ya shule za awali na msingi kwani njia mojawapo ya kuinua kiwango cha elimu hapa nchini ni kuwapa watoto wetu mazingira mazuri na yenye usalama wawapo hapo shuleni.

 Nae meneja wa Airtel wa huduma kwa jamii Hawa Bayumi alisema,"madarasa mazuri ni muhimu kwa usalama wa wanafunzi lakini pia huleta hamasa ya mahudhurio hivyo ni lazima wazazi wawe tayari kusaidia hatua za haraka kufanyia matengenezo ya mara kwa mara ili kuepusha hatari na gharama kubwa ya fedha. Kwa njia hiyo madarasa haya yatadumu."

 "Leo tumeshiriki zoezi hili katika shule ya msingi ya Ushindi lakini kazi hii imekuwa ikifanyika sehemu mbali mbali nchini kupitia mradi wa “Airtel Tunakujali” ambao unawawezesha wafanyakazi wa Airtel nchi nzima kushiriki katika shughuli za kijamii hususan zinazoinua sekta ya elimu

Tunajisikia furaha kuwekeza katika jamii kwa kiwango ambacho kinaleta tofauti kubwa. Siku zote tumelenga kufikisha huduma bora na za gharama nafuu kwa watanzania huku tukitambua na kupambana na changamoto mbalimbali za jamii inayotuzunguka Leo nanyi mnashuhudia utofauti wetu na makampuni mengine, Airtel sio tu inaongoza katika mtandao ulio bora hapa nchini bali pia namna tunavyojali wanaotuzunguka" aliongeza Bayumi.

RC PWANI AWACHARUKIA MA DC AWATAKA KUIMARISHA ULINZI KWA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo.
VICTOR MASANGU, PWANI 

MKUU  wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo amewaagiza wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanalivalia njuga suala la mauaji ya kikatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi “Albino’ kwa kuimarisha ulinzi na usalama usiku na mchana kwa lengo la kuweza kuwabaini wale wote  wanahusika  na matukio hayo.

Agizo hilo la Injinia ndikilo amelitoa kwa masikitiko makubwa wakati wa sherehe za kuwakaribisha wakuu wa wilaya wapya walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni pamoja na kuwakabidhi vitendea kazi kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu katika Wilaya zao.
Ndikilo amesema kwamba kwa sasa wimbi la mauaji ya kikatili dhidi ya albino yanazdi kushika kasi katika maeneo mbali mbali ya nchi,pamoja na uvamizi wa vituo vya polisi hivyo kunahitajika nguvu ya ziada katika kuimarsiha ulinzi na usalama ili kuweza kuwepo kwa hali ya amani na utulivu.
 BOFYA PLAY MSIKILIZE RC NDIKILO.

Aidha Ndikilo katika hatua nyingine amewataka wakuu hao wa wilaya kwa kushirikina na viongozi wengine kujipanga kikamilifu katika kulitafutua ufumbuzi suala la migogoro ya ardhi katika Mkoa wa Pwani kwan limeonekana kuwa ni changamoto kubwa ambayo inasababisha hali ya vurugu kwa wananchi wenyewe hususa wakulima na wafugaji.
MSIKILIZE NDIKILO.

Kwa upande wake Mkuu mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga alikuwa na haya ya kusema kuhusina na maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa pamoja na mikakati yake katika kupambana na changamoto hizo.
MSIKILIZE MKUU WA WILAYA YA BAGAMOYO.

WAKUU wa Wilaya ambao wamebadilishwa kutoka maeneo mengine na kupelekwa katika Mkoa wa Pani ni pamoja na pamoja na Subira Mgalu ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Majid Mwanga Bagamoyo,Abdlah Kiato Wilaya ya Mkuranga pamoja na Dr Nassor Amid Wilaya ya Mafia.

WANANCHI WA MKOA WA NJOMBE NI MFANO WA KUIGWA KATIKA ZOEZI LA BVR

Kazi ya kuandikisha wananchi katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kupitia mfumo wa Biometrick Voters Registration (BVR), ambao huhusisha uchukuaji wa alama za vidole na picha, jana iliingia siku ya tatu, huku baadhi yao wakipongeza utendaji wake.
Kwa mujibu wa ripoti iliyokusanywa na mwandishi wetu inasema kuwa tokea siku ya kwanza lilipoanza zoezi hilo lilionyesha matumaini maana wananchi wetu walijitokeza kwa wingi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi katika vituo vya uandikishaji, wananchi hao walisema kuna mabadiliko ukilinganisha na siku zilizopita, hivi sasa kazi zinafanywa haraka.
“Watu wanaokwenda kwenye vituo kujiandikisha idadi yao ni kubwa kuliko hata makadirio ya tume, kama hawataongeza muda au vifaa, siku saba walizopanga, hazitatosha na wengi wataachwa bila ya kujiandikisha,” alisema.

Baadhi ya waandikishaji na wasimamizi wa mashine wameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kuongeza muda ili kazi hiyo ifanyike kwa ufanisi zaidi.
66
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua  Uborereshaji wa Daftari kla Kudumu la Wapigakura  katika mji mdogo wa Makambako Februari 24, 2015. Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva na Katikati ni Katibu wa Tume hiyo, Ndugu Malaba.
02
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mwenyekititi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva (kushpoto) , Naibu Katibu Mkuu  na Katibu Mwenezi wa CHADEMA, John Mnyika (kulia), Yusufu Mbungiro ambaye ni Afisa Uchaguzi na Mafunzo taifa wa Chama cha CUF (wapili kushoto) na Allan Bujo ambaye ni Mkuu wa Ulinzi wa CHADEMA baada ya kuzinua Uborereshaji wa Daftarila Kudumu la Wapigakura  katika mji mdogo wa Makambako.
03
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama kazi ya uandiskishaji wapiga kura baada ya ya kuzinua Uborereshaji wa Daftari kla Kudumu la Wapigakura  katika mji mdogo wa Makambako.
 .06
Baadhi ya watalaamu wa kuandikisha wapiga  wakiwa na zana  za kazi kabla ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ya kuzindua Uborereshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura  katika mji mdogo wa Makambako.

JAHAZI MODERN TAARAB NA MASHAUZI CLASSIC JUKWAA MOJA MACHI 22


JAHAZI MODERN TAARAB NA MASHAUZI CLASSIC JUKWAA MOJA MACHI 22 …
Usiku wa Baba naMwana Hatimaye makundi mawili yanayoaminika kuwa na mashabiki wengi zaidi katika taarab, Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic yatafanya onyesho la pamoja mwezi ujao.

Onyesho hilo litafanyika Travertine Hotel Magomeni jijini Dar es Salaam, Jumapili ya tarehe 22 mwezi Machi.

Hii inakuwa ni mara ya pili kwa makundi hayo mawili kufanya onyesho la pamoja (bila kushirikishwa makundi mengine).

Onyesho la kwanza lililopewa jina la Usiku wa Baba na Mwana lilifanyika miaka minne iliyopita ndani ya ukumbi huo huo na inaaminika kuwa hadi leo bado rekodi yake ya mahudhurio pale Travertine haijavunjwa.

Mzee Yussuf na Isha Mashauzi ambao ni wamiliki wa makundi hayo, wameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo ni “Usiku wa Baba naMwana …Season 2”.

Viongozi hao wamesema onyesho hilo ni la kukuza udugu pamoja na kuwakutanisha pamoja mashabiki wao na kamwe halina hata chembe ya wala mpambano.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI KUAGA MWILI WA MAMA MZAZI WA DKT. EDWARD HOSEA, JIJINI DAR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kwenye Kitabu cha maombolezo ya marehemu Esther Gigwa, Mama mzazi wa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea, wakati alipofika kushiriki kuaga mwili huo nyumbani kwa mkurugenzi huyo, Masaki jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu mama mzazi wa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Ewdard Hose, Mama Esther Gigwa, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika nyumbani kwa Mkurugenzi huyo, Masaki jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea, wakati alipofika kushiriki kuaga mwili wa marehemu mama mzazi wa Mkuruenzi huyo nyumbani kwake, Masaki jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiifariji, Familia ya wafiwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea na nduguze, waliofiwa na mama yao mzazi wakati Makamu alipofika kushiriki katika shughuli ya kuaga, Masaki jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015. Picha na OMR
Wanafamilia wafiwa wakiwa katika shughuli hiyo ya maziko.

BLOGGERS KUKUTANA LEO KATIKA HOTELI YA SERENA JIJINI DAR ES SALAAM KATIKA PATI YA KIHISTORIA


Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network  (TBN) na mmiliki wa Blog ya The Habari.com Joachim Mushi (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi. Kutoka kushoto ni  mjumbe wa TBN Mkala Fundikira,  Afisa wa kampuni ya mawasiliano na matangazo ya AIMS, Shafiq Mpanja wa AIM, Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale na mjumbe wa TBN Khadija Kalili.
Katika mkutano huo TBN imesema kesho Jumamosi jioni Bloggers takriban 100 kutoka sehemu mbalimbali nchini watakutanika katika ukumbi wa hoteli ya Serena jijini Dar es salam kwa ajili ya hafla ya mwaka mpya itayohudhuriwa pia na wadhamini na marafiki wa Bloggers.
 Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale akifafanua jambo wakati wa mkutano.
Mmiliki wa Blog ya Bongoweekeend Khadija Kalili akizungumza wakati wa mkutano.
Father Kidevu (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano.
Baadhi ya Bloggers na waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari wakifuatilia jambo wakati wa mkutano uliofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari Maelezo Dar es Salaam.

Thursday, February 26, 2015

WACHIMBAJI WATAKIWA KUPEWA UTARATIBU WA MAOMBI YA LESENI NA MIKOPO FEDHA OFISI ZA KANDA ZA MADINI


NA PETER FABIAN, MWANZA.

WACHIMBAJI wadogo wa Madini waliojiunga katika vikundi na kupata leseni za uchimbaji madini wametakiwa kufika katika Ofisi za Kanda ili kupewa taratibu wa kuomba mikopo ya fedha za ruzuku zilizotolewa na serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini.

Kauli hiyo imetolewa na Kamishina Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa, David Mlabwa jana Ofisini kwake jijini Mwanza, alisema kuwa serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini tayari imetenga kiasi cha Sh bilioni tisa ikiwa ni ruzuku kwa ajili ya kuwakopesha wachimbaji wadogo wa madini nchini.

“Wachimbaji waliojiunga katika vikundi na kupewa leseni za uchimbaji wafike katika ofisi zetu za Kanda jijini Mwanza, Geita na Kagera ili kupewa utaratibu utakaowawezesha kujaza fomu maalumu za mkopo kabla ya kupewa mikopo kutafanyika mchujo kuona vikundi vilivyokidhi sifa za uombaji kulingana na taratibu zilizopo,”alisema.

Mlabwa alisema kuwa hivi karibuni na Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na madini anayeshughulikia Madini, Charles Kitwanga “Mawe matatu” wakati akiwa katika ziara ya kutembelea jimboni kwake na kuzungumza na wananchi na wachimbaji katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mwagimagi na Mwamala Kata ya Ilujamate wilayani Misungwi aliagiza tuwape utaratibu wa kuomba leseni na walio na vikundi tayari waombe mikopo ya fedha.
“Naibu Waziri Kitwanga alisema wachimbaji wadogo walio kwenye vikundi na tayari wamepewa leseni za uchimbaji mdogo wa madini tuwapatie utaratibu wa kuomba mikopo ili kuwasaidia kupata mitaji ya kununua vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuchimba kwa vyenzo za Teknolojia kwenye maeneo,”alisema.

Aidha aliongeza kuwa Naibu Waziri, Kitwanga aliagiza kuwa katika maeneo ya uchimbaji ya kijiji cha Ishokelahela Kata ya Ilujamate wilayani Misungwi kuna tatizo linalolalamikiwa na wachimbaji wagodo kukosa maeneo ya uchimbaji na ameelekeza kukaa nao kuona jinsi ya kuwagawia maeneo ili kuwawezesha kuchimba kwa utaratibu wa kufuata sheria ya madini ya mwaka 2010 .

Kamishina Msaidizi Mlabwa alisema kuwa Wizara ya Nishati na Madini imeisha towa maelekezo juu ya wachimbaji wadogo katika maeneo yenye migogoro ili Ofsini za Kanda kukaa na wachimbaji wadogo kuwashirikisha kupitia viongozi wa serikali za vijiji, Kata na Wilaya ili kuwapatia maeneo ya uchimbaji kwa taratibu na sheria.

Wito wangu kwa wachimbaji wadogo katika maeneo waliyopewa kuchimba ni kufuata taratibu na sheria za uchimbaji kwa kuzingatia utunzaji wa mazingira na kushirikiana kwa kuanzisha, kujiunga katika vikundi vya uchimbaji ili kuomba leseni na kupewa mikopo itakayowezesha kuwa wachimbaji wanaochimba kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

WASHINDI WA PROMOSHENI YA AIRTEL YATOSHA ZAIDI WAKABIDHIWA MAGARI YAO.

Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange (kulia), akikabidhi funguo za gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 782 DCZ, kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Donald Fred Baruti katika hafla iliyofanyika nyumbani kwa mshindi huyo, Mtaa wa Ngala, eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (katikati) ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando.
Mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Donald Fred Baruti akilijaribu gari lake jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 782 DCZ, baada ya kukabidhiwa na Airtel, katika hafla iliyofanyika nyumbani kwake, Mtaa wa Ngala, eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (kushoto), akikabidhi kadi ya umiliki wa gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 782 DCZ, kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Donald Fred Baruti katika hafla iliyofanyika, Mtaa wa Ngala, eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (wa pili kushoto) ni Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange.
Mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Donald Fred Baruti akiteremka kutoka kwenye gari lake jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 782 DCZ, baada ya kukabidhiwa na Airtel, katika hafla iliyofanyika nyumbani kwake, Mtaa wa Ngala, eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange (kushoto), akikabidhi funguo za gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 464 DDD, kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, ambaye ni Wakala wa Mtandao huo, John Fred Kiwale katika hafla iliyofanyika, Mtaa wa Togo, eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam jana. Wa (pili kushoto) ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando na (kulia) ni Mke wa mshindi huyo, Anna Kiwale na motto wake, Sylvia John.
Meneja Masoko wa Airtel, Upendo Nkini (katikati) akikabidhi funguo za gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 465 DDD, kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, ambaye ni Kondakta wa Malori, Jastini William Dodoo katika hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde.
Mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Jastini William Dodoo akiwa mwenye furaha ndani ya gari lake jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 465 DDD, baada ya kukabidhiwa na Meneja Masoko wa Airtel, Upendo Nkini (kushoto), katika hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana
Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde (katikati), akifafanua jambo kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Jastini William Dodoo (kulia), baada ya kumkabidhi gari lake jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 465 DDD, katika hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana.