ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 23, 2024

BILIONI 161.4 ZA RAIS DKT SAMIA ZAIWEZESHA TANGA UWASA KUTEKELEZA MIRADI 20 YA KIMKAKATI

 

MKUU wa wilaya ya Muheza Zainabu Abdallah wa kwanza kushoto akikapata utepe kuashiria makabidhiano ya mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Maji Taka wilayani Muheza pamoja na kukabidhi Vyoo vilivyojengwa ikiwa ni sehemu ya Ujenzi wa Mradi huo kwa shule ya Sekondari Bonde,Shule ya Msingi Mdote na Soko la Majengo wilayani Muheza uliotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) Kulia Diwani wa Kata na anayefuatia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani

MKUU wa wilaya ya Muheza Zainabu Abdallah akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo
Kaimu Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shaban akizungumza kuhusu mradi huo

Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Bonde akieleza taarifa yake wakati wa makabidhiano hayo
Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Bonde wakiwa kwenye halfa hiyo ya makabidhiano


Na Oscar Assenga, MUHEZA

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa ) wamesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt Samia Suluhu Serikali imewawezesha ujenzi wa miradi ya kimkakati 20 ya maji safi yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 161 ambayo imekuwa chachu kubwa kuwezesha wananchi kupata huduma ya maji safi na hivyo kuondokana na changamoto walizokuwa nazo awali.

Hayo yalisemwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) Mhandisi Rashid Shaban wakati wamekabidhi mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Maji Taka wilayani Muheza pamoja na kukabidhi Vyoo vilivyojengwa ikiwa ni sehemu ya Ujenzi wa Mradi huo kwa shule ya Sekondari Bonde,Shule ya Msingi Mdote na Soko la Majengo wilayani Muheza.

Mhandidi Shaban alisema pamoja na hilo pia ipo miradi 6 ya maji taka yenye thamani ya Bilioni 4.2 ukiwemo wa ujenzi wa miundombinu ya kupokea na kuchakata majitaka wenye thamani ya Bilioni 1 ambao umetekelezwa na hivyo kusaidia kuondosha kero ambayo ilikuwa ikiwkumba wananchi.

Alisema kutokana na uwezeshwaji huo kwa sasa mamlaka hiyo inatoa huduma ya maji safi na salama kwa wastani wa asilimia 92.5 ya wakazi wa Jiji la Tang (96.1%), Pangani (70%) na Muheza (71%) ambapo miaka mitatu iliyopita kabla ya utawala wa Serikali ya awamu ya sita huduma ya maji ilikuwa inapatikana kwa wastani wa asilimia 83.2 ya wakazi hao (Tanga 89%, Muheza 33% na Pangani 60%).

Aidha alisema hivi sasa maji safi yanapatikana kwa wastani wa saa 15 kwa siku katika miji ya Muheza ambapo miaka mitatu iliyopita huduma ya maji ilikuwa inapatikana kwa wastani wa masaa matatu na wakati mwengine siku moja baada ya Juma Zima.

Akizungumzia huduma ya uondoshaji wa maji Taka, Kaimu Mkurugenzi huyo alisema huduma hiyo hufanywa kupitia mtandao wa mabomba unaowahudumia wakazi wapatao 20,615 sawa na asilimia 5.2 ya wakazi Tanga Mjini, Maeneo ya Muheza, Pangani na maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Tanga ambayo hufanywa kwa kutumia mifumo mingine ya uondoshaji majitaka ikiwemo vyoo vya shimo na vyoo vya kunyonywa na magari vikishajaa.

Hata hivyo akielezea ujenzi wa vyoo na ombi la kukabidhi kwa watumiaji ,Mhandisi Rashid alisema kwamba kwa kua mradi huo unahusiana na usafi wa mazingira,Tanga Uwasa iliona ijenge aina hiyo ya vyoo ili kuonesha mfano wa vyoo bora vinavyotakiwa kujengwa katika jamii ikiwemo faida ambazo zinapatikana kupitia mradi huo.

Alisema faida ni kuwaepusha uchafuzi wa maji ya ardhini, uwepo wa huduma karibu na wananchi kupitia gari la kunyonya majitaka toka na hivyo kuondoa changamoto ya utupaji mbali na wakati mwengine katika maeneo yasiyorasmi.

“Pia kupungumza changamoto ya ufinyu wa vyoo katika shule za Msingi Mdot,Shule ya Sekondari Bonde na Soko la Majengo ambapo gharamaa nafuu kwani kutumia eneo dogo la ardhi na hudumu muda mrefu pia upatikanaji wa mbolea inayoweza kutumika kwa kilimo lakini tunaishukuru Serikali kupitia Wizara ya Maji kwa kuwezesha ujenzi wa mradi huu”Alisema

“Sisi Tanga Uwasa tumeona ujenzi wa vyoo umekamilika na vipo tayari kutumika tunadhani hakuna haja ya kuendelea kusubiri hadi ujenzi wa miundombinu pale Kilapula ukamilike ikiwa wanafunzi na wananchi sokoni wanauhitaji mkubwa hivyo tunakuomba ukabidhi vyoo hivi kwa uongozi wa shule ya Sekondari Bonde, Shule ya Msingi Mdote na Soko la Majengo vianze kutumika na hivyo kusaidi kupunguza changamoto iliyopo ya uhitaji wa matundu ya vyoo”Alisema

Awali akizungumza mara baada ya kupokea mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Maji Taka wilayani Muheza pamoja na kukabidhi Vyoo vilivyojengwa ikiwa ni sehemu ya Ujenzi wa Mradi huo kwa shule ya Sekondari Bonde, Shule ya Msingi Mdote na Soko la Majengo wilayani Muheza, Mkuu wa wilaya ya Muheza ZainabuAbdallah alisema miaka mitatu ya nyuma hali ya upatikanaji wa maji ilikuwa ni asilimia 33 lakini miaka mitatu sasa hivi himefikia 71 hiyo ni kazi kubwa anayoifanya Rais Dkt Samia Suluhu.

Katika miaka mitatu ya Rais Dkt Samia wamefanikiwa kutekeleza miradi mikubwa ya kikamkati 20 yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 161.4 ya Maji Safi na Maji Taka miradi sita yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 4.2 ambapo hiyo ni kazi kubwa na nzuri inayofanya na Rais Samia.

Alisema wamefika katika hafla hiyo kuungana na Tanga Uwasa katika tukio hilo huku akimpongeza Waziri wa Maji Jumaa Aweso kutokana na kazi kubwa anayofanya kuhakikisha huduma ya maji kwenye mkoa wa Tanga inakuwa nzuri na Muheza wanatekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa miundombinu ya maji taka wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 1 ambapo kwenye mradi ho wamepata gari la maji taka, gari ya usimamizi wa mradi na wamepata matundu ya vyoo,shule ya sekondari na Msingi pamoja na Soko .

Friday, March 22, 2024

RUNGU LAJA WANAOTIRIRISHA MAJI TAKA ZIWA VICTORIA - TBL YATOA SOMO KWA WANANCHI UTUNZAJI MAZINGIRA.

 NA ALBERT G. SENGO

Kutunza mazingira ni wajibu wa kila mwananchi, jamii imehimizwa kuhakikisha inatimiza wajibu huo, kwa kutunza mazingira na kulinda vyanzo vya maji ikiwemo kupanda miti majumbani pamoja na kutunza mito na fukwe za Ziwa Victoria. Wito huo umetolewa leo ijumaa 17 Machi 2024 na KAIMU MKUU WA KIWANDA CHA TBL MWANZA BERNARD MUSA - wakati wa zoezi la kufanya usafi na utoaji wa elimu juu ya kutunza mazingira, uliowashirikisha pia wafanyakazi wa Kampuni hiyo katika eneo la mto Vuka, uliopo Furahisha, Kirumba jijini Mwanza unao kusanya maji kutoka viunga mbalimbali kuyatiririsha ziwa Victoria.

DKT. BITEKO AAGIZA WIZARA YA MAJI KUHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA MAJI SAFI NA SALAMA

📌 Asisitiza Wananchi kutoa maoni utunzaji wa mazingira katika Dira 2050 📌 Ataka Bodi za Mabonde ya Maji/NEMC kudhibiti uchafuzi wa mazingira 📌 Uvunaji wa Maji ya Mvua wasisitizwa ngazi ya Kaya, Taasisi hadi Taifa 📌 Amtaja Rais Dkt. Samia kinara wa kumtua Mama ndoo kichwani Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameitaka Wizara ya Maji kuhakikisha watanzania wanapata huduma ya maji safi na salama ili kuendana na thamani halisi ya miundombinu ya maji iliyojengwa na Serikali kwa gharama kubwa ili kuwapa huduma wananchi kwa ufanisi. Dkt. Biteko ametoa agizo hilo Jijini Dodoma tarehe 22 Machi, 2024 wakati akifunga Maadhimisho ya Wiki ya Maji Tanzania ambayo yameenda pamoja na Siku ya Maji Duniani. Ameagiza Wizara na Mamlaka za Maji zijielekeze kwenye ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo mabwawa ya kuvuna maji ya mvua katika maeneo yasiyo na vyanzo vya maji vya uhakika na kusisitiza kuwa suala hilo lisisubiri rasilimali fedha ya kutosha bali waanze kutekeleza na rasimali zitaendekea kuja wakati utekelezaji umeshaanza. Vilevile ametoa wito kwa mwananchi mmoja mmoja, Taasisi za Serikali, Binafsi, Madhehebu ya Dini na makundi mengine kuweka miundombinu ya kuvuna maji ya Mvua kwenye nyumba zao ili kuimarisha upatikanaji wa maji kutokana na mvua zinavyopatikana. Akizungumzia hifadhi na utunzaji wa mazingira, Dkt. Biteko amewataka Wananchi wajitokeze kutoa maoni katika mkakati wa hifadhi vyanzo vya maji wakati huu Serikali ikiendelea na utayarishaji wa Dira ya Taifa ya Mwaka 2050 ili suala la hifadhi za vyanzo vya maji lipewe kipaumbe kinachostahili. Aidha ameagiza Bodi za Maji na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuongeza jitihada za kudhibiti uchafuzi wa mazingira na hata wawekezaji wanapokuja nchini lazima wazingatie utunzaji wa mazingira ili yasiathirike. Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amezishukuru Sekta Binafsi na Wadau wa Maendeleo kwa ushirikiano wanaoutoa kwa Serikali katika Sekta ya Maji na kuwaasa kuendelea kukuza ushirikiano ili kuwasambazia wananchi maji kwani bado kuna kazi kubwa ya kuwapelekea wananchi Maji. Vilevile ameitaka Wizara ya Maji kusimamia kikamilifu maeneo yote yenye vyanzo vya maji, kujengea uwezo wataalam wake katika kuandaa maandiko ya maji yatakayowezesha kupata fedha zaidi za mabadiliko ya tabia nchi zitakazosaidia kupata fedha za utunzaji wa mazingira na pia Sekta zinazohusiana na maji zishirikikine kwa karibu katika usimamizi na si kila mtu kuwa na sheria yake hali inayoleta ukinzani katika utendaji wa kazi. Kuhusu mpango uliopo wa uhifadhi wa vidakio vya maji ambao gharama yake ya utekelezaji ni shilingi bilioni 875 ambazo zinapaswa kutoka Sekta mbalimbali, Dkt. Biteko ameagiza Wizara ya Maji kutenga fedha kwenye bajeti yake ili kuhakikisha kuwa mpango huo unatekelezeka. Amesema vyanzo vingi vya maji vimeharibika na vingine vinaendelea kuvamiwa hivyo Siku ya kilele cha Wiki ya Maji kila mtu ajitathmini na kuchukua hatua kuhusu juhudi zinazowekwa kwenye utunzaji wa mazingira ili vizazi vinavyokuja vikute mazingira yaliyo salama. “ Tafiti za maji za mwaka 2019 zinaonesha kuwa, kiasi cha maji kinachopatikana kwa mtu kwa mwaka kinaendelea kupungua siku hadi siku kutoka mita za ujazo 12,600 katika kipindi cha Uhuru hadi mita za ujzo 2,105 kwa mwaka 2022 hivyo tusipochukua hatua na jitihada za makusudi hali hii itaendelea kushuka kila mwaka kwa sababu maji yanaendelea kupungua katika vyanzo,” Amesema Dkt. Biteko Dkt. Biteko ametoa pongezi kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara wa kumtua mwanamke ndoo kichwani kwa kutenga fedha, kutoa maelekezo na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maji nchini. Awali, Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso alisema kuwa miaka ya nyuma Wizara hiyo ilikuwa ya kero na lawama lakini kutoka Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aingie madarakani ameibadilisha na kuendelea kumtua mama ndoo kichwani na pia ametekeleza miradi mingi ambayo huko nyuma ilikwama. Amesema katika Vijiji 12, 318 tayari vijiji 9,737 vimesambaziwa maji ambapo amewataka wataalam katika Wizara hiyo kutozoea shida za Wananchi hivyo popote pale ambapo maji yanahitajika basi wananchi wapate maji ikiwemo kuchimba visima vitakavyowasaidia wananchi kupata maji. Viongozi mbalimbali waliohudhuria Maadhimisho hayo ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Selemani Jafo na Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar, Joseph Kilangi.

MGODI WA BARRICK BULYANHULU WAONGEZEWA MUDA WA LESENI YA UCHIMBAJI

 

Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba (kushoto) akimkabidhi leseni ya kuongezewa muda wa uchimbaji wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido katika hafla hiyo , wanaoshuhudia nyuma (kushoto) ni Waziri wa Madini, Mh.Antony Mavunde na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha. Leseni hii mpya iliyotolewa ni ya kipindi cha miaka 27.
---
Serikali kupitia Wizara ya Madini imeongeza muda wa leseni ya uchimbaji wa dhahabu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, uliopo katika wilaya za Kahama na Nyang’hwale mkoani Shinyanga kwa kipindi cha miaka 27 kuanzia mwaka huu.

Hafla ya kukabidhi leseni hiyo ilifanyika jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Maofisa waandamizi kutoka Wizara ya madini, Wakuu wa mikoa ya Tanga na Shinyanga na wadau mbalimbali kutoka sekta ya madini ambapo Mgeni Rasmi alikuwa ni Waziri wa Madini, Mh.Antony Mavunde.
Aliyekabidhi leseni hiyo ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, na Mwakilishi wa Barrick, aliyepokea leseni hiyo kwa niaba ya kampuni ni Meneja wa Barrick Tanzania, Melkiory Ngido.

Mgodi wa Bulyanhulu tangu uanze kuendeshwa na kampuni ya Barrick kwa kushirikiana na Serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals, umefanikisha kuleta mafanikio chanya katika kukuza uchumi wa nchi ,kuongeza fursa za ajira sambamba na kutekeleza miradi mikubwa ya kijamii kupitia fedha za uwajibikaji wa jamii (CSR) ambayo inazidi kuboresha maisha ya wananchi katika maeneo yanayozunguka mgodi huo hususani katika sekta ya afya na elimu.
Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido (kushoto) katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa makampuni ya uchimbaji wa madini waliokabidhiwa leseni katika hafla hiyo.

Maofisa Waandamizi wa Barrick waliohudhuria hafla hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu.

Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido (kulia) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita wakati wa hafla hiyo.
 Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini, Antony Mavunde katika hafla hiyo.

Tuesday, March 19, 2024

KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA MSANGANI ZAFUNGWA KWA NEEMA YA MUNGU MGOMBEA ABEBWA JUU

 

NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 


Heka heka za kampeni zilizodumu kwa takribani
zaidi ya siku 14 kwa ajili ya kuwania nafasi ya Udiwani katika  Kata Msangani Jimbo la Kibaha mjini  zimetamatika hii leo kwa kishindo cha aina yake huku chama cha   CCM kikitamba  kushinda kwa kishindo.

Kampeni hizo  ambazo zimefungwa rasmi na Mwenyekiti wa jumuiya wa wazazi ya chama chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Jakson Kituta na kuhudhuliwa na wananchi,wanachama pamoja na viongozi wa CCM wa ngazi mbali.mbali.
Akifunga kampeni hizo Mwe nyekiti huyo aliwahasa wananchi wa kata ya Msangani  kuhakikisha kwamba  wanamchagua kwa kishindo  mgombea wa CCM  ili  aweze kuwaletea maendeleo.

Alisema kwamba  ana imani kubwa na mgombea huyo endapo akichaguliwa kuwa diwani wa Kata ya Msangani  ataweza kushirikiana bega kwa bega katika kuweka mipango madhubuti ya kimaendeleo.

"Nawaomba wananchi wa kata hii ya Msangani msifanye makosa kabisa hata kidogo kikubwa nimekuja hapa ili kuweza kumnadi mgombea wetu kwa hiyo kitu kikubwa mjitokeze kwa wingi kumpigia kura na tutashinda kwa kishindo ,"alisema Mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha Mji Mwalimu Mwajuma Nyamka alisema lengo la CCM ni kutekeleza ilani ya Chama hivyo wananchi wamchague mgombea wao ambaye ataweza kusikiliza kero na changamoto za wananchi.

Nyamka alibainisha kwamba mgombea wao ana sifa zote hivyo  wananchi wa kata ya Msangani wanapaswa kumpa kura nyingi mgombea wa CCM ili aweze kushinda kwa kishindo na kuwaletea mabadiliko.
"Hapa leo tumekuja kumnadi mgombea wetu na kitu kingine mambo ya utekelezaji wa Ilani ya chama  tulishaisema katika uchaguzi uliopita kwa hivyo hapa tumekuza kukazia tu mambo tuliyoyafanya katika miradi ya maendeleo,"alisema Mwalimu  Nyamka.

Kwa upande wake mgombea udiwani katika kata hiyo ya Msangani Yohana Gunze  alikishukuru kwa dhati chama chake cha CCM  kwa kuweza kumuamini kugombea katika  nafasi hiyo.

Gunze alisema kwamba endapo atashinda katika nafasi hiyo atowaangusha kabisa wananchi na badala yake atashirikiana nso kwa hali na mali katika masuala mbali mbali ya kiuchumi na kimaendeleo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha mjini Mussa Ndomba alibainisha kwamba katika kata hiyo ilani ya chama imetekelezeka kwa kiwango kikubwa katika sekta mbali mbali ikiwemo afya,elimu,maji mindimbinu ya barabara na mambo mengine.
Nao badhi ya madiwani kutoka kata mbali mbali waliohudhulia katika ufungaji wa kampeni hiyo walimnadi mgombea huyo na kumuahidi kumpa ushirikiano wa kutosha pindi atakaposhinda.

Naye Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) Issack Kalleiya aliwataka wanachama na wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura huku akiwataka siku hiyo ya uchaguzi wasivae sare yoyote ya chama.

Uchaguzi wa kujaza nafasi ya udiwani katika kata ya Msangani na maeneo mengine ya Jimbo la  Kibiti pamoja   Jimbo la Bagamoyo unatarajiwa kufanyika Machi 20 mwaka huu.

SAO HILL HUZALISHA MICHE MILIONI 5 YA MITI KILA MWAKA

 

Mhifadhi mkuu wa shamba la miti Sao Hill PCO Tebby Yoram alisema kuwa miche hiyo huoteshwa kwa ajili ya kupandwa katika shamba hilo na mingine kugaiwa wananchi,wadau na taasisi mbalimbali.
Baadhi ya miti ikivunwa katika shamba la miti Sao Hill wilaya ya Mufindi mkoani Iringa 
Mhifadhi mkuu wa shamba la miti Sao Hill PCO Tebby Yoram alisema kuwa miche hiyo huoteshwa kwa ajili ya kupandwa katika shamba hilo na mingine kugaiwa wananchi,wadau na taasisi mbalimbali.


Na Fredy Mgunda, Iringa.

SHAMBA la miti Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa huotesha miche milioni 5 ya miti kila mwaka katika bustani tatu zilizopo katika shamba hilo.


Akizungumza na waandishi wa habari Mhifadhi mkuu wa shamba la miti Sao Hill PCO Tebby Yoram alisema kuwa miche hiyo huoteshwa kwa ajili ya kupandwa katika shamba hilo na mingine kugaiwa wananchi,wadau na taasisi mbalimbali.


PCO Yoram alisema kuwa lengo la kubwa la kugawa miche hiyo ni kuendeleza uhifadhi wa misitu kwa wananchi na taasisi hizo kuendelea kupanda miti kwa wingi katika mashamba na kushiriki katika kuhifadhi shamba hilo.


Alisema kuwa kuelekea kilele cha siku ya upandaji miti kitaifa itakayofanyika katika wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro na uongozi wa shamba hilo umejipanga kupanda miti kwenye vyanzo vya maji vilivyopo katika shamba hilo.


PCO Yoram alisema kuwa wanapanda miti kwenye vyanzo vya maji kwa lengo la kuendelea kutunza vyanzo vya maji na shamba la miti Sao Hill hupanda hekta 2500 hadi hekta 300 kila mwaka.


Aidha PCO Yoram alisema kuwa licha ya kupanda miti mingi lakini shamba hilo huvunwa Laki 6 hadi 7 ujazo wa uvunaji wa mazao ya miti katika shamba hilo kwa kuvinufaisha viwanda 400 ambavyo hutumia malighafi za misitu.

KAMATI YA PIC YARIDHISHWA NA MIRADI INAYOTEKELEZWA NA TANGA UWASA

 

Na Oscar Assenga,TANGA

KAMATI ya Bunge Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) imeridhishwa na miradi inayotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) huku wakizitaka mamlaka nyengine nchini kwenda kujifunza ubunifu ambao wanautumia katika kutekeleza miradi yao na hivyo kuwawezesha kuondoa changamoto hiyo kwa wananchi.

Hayo yalisemwa  na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Deus Sangu wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua miradi inayotekelezwa na Tanga Uwasa ambapo wameridhishwa na miradi hiyo huku akiipongeza Serikali kwa namna inavyopeleka msukumo kwenye uwekezaji hasa kwenye sekta ya ya maji .



Alisema kamati hiyo imejionea shuguli uwekezaji na kuona ubunifu kamati imekagua mradi huo imerdhishwa na ubunifu huo huku kuwataka mamlaka nyengine ziweze kuiga mfano wa kuona namna ya kutatua changamoto ya maji katika maeneo yao.

“Mradi huu umetekelezwa kwa mkopo kutoka benki ya maendeleo asilimia 75 na sehemu inayobakia kama bilioni 3 ni makusanyo ya ndani hivyo mradi huu zaidi ya Bilioni 10 na umeleta mapinduzi makubwa sana kwa maana mahitaji ya maji jiji la Tanga lita milioni 45,000,000 “alisema

Aidha alisema wao kama kamati wameridhishwa na namna ambavyo Tanga Uwasa walivyoweza kubuni vyanzo vya kufadhili miradi yao na wameona mamlaka za maji wanategemea vyanzo kutoka serikali kuu lakini wao wenyewe wamebuni na kwenda kukopa fedha benki na mapato yao ya ndani wakaleta mapinduzi na kutatua changamoto ya maji karibunia takribinia asilimia 96.

Alisema pia kwanza kuja na hati fungani wamekuja na ubunifu wa kipekee kwa taaswanza Tanzania kuja na hati fungani ya kijani yenye thamani ya bilioni 53 itakayosaidia kuongeza kiwango cha maji kwa kiasi kikubwa huo mradi kwa kikasi kikubwa ilikuwa iongeze hiy ni heshima ya kipekee kwa Tanga Uwasa kuanzisha kwa jambo hilo.

“Sisi kama tunawapongeza na kuzitaka mamlaka za maji kuona namna kujifunza Tanga uwasa kwa jinsi wanavyofanya a Tanga Uwasa walivyotumia mapato yake ya ndani kuweza kwa kutekeleza miradi yake na kuwa na tija kubwa”Alisema

Awali akkizungumza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo aliishukuru hiyo kwa kuwapa ushauri na maelekezo na ushauri wao ndio wameweza kufika hapo hiyo ni sehemu ya awamu ya awali ya mradi ambao baada ya kuchukua mkopo wa awali wa shilling zaidi ya bilioni 7.

Alisema hivyo walikuwa wanajenga uhalali na uzoefu wa kuchukua mkopo mkubwa zaidi na wanataraji kuanzia mwezi wa nne mwaka huu wataanza kutekeleza miradi mingine zaidi ili kufikia lita milioni 60 na kufikia wananchi wote wa Tanga,Pangani,Muheza,Pangani na Mkinga.

“Hivyo niwashukuru bodi kuhakikisha tunakuja na mipango mizuri ya kuhakikisha hkila siku hawalali na kuhakikisha wanakuja na mipango mipaya kuhakikisha wananchi waondokana na gharama za kugharamia huduma mbalimbali”alisema

Monday, March 18, 2024

MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU AWATAKA WAKALA WA MAJENGO KUFANYA HAYA.

 NA ALBERT GSENGO/MWANZA

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu Seleman Kakoso amewataka wakala wa Majengo Tanzania TBA kuwa na ubunifu katika ujenzi wa majengo mazuri na yenye mvuto wa kibiashara ili wawe na uwezo mkubwa wa kukusanya kipato chao binafsi na kuacha kuitegemea serikali. Kakoso amesema hayo alipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la kupangisha lililopo eneo la Ghana wilayani Ilemela jijini Mwanza na kuongeza kwa kumwagiza waziri wa ujenzi Innocent Bashungwa kuhakikisha anawasaidia TBA waweze kukusanya madeni ambayo wanaidai serikali kupitia taaisisi zake. Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TBA Daud Kondoro amesema ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 50 ambapo amesema wao kama TBA waliona Jiji la mwanza lina uhitajia mkubwa wa Majengo ya kupangisha hivyo ni wajibu wao kuyaendeleza maeneo yote nchi nzima. #samiasuluhuhassan #jembefm #mwanza

MAKARANI WA KUSIMAMIA UCHAGUZI UDIWANI KATA YA MSANGANI WAPIGWA MSASA


 NA VICTOR MASANGU KIBAHA


Katika kuelekea katika uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya Udiwani kata ya Msangani iliyopo Halmashauri ya mji Kibaha makarani wa kusimamia uchaguzi huo wamepatiwa mafunzo maalumu kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.

Uchaguzi huo wa kujaza nafasi ya udiwani wa kujaza  nafasi hiyo unnatarajiwa kifanyika machi 20 mwaka huu ambapo utawashirikisha wananchi wa kata ya Msangani.

Kadhalika  Makarani hao  waongozaji licha ya kupata  mafunzo hayo wamepata  kiapo cha kutunza Siri Chini ya Kanuni ya 16(1) (a) na 50 (4) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge,2020 na Kanuni ya 14 (1)(a),(2) na 43(4) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani),2020 Mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi Salum Papen.

Aidha,Mafunzo hayo yametolewa na Maria Israel,Benjamin Mputtu wakisaidiana na Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Optuna Kasanda ambao wamewasisitiza kwenda kufanyakazi kwa kuzingatia Sheria,Kanuni na taratibu za Uchaguzi

Akifungua Mafunzo hayo,Msimamizi wa Uchaguzi,Mwanasheria nguli wa Mahakama kuu na zilizo chini yake Salum Papen amesema.." _Tume imewateua ninyi kwa mujibu wa sheria na Kwa kuzingatia uzoefu wenu katika masuala ya Uchaguzi_ "katendeni haki amesisitiza Papen

Papen ametoa rai kwa Makarani waongozaji kujiamini na kujitambua,kufanyakazi kwa kuzingatia Katiba ya Nchi,Sheria za Uchaguzi na Kanuni zake,Maadili ya Uchaguzi na Maelekezo mbambali yanayotolewa na Time

Katika hatua nyingine Makarani wametia tamko la kujitoa uanachama au kutokuwa na Chama cha Siasa chini ya Kanuni ya 16 (1)(b) na ( 3 ) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge,2020 na Kanuni 14(1) (b) na (3) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,(Uchaguzi wa Madiwani),2020 mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi,Mwanasheria Salum Papen

Aidha,Andrea Isamaki Ofisa kutoka Tume ya Taifa ya  Uchaguzi (NEC) ameshiriki kushuhudia Mafunzo,kiapo cha kutunza Siri na tamko la kujitoa uanachama kwa Makarani waongozaji

Nadia Issa na Benson Shawa,Makarani waongozaji wamesema wanakwenda kufanya kazi kwa weledi mkubwa kwa kuzingatia Sheria,Kanuni na taratibu za Uchaguzi 

Uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya udiwani katika Kata ya Msangani unatarajiwa kufanyika machi 20 mwaka huu  kutokana na kifo cha Mhe.Leonard Mlowe kilichotokea tarehe 23 Disemba,2023 ambapo jumla ya vyama nane (8) vya Siasa vinatarajia kushiriki.