Wabunge, Bw. Paul Kimiti (Sumbawanga Mjini) kushoto na Bw. Chrisant Mzindakaya (Kwela) wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma huku wakipunga mikono kuashiria ukomo wa ubunge wao wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu. Wabunge wote hao wameshatangaza kutowania tena nafasi hizo baada ya kutumikia kwa muda mrefu.
(Picha na Peter Twite)
GAZETI LA MAJIRA.
Thursday, July 15, 2010
FIESTA
AWALI NGOMA YA FIESTA 2010 ILIPANGWA KUMALIZIKA MWANZA TAREHE 7 AUGUST 2010 PALE YATCH CLUB, LAKINI KWA MUJIBU WA KIKAO CHA KAMATI YA FIESTA KILICHOKETI JANA USIKU NAKUMALIZIKA MIDA IKIWA IMEENDA SANA. HATIMAYE PEPA LIMEPENYEZWA NA RATIBA KUSOMEKA KUWA WAKAZI WA MWANZA KUHUSIKA NA BURUDANI ZA FIESTA JIPANGUSE! TAREHE 31 JULY (YATCH CLUB) NA TAREHE 1 AUGUST CCM KIRUMBA.
MKAZI WA KANDA YA ZIWA KAA TAYARI KWA BURUDIKO HILO LA ROHO, MWILI NA NAFSI HUKU TUKIHAMASISHANA KATIKA SUALA ZIMA LA UWAJIBIKAJI KUIJENGA NCHI.
NIKISEMA - Jipanguseeeeee!
UNASEMA - Rrrrrrraaaaaaaa!
Wednesday, July 14, 2010
MWANZA
Wednesday, July 14, 2010
BANGO
MWANDISHI MAHIRI WA SIKU NYINGI WA MAGAZETI YA UHURU, MZALENDO NA BURUDANI BI. EVA SWEET ISRAEL MUSIBA (PICHANI) AMETANGAZA NIA, KUGOMBEA UBUNGE VITI MAALUM (UWT) MKOA WA MARA KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM).
AKIZUNGUMZA NAMI HIVI MAJUZI MJINI MUSOMA BI. EVA-SWEET MUSIBA AMESEMA KUWA PAMOJA NA KUTANGAZA NIA HIYO, UWEZO ANAO , SIFA ANAZO HIVYO KILICHOBAKI NI MUDA NA WAKATI UFIKE NAE ACHUKUWE FOMU, KISHA KUHUSIKA NA MCHAKATO MZIMA.
MWISHO BI EVA-SWEET AMEOMBA BARAKA ZA KILA MTANZANIA MPENDA MAENDELEO.
MARA BAADA YA SHUGHULI PEVU YA KUTABIRI VYEMA USHINDI WA MICHEZO NANE YA KOMBE LA DUNIA PAMOJA NA ILE YA FAINALI. PWEZA PAUL MWENYE MIAKA MIWILI NI WAKATI KWAKE KUTENGENEZA FEDHA KWANI LICHA YA KUGOMBEWA NA NCHI KADHAA JUU YA URAIA WAKE, PWEZA HUYO AMEKUWA AKIHITAJIKA KUDHURU KASRI ZA NCHI MBALIMBALI KWA KIWANGO CHOCHOTE CHA PESA.
WATU WENGI HUSUSANI WACHEZA KAMALI WALIKUWA WAKIWEKA FEDHA KATIKA KAMALI MARA BAADA YA KUSIKIA UTABIRI WA PWEZA HUYO WA UJERUMANI ANASEMA NINI ILI NAO WATABIRI NAYE. NI AJABU LAKINI AMEKUWA AKIPATIA KILA SIKU.
Tuesday, July 13, 2010
BANGO