ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 15, 2023

'MZEE' NGASSA AMWAGA SIRI ZA SIMBA NA YANGA AMPA USHAURI HUU FEI TOTO

 Mzee KHALFAN NGASSA Baba Mzazi Wa Mchezaji @mrisho_khalfan_ngassa Akizungumza na @mc_suzuki

Amezungumza katika Maisha yake ya soka Ni Mchezo upi kati ya Simba na Yanga Ambao anaukumbuka zaidi akiongeza kuwa Mchezaji SAID SUED 'SCUD' ni Moja ya Mchezaji ambaye hatokuja kumsahau kwenye Derby. . . . Wewe ni Derby Gani unaikumbuka Zaidi

MASANJA MKANDAMIZAJI, MC PILIPILI, PASTOR MYAMBA WOTE NI EMMANUEL KUNA SIRI GANI KATIKA JINA HILO?

 PASTOR EMMANUEL MYAMBA Akijibu swali la @mc_suzuki juu ya uhusiano Wa Jina Emmanuel na Uhuduma inayofanana anayoitoa yeye pamoja na @mcpilipili_ @mkandamizaji Ikiwa Wote majina Yao ni EMMANUEL

. . . Full interview inapatikana kwenye YouTube channel yetu JEMBE FM . . . . #jembefmupdates #jembefmkimewaka2023🔥🔥

BARABARA NJIA NNE KUTATUA KERO DARAJA LA MKUYUNI MWANZA

 Meya Wa Jiji la Mwanza @sima_constantine_sima Akizungumza kupitia Mchakamchaka kuhusu Kero ya Daraja la Mkuyuni Jijini Mwanza ambalo limekuwa likiwapa Changamoto watumiaji Wa Barabara hiyo nyakati za Mvua.

. . . . #jembeupdates #jembefmkimewaka2023🔥🔥

KAMA KANUMBA ANGEKUWEPO BONGO MOVIE INGEKUWA WAPI? - PASTOR MYAMBA

 - Maono ya pastor Emmanuel Myamba juu ya Bongo Movie.

- Jeh umewahi kujutia au kutamani baadhi ya vipande vya uigizaji enzi zako vingefutwa? - Pastor Emmanuel Myamba akifanya mahojiano na mwanahabari wetu Mc. Suzuki wa 93.7 Jembe Fm ambapo humo pia kazungumza kuhusu marehemu #kanumba Jinsi alivyomuita katika tasnia ya uigizaji filamu. - Kuna vitu vingi watanzania wanavimisi toka kwa marehemu Kanumba. Hakuwa mchoyo kuwavuta watu kwenye tasnia ya uigizaji, ushuhuda upo.

Friday, April 14, 2023

MASHABIKI WA SIMBA SC v YANGA SC WAFANYAKAZI IDARA YA MAJI MWANZA (MWAUWASA) KUKIPIGA JUMAMOSI HII

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Kabla ya Simba Sc kukutana uso kwa uso dhidi ya watani wao Yanga Sc katika Kariakoo Derby pale jijini Dar es salaam, upande wa pili jijini Mwanza mashabiki wa timu hizo ambao ni wafanyakazi kutoka Idara ya Maji safi na Maji taka Mwanza (MWAUWASA) wanasema wao ndiyo wenye funguo za utabiri kwa matokeo ya mchezo huo watakutana katika mchezo uatakaopigwa viwanja vya TTC Butimba wilayani Nyamagana jijini Mwanza. Mchezo huo wa kirafiki wa mashabiki wa Simba na Yanga Idara ya maji safi na maji taka jijini Mwanza utachezwa Jumamosi hii ya tarehe 15 April 2023 majira ya saa 3 kamili asubuhi.

Thursday, April 13, 2023

TUNAWAAMBIA WATANZANIA WASITUMIE PODA YA JOHNSON &JOHNSON KWA SASA’- MKURUGENZI WA TBS


Shirika la Viwango nchini Tanzania(TBS) limewataka Watanzania kuacha kutumia poda ya Johnson & Johnson hadi uchunguzi kuhusu poda hiyo utakapokamilika.

Juma lililopita ilifahamika kuwa Shirika la viwango Tanzania, linachunguza poda aina ya Johnson inayouzwa katika maduka mbalimbali nchini humo na kwingineko duniani.

Uchunguzi huo unatokana na kampuni inayotengeneza bidhaa hiyo, Johnson & Johnson ya Marekani kukubali kulipa fidia ya dola za Marekani bilioni 8.9 kwa sababu ya kesi zaidi ya elfu 38 za madai kuwa madini ya talcum yaliyomo kwenye poda hiyo ya watoto na bidhaa nyingine yanasababisha saratani ya mfuko wa mayai ya uzazi kwa watumiaji.

Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athumani Yusuph Ngenya amesema

Poda hiyo ina madhara ambayo yamepigwa marufuku.

‘’Kitu chochea kinachozungumzwa kwamba kina madhara ni bora na ni busara kukiweka kando mpaka uchunguzi ukamilike’’ , alisema na kusisitiza kuwa:’’Tunawaambia Watanzania wasitumie poda ya Johnson & Johnson’’ iliyopo madukani hadi uchunguzi utakapokamilika.

Bw Dkt. Athumani Yusuph Ngenya, amesema uchunguzi kuhusiana na poda ya Jojnson &Johnson ambayo kwa sasa ipo madukani, nchini humo utakamilika katika kipindi cha wiki mbili au wiki tatu zijazo.

MWANAMUME AOA DADA WAWILI, AJALIWA WATOTO 14 NAO: "NINAWATOSHELEZA WOTE"

 


Mwanamume mmoja anahisi fahari kwa hatua yake ya kuwaoa wake wawili na familia hiyo inaishi kwa amani katika nyumba moja.

Wanawake hao wawili wanaoshiriki mwanamume mmoja ni dada wa tumbo moja  na wanaishi kwa amani katika nyumba moja

Mwanamume huyo amesema hapo awali alikuwa ameoa mke wake wa kwanza kwa takriban muongo mmoja kabla ya kuoa mwingine, dada ya mkewe.

Mukama Mugenimwana alipendana na kuoa dadake Juliet, Namirembe Harriet, ambaye alikuwa akiwasaidia kulea watoto wao.

Juliet alikuwa amemwomba Namirembe kuwasaidia wenzi hao kutunza watoto wao wachanga alipojifungua mtoto wake wa tano.

“Nimefurahi kuwa nao wote wawili upande ingawa safari ya kuwaoa imekuwa ngumu, lakini mimi ni mume wa kujivunia, na sina aibu kwa wake zangu.

Mke wangu wa kwanza, ambaye tumeishi naye kwa takriban miaka 20, ana watoto 10 naye mke wangu wa pili ana watoto wane.

Kwa miaka minne, Mukama kwa kawaida alikuwa akimvizia Namirembe kutokana na urembo wake.

Baadaye alimeza chambo, na Namirembe akapata ujauzito wa mwanamume huyo kutoka Uganda ambaye alisema alikuwa na matatizo na mke wake wa kwanza.

"Tulikuwa na ugomvi katika maisha yetu ya kila siku hapa nyumbani na hivyo ndivyo nilivyoishia kushikana na dadake," Mugenimwana alijitetea.

Juliet alimshinikiza Namirembe amwambie ni mimba ya nani naye akamwambia kuwa ilikuwa ya mumewe

Alikusanya virago vyake akarudi nyumbani kwa wazazi ambao aliishi nao kwa muda.

Mugenimwana alilazimika kumlipia mahari Namirembe ili awachukue dada wote wawili kama wake zake na kusamehewa na wazazi wa dada hao.

Anaishi nao kwa amani na inadaiwa ni mjamzito na vile vile anatazamia kupanua familia yake.

 "Siri ya kuwapa raha wake zako ni kugawana nao kila kitu kwa usawa katika nyumba, najaribu kuwaridhisha wake wote wawili, ninawapa kila nilichonacho, nawapenda wote wawili, nafanya hivyo ili kuepusha shida.

Sitaki vita. Sitaki hata mmoja wao ahisi kutishiwa au kutothaminiwa," alisema.

MAJENGO YALIYOJENGWA HOLELA KUBOMOLEWA MWANZA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

"Mwanza tulizindua master plan 2000-2025 ambapo inatuelekeza hususani maeneo ya mjini kati yanapaswa yaweje, inaenda mbali master plan hiyo na kuelekeza hadi majengo yanayopaswa kujengwa" "Moja ya ugomvi wangu mkubwa ni ujenzi holela............." Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Costantine Sima akizungumza na Paul Kadushi wa kipindi cha Mchakamchaka ya Jembe Fm.

TWENZETU KWENYE KARIAKOO DARBY.


 TAWI LA YANGA MWANZA MJINI 

👉Kamati Tendaji Tawi la Yanga Mwanza mjini,Inawatangazia safari ya kwenda Dar es salaam kwenye Darby kati ya "Simba v Yanga" itakayochezwa tarehe 16/04/2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa(Lupaso)


Kuchangia safari ya kwenda:-

👉🏽Wanachama/Wapenzi na Mashabiki wanaokwenda na kurudi ni Tshs.70,000/

👉🏽Wanachama wasiosafiri watachangia kuanzia Tshs. 5,000/= na kuendelea


👉Wanachama, Wpenzi na Mashabiki wa Yanga Mkoa wa Mwanza na viunga vyake nyote mnakaribishwa sana

 

Tuma muamala wako kwenda no:-


0744635402 

Jina:- 

YANGA MWANZA MJINI


"Tuma pesa na kisha fika ofisini mtaa wa Rufiji Upate risiti yako"


Mwisho wa kupokea

 Nauli ni  tarehe:

 12/04/2023

MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA MAKAMU WA RAIS ILEMELA JIJINI MWANZA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Philipo Isdor Mpango akiwasalimu wananchi wa eneo la Buswelu wilayani Ilemela jijini Mwanza.

#April 12, 2023 Jumatano 

Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hasan Elias Masala pamoja na mkurugenzi wa manispaa hiyo Mhandisi Modest Apolinary wamewaongoza wananchi wa wilaya ya Ilemela katika mapokezi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Philipo Isdor Mpango alipofanya ziara katika wilaya ya Ilemela na kuzungumza na wananchi katika eneo la  Buswelu senta.

 Mkutano ambao pia umehudhuriwa na viongozi wengine akiwemo Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe Adam Malima, Waziri wa Maji Mhe Juma Aweso, Naibu Waziri wa OR TAMISEMI Mhe Deogratius Ndejembi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Mhe Sixbert Reuben na Mbunge wa Jimbo hilo ambae pia ni Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula (MNEC)

 ambapo Mhe Dkt Mpango alipata wasaa wa kuhutubia wananchi  sanjari na kuelezea shughuli za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hasan, kusikiliza kero zinazokabili wananchi na kisha kuzipatia ufumbuzi








Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Mhe Sixbert Reuben.
Mbunge wa Jimbo hilo ambae pia ni Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula (MNEC)
Naibu Waziri wa OR TAMISEMI Mhe Deogratius Ndejembi.
Waziri wa Maji Mhe Juma Aweso.



' Ilemela ni yetu, tushirikishane kuijenga '

Wednesday, April 12, 2023

JAMAA AFUMANIWA NA MKE WA BOSI WAKE NAIVASHA.


Mwanadada huyo anasemekana kuwa alikuwa na shauku kuhusu mahusiano ya mumewe na mkwe wa bosi wake kabla ya tukio hilo ila alikosa uthibitisho kamili wa iwapo ni kweli wawili hawa walikuwa mahawara.

Mwanadada huyo anayefahamika kwa jina la Mercy anasemekana kuwasikia wawili hawa wakiwa na maongezi yaliyoashiria kuwa walikuwa wanatongozana wakati ambapo bosi  wa mumewe na mke wake walipowatembelea nyumbani.

Siku ya ujio wa boss wa Robert  anasemekana kuwa na kumbukumbu ya mazungumzo waliokuwa nayo kama ifuatavyo.

Leo ni siku ya maana katika maisha yangu. bosi wangu anastahili kuona nyumba yetu ikiwa katika hali safi. Unanisikiza kweli Mecy? Mume wangu alisema kwa hasira lakini nilikwa nimezoea jinsi alivyokuwa akizungumza,""Ndio Robert nimekusikiza. Nimemtengenezea bosi wako chakula anachokipenda na nikizuri," Nilijibu

"Kabiruni ndani ya nyumba Bwana na Bi Teddy. Habari za jioni Bi Teddy, nimefurahi kukuona,” nilimsikia mume wangu akiwaeleza wageni wetu walipofika.

Inasemekana kuwa baada ya muda kidogo Bi Teddy aliomba kuonyeshwa sehemu tofauti za nyumba ya Robert wakati ambapo Mercy alikuwa akitayarisha vinyuaji.

Katika safari ya kuonyeshwa nyumba wawili hawa wanasemekana kuchukua muda mwingi kabla ya kurejea sebuleni na hapo ndipo Mercy akaamua kuwafuata na kubaini kilichokuwa kinaendelea.

Mercy anasemekana kukosa kuingia katika chumba walimo kuwa wawili hawa kwani alichosikia ni ishara kuwa wawili hawa walikuwa na mahusiano.

Kwani leo hauna kitu kwa ajili yangu?" Bi Teddy alimuuliza Robert"Bila shaka, mpenzi wangu,” Robert alijibu na hapo nikasikia sauti ya kupeana busu.

Mercy anasema japo tukio hilo lilimthibitishia kuwa mumewe na mke wa bosi wake walikuwa na mahusiano alihitaji uthibitisho zaidi.Wageni walipoondoka Mercy anasemekana kukosa kumzomea mume wake lakini badala yake akaamua kuenda kutafuta huduma za daktari wa kienyeji Wema Kamaliza.

Siku chache baada ya Kamaliza kufanya mambo yake Robert na mke wa bosi wake wanasemekana kugandana wakifanya ngono katika Lodge huko Naivasha.

Mecry alisema kuwa alikwenda kwenye gest hiyo baada ya kupigiwa simu na mumewe na kisha kuwaeleza alichokifanya na pia kuwaeleza aliyosikia wakizungumza wakati walipowatembea katika makaazi yao.

Baada ya mazungumzo na majadiliano Mercy aliwasiliana na Kalumanzila wake  ambaye alikuja na akawatenganisha wawili hawa.

KWELEAKWELEA WAHARIBU MASHAMBA YA WAKULIMA

 


TAKRIBANI heka 1,600 za mashamba ya mpunga Kata ya Kagu, Halmashauri ya Wilaya ya Geita mkoani hapa, zipo hatarini kushambuliwa na ndege aina ya kweleakwelea.

Ofisa Kilimo wa Halmashauri, Malick Athuman amesema tayari mawasiliano na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatirifu (TPHPA) yamefanyika, ili kuwadhibiti ndege hao ambao idadi yao inaonekana kuongezeka katika eneo hilo.

Amewahakikishia wakulima kwamba changamoto hiyo itaisha, kwa uendelevu wa zao hilo la chakula na biashara.

 Pamoja na kuwathibiti kweleakwelea shambani, mamlaka itapulizia dawa kwenye mazalia yao kwa kutumia helikopta, ili kuangamiza kabisa chimbuko lao,  

Amedai kuwa kawaida ndege hawa huvutiwa na mazao mengi, ikiwemo alizeti, lakini wamegundua wanapendelea zaidi mpunga kiasi kwamba wanaweza kuhama haraka kutoka shamba moja kufuata jingine.Kuwadhibiti ni lazima kwa sababu wanafanya uharibifu mkubwa kwa kuanza kushambulia mmea wenyewe, hadi pale mpunga unapoelekea kukomaa.

Ilifahamika zaidi kwamba kweleakwelea wana uwezo wa kuharibu shamba zima kwa asilimia 100, kiasi cha mkulima kutopata hata punje ya mavuno.

DC SAME AMSHUKURU RAIS DKT SAMIA KWA KUIWEZESHA HIFADHI YA TAIFA YA MKOMAZI KUONGEZA WATALII

 MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi lengo likiwa ni kuhamasisha utalii wa ndani

MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni  kushoto akizungumza na Afisa Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Happiness Kiemi wakati alipofika kwenye hifadhi hiyo kuitembelea ikiwa ni  kuhamasisha utalii wa ndani
Afisa Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Happiness Kiemi akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu maboresho makubwa yaliyofanywa kwenye Hifadhi hiyo na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu 



Afisa Utalii wa Hifadhi wa Taifa ya Mkomazi Happiness Kiemi  kulia akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni wakati wa ziara yake kwenye hifadhi hiyo
Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni katika akiwa ni Meneja wa Benki ya CRDB wilaya ya Same kulia  
Watalii wakifurahia utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi wilayani Same Mkoani Kilimanjaro
Faru katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi
Faru katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi
Faru katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi
Tembo akiwa na mtoto wake katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi


Twiga akiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi



Na Oscar Assenga aliyekuwa KILIMANJARO

MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni amesema wanamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa ubunifu mkubwa alioufanya kupitia Filamu yake ya Royal Tour na matunda yake kuonekana kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watalii kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.

Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati alipofanya ziara katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kuhamasisha utaliiwa ndani ambapo alisema kwamba baada ya ziara hiyo watalii wanaoingia kwa mwaka sasa wameongezeka na kufikia zaidi ya 7000.

Alisema kwamba huo ni ubinifu wa kipekee ambao umefanywa na Mkuu huyo wa nchi katika kuhakikisha anatangaza vivutio vya utalii hapa nchini ikiwa ni kuhamasisha watanzania na w ageni kutoka nje kutembelea hifadhi zilizopo hapa nchini.

Mkuu huyo wa wilaya alisema pia Rais Dkt Samia Suluhu kupitia fedha za Tozo na Fedha za Covid 19 zimewasaidia kuimarisha miundombinu ya hifadhi nchini ambapo miongoni mwa hifadhi ambazo zimenufaika ni mkomazi ambapo kuna majengo ya utawala na barabara nzuri ambao zinahamasisha watalii hivyo Rais amekuwa mfano nzuri wa uhifadhi nchini.

Aidha pia alisema wanapokuwa na hifadhi inayofikika kirahisi wanapata watalii wengi ambazo wanasaidia kukuza uchumi wa nchi yetu

Hata hivyo aliwahimiza watanzania kutembelea hifadhi za hapa nchini ili kuweza kujionea vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo kuwataka pia wananchi wa wilaya ya Same watumie wikiendi zao kuweza kufika mkomazi kuweza kuona vivutio vilivyopo na hivyo kusaidia serikali kuingiza mapato ambayo yatasaidia maendeleo kwenye wilaya yao.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo, Afisa Utalii wa Hifadhi wa Taifa ya Mkomazi Happiness Kiemi alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kutokana na kupelekea fedha za Uviko ambapo waliweza kuzitumia kujenga lango maalumu ambalo ni la kuingilia wageni wanaofika kutembelea hifadhi hiyo na kuweza kupata huduma nzuri za utalii.

Alisema kwamba kupitia fedha hizo wameweza kujenga barabara nzuri yenye utefiu wa zaidia ya kilomita 140 na pia kutengeneza viwanja vya ndege na hiyo imetoa fursa kwa wageni ambao hawana muda wa kutembea kwenye magari kwa muda mrefu wakati wa safari zao kutoka maeneo mbalimbali kwenda kuitembelea hifadhi hiyo

Happiness alisema kwa kujengwa uwanja huo kumesaidia wageni kusafiri kutumia ndege kufika hifadhi ya Taifa ya Mkomazi moja kwa moja kutoka kwenye viwanja vyengine

DC KALLI AKABIDHI GODORO GEREZA LA (BANGWE)KIGOMA.


Na. Sebastian Salum.

Mkuu wa wilaya ya kigoma Salum Kalli, amekabidhi magodoro 35,katika gereza la wilaya Bangwe kigoma.


Akikabidhi magodoro hayo yaliyotolewa na mkurugenzi wa Radio Joy bw.Mwenge Muyombi.




Mh.Kalli ameiasa jamii, na taasisi mbalimbali, kuendelea kujitoa ili kuimaliza changamoto ya magodoro, katika gereza hilo, ikiwa ni sehem ya jamii ya kigoma, na sehem ya mafunzo ya tabia kwa wananchi.


Kwa upande wake Mratibu mwandamizi wa magereza, Bakari kasenga. ambae ni Mkuu wa gereza hilo, amemshukuru Mkuu huyo, pamoja na Uongozi wa Radio Joy,kutatua changamoto ya upatikanaji wa magodoro,kwa kuwakabidhi jumla ya godoro 35 mbapo awali Walipokea pia godoro 30 kutoka Uongozi wa Radio Joy.

Mkuu huyo ametumia tukio hilo, kutembelea kiwanda kidogo cha utengenezaji wa samani mbali mbali za nyumbani, ikiwa ni sehem mojawapo ya mafunzo.

MBUNGE NYAMOGA AONGOZA HARAMBEE KUCHANGIA UJENZI WA SHULE YA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA HURUMA CENTER

 

Mbunge wa Jimbo la Kilolo mkoani Iringa Justine Nyamoga akiongea wakati wa zoezi la uchangishaji wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi ya Huruma Center.
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Iringa Blastoni Gavile akiongea wakati wa zoezi la uchangishaji wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi ya Huruma Center
Mbunge wa Jimbo la Kilolo mkoani Iringa Justine Nyamoga akiwa sambamba na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Iringa Blastoni Gavile wakiwa viongozi mbalimbali katika eneo la ujenzi wa shule ya msingi ya Huruma Center.


Na Fredy Mgunda, Iringa

MBUNGE wa Jimbo la Kilolo, Mkoani Iringa Justine Nyamoga ameongoza harambee kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Shule ya Msingi matika Kituo cha Watoto Yatima cha Huruma.


Kituo hicho kinachomilikia na Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa mbali na watoto yatima kimekuwa kikihudumia watoto waliofanyiwa ukatili ikiwemo ulawiti na ubakaji.


Akizungumza katika harambee hiyo aliyokusanya zaidi ya Sh40 Milioni, Nyamoga ameishauri jamii kujitoa kwa ajili ya kuwasaidia watoto walio katika mazingira magumu.


Kwa upande wake Askofu wa KKKT Dayosisi ya Iringa Blastoni Gavile alimpongeza Nyamoga kwa upendo na kukubali wito wa kushiriki harambee hiyo.


"Hiki ni kituo chetu wenyewe tunapaswa sisi tuanze kujitoa kuliko wengine, Kuna Baraka nyingi unachuma unapotoa," amesema Nyamoga.


Askofu Gavile alisema lengo laa kituo hicho ni kuwapa uhakika wa elimu watoto wanao walenda ndani ya kituo.


"Mungu akubariki sana Mbunge wetu kwa utayari wako kuja kuwasaidia watoto Hawa," amesema Askofu Gavile.

Tuesday, April 11, 2023

WAUGUZI HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO WAFUNDISHWA NAMNA YA KUPIMA USIKIVU WA WATOTO WANAPOZALIWA

 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt Edwin Liyombo akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani kuhusu mafunzo walioyatoa kwa wauguzi waliopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo namna ya kupima usikivu wa watoto wadogo wanapozaliwa ili kuweza kutoa huduma hiyo kwa ufanisi na tija kubwa kwa wananchi wanaowahudumia

Muuguzi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Prisca Massawe kushoto akimpima usikivu mtoto aliyezaliwa katika hospital hiyo wakati wa mafunzo ya kuwafundisha namna ya kupima usikivu kwa watoto wachanga wanapozaliwa kulia ni mkufunzi wa mafunzo hayo Hamisi Shaban Mtitho kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Na Oscar Assenga,TANGA
WAUGUZI katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo wamefundishwa namna ya kupima usikivu wa watoto wadogo wanapozaliwa ili kuweza kutoa huduma hiyo kwa ufanisi na tija kubwa kwa wananchi wanaowahudumia

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo mwishoni mwa wiki ,Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt Edwin Liyombo alisema kwamba wameamua kuwafundisha wauguzi program ya kupima usikivu kwa watoto wanaozaliwa ili kuweza kuwasaidia watoto wanaokuwa na shida hiyo pindi wanapozaliwa.

Alisema kwa sababu imeonekana kuna watoto wengi wanajulikana wana matatizo ya usikivu na wanashindwa kuongeza pindi wanapokuwa na umri wa kuanza kwenda shule ikiwemo wanaozaliwa hawawezi kuongea hivyo mpango huo unasaidia kugundua mtoto pale anazaliwa mpaka mwezi mmoja.

Aidha alisema kwa sababu kuna mashine maalumu ya kuwapima kama wana matatizo na wakibainika mapema inawasaidia kuweza kuona namna ya kulipatia ufumbuzi.

“Tunawafundisha wauguzi jinsi ya kufanya uchunguzi na baadae itakwenda nchi nzima kwani hawa wanaowafundisha baadae watakuwa walimu na kufundisha wengine lakini tutawaleta mashine ndogo itakayotumika kupima watoto wanapozaliwa”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba wanaomba watu wajitokeze wakati wa mpango huo wa kupima usikivu huku akieleza kwamba katika zoezi lao wamepima watoto 20 wengi hawana matatizo kadri watakavyopima wengi watajua hali ipo vuzri na hivyo kuisaidia wizara kupanga bajeti ili kuona namna ya kuwasaidia.

Katika hatua nyengine Dkt Edwin alisema kwamba takwimu zinaonyesha kwamba kati wa watu 100 watu 7 wana tatizo la usikivu na watoto wadogo na ndio sababu Hospitali ya Taifa ya Muhimimbiili walianzisha program ya kuweka kipandikizi kwa ajili ya kusikia ambayo tokea mwaka 2017 mpaka sasa watoto 57 wamekwisha kufanyiwa.

Alieleza kwamba watoto wengi wanakuwa na matatizo wakati wanazaliwa au wakiwa na umri mdogo wameona wakiwagundua mapema inasaidia kufuatilia kuona ni sababu zipi zinapelekea kuwepo kwa hali hiyo kwa watoto ili kuweza kuzuia lisiweze kujitokeza.