Mwanamume mmoja anahisi fahari kwa hatua yake ya kuwaoa wake wawili na familia hiyo inaishi kwa amani katika nyumba moja.
Wanawake hao wawili
wanaoshiriki mwanamume mmoja ni dada wa tumbo moja na wanaishi kwa amani katika nyumba moja
Mwanamume huyo amesema hapo
awali alikuwa ameoa mke wake wa kwanza kwa takriban muongo mmoja kabla ya kuoa
mwingine, dada ya mkewe.
Mukama Mugenimwana
alipendana na kuoa dadake Juliet, Namirembe Harriet, ambaye alikuwa akiwasaidia
kulea watoto wao.
Juliet alikuwa amemwomba
Namirembe kuwasaidia wenzi hao kutunza watoto wao wachanga alipojifungua mtoto
wake wa tano.
“Nimefurahi kuwa nao wote
wawili upande ingawa safari ya kuwaoa imekuwa ngumu, lakini mimi ni mume wa
kujivunia, na sina aibu kwa wake zangu.
Mke wangu wa kwanza, ambaye
tumeishi naye kwa takriban miaka 20, ana watoto 10 naye mke wangu wa pili ana
watoto wane.
Kwa miaka minne, Mukama kwa
kawaida alikuwa akimvizia Namirembe kutokana na urembo wake.
Baadaye alimeza chambo, na
Namirembe akapata ujauzito wa mwanamume huyo kutoka Uganda ambaye alisema
alikuwa na matatizo na mke wake wa kwanza.
"Tulikuwa na ugomvi
katika maisha yetu ya kila siku hapa nyumbani na hivyo ndivyo nilivyoishia
kushikana na dadake," Mugenimwana alijitetea.
Juliet alimshinikiza
Namirembe amwambie ni mimba ya nani naye akamwambia kuwa ilikuwa ya mumewe
Alikusanya virago vyake
akarudi nyumbani kwa wazazi ambao aliishi nao kwa muda.
Mugenimwana alilazimika
kumlipia mahari Namirembe ili awachukue dada wote wawili kama wake zake na
kusamehewa na wazazi wa dada hao.
Anaishi nao kwa amani na
inadaiwa ni mjamzito na vile vile anatazamia kupanua familia yake.
"Siri ya kuwapa raha wake zako ni
kugawana nao kila kitu kwa usawa katika nyumba, najaribu kuwaridhisha wake wote
wawili, ninawapa kila nilichonacho, nawapenda wote wawili, nafanya hivyo ili
kuepusha shida.
Sitaki vita. Sitaki hata
mmoja wao ahisi kutishiwa au kutothaminiwa," alisema.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.