Mwonekano kwa mbele..
Ngoma zilizomo.
Host wa kipindi cha Ala za Roho loveness Love on air clouds Tv...
Music live toka kwa wasanii uling'arisha usiku wa Ala za Roho...
Q. Chief aliachia new track usiku huo akimshirikisha mwanadada huyu pichani...ambapo vilevile kitu kilipigwa live
Best collabo la RnB..
Diva akisain OUT... kwa mujibu wake utamaduni huu wa live kupitia Clouds Tv sanjari na Clouds Tv hufanyika mara moja kila mwezi hivyo next tyme uskoseEee..
Wakati mshambuliaji wa Ivory Coast Didier Drogba ambaye ni 'supa staa' wa afrika akiwa uwanjani, mama yake anawapikia chakula mashabiki wa nchi yake katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, hii inadhihirisha wazi kuwa familia hiyo haichagui kazi bali yatumia kila nafasi ya kujipatia kipato inayojitokeza ndani ya jamii kama watu wengine.
Clotilde Drogba amefungua mgahawa karibu na uwanja wa mpira katika viunga vya mji mkuu wa Equatorial Guinea, Malabo, limeripoti shirika la habari la AP. Mama huyo anapika kuku na samaki na wali, ndizi na vyakula vingine kwa ajili ya mashabiki, wakati mwanaye akila chakula cha hoteli aliyofikia pamoja na wachezaji wenzake.
Mama yake Drogba pia alipika chakula kwa ajili ya mashabki wakati wa Kombe la Dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani.
Drogba ni mmoja wa watu maarufu sana nchini Ivory Coast, na mwaka jana alijumuishwa katika Tume ya Ukweli na Maridhiano iliyoundwa ili kupunguza mvutano uliotokana na utata wa matokeo ya uchaguzi na miaka mingi ya mgawanyiko.
Kundi la mashabiki wapatao 60 limesafiri kwenda Equatorial Guinea, ambapo Ivory Coast inacheza mechi zake za awali, na kila siku mashabiki hao wanapata chakula chao cha asili kilichopikwa na mama wa mshambuliaji wao mashuhuri.
Amesema ana imani ya kutazama mechi ya nusu fainali kwenye uwanja wa Bata - iwapo Drogba na timu yake watafuzu, anaheshimu sheria, na hiyo ina maana kuwa mwanaye hawezi kula chakula chake wakati huu - anatakiwa kula chakula cha hotelini tu kwa mujibu wa utararibu.
Shijani Mtunga meneja Villa Park.
Thomas Gikiro Meneja PSI Mwanza.
Abdalah Kijangwa
Zawadi nyingine ni Comlimentary ya kuhudhuria matukio muhimu Villa Park na usiku moja uliolipiwa katika hotel ya Gold Crest na mengine kibao... Chini ya Udhamini wa PSI, Tanzania Breweries LTD, Precision Air, Coca Cola NBCL, Gold Crest Hotel na Semira Electronics.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow akikabidhiwa rasmi mchango wa matairi 50 yaliyotolewa asubuhi ya leo na mfanyabiashara maarufu Zuri Nanji kwaajili ya makarandinga ya jeshi hilo.
Mfanyabiashara Zuri Nanji amesema kuwa msaada huo ni kielelezo tosha cha utendaji bora wa jeshi la polisi Mwanza na amesihi jeshi hilo kuendeleza sera yake ya ulinzi shirikishi.
Kamanda Barlow akikagua umadhubuti wa matairi hayo yenye jumla ya thamani ya shilingi milioni 20.
Sehemu ya maafisa wa jeshi la polisi walioshiriki makabidhiano hayo yaliyofanyika mbele ya ofisi za jeshi la polisi Mwanza.
Mfanyabiashara maarufu Josephat Musukuma (anayezungumza) alitoa shilingi milioni moja kwaajili ya mfuko wa magari ya doria ambayo yamekuwa yakikumbwa na kadhia ya kukwama kufika sehemu za matukio kutokana na uhaba wa mafuta sambamba naye Mfanyabiashara Riziki Mbise wa Kampuni ya Mambo ya Chinga Investiment (katikati) akikabidhi mchango wake wa milioni moja taslimu kwa katibu wake wa mfuko wa wafanyabiashara kwenda kwa jeshi la polisi.
Kamanda wa kikosi cha Doria na Ulinzi shirikishi Philip Karage akitoa shukurani kwa mchango huo.
'KITU KASHATA MMmma' ni karandinga lililofungwa tairi zote mpya.
Naye mfanyabiasha Rashid alitoa lita 400 za mafuta kwaajili ya vyombo vya doria, msaada huo utalinusuru jeshi la polisi na aibu ya makarandinga yake na pancha za mara kwa mara wakati wa safari zake pamoja na kukwama kutokana na uhaba wa mafuta.
Brogu hii ya jamii http://www.gsengo.blogspot.com/ hivi karibuni ilialikwa kuhudhuria uzinduzi wa jukwaa la Wanamabadiliko, Safari ilianza kuelekea Rubondo National Park mahala palipo chaguliwa kwa tukio.
Kisiwa cha utalii Rubondo kina visiwa vyake vidogovidogo na hiki ni moja wapo yaani ni 'full green' mwaka mzima.
Wanamabadiliko walitia nanga hapa mara baada ya safari yenye misukosuko ya takribani saa mbili.
Kaunta ya bar iliyotengenezwa mithili ya mtumbwi.
Safari ya Wanamabadiliko kuelekea sehemu za mapumziko..
Ajabu-Njiani tulimwokota samaki huyu fresh aina ya sato akiwa ameliwa macho yote na ndege.
Swali ni kwamba kwanini aliliwa macho tu?
Kuna vyumba vya hotel lakini nilichaguwa kujipumzisha humu.
Kutoka kushoto ni Mwanamuziki Ismail, CEO wa blogu hii, Fred Katulanda na Richard Mabala.
Mti ndani ya maji uliojaa vichale vya ndege...
Mwanamabadiliko Wilhelmin aka Masai akiota moto ndani ya night kali'
Nyama choma zilichomeka kinoma noma...
Kisha baadaye msosi hapa ilikuwa mishale ya saa saba hivi mara baada ya uzinduzi wa Jukwaa la Wanamabadiliko.
Msosi na 'fulu sevisi mboga saba kujisevia...'
Niasubuhi tena mapemaaa.. na atuamshaye hapa ni Katibu wa jukwaa F. Katulanda kwa ajili ya safari kurejea 'mAhOmU' nakumbuka Usiku tuliinjoi kweli sauti za Hipopotamus kula nyasi pembezoni mwa tents na ngurumo zao.
Wanamabadiliko wakiongozwa na mr. Katulanda (C) wakipata flash nyuma yao mmeona lakini....
Taswira ndiyo hii...
Safari imeiva, bai bai kisiwa cha Rubondo.
Ni askari wa hifadhi hii aliyetupa eskoti kuhakikisha tunafika salama.