ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 31, 2012

SAFARI YA WANAMABADILIKO KISIWA CHA UTALII RUBONDO

Brogu hii ya jamii http://www.gsengo.blogspot.com/ hivi karibuni ilialikwa kuhudhuria uzinduzi wa jukwaa la Wanamabadiliko, Safari ilianza kuelekea Rubondo National Park mahala palipo chaguliwa kwa tukio.

Kisiwa cha utalii Rubondo kina visiwa vyake vidogovidogo na hiki ni moja wapo yaani ni 'full green' mwaka mzima.

Wanamabadiliko walitia nanga hapa mara baada ya safari yenye misukosuko ya takribani saa mbili.

Kaunta ya bar iliyotengenezwa mithili ya mtumbwi.

Safari ya Wanamabadiliko kuelekea sehemu za mapumziko..

Ajabu-Njiani tulimwokota samaki huyu fresh aina ya sato akiwa ameliwa macho yote na ndege.

Swali ni kwamba kwanini aliliwa macho tu?

Kuna vyumba vya hotel lakini nilichaguwa kujipumzisha humu.

Kutoka kushoto ni Mwanamuziki Ismail, CEO wa blogu hii, Fred Katulanda na Richard Mabala.

Mti ndani ya maji uliojaa vichale vya ndege...

Mwanamabadiliko Wilhelmin aka Masai akiota moto ndani ya night kali'

Nyama choma zilichomeka kinoma noma...

Kisha baadaye msosi hapa ilikuwa mishale ya saa saba hivi mara baada ya uzinduzi wa Jukwaa la Wanamabadiliko.

Msosi na 'fulu sevisi mboga saba kujisevia...'

Niasubuhi tena mapemaaa.. na atuamshaye hapa ni Katibu wa jukwaa F. Katulanda kwa ajili ya safari kurejea 'mAhOmU' nakumbuka Usiku tuliinjoi kweli sauti za Hipopotamus kula nyasi pembezoni mwa tents na ngurumo zao.

Wanamabadiliko wakiongozwa na mr. Katulanda (C) wakipata flash nyuma yao mmeona lakini....

Taswira ndiyo hii...

Safari imeiva, bai bai kisiwa cha Rubondo.

Ni askari wa hifadhi hii aliyetupa eskoti kuhakikisha tunafika salama.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.