ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 29, 2016

MAFUNZO YA MPIRA WA KIKAPU KWA WATOTO NA VIJANA YAANZA KATIKA UWANJA WA MPIRA WA KIKAPU KILOLELI MWANZA

Chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Mwanza (MRBA) kupitia Kamisheni yake ya Watoto, Vijana na maendeleo ya shule kwa kushirikiana na shirika la kijamii linalojishughulisha na michezo, Planet Social Development (PSD) na timu ya Mwanza Eagles tunaendesha mafunzo ya mpira wa kikapu kwa watoto na vijana katika uwanja wa mpira wa kikapu Kiloleli ambayo yatakuwa yakifanyika kwa siku za jumamosi saa 2 asubuhi, Jumanne na Alhamis kuanzia saa kumi jioni.

Kwa kushirikiana na Kocha Amin Musira ambaye ni kocha wa muda mrefu hapa Mwanza, tumeanza kufundisha watoto hawa wanaotoka/wanaishi maeneo ya karibu na uwanja huu na pia wanaosoma katika shule za msingi za Pasiansi, Kilimani, Kiloleli, Hekima na Muungano na pia shule za Sekondari Kiloleli, Nyamanoro, Pasiansi, Kilimani na zingine zilizo karibu na uwanja huu.

Tumeanza na utaratibu huu kwa sababu watoto hawa wataweza kufika uwanjani bila kutumia usafiri wa gari kwa maana ya nauli kitu ambacho kimekuwa kikwazo kikubwa kwa watoto kufika katika viwanja vya mbali na wanapoishi. Na bahati nzuri ni kwamba uwanja huu upo katikati ya makazi ya watu na ndio sahihi kwani watoto wataweza fika uwanja masaa yote wapatapo nafasi mara baada ya muda wa masomo na shughuli za nyumbani.

Mafunzo haya yanalenga kuibua vipaji vya watoto hawa na kuwaendeleza katika mchezo huu ili tuweze kurudisha mchezo huu katika hadhi yake kama ilivyokuwa awali katika mkoa wa Mwanza na Tanzania kwa ujumla.

Pamoja na kutambua, kuibua na kuendeleza vipaji vya watoto katika mchezo huu, pia washiriki watapata nafasi ya uelewa kuhusu masomo na michezo na pia michezo na afya ili waweze kusoma kwa bidii na kuwa na afya njema wakati wote. Pia tuna mpango wa kufundisha makocha (walimu) kutoka katika shule za msingi na sekondari za hapa Mwanza ili watoto hawa waweze kupata nafasi ya kujifunza katika vipindi vya michezo wawapo shuleni.

Katika kufanikisha mafunzo haya vizuri, bado tunahitaji kupata vifaa mbalmbali ikiwepo mipira angalau 50 kwa kuanzia, cone, sare/jezi na dawa za huduma ya kwanza.

Hivyo, tunawakaribisha na kuwaomba wadau wajitokeze katika kusaidia kufanikisha mafunzo haya kwa kutoa mahitaji mbalimbali yanayoitajika. Kwa yeyote mwenye kuweza kutupatia vifaa vinavyoitajika afike katika ofisi ya Utamaduni na Michezo ya Manispaa ya Ilemela aonane na Afisa michezo ambae ndie mratibu wa mafunzo haya au afike shule ya msingi Nyanza aonane na Kaimu mwenyekiti wa MRBA Ndg. Juvenile Kaiza ambaye ni mwalimu mkuu wa shule hii ama afike uwanjani Kiloleli.

Imetolewa na:

Kizito Sosho Bahati
Mratibu wa Mafunzo

0764 993 000/0784 970 235

VIONGOZI WA SIASA,WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUWATHAMINI WALEMAVU

 Kaimu katibu  mkuu wa UVCCM taifa Shaka Hamdu shaka akiwa anapokea risala kutoka kwa moja wa mwanafunzi  mlemavu wa viungo.


 kaimu katibu mkuu akiwa anaangalia jinsi mtoto ambaye ni mlemavu  wa akili alivyoandika katika karatasi yake


 mmoja wa mtoto ambaye ni mlemavu wa viungo akiwa anasoma risala fupi mbele ya mgne rasmi


 mkuu wa shule ya msingi  Mreyai  Nuruel Laizer akiwa anampa maelekezo ya ujenzi wa choo cha watoto wenye ulemavu kaimu katibu mkuu wa UVCCM taifa


 kaimu katibu mkuu wa UVCCM  taifa akiwa anakata mti tayari kwa kupanda katika shule ya watoto wenye ulemavu



 kaimu katibu mkuu wa uvccm taifa shaka hamdu  shaka akiwa amembeba mmoja ya mtoto mwenye ulemavu wa akili
 Na Woinde  Shizza, Rombo
Viongozi wa kisiasa, wafanyabiashara, viongozi wa kiserikali na wafanyajazi
wametakiwa kuwajali na kuwathamini sana watoto  wenye ulemavu na wanaoishi
kwenye mazingira magumu kwani wao pia  ni binadamu wanao sitahili kupata
haki na mahitajj muhimu ya kibinadsmu
Hayo yamebainishwa na leo na kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu
Shaka wakati alipotembelea shule ya msingi Mreyai iliyopo wilayani Rombo
mkoani Kilimanjaro yenye jua huduma watoto wenye ulemavu wa viungo na MTI
ndio wa akili.
Alisema kuwa ni muhimu kuwajali sana watoto wenye ulemavu kwani
wakitengenezwa vizuri na kuandaliwa vizuri kwa kupewa elimu  watakuwa
viongozi wazuri wa baadae.
Aidha alivitaka vyama Vya siasa vijielekeze kutatua changamoto na ma tatizo
ya watoto ambao ni Walemavu na sio kuendeleza Kufanya siasa ata sehemu
ambayo aitakiwi siasa.
"napenda kuviambia vyama vingine vya siasa sasa ivi uchaguzi imeisha ni
kipindi cha kufanya kazi na kuachana na siasa sasa ivi ni kipindi cha
kufanya kazi na kutatua ma tatizo ya wananchi " alisema Shaka.
Kwa upande wa Mkuu wa shule ya msingi Mreyai, Nuruel Laizer alisema kuwa
shule hiyo inahudumia wanafunzi wenye Mtindio wa akili na wanafunzi ambao
ni walemavu wa viungo ambapo alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa chakula cha wanafunzi, ukosefu
wa vitanda na mgodoro ya kulalia Wanafunzi ambao ni walemavu ,baskeli kwa
ajili ya watoto ambao ni walemavu wa miguu.
Alisema kuwa Wanafunzi hao wanakaa katika ma bweni apo shule ni lakini
wanaupungufu mkubwa wa vitanda na mgodoro  kwani vitanda ambavyo wana vitu
mia wameviazima kutoka kwa watu na mda wowote wenyewe wanaweza kuja
kuchukuwa.
Aliomba serekali pamoja na wadau mbalimbali kujitokeza kuwasaidia kitu icho
ili watoto hao waweze kuishi kwa amani na furaha kama watoto.
"watoto hawa wanawazazi lakini wazazi hao hawana uwezo na ndio maana wa me
wamewaleta Hapa ili wapate elimu hivyo tu naomba sana serekali na wadau
mbalimbali wajitokeze kutusaidia"alisema laizer
Shule hii ya msingi Mreyai imepata msaada wa chakula, maharage, malindi,
sabuni, mafuta, miswaki na kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu
Shaka aliaidi kusaidia shule hii vitanda Nane na mgodoro kwa ajili ya
wanafunzi hawa wenye ulemavu wa viungo pamoja na Mtindio wa ubongo.
kaimu katibu mkuu wa uvccm taifa akiwa anaongea na wanafunzi wa shule ya msingi Mreyai



mkuu wa shule ya msingi Mreyai Nuruel Laizer  wa kwanza kushoto akifuatiwa na mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa kilimanjaro Juma Rahibu Juma akifuatiwa na kaimu  katibu mkuu UVCCM taifa katika makabidhiano ya baadhi  ya msaada ambao ulipelekwa shuleni hapo


 kaimu katibu mkuu akiwa na wanafunzi
 Omary ngwanangwelu akiwa anasalimiana na mmoja wa mtoto ambaye ni mlemavu wa akili

NICO NJOHOLE NA RENATUS NJOHOLE WAWASILI DALLAS, MTANANGE WA SIMBA NA YANGA JUMAMOSI

Renatusi Njohole akiwa katika picha ya pamoja na kaka yake
 Benchi la ufundi la Yanga Bwn. Gerry Mshana(kulia) akipata picha ya kumbukumbu na Nico Njohole siku ya Alhamisi Dallas, Texas. Nico na Renatus wamekuja maalum kuhudhuria mkutano wa DICOTA na kuchezea Simba kwenye mtanange wa watani wa jadi.
  Kutoka kushoto ni Gerry Mshana, Mary Maswanya (dada mkubwa wa Nico na Renatus), Renatus, Nico na Rais wa DICOTA, Ndaga Mwakabuka walipopata picha ya kumbukumbu. 
 Rais wa DICOTA Bwn. Ndaga Mwakabuta akiwa katika picha ya pamoja Nico na Renatus
 Kutoka kushoto ni Jerry, Nico, Ndaga Mwakabuta, Renatus, na Gerry Mshana wakiwa kwenye picha ya pamoja

WANANCHI JIJINI MBEYA WAJITOKEZA KUPATIWA DAWA ZA KINGA TIBA KWA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Nyilembe Munasa akitoa Dawa za kinga tiba kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa wananchi wa Jiji la Mbeya katika eneo la kituo cha Mabasi madogo(Daladala)Kabwe April 29 -2015 mara baada ya kuzindua rasmi .

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyilembe Munasa akiongoza zoezi la ugawaji wa Dawa za kinga tiba kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ,Magonjwa hayo ni Minyoo ya Tumbo,Matende ,Ngirimaji na Usubi, ambapo dawa hizo zinatolewa kwa wananchi wote kuanzia miaka Mitano (5)na kuendelea .


Wananchi eneo la kwabwe jijini Mbeya  stendi wakisubiri kwa hamu kupatiwa dawa za kinga tiba kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ambapo zoezi hilo linatarajiwa kuanza rasmi mei 2 hadi 5 mwaka huu .Picha EmanuelMadafa,Jamiimojablog-Mbeya .

SSS

UVCCM : SUMAYE ACHA KUMBUGHUDHI DR. MAGUFULI.

Na Woinde Shizza, Kilimanjaro
Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi umemtaka Waziri mstaafu Frederick Sumaye hana vigezo wala sifa zozote zinazoweza kumfanya awe na uwezo wa kumkosoa Rais Dk John Magufuli katika uendeshaji wa serikali na masuala ya utawala. 

Sumaye ametakiwa amuache Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Magufuli ili atimize majukumu yake kwasababu alipewa dhamana ya kuwa Waziri mkuu lakini hajufikia hata thukuth ya utendaji unaofanyika sasa.   

Msimamo huo umetolewa jana na Kaimu katibu mkuu wa uvccm shaka hamdu shaka alipokuwa akizungumza na wanachama wa ccm wa kata mbili za kwandele na mbichi jimbo Rombo mkoani kilimanjaro.

Shaka alisema anachokifajya sumaye na baadhi ya wanasiasa muflis wanaojaribu kukosoa utendaji katika utawala wa serikali ya awamu ya tano ni kutaka nao wasikike wakidhani yale walioyafanya wakati wakiwa madarakani wananchi wameyasahau. 

Alisema kama yupo waziri mkuu ambaye ameonyesha udhaifu katika  utendaji na usimamizi wa serikaki huku akishindwa kumsaidia Rais hakuna atakayempita Sumaye. 

"Amekuwa waziri mkuu kwa miaka kumi kuliko waziri mkuu yeyote na kwa bahari mbaya sana ndiye waziri mkuu zero kuliko mwingine yeyote tokea tupate uhuru mwaka 1961 "alisema shaka. 

Aidha Kaimu huyo katibu mkuu alimuonya sumaye akimtaka aache kumfuatafuata Dk Magufuli katika mikakati yake ya kutumikia nchi na juhudi anazichukua dhidi ya mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma nchini. 

Alisema wakati Rais Magufuli akiwa katika dhamira njema na nia ya wazi iuwatumikia wananchi kwa uadilifu, uaminifu na heshima alisema  kina sumaye na wenzake  wafumbe midomo yao na waache mara moja kumbughudhi Rais kwa ajili ya kusaka umaarufu wa kisiasa. 

"Sumaye aacha kufuatafuata Rais na kujifanya unajua wakati mambo yalikushinda wakati ukiwa PM, kama huna maneno ya kusema rudi Hanang ukalime maharage na karanga "alisema

Pia shaka aliwataka wananchi wa jinbo la Rombo kujitatayarisha ili kumpiga chini mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya chadema Joseph Selasini kwasabahu ni dhaifu na hatoshi kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.

"Siku zake za kuitwa mbunge wa Rombo sasa zinahesabika, selasimi hajui anavhokufanya wala hajali shida na matatizo yaliopo katika jimbo lake,lazima adui huyo apigiwe mwaka 2020 "alisisotiza shaka 

Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti wa uvccm mkoa wa kilimanjaro Juma Raib Juma aliwakanya wananchi wa kanda ya Kaskazini kuacha mara moja tabia ya kushiriki na kuchagua vyama na wagonbea wa nafasi mbali mbali kwa ukabila, ujimbo au nasaba. 

Raibu alisema ikiwa wananchi wa kaskazini sasa wanaishi katika Mikao yote ya Tanania, si jambo la maana wao wakahesabiwa kama ni wabaguzi kwa misingi ya asili au ujamaa. 

"Tunachotaka kukisafanya baadhi ya wananchi wa Mikao ya Kaskazini ni kumuasi baba wa Taifa marehemu Mwalimu julius Nyerere, haiutuacha tukiwa tumegawahyika  , tumeishi miaka yote hatukuongozwa kwa ukabila au udini, chadema acheni kwasabahu hilo ni baa au janga katika jamii "alisema Raib. 

Jumla ya wananchi wapya 103 wa ccm na jumiya zake walijiunga na chama cha mapinduzi pia shaka alipata nafasi ya kuangalia mechi ya soka kati ya timu za kata za makiidi na mahare wilaya Rombo.

Thursday, April 28, 2016

WANANCHI WA ITOBO, ITIRIMA - SIMIYU WAASWA KUZAA KWA KUFUATA UZAZI WA MPANGO

Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu mapema wiki iliyopita. Elimu hiyo ya uzazi wa mpango iliendana na huduma ya upimaji wa afya ikiwa ni pamoja na kutoa huduma ya uzazi wa mpango. Picha/Video na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu wakipatiwa elimu ya uzazi wa mpango.

--- Na Cathbert Kajuna - Itirima, Simiyu. 

 Wananchi wa Kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu wameaswa kuachana na mila za kuzaa watoto wasio kuwa na idadi ili kuepusha taifa lenye wategemezi wengi.

 Akizungumza katika mafunzo ya Uzazi wa Mpango yaliyotolewa wiki iliyopita na Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena alisema kuwa kuna haja ya wazazi hasa waishio vijinini kuacha dhana ya kuzaa ovyo kama wanyama bila mpangilio jambo linalowafanya kuendea kuwa maskini.

Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima. 
 "Nawaasa wananchi wa Kijiji cha Mitobo kuache mila potofu za kuzaa kila mwaka mimba kila mwaka mtoto maana mtakosa kuwa na maendeleo, nnakuta mtu anawatoto 10 - 15 jambo linalopelekea kuwa omba omba kwa vile atashindwa kuwahudumia," alisema Meena.

 Bi. Meena aliwashukuru wananchi wa Kijiji cha Mitobo kwa kuweza kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya uzazi wa mpango. 

 Akiongea mara baada ya kumaliza mafunzo hayo Bi. Ester Meena alisema kuwa muitikio wa wananchi katika kupata elimu ya uzazi wa mpango umekuwa mkubwa jambo linaloleta faraja kwa vile linaweza kupunguza idadi ya watu.

HIVI NDIVYO MWILI WA PAPA WEMBA ULIVYOPOKELEWA DRC.

Maelfu ya watu wamekusanyika leo nje ya uwanja wa ndege wa Kinshasa kuupokea mwili wa mwanamuziki Papa Wemba uliowasili nchini humo kutoka Abidjan
Mwanamuziki huyo ambaye ametajwa kuwa mmoja ya waanzilishi wa muziki wa kizazi kipya cha Soukous anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne baada ya mwili huo kuwekwa katika uwanja wa mpira kwa raia kutoa heshima zao za mwisho.
Mjane wa marehemu, Mama - Marie Lozolo Amazone akisaidiwa na baadhi ya wanafamilia wake pamoja na maafisa kadhaa wa Serikali wakati akiwasili mjini Kinshansa. 
 Maafisa wa serikali na wanadiplomasia watahudhuria ibada ya kumkumbuka mwanamuziki huyo katika uwanja wa ndege kabla ya mwili huo kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Maelfu ya watu wamekongamana nje ya uwanja wa ndege wa Kinshasa kuupokea mwili wa mwanamuziki Papa Wemba uliowasili nchini humo kutoka Abidjan
Hata eneo la daraja kuu mjini humo lilijaa umati mkubwa almuradi tu kutoa heshima zao kwa mwili wa mwanamuziki Papa Wemba uliowasili nchini humo kutoka Abidjan
Mwili wa Marehemu Papa Wemba umepokelewa pia umati mkubwa wa wanamuziki wengine wakiwa sehemu ya kamati ya mazishi ya nyota huyo Nyoka Longo, Malaika Munan, Koffi olomide, Werra son, Tshala Muana, Fally Ipupa na jamaa aliyekuwa swahiba mkubwa wa Papa Wemba mwanamuziki Reddy Amisi.
Kwa mujibu wa mmoja wa wasemaji wa Familia, amesema kuwa Papa Wemba alikuwa nje ya shughuli za muziki wa majukwaa kwa kipindi kirefu akipata matibabu mjini Paris kabla ya afya yake kutengemaa na hatimaye kuhudhuria tamasha kubwa la Burudani huko Abijan. Kifo chake kimeleta mshtuko kwa wengi. 
Mkongwe mkali mwingine aliyefanya kazi kipindi kirefu na Papa Wemba kwa karibu Nyboma Mwandidi katika zama hizi za kuelekea kuusitiri mwili wa rafiki yao ili kumuenzi wamepanga kuvaa kama alivyopenda kuvaa nguli huyo aliye tangulia mbele za haki.  
“We want to celebrate what Papa Wemba was known to promote in terms of attire and music,” he said.
Similar gatherings will be held in London, Brussels and Nairobi led by promoters JC Motindo and Jules Nsana, and Ms Paulin Wanga, a fan.
Tamasha la bure la usiku kucha lilifanyika mjini Abidjan ambapo mwanamuziki huyo alianguka alipokuwa akiimba. Mwanahabari wa BBC Tamasin Ford anasema kuwa mashabiki wengi walivalia nguo nyeusi na kubeba mishumaa ili kutoa heshima kwa nguli huyo wa muziki.

PICHA ZOTE NA http://news.abidjan.net/

YALIYOJIRI BUNGENI


Mhe.Shangazi aihoji serikali juu ya kurejesha silaha kwa wananchi waliopokonywa silaha wakati wa oparesheni tokomeza;  


Mhe.Mwita aitaka serikali kusimamia wakandarasi kuhakikisha wanajenga mifereji mikubwa katika barabara zote ili kuzuia mafuriko;  


Mhe.Kuchaukaa aihoji serikali juu ya utekelezaji wa sera ya ujenzi kama alivyoahidi rais Magufuli katika kampeni; 


Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa atoa ufafanuzi juu ya kukabiliana na balaa la njaa kwa wananchi wa Igunga waliokubwa na mafuriko. 

GSM FOUNDATION NA MOI WAANZA KAMBI ZA UPASUAJI BUGANDO.

 Na Mwandishi Wetu
Jumla ya watoto 120 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza, kufuatia tatizo la kichwa kikubwa walilozaliwa nalo chini ya udhamini wa taasisi ya GSM ambayo imedhamini zoezi hilo litakalofanyika katika mikoa mitano ikiwa ni awamu ya kwanza kati ya nne zinazotarajiwa kufanyika tanzania nzima. 

Akiongea na waandishi wa habari katika uzinduzi wa zoezi hilo linalojumuisha madaktari Bingwa 10 kutoka Taasisi ya mifupa na Upasuaji MOI, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Profesa Kien Mteta aliishukuru taasisi ya GSM kwa kuamua kulichukua tatizo hilo ambalo ameliita kuwa ni kubwa ukilinganisha na jinsi linavyochukuliwa na jamii ya watanzania.

Dk Kien aliwaambia wanahabari kwamba jumla ya watoto 2000 huzaliwa na vichwa vikubwa katika kanda ya Ziwa peke yake, na mtaalamu wa kuhudumia wagonjwa wa namna hii ni mmoja tu ambapo pia kwa Tanzania nzima, wataalamu wa upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa wako tisa tu.

Cha kusikitisha ni kwamba kati ya hao, ni wachache sana hurudi kwa ajili ya matibabu bali wengi wao hufariki kwa kufichwa ndani na wazazi wao aidha kwa imani za kishirikina ama kushindwa kwa wazazi kumudu gharama za matibabu.

PICHANI JUU: Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Profesa Kien Mteta(kushoto) akiongea na wanahabari huku akisikilizwa kwa umakini na Halfan Kiwamba(kulia) na Mkurugenzi wa taasisi ya Mifupa na upasuaji Dk Othman Kiloloma(katikati)

 Mtaalamu wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya Fahamu, Dk Gerald Mayaya akitoa ufafanuzi kwa wanahabari kuhusiana na kambi ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa katika Hospitali ya Bugando
 Meneja Mkuu wa taasisi ya GSM, Shannon Kiwamba (katikati) akiongea na wanahabari kuhusiana na sera yao mpya ya kusaidia watanzania katika masuala ya elimu na Afya, kulia kwake ni Mkuu wa Hospitali ya Bingando, Prof Kien Mtena na kushoto kwake ni Mkuu wa mawasiliano wa Taasisi ya GSM, Halfan Kiwamba
 maelezo ya ufafanuzi yakiendelea kutolewa na Halfan Kiwamba(Wa pili kutoka kushoto) kutoka GSM Foundation
 Mkuu wa kitenngo cha Upasuaji na Mifupa ambaye ndio mratibu wa kambi ya tiba ya watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi akifafanua jambo kwa wanahabari(hawapo pichani)
 Baadhi ya wahudumu wanaoshiriki kambi ya watoto wenye vichwa vikubwa wakisikiliza viongozi wao wakatiwakiongea na wanahabari
 Wanahabari kazini

 Ufafanuzi ukiendelea...
 Picha ya pamoja ya wawezeshaji wa zoezi la kambi ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi 
 Mkuu wa Hospitali ya Bingando, Prof Kien Mtena (kulia) katika picha ya pamoja na mwanahabari wa Jembe Fm Mwanza G. Sengo.
Taarifa kwa umma kupitia mabango ya Hospitali ya Rufaa Bugando.