ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 5, 2009

NEWS KWA WIKI MARA MOJA.



MAGAZETI YA ROCK CITY YANATOKA KIMACHALE MARA MOJA TU KWA WIKI KILA GAZETI NA SIKU YAKE.. KIZURI NI KWAMBA YAMESHEHENI HABARI ZA NGUVU. KASI MPYA NA KURUGENI WAKE BWANA MASATU.

NIMEPAMIS HOME



NIMEFIKA HOME SIKUKUTA MTU ZAIDI YA MAJIRANI.... MAMDOGO AMEKWENDA HOSPITAL KUPATA MATIBABU, NIKATUA MZIGO WANGU NA MAJI YANGU NILIYONUNUA SAFARINI ATUA KUMI NA TANO NAITIZAMA NYUMBA NATATHIMINI:- UOTO WA ASILI WA MAJANI MABICHI, HALI NZURI YA HEWA ISIYO HITAJI FENI WALA KIYOYOZI, NG'OMBE WA MAZIWA, MITI MIZURI IZUNGUKAYO MAZINGIRA YA NYUMBA, MITI YENYE MATUNDA YA KILA AINA, MIGOMBA YENYE KUTOA NDIZI KISUKARI, NDIZI MSHALE, NDIZI MAKUNDUU, NDIZI LAINI AAAAH! NA NYINGINE NYINGI NIMEZISAHAU KWASABABU YA KUISHI KIPINDI KIREFU MBALI NA HOME. WHERE IS MAMA MDOGO ANIPE MICHAPO? AAAH! WACHA NIMSUBIRI

Friday, September 4, 2009

ROCK CITY JIONI YA LEO.

NI MAJIRA YA JIONI JUA LINAZAMA WENGI WANATOKA KUCHUMA JUANI KUELEKEA KIVULINI PA MAAKULI, KTK KIPINDI HIKI CHA MWEZI WA TOBA NAPENDA KUWATAKIA KILA KHERI HAPA NAMAANISHA RAMADHANI NJEMA KWA NDUGU ZANGU WOTE WAISLAMU. KAKA MICHUZI JR. UPO?

MWANZA MWANZA!! BAKWINE!!!!!!!!!

SI SAMAKI WATAMU PEKEE BALI HATA MAANDARI TULIVU NA UPEPO MWANANA WA ZIWA VICTORIA VYOTE HIVYO VITAKUFANYA SOMETIMES UPAMIS HOME.

MAONESHO YA NNE YA BIASHARA MWANZA.




MAONESHO HAYA YA BIASHARA YA AFRIKA MASHARIKI YALIYOFANYIKA JIJINI MWANZA NA KUMALIZIKA HIVI KARIBUNI YALIANZA RASMI TRH 14 HADI 26 AUGUST 2009. MAONESHO HAYO YALIYOFUNGULIWA NAYE NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA, BW. CYRIL CHAMI NI MAONESHO YA NNE LAKINI KASI YAKE KTK MAENDELEO 120. WAANDAAJI TANZANIA CHAMBER OF COMMERCE INDUSTRY AND AGRICULTURE (TCCIA MWANZA) HAMNA BUDI KUPONGEZWA.

KILIMO KWANZA



KWA WALE NDUGU ZANGU TUNAOISHI TOWN AMINI TUNAWEZA KULA MBOGA KWA KUPITIA SHAMBA LA STYLE HII. UBUNIFU HUU NILIKUTANA NAO NDANI YA MAONESHO YA NNE YA BIASHARA VIWANDA NA KILIMO TCCIA YALIYOFANYIKA VIWANJA VYA SABASABA ILEMELA JIJINI MWANZA.

KIBO SEEDS MSHINDI WA JUMLA 2009.





MAONESHO YA NNE YA KIMATAIFA YA VIWANDA,BIASHARA NA KILIMO YALIYOMALIZIKA HIVI KARIBUNI JIJINI MWANZA YAMELETA CHANGAMOTO KUBWA KATIKA SUALA ZIMA LA MAENDELEO NCHINI. KWA WALIO TEMBELEA ENEO LA KIBO SEEDS ''KWELI KILIMO KWANZA PAMOJA TUNAWEZA''

WALA MJOMBA HAJAPOTEA!

KUNA TANGAZO MOJA LA MTANDAO WA SIMU LA JAMAA SAFARINI AKAENDA KUCHIMBA DAWA mara BASI LIKAMWACHA bahati nzuri SIMU IKAMSAIDIA. TEHE!! PICHANI NI POZI TU LA MJOMBA HAPA AKIOTA JUA LA ASUBUHI LENYE VITAMINI D, POLENI SANA NDUGU ZANGU MKURUPUKAO ALFAJIRI KWENDA KAZINI NAKUJIFUNGIA KWENYE OFISI ZENU ZENYE FULL AC MPAKA MACHWEO...

Thursday, September 3, 2009

LIVE NDANI YA SRAR TV.



SHINDANO LA WALEMAVU MUSIC STAR SEARCH NDANI YA STAR TV LIMEPAMBAMOTO WASHKAJI WANAKAZA ILE MBAYA!!. KAMA VIPI JUMAMOSI SAA 5USIKU NA MARUDIO JUMAPILI SAA 7MCHANA. HOPE IMEKAA NJEMA.....

KILA SIKU ZA WIKI NI MIKIKI MIKIKI!

NILIKUWA KIMYA KITAMBO BUT NOW AM BACK TIME HII SINTOKUANGUSHA SHABIKI WANGU...... "HOPE UKO NAMI MZAZI KAMA KUKU NA MAGOYA""

UMEONA NINI?



CHUNGUZA HIZI PICHA HATUA KWA HATUA KISHA NAMBIE UMEONA NINI? PICHA HII IMECHUKULIWA KATIKATI YA BARABARA YA NYERERE JIJINI MWANZA KWA KUKUSAIDIA ILIKUWA NI KATIKA MSAKO WA WAENDESHAO PIKIPIKI BILA KOFIA MAALUM (HELEMENT). CHUNGUZA MJOMBA UTABAINI....

GARI LA PAPA JOHN PAUL WA PILI



GARI HILI LILIMCHUKUA BABA MTAKATIFU YOHANA PAULO WA PILI TAREHE 3 HADI 4 SEPT 1990 MWANZA. KWA NCHI ZILIZOENDELEA USAFIRI KAMA HUU UNGEHIFADHIWA KAMA KUMBUKUMBU LAKINI KIBONGOBONGO GARI HILI LIKO BARABARANI. TUTAFANYAJE!

SAA NANE ISLAND


,
PICHA YA KWANZA JUU KAUNTA YA BAR ENEO LA MAPUMZIKO, BAR AMBAYO IKO MBIONI KUBOMOLEWA KISHA KUJENGWA UPYA KITALII ZAIDI PICHA INAYOFUATA NI KORIDO KATIKA MWAMBA MAHALA AMBAPO UNAPOWEZA KUSIMAMA NAKUJIONEA MAANDALI YA USO WA DUNIA, CHINI NI MOJA YA MAENEO YA MBELE. HABARI NI KWAMBA:- KISIWA HIKI KIKO KATIKA UKARABATI MZITO, AWALI KILIKUWA KIKISIMAMIWA NA GAME HIVI SASA KINAMILIKIWA NA TANAPA.

HAKIKA HUU NDIYO UZALENDO BUTIAMA HADI MWANZA KWA MGUU SI MCHEZO!


HATUA KADHAA (kama 50 za miguu) KUTOKA ENEO LA MAKABURI YA MV BUKOBA KUNA SEHEMU YA KIHISTORIA ENEO AMBALO BABA WA TAIFA JK. NYERERE ALIPO PUMZIKA BAADA YA KUTEMBEA KWA MIGUU KUTOKA BUTIAMA HADI MWANZA KUUNGA MKONO AZIMIO LA ARUSHA MWAKA 1967. MNARA HUU ULIKUJA KUJENGWA HIVI MAJUZI KUHAKIKISHA ENEO HILI LINAKUMBUKWA. NINA MASWALI MAWILI, JE! ENEO HILI LITATUNZWA? JE! WADAU WANATUMIA NJIA GANI KULITANGAZA KAMA SEHEMU YA HISTORIA? NI HAYO TU!!!!!

MV. BUKOBA


HII NI FAMILIA YA ALIYEKUWA MLINZI NA MFANYA USAFI WA ENEO LA MAKABURI YA MV. BUKOBA LILILOKO IGOMA JIJINI MWANZA, BW. ABEL (katikati mwenye shati ya pinki). MLINZI HUYU ALIPOKEA BARUA KUSIMAMISHWA KAZI BILA MALIPO YOYOTE MIAKA MIWILI ILIYOPITA MARA BAADA YA KUFANYA KAZI MIAKA KUMI NA MBILI TANGU 1996. MARA BAADA YA HATUA HIYO HAKUNA HATUA ZOZOTE ZILIZOFUATA. KWA SASA ENEO HILI LIMETELEKEZWA HALINA MLINZI WALA MFANYA USAFI. JE! NIA YA SERIKALI YA KUTUNZA MAENEO KAMA HAYA KUWA SEHEMU YA HISTORIA KWA WATALII SANJARI NA KUMBUKUMBU KWA VIZAZI VYETU VIJAVYO ITAFANIKIWA?

ENEO LA MAKABURI YA MV BUKOBA




HII NDIYO HALI YA SASA YA ENEO LA MAKABURI YA WATU WALIOKUFA MAJI KWENYE AJALI YA MV BUKOBA ILIYOZAMA KWENYE ZIWA VICTORIA TAREHE 21 MEI 1996. SIKU NATEMBELEA ENEO HILI NIKIWA NA ALIYEKUWA MLINZI NA MFANYA USAFI WA MAKABURI HAYA ALIYE SIMAMISHWA KAZI MIAKA KADHAA ILIYOPITA TULIJITOLEA KUSHIRIKI KTK USAFI WA KUNG'OA MAJANI IKIWA NI ISHARA YA SALA KWA NDUGU ZETU WALIOKUFA. KIASI LIKAWA LINATIZAMIKA. SERIKALI YA MKOA MKO WAPI?

TASWIRA YA TAIFA



BANGO LA ENEO LA MAKABURI YA WATU WA AJALI YA MV BUKOBA JUU YAKE KUNA SANAMU YA MFANO WA MELI HIYO ILOZAMA. SANAMU HIYO IMEGEUKA KUWA MZINGA WA NYUKI (hata uchukuaji wa picha ilibidi uwe wa mbali kwani nyuki wanarandaranda eneo hilo) LICHA YA HILO IMESHIKA KUTU HIVYO KUHATARISHA UWEPO WAKE SIKU ZA USONI.