ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 11, 2022

VIDEO:- AJALI MBAYA YAPOTEZA MAISHA YA WAANDISHI WA HABARI MWANZA

 

Ajali ya Gari – Simiyu.

Watu kumi na wanne wakiwemo waandishi wa habari watano, leo wamepoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea wilayani Busega mkoani Simiyu, baada ya gari lililokuwa limewabeba waandishi wa saba, kugongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Hiace.

Hili ni pigo kwa tasnia ya habari na Watanzania kwa ujumla, baada ya kutokea ajali hiyo katika kijiji Kijiji cha kalemela, ikihusisha gari lililowabeba waandhishi wa habari aina ya Land Cruiser Hard Top, waliokuwa kwenye msafara wa mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel.

Msafara huo ulikuwa ukihusisha ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo wilayani wilayani Ukerewe, ambapo kabla ya waandishi hao kutimiza jukumu lao katika safari hiyo, ajali inayodaiwa kuwa chanzo chake ni mwendo kasi ikakatiza uhai wao.

Waandisi wa habari waliofariki Dunia ni Husna Mlanzi wa ITV, Anthony Chuwa wa Dailly News Digital, Johari Shan wa Uhuru Digital, afisa habari wa mkoa wa Mwanza Abeli Ngapemba, afisa habari wilaya ya Ukerewe Steven Msengi na Dereva wa gari lililowabeba.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika chanzo cha ajali hiyo, waliofariki katika gari dogo la abiria aina ya Hiace ni wanane, ambao hadi wakati huu wanaendelea kutambuliwa na ndugu jamaa na marafiki, waliofika katika kituo cha afya nasa wilayani Busega mkoani simiyu.

Tayari miili ya waandishi wa habari waliopoteza maisha wilayani Busega mkoani Simiyu, imeshawasili Jijini Mwanza, kwa ajili ya kuhifadhiwa katika hospitali ya mkoa huu Sekouture, kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Kutokana na ajali hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan, ametuma salam za pole kwa watanzania.

Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

Monday, January 10, 2022

Penati zote Azam FC (9-8) Yanga SC | Mapinduzi Cup, nusu fainali - 10/01/2022

 Azam FC wanatinga fainali kwa mikwaju ya penati..... muuaji wa penati ya mwisho akiwa ni Mudathir Yahya huku Yassin Mustapha akikosa penati yake upande wa Yanga.