Ajali ya Gari – Simiyu.
Watu kumi na wanne
wakiwemo waandishi wa habari watano, leo wamepoteza maisha katika ajali ya gari
iliyotokea wilayani Busega mkoani Simiyu, baada ya gari lililokuwa limewabeba
waandishi wa saba, kugongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Hiace.
Hili ni pigo kwa tasnia
ya habari na Watanzania kwa ujumla, baada ya kutokea ajali hiyo katika kijiji
Kijiji cha kalemela, ikihusisha gari lililowabeba waandhishi wa habari aina ya
Land Cruiser Hard Top, waliokuwa kwenye msafara wa mkuu wa mkoa wa Mwanza
Mhandisi Robert Gabriel.
Msafara huo ulikuwa ukihusisha
ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo wilayani wilayani Ukerewe, ambapo kabla
ya waandishi hao kutimiza jukumu lao katika safari hiyo, ajali inayodaiwa kuwa
chanzo chake ni mwendo kasi ikakatiza uhai wao.
Waandisi wa habari
waliofariki Dunia ni Husna Mlanzi wa ITV, Anthony Chuwa wa Dailly News Digital,
Johari Shan wa Uhuru Digital, afisa habari wa mkoa wa Mwanza Abeli Ngapemba,
afisa habari wilaya ya Ukerewe Steven Msengi na Dereva wa gari lililowabeba.
Kwa mujibu wa taarifa
kutoka katika chanzo cha ajali hiyo, waliofariki katika gari dogo la abiria aina
ya Hiace ni wanane, ambao hadi wakati huu wanaendelea kutambuliwa na ndugu
jamaa na marafiki, waliofika katika kituo cha afya nasa wilayani Busega mkoani
simiyu.
Tayari miili ya
waandishi wa habari waliopoteza maisha wilayani Busega mkoani Simiyu,
imeshawasili Jijini Mwanza, kwa ajili ya kuhifadhiwa katika hospitali ya mkoa
huu Sekouture, kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Kutokana na ajali hiyo,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan, ametuma salam
za pole kwa watanzania.
Bwana ametoa na bwana
ametwaa jina lake lihimidiwe.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.