ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 26, 2010

YAPATA MIAKA 3 SASA, TANGU AMINA CHIFUPA KUTUTOKA.


LEO NI MIAKA 3 KAMILI TOKEA MH. AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIA (PICHANI) ATUTOKE. KIFO CHAKE, KILICHOTOKEA GHAFLA, KILITIKISA NCHI NZIMA NA WATANZANIA WOTE KWA JUMLA YAO WALIBAKI MIDOMO WAZI KWA KUONDOKEWA NA MBUNGE HUYU KIJANA ALIYEJIPATIA UMAARUFU KWA MENGI, KUBWA LIKIWA MSIMAMO WAKE WA KUPAMBANA NA JANGA LA MADAWA YA KULEVYA. NA LEO, IKIWA NI SIKU YA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA, GLOBU YA JAMII INAJIUNGA NA WANAHARAKATI KAMA AMINA CHIFUPA KUADHIMISHA SIKU HII HUKU TUKIMKUMBUKA MWAHARAKATI HUYU.
Habari na picha kwa hisani ya michuzi jr.

KUELEKEA UCHAGUZI 2010.


MGOMBE BINAFSI AJITOKEZA.

MGOMBEA BINAFSI NAFASI YA UBUNGE 2010 JIMBO LA... HAKIKA AKILITAJA WATU WATAANGUKA KWA PRESHA) MH.MUSHI MC.BONKE STAREHE, AMINI USIAMINI JAMAA KAJITOKEZA KUTANGAZA NIA AKIWA MGOMBEA BINAFSI, KAMA UNGEPENDA KUMCHANGIA AWEZE KUSHINDA NUNUA VOCHA YA ZAIN 0784239303 NA VODA.07672393903 KIASI CHOCHOTE NA KISHA TUMA KWENYE NAMBA HIZO.
HIMA HIMA EWE MZALENDO, TUMA SASA UMWEZESHE KUSHINDA, KWANI USHINDI KWAKE NI USHINDI KWAKO.
YES WE CAN!

Friday, June 25, 2010

KOSHA MACHO.

BRO MOHAMED OMAR WA LIVERPOOL HIKI NDICHO KIPITA SHOTO CHA BARABARA YA NYERERE NAMUONEKANO WAKE MIAKA YA SASA.

MABINGWA WATETEZI ITALIA WAMEAGA KWA AIBU FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA KATIKA HATUA ZA MAKUNDI WAKIWA MKIANI WALIPOCHAPWA 3-2 NA SLOVAKIA. JANA NDO NILIGUNDUA KUWA ROCK CITY INA WAPENZI WENGI WA ITALIA KWANI HAWAKUAMINI FILIMBI YA MWISHO.

BILA SHAKA WAWAJUA HAWA!!
Sanaa ni usanii wowote, yaani utendaji wa binafsi au wa pamoja ambao, kwa kutumia vipaji vya kuzaliwa navyo au mbinu zinazotokana na mang'amuzi na masomo, unabuni na kuleta uzuri. Sanaa imegawanyika sehemu nyingi: k.mf. muziki, uigizaji, uchezaji, uchoraji, upigaji picha, sinema, ushonaji, uhariri, uchongaji, uandishi, ushairi n.k.

MEZA MATE!.

Thursday, June 24, 2010

AAH! ALADJI! ALADJI!

MAONESHO YA UTUMISHI WA UMMA YAMEMALIZIKA JANA YAKIWA NA SIFA KEDE KEDE. PICHANI ASKARI WANYAMA PORI RAYMOND NKAMBI AKIFAFANUA JAMBO KWA WAUNGWANA WALIOZURU BANDA LA HIFADHI WANYAMA PORI.

YALE MATAABIKO YA KUSAKA WATAALAM WA KUREMBESHA BUSTANI ZETU TIBA YAKE HII HAPA...
TUPO ILEMELA MWANZA,
KUPATA HUDUMA PIGA SIMU 0786048818.


WAKAZI WA ILEMELA MAENEO YA PASIANSI, BWILU, SABASABA, KISEKE, MALIASILI, LUMALA, IGOMBE, AIR PORT HUDUMA ZA SHIRIKA LA UMEME NCHINI TANESCO ZIMEWAFUATA HUKO HUKO OFISI ZINAPATIKANA NJIA YA KUELEKEA TBL.

UTAIFA MBEEEELE! BANDA LA WAPASHAJI HABARI WA SERIKALI NCHINI, LILI SHINE ILE KISAWASAWA.

AFYA BORA NDIYO RASILIMALI MUHIMU KULIKO NYINGINE ZOTE KATIKA MAISHA YA BINADAMU YEYOTE. LAKINI WENGI TU WAZITO KUPIMA AFYA ZETU MARA KWA MARA. PICHANI AFISA MASOKO CLOUDS MWANZA HUMPHREY SIMON AKIPIMA AFYA KWA WATAALAM WA BIMA YA AFYA (NHIF).

LAITI ULE UKARIMU NA MAKARIBISHO MAZURI KATIKA MAONESHO YA UTUMISHI WA UMMA UNGEHAMIA KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA KILA SIKU YA IDARA HIZO ZA SERIKALI, AAAAAAAHHH! ALADJI! ALADJI! TZ YETU INGEKUWA MWAAAAAH! KINOMANOMA.

KWEA PIPA MWANZA HAOOOO........SAUZI!

WASHINDI WA KWEA PIPA NA COCA COLA TOKA KANDA YA ZIWA WAMEKWEA PIPA LEO, WASHINDI HAO WAPATAO 76 WALIUPAMBA UWANJA WA NDEGE WA MWANZA KWA RANGI ZA MAVAZI YAO.

JAPO BAADHI PICHA PICHA YA CREW YA WAKWEAJI.

DADAZ KWEA PIPA NA COCA COLA.

KULIA MANAGER WA CLUB BORA JIJINI MWANZA KWA MABURUDANIZ NA MASERVICE YA VYAKULA 'VILLA PARK' BW. ANTHONY YU MMOJA KATI YA WAKWEA PIPA WALIOSHINDA TIKETI ZA VIP'

NAE REMMYSON UISO MANAGER WA PUB YA SAMAKI CHOMA NA BIA ZA KUKAANGA (TEHE! WASHANGA!?)NI MKWEAJI TIKET ZA VIP' MCHEZO ULIO CHEZESHWA TAREHE 25 MWEZI MEI 2010 NA KUJUMUISHA WAMILIKI WA SEHEMU MAARUFU ZA UUZAJI BIDHAA ZA COCA COLA..

MSHKAJI NAE HUYOOOOO!

AFISA UHUSIANO NYANZA BOTTLING CO LTD BW. MAGINGA AMESEMA WASHINDI HOA 76 WATAUNGANA NA WENZAO WA MIKOA MINGINE KTK JIJI LA DAR ES SALAAM NA KISHA LEO JIONI KUUNGANISHA KWENDA SOUTH KUSHUHUDIA MECHI YA SOKA KOMBE LA DUNIA KATI YA URENO NA BRAZIL MCHEZO UNAOCHEZWA KESHO TRH 25 JUNI 2010 KAMA AHADI YA COCA COLA KUPITIA MCHEZO ULIOISHA HIVI KARIBUNI.

SURA YA BILL CLINTON: YAASHIRIA MCHEZO WA SOKA KUWAINGIA DAMUNI WAMAREKANI.


Former President William Jefferson Clinton was on hand to witness the USA beat Algeria 1-0 yesterday, but that's not why we know soccer has arrived in America. It's Clinton's face. Just look at it. Look at how red with stress it is. Look at his lower lip, chewed up like a bit of gristle on the end of a nice, Southern barbecued steak.

More importantly, look at Clinton's left hand. This man is stressed out about the game; he does not want to have to listen to Sepp Blatter make awkward small talk anymore. Clinton — a renowned international charmer and the husband of one of the most important diplomats in the world — is very unsubtly telling Blatter to shut his gob and just watch the game already, because DeMarcus Beasley has come on and Clinton needs to think about whether he should go down and open a can of Arkansas whupass on Bob Bradley's face.

Wednesday, June 23, 2010

UZINDUZI WA WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA NA TAASISI YA MAENDELEO NA USIMAMIZI WA MAJI MWANZA.

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA MH. HAWA ABDURAHMAN GHASIA AKIHUTUBIA KATIKA UZINDUZI WA WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA NA TAASISI YA MAENDELEO NA USIMAMIZI WA MAJI MWANZA 23 JUNE 2010 UKUMBI WA NYUMBANI HOTELS.

LENGO KUU LA KUUNDA WAKALA HIZI ZA SERIKALI NI KUSAIDIA SERIKALI KUFANYA MAJUKUMU AMBAYO SIYO LAZIMA YAFANYWE NDANI YA MUUNDO WA SERIKALI KUU NA KUTIA CHACHU YA KULETA HUDUMA BORA KWA UMMA KWA KUZINGATIA VIGEZO VILIVYOWEKWA.

KWA NIA YA KUSUKUMA GURUDUMU LA KUBORESHA UTOAJI HUDUMA KWA UMMA WA WATANZANIA WAZIRI AKIKATA UTEPE KUASHIRIA UZINDUZI WA WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA (TMAA) NA TAASISI YA MAENDELEO NA USIMAMIZI WA MAJI(WDMI).

WAZIRI AKIKABIDHI MWONGOZO KWA BW. DAVID K.JAIRO KATIBU MKUU NISHATI NA MADINI MARA BAADA YA UZINDUZI.

MH.WAZIRI AKIKABIDHI MWONGOZO KWA BW. SHAURI MWAKILISHI KATIBU WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI (WDMI)

MKURUGENZI WA JIJI LA MWANZA BW. WILSON KABWE (MWENYE SUTI) ALIAMUA KUKAA KATIKATI YA WADAU WA HABARI NDANI YA UZINDUZI HUO.

WATUMISHI WA UMMA KTK POZI.

NAKO UWANJA WA CCM KIRUMBA KATIKA UFUNGAJI WA MAADHIMISHO WIKI YA UTUMISHI WA UMMA LEO TAREHE 23 JUN 2010.

PICHA YA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA MH. HAWA ABDURAHMAN GHASIA NA VIONGOZI IDARA MBILI ZA WAKALA ZILIZO ZINDULIWA LEO JIJINI MWANZA.

Tuesday, June 22, 2010

HAPA NA KULE.

BUGANDO HILL. WAKAZI WA PANDE HIZI WANAJIITA WAZEE WA MAGOROFANI.

ISAKA NI JINA LA KATA YA WILAYA YA KAHAMA KATIKA MKOA WA SHINYANGA, KWA MUJIBU WA SENSA ILIYOFANYIKA MWAKA 2002, KATA INA WAKAZI WAPATAO 19,486 WAISHIO HUMO. LAKINI KWA SASA IDADI HIYO YAWEZA KUWA MARA MBILI KUTOKANA NA UPATIKANAJI WA HUDUMA MUHIMU.

KITUO CHA POLISI MSIGIRI NI MOJA YA VITUO MAARUFU SANA BARABARA NJIA YA KATI, VITENDO VYA UHALIFU VINARIPOTIWA KUPUNGUA KWA KASI NA MAENDELEO KUJA JUU, MARA BAADA YA KUKAMILIKA KWA BARABARA YA MSIGIRI - BOMANI ILIYOJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI NA KAMPUNI YA KICHINA YA CHICO.

TUELEKEE SINGIDA.

PENGINE ENEO HILI LILILOKO MKOANI SINGIDA NDILO LINALOONGOZA KWA UZURI, CHAKULA KIZURI NA HUDUMA NZURI NJIA YA KATI. LAITWA 'QUICK FOOD CAFETERIA' UNABISHA!
PLIZ BISHA NA PICHA.

NANI HUYU?

NIKUSAIDIE; NI MWANASOKA WA ZAMANI WA TIMU YA TAIFA YA U...SA.

AKYAMUNGU NAANZISHA KAMPUNI!

WADAU HAWA WAKIVIZIA KUJICHOMEKA KATIKA KATIKA MSAFARA WA MAANDAMANO MLANGONI KUINGIA UWANJANI.

SIKU YA UFUNGUZI WA WIKI YA NANIHINO... KUNDI HILI LA WANAFUNZI NA WAHUSIKA KIDUCHU' LILILOTOKEA KATIKATI YA JIJI LILIKUTANA HATUA CHACHE KABLA YA KUINGIA KIWANJA CHA MASHUGHULI NA LILE LA WENYE SHUGHULI WENYEWE AMBALO LILIANDAMANA TOKEA PASIANSI.
NOW DAYS NIMESHUHUDIA MAANDAMANO YA MAADHIMISHO YA SHUGHULI MBALIMBALI ZA KISERIKALI, MASHIRIKA YA UMMA HATA MASHIRIKA BINAFSI, YANAPOTAMKA KUWA KUTAKUWA NA MAANDAMANO MWISHO WA SIKU IDARA ZA MATAYARISHO HUZAMA MASHULENI KUWAOMBA WANAFUNZI WAKAWAJAZIE UMATI ILI ALMURADI KUKAMILISHA ZOEZI LA KUANDAMANA HATA KAMA NI MAPUMZIKO SIKU YA TUKIO.
TOFAUTI NA MIAKA YA ZAMANI AMBAPO MAANDAMANO YALIKUWA MAANDAMANO KWELI YA WAHUSIKA KWELI! LAKINI MIAKA YA SASA! MMH! HATA TUANDAMANE NA MAGARI HUMPATI MTU!
HII INAMAANISHA NINI?
SIJUI!!!!

Sasa basi ilikuwaondoshea usumbufu wanafunzi kukesha njaa na kufanya kazi hii bila malipo wala kifuta jasho cha hata sabuni.
NINAANZISHA KAMPUNI ITAKAYOSHUGHULIKA NA:-
1.MAANDAMANO (UNATAJA UKUBWA GANI WATAKA)
2.WATU WA KULIA MSIBANI (KUNA STYLE UNACHAGUA MF. CLASSIC, NORMAL NA NK)
3.NA SHANGWE ZOTE VUVUZELA, MATARUMBETA .....

Monday, June 21, 2010

JE HUU NDIO MWANZO WA MAGOLI MENGI KOMBE LA DUNIA?


MDAU MPENDA SOKA ONDOSHA ILE KIU YA KUONA MAGOLI MENGI KATIKA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA ZINAZOENDELEA AFRIKA YA KUSINI.
PICHANI: WACHEZAJI WA TIMU YA PORTUGAL TIAGO (L) NA PEDRO MENDES WAKISHEREHEKEA GOLI LILILOFUNGWA NA MIDFIELDER WA TIMU HIYO Raul Meireles (usneen) ALIYEFUNGA KATIKA MCHEZO WA SOKA KOMBE LA DUNIA KUNDI G ROUND YA KWANZA 2010, AMBAPO NORTH KOREA IMEPOKEA KICHAPO CHA MAGOLI 7-O, MCHEZO ULIOCHEZWA LEO MJINI CAPE TOWN GREEN POINT STADIUM. WAKATI HUO HUO TIMU ZA AFRIKA ZIMEENDELEA KUWA KERO, ZIKIKATISHA TAMAA MASHABIKI WAKE WALIOJIANDAA KWA NIA MOJA KUSHANGILIA TIMU HIZO, BAADA YA IVORY COST KUKUBALI KICHAPO CHA BAO 3-1 TOKA KWA BRAZIL......... SIENDELEI...

BOMOA BOMOA IMEIVA! NA SAFARI HII ENEO LA MAKOROBOI LINATOKOTA.

Zoezi la bomoa bomoa katika jiji la Mwanza linatarajiwa kuukumba mtaa maarufu wa makoroboi nia ni kupisha ujenzi wa majengo ya vitega uchumi.

Ubomoaji utatekelezwa na idara ya Mipango miji ya jiji la Mwanza eneo linalojulikana kama city park Garden, vile vile inadaiwa kwamba eneo hilo limekuwa likijengwa vibanda bila kibali cha ofisi ya Mipango Miji huku ikidaiwa ni kinyume cha sheria ya ujenzi ya mipango miji.

Habari kutoka ndani ya ofisi za jiji la Mwanza zimedai kuwa eneo hilo linaweza kubomolewa wakati wowote ili kupisha ujenzi wa uwekezaji mkubwa wa majengo kama yale ya NSSF na PPF yaliyopo katikati ya jiji la Mwanza.

Eneo hilo ambalo pia hujulikana 'KWA WAMBURA' limekuwa na mgogoro wa muda mrefu kati ya halmashauri ya jiji na mfanyabiashara huyo ambapo kesi ya kumiliki eneo hilo ilifikishwa mahakamani na Bwana Wambura akashinda kesi hiyo.

Inadaiwa kwamba baada ya Wambura kushinda kesi hiyo, alipewa kibali cha kulitunza eneo hilo kutokana na masharti kwamba atengeneze michoro ya kuwekeza kwenye eneo hilo, ambayo itapitishwa na Mipango miji ya jiji la Mwanza.


Hoja iliibuka hivi majuzi ndani ya kikao cha madiwani ambapo jibu kutoka kwa mwenyekiti wa kamati ya mipango miji na mazingira bw. Richard Rukambura lilisema kuwa mfanya biashara huyo alishapewa masharti ya kupeleka michoro akashindwa na haijulikani kinachoendelea.

Nae bw. Wambura amesema kuwa yeye aliandaa michoro ya majengo, lakini uongozi wa jiji ukakataa mchoro aliouandaa kwa madai kuwa haufai, hivyo akawaomba wamsaidie kuchora mchoro wanaotaka wao wakakataa bila kutoa ufafanuzi, ndipo naye akaamua kukaa kimya akisubiri kuitwa au kupewa maelekezo toka uongozi huo wa jiji.


Imedaiwa kuwa bomoabomoa hiyo itakumba hadi maeneo jirani anayofanyia biashara Wambura kwani yanatambulika kuwa eti ni bustani ya jiji na majirani hao hawana hati miliki ya eneo hilo kama ilivyo kwa Wambura.

Swali jingine: Hatma ya Hospitali ya mwananchi na kituo cha polisi ndani ya eneo hilo.