Friday, February 24, 2023
BMH, BOMBO KUENDESHA KAMBI YA HUDUMA MBALIMBALI ZA KIBINGWA JIJINI TANGA
Na Oscar Assenga, Tanga
HOSPITALI ya Benjamini Mkapa (BMH) ikishirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo wanatarajia kufanya kambi ya huduma mbalimbali za kibingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo kuanzia February 27 hadi Machi 3 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga –Bombo Dkt Naima Yusuf (Pichani) alisema kwamba maandalizi ya kuelekea kambi hizo yanaendelea vizuri huku akieleza huduma za kibingwa zitakazotolewa.
Dkt Naima alisema huduma zitakazotolewa ni Upasuaji Mishipa ya Fahamu ,Mifupa, Mfumo wa Haja ndogo (Mkojo),Magonjwa ya ndani,Tiba ya Figo,Tiba ya Moyo kwa watoto na watu wazima.
Alizitaja huduma nyengine zitakazotolewa ni Magonjwa ya watoto Magonjwa ya macho,Tiba ya Kinywa na Meno pamoja na Magonjwa ya Uzazi kwa akina Mama.
Hata hivyo Dkt Naima alisema kwamba katika kambi hiyo wateja wa bima ambao watapokelwa ni wa Jubilee Insurance,Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Assemble Insurance na Strategis Insurance.
.
WANAUME WANAOPIGA WAKE ZAO VIBAO/MAKOFI CHANZO CHA UKIZIWI - KUELEKEA SIKU YA USIKIVU DUNIANI PT 1
NA ALBERT G. SENGO/MWANZA Tatizo la usikivu linazidi kuongezeka siku hadi siku. Inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 5 ya watu duniani wana tatizo la usikivu. Kipigo na makofi karibu na maeneo ya sikio imesababisha watu wengi hususani akinamama kuwa viziwi. Kuelekea Maadhimisho ya 'SIKU YA USIKIVU DUNIANI' inayoadhimishwa kila mwaka na kilele chake Tarehe 3 mwezi March, tunazungumza na Dr. Olivia Michael Kimario ambaye ni daktari bingwa wa kichwa, koo, pua, masikio na shingo, kutoka Hospitali ya Rufaa ya Bugando ambaye sanjari na kutoa elimu pia ametoa wito kwa kila mmoja wetu kuchukua hatua kujikinga na vitendo vinavyosababisha changamoto hiyo ikiwemo jamii hususani akinababa kuepuka kuwapiga wapenzi wao vibao au ngumi masikioni. Kuelekea maadhimisho hayo Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza imeandaa kliniki kwa wananchi kuonana na wataalamu na fanyiwa uchunguzi bure.
IRINGA DC WAPITISHA BAJETI YA BILIONI 60.24
WACHIMBAJI MZINGATIE SHERIA YA USALAMA WA MAZINGIRA NA MATUMIZI SALAMA YA BARUTI-PROFESA KIKULA
Thursday, February 23, 2023
MHUDUMU WA AFYA AKALIA KUTIKAVU IRINGA
Na Fredy Mgunda, Iringa.
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Iringa Limeagiza kufanyika uchunguzi wa haraka dhidi ya Mhudumu wa afya katika Zahanati ya Kijiji ya Tungamalenga, anayedaiwa kutumia singano iliyotumika kumtibu mgonjwa
Akizungumza wakati wa baraza la Madiwani,Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Stephen Mhapa alitoa agizo kwa Idara ya afya baada ya hoja ya malalamiko dhidi ya Mhudumu huyo wa afya anayedaiwa kukiuka misingi ya utumishi akijihusisha na vitendo vya utovu wa nidham ikiwemo ulevi wa kupindukia nyakati za kazi.
Mhapa alisema Halmashauri hiyo haitovumilia utovu wa nidham unaopelekea ukiukwaji mkubwa wa misingi ya kitaaluma na kuhatarisha afya za wagonjwa wanaopata huduma katika zahanati hiyo kwani kitendo cha kutumia sindano iliyotumika kumtibu mgonjwa mwingine kinaweza kusababisha kusambaa kwa maambukizi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo maambukizi ya virusi vya ukimwi
"Tumeagiza uchunguzi ufanyike haraka iwezekanavyo kwenye zahanati zote na Mimi kama mwenyekiti napenda kutoa onyo kwa watumishi wote wa Halmashauri hii ninataka kupata taarifa kamili katika Baraza la madiwani lijalo ili tushughulike na hao watendaji"alisema Mhapa
Aliyasema hayo baada ya Diwani wa viti maalum tarafa ya Idodi Wilayani Iringa Shani Msambusi kuwasilisha malalamiko hayo katika baraza la madiwani na kumtaja mhudumu huyo wa afya aliyefahamika kwa jina la Johavina Mjuni kuwa ni kero kwa wananchi wanaopata huduma katika zahanati hiyo kutokana na utovu wa nidham uliokithiri na kushindwa kufanya kazi kwa weledi.
Diwani Msambusi alilielezabaraza la Madiwani kuwa Wananchi wanaiomba Serikali kuchukua hatua kwani hawako tayari kuendelea kuhudumiwa na Mhudumu huyo na kusisitiza Serikali kumuhamisha kwa kuwa hawana imani tena na huduma za kiafya anazozitoa.
Msambusi alisema kuwa mhudumu huyo wa afya amekuwa anatumia vilevi kupitiliza kipindi cha kazi hadi kushindwa kufanya kazi kwa weledi wake wa kuhudumia wananchi wagonjwa.
Kufuatia malalamiko hayo Kaimu mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa,Luvanda Witson alisema wanaanzisha uchunguzi wa haraka dhidi ya madai hayo na pindi watakapojiridhisha hatua za kinidham zitachukuliwa na kulijulisha baraza la madiwani kuhusu hatua hizo.
CRDB YAWAPA UBALOZI WACHEZAJI WA SIMBA NA YANGA KAMPENI YA BENKI NI SimBanking
KAMPUNI YA TANZANIA, YAKAMILISHA UJENZI WA KIVUKO KIPYA CHA MV PALM CHA NCHI YA UGANDA.
Hii tunaiita Mv Palm made in Tanzania, ni ndani ya Ziwa Victoria mara baada ya kujengwa na kushushwa majini.
Hii tunaiita Mv Palm made in Tanzania, ni ndani ya Ziwa Victoria mara baada ya kujengwa na kushushwa majini.
Hii tunaiita Mv Palm made in Tanzania, ni ndani ya Ziwa Victoria mara baada ya kujengwa na kushushwa majini.
KAMPUNI YA SONGORO MARINE LTD YA TANZANIA, YAKAMILISHA UJENZI WA KIVUKO KIPYA CHA MV PALM CHA NCHI YA UGANDA. MAJOR AMPONGEZA RAIS SAMIA.
Tuesday, February 21, 2023
ORYX GAS YAGAWA BURE MAJIKO NA MITUNGI KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI MKOANI TANGA, MBUNGE UMMY AWASHUKURU KWA KUWAWEZESHA WAKINA MAMA HAO
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Duka la Kuuzia Gesi Kampuni ya Oryxs lililopo barabara ya 7 Jijini Tanga kulia Mkurugenzi wa ORYX GAS Araman Benoite kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katikati akiwa na o na Mkurugenzi wa ORYX GAS Araman Benoite kushoto wakimkabidhi Mtungi wa Gesi mmoja wa wajasiriamali Jijini Tanga leo
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katikati akiwa na o na Mkurugenzi wa ORYX GAS Araman Benoite kushoto wakimkabidhi Mtungi wa Gesi mmoja wa wajasiriamali Jijini Tanga leo
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katikati akiwa na o na Mkurugenzi wa ORYX GAS Araman Benoite kushoto wakimkabidhi Mtungi wa Gesi mmoja wa wajasiriamali Jijini Tanga leo
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katikati akiwa na o na Mkurugenzi wa ORYX GAS Araman Benoite kushoto wakimkabidhi Mtungi wa Gesi mmoja wa wajasiriamali Jijini Tanga leo
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katikati akiwa na o na Mkurugenzi wa ORYX GAS Araman Benoite kushoto wakimkabidhi Mtungi wa Gesi mmoja wa wajasiriamali Jijini Tanga leo
KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania imekabidhi mitungi ya gesi pamoja na majiko yake 600 kwa wanawake 600 kutoka vikundi mbalimbali vikiwemo vya wajasiriamali katika Mkoa wa Tanga ikiwa ni mkakati wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa yanayoharibu mazingira.
Huku Mbunge wa Jimbo la Tanga ambaye pia ni Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiishukuru Kampuni ya Oryxs Gas Tanzania kwa kuridhia ombi lake la kukubali kuwasaidia wanawake wajasiriamali kutoka vikundi mbalimbali vilivyopo kwenye Kata zote za Jimbo lake
Akizungumza wakati wa kukabidhi mitungi hiyo ya gesi mbele ya Waziri wa Afya ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu, Mkurugenzi wa ORYX GAS Araman Benoite amesema kutokana na madhara ya gesi ya ukaa duniani, kampuni ya Oryx Tanzania (OGTL) iko mstari wa mbele kusaidia kuhamasisha matumizi ya gesi safi ya kupikia kwa kutoa mchango mwingine wa vifaa vya gesi mkoani Tanga ambako matumizi ya mkaa ni makubwa.
Amesema matumizi ya mkaa yana athari kubwa kwa mazingira na husababisha jangwa huku akifafanua Tanga ni miongoni mwa mikoa hapa nchini ambayo ina hali ya juu ya ukataji miti kwa ajili ya mkaa, hivyo wao wanaamini mpango huo wa kusaidia vifaa utasaidia wakazi wa Tanga, hasa wanawake ambao wanaathirika na moshi utakanao na kuni na mkaa.
"Kampuni inawekeza kwa kutekeleza miradi ya kutoa elimu juu ya gesi safi ya kupikia, inachangia vifaa vya gesi ya kupikia katika baadhi ya mikoa.Pia tunahamasisha matumizi ya gesi kwa kufanya mauzo makubwa ya mitungi kwa bei nafuu.
"Juhudi zote hizi zinalenga kufanya Watanzania wengi wanaanza kutumia gesi safi ya kupikia kama alivyoahidi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan.
Rais Samia ambaye ameweka malengo kuwa ifikapo mwaka 2030 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia gesi safi ya kupikia.
"Kampuni ya Oryx Gas Tanzania pia imeitikia wito wa kidunia ya kupunguza hewa ukaa kutoka viwandani na shughuli za kibinadamu Kupitia promosheni ya LPGOGTL kampuni is furaha kuungana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika juhudi za kuboresha Maisha ya Watanzania kwa kupunguza hewa ukaa. Tunasikia faraja kusaidia utekelezaji wa ajenda ya LPG ambayo inainufaisha Tanzania,amesema Benoit.
Awali akizungumza Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu alimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oryx Tanzania kuwa kuwasaidia kuwezesha majiko ya gesi kwa wanawake wajasiriamali kwenye Jiji hilo.
Alisema kwamba msaada huo umekuja wakati na hivyo kuwa mkombozi mkubwa kwa wana Tanga kutokana na kwamba lazima lifanane na watu na hali halisi hivyo mahitaji ya gesi ni muhimu na hayaweze kukwepeka kwa wananchi.
“Ndugu zangu wana Tanga Oryxs Gas ni Kampuni Bora na nzuri na labda niwaambie kwamba hawapunyi kwenye vipimo vyao lakini niwashukuru kwa kufungua duka hilo na wao kama Tanga Jiji wamepata mlipa kodi mpya “Alisema
Hata hivyo Waziri Ummy alimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Oryxs Gas Tanzania baada ya kumwambia kwamba Tanga kuna wasiriamali na wangependa kuwasadia majiko ya gesi kwa ajili ya kurahisisha shughuli zao kujipatia kipato na kuandaa chakula .
“Hivyo tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha jambo hilo,alisema kwamba yeye anataka kuwasaidia na kuwainua wananchi wa kipato cha chini na kuwaambia kwamba atamsaidia kufanikisha hilo lakini pia matumizi ya gesi yataweza kusaidia kuondokana na matumizi ya mkaa ambayo ni gharama kubwa “Alisema
Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa alisema kitendo kilichofanywa na Mbunge huyo kitaacha alama na wanaona wanakwenda kutibua sehemu ya changamoto kwenye jamii ya ukataji wa miti ambayo mwisho wa siku inapelekea kuharibu mazingira.
“Matumizi ya gesi nchini bado yanakwenda kwa kusuasua kwa hiyo kupitia hili kutakuwa na ushawishi mkubwa kwa kuhakikisha jamii inatumia nishati mbadala ya gesi ambayo itasaidia kutunza mazingira na kuondoa uharibifu wa mazingira” Alisema
Hata hivyo kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Tanga Al- Shaymaa Kweygir alisema kwamba wanashukuru Mbunge Ummy Mwalimu kwa kuwajali wakina mama kwa sababu wao wana mchango mkubwa kwa maendeleo .
Kweygir alisema kwamba kitendo cha kuwezeshwa majiko ya Gesi kwa wajasiriamali wanawake itawasaidia kuwakomboa kichumi kwa sababu wanapokuwa kwenye shughuli zao watakuwa wakitumia muda mchache kuandaa na kuwahuduma wateja wao.
Naye kwa upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shiloo alimshukuru Mbunge Ummy kwa kuendelea kuwajali wananchi na Baraza la Madiwani linamshukuru kwa kuhakikisha maendeleo kwenye Jimbo hilo yanaendelea kupaa.
Hata hivyo alisema kwamba Mbunge huyo ni wa kipekee kutokea tokea Jimbo hilo lilipoanzishwa ameacha alama na kuvunja rekodi ya wabunge wengine waliowahi kuliongoza Jimbo hilo .
SIMBA NA AZAM FC ATAKAYECHUKULIA POA MCHEZO HUU AMELIWA
NA SUZUKI DRUMDRUM
KAZI kubwa inatarajiwa kufanyika jioni ya leo saa moja kamili, Uwanja wa Mkapa kwa Dabi ya Mzizima kati ya Simba v Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.
Unakuwa ni mchezo wa pili kwa wababe hawa kukutana baada ya ule uliopita wa mzunguko wa kwanza ubao kusoma Azam FC 1-0 Simba na kuwafanya Simba kuyeyusha pointi tatu muhimu. Msafiri Madanya wa Sports Ripoti ya Jembe Fm anafanya uchambuzi wa mchezo huo.UGANDA: MUUGUZI AKAMATWA KWA KUWABAKA WAGONJWA WAJAWAZITO
Polisi nchini Uganda wamemkamata muuguzi kwa tuhuma za kubaka na jaribio la kuwabaka wagonjwa wawili wajawazito katika Hospitali ya Entebbe Grade B.
Muuguzi huyo aliye mafunzo alikamatwa Jumamosi, Februari 18, jioni na kwa sasa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Entebbe Central.
Naibu Msemaji wa Polisi wa Jiji la Kampala, Luke Owoyesigire alisema mshukiwa, Kutesa Denis, alikuwa akiwatambua waathiriwa wake kutoka wodi ya Wanawake.
Kisha aliwawekea dawa ya kuwapoteza fahamu inayoshukiwa kuwa chloroform kabla ya kuwanyanyasa kingono.
"Dawa inayoshukiwa kuwa ya chloroform ilipatikana kutoka kwa makazi yake katika hospitali hiyo, na barua ikapatikana ambapo aliomba kuombewa dhidi ya mawazo machafu aliyokuwa nayo," Owoyesigyire alisema kwenye taarifa, akiwataka waathiriwa wengine kujitokeza, akisema kwamba inawezekana mtuhumiwa aliwanyanyasa wanawake wengine.
Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Peterson Kyebambe alisema kuwa tukio hilo sasa limewachochea kuongeza tahadhari na na kuimarisha usalama kwa kufunga kamera zaidi za CCTV.
Daktari bandia
Kwingineko humu nchini, daktari bandia James Mugo Ndichu almaarufu Mugo Wairimu aliongezewa kifungo cha miaka 29 jela. Mugo ambaye tayari alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 11 gerezani, alisukumwa jela bila faini baada ya kupatikana na hatia ya kuwadunga wagojwa wanawake dawa za kuwafanya wapoteze fahamu kabla ya kuwadhulumu kimapenzi.
Akitoa hukumu hiyo Novemba 2022, Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Milimani, Wendy Kagendo Micheni alisema Mugo ni hatari kwa usalama wa wanawake na anastahili kutengwa na jamii ya waungwana wanaopenda amani na haki.
Kwa shtaka kuwapotezea fahamu wagonjwa na kuwabaka, Micheni amemfunga Mugo miaka 22.