ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, February 21, 2023

UGANDA: MUUGUZI AKAMATWA KWA KUWABAKA WAGONJWA WAJAWAZITO


Polisi nchini Uganda wamemkamata muuguzi kwa tuhuma za kubaka na jaribio la kuwabaka wagonjwa wawili wajawazito katika Hospitali ya Entebbe Grade B. 

Muuguzi huyo aliye mafunzo alikamatwa Jumamosi, Februari 18, jioni na kwa sasa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Entebbe Central. 

Naibu Msemaji wa Polisi wa Jiji la Kampala, Luke Owoyesigire alisema mshukiwa, Kutesa Denis, alikuwa akiwatambua waathiriwa wake kutoka wodi ya Wanawake. 

Kisha aliwawekea dawa ya kuwapoteza fahamu inayoshukiwa kuwa chloroform kabla ya kuwanyanyasa kingono. 

 "Dawa inayoshukiwa kuwa ya chloroform ilipatikana kutoka kwa makazi yake katika hospitali hiyo, na barua ikapatikana ambapo aliomba kuombewa dhidi ya mawazo machafu aliyokuwa nayo," Owoyesigyire alisema kwenye taarifa, akiwataka waathiriwa wengine kujitokeza, akisema kwamba inawezekana mtuhumiwa aliwanyanyasa wanawake wengine. 

Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Peterson Kyebambe alisema kuwa tukio hilo sasa limewachochea kuongeza tahadhari na na kuimarisha usalama kwa kufunga kamera zaidi za CCTV. 

Daktari bandia 

Kwingineko humu nchini, daktari bandia James Mugo Ndichu almaarufu Mugo Wairimu aliongezewa kifungo cha miaka 29 jela. Mugo ambaye tayari alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 11 gerezani, alisukumwa jela bila faini baada ya kupatikana na hatia ya kuwadunga wagojwa wanawake dawa za kuwafanya wapoteze fahamu kabla ya kuwadhulumu kimapenzi. 

Akitoa hukumu hiyo Novemba 2022, Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Milimani, Wendy Kagendo Micheni alisema Mugo ni hatari kwa usalama wa wanawake na anastahili kutengwa na jamii ya waungwana wanaopenda amani na haki. 

Kwa shtaka kuwapotezea fahamu wagonjwa na kuwabaka, Micheni amemfunga Mugo miaka 22. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.