ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 11, 2014

ARIEL SHARON AFARIKI DUNIA.

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Israel, Ariel Sharon, amefariki dunia.

Bwana Sharon ambaye amekuwa kwenye umahututi kwa miaka nane.
Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kuugua ugonjwa wa kupooza toka mwaka 2006 wakati akiwa kwenye zama za juu za maisha yake ya kisiasa.
Hali yake ilizidi kuzorota katika siku za karibuni na kufanya baadhi ya viungo vyake kushindwa kufanya kazi ikiwemo figo zake.
Bwana Sharon ni mtu muhimu kwenye historia ya taifa la Israel tangu akiwa jenerali wa jeshi na baadaye mwanasiasa. Lakini atasalia kiongozi aliyekuwa na utatanishi mkubwa

BUSHIRI KAUBANIKA AFUNGA NDOA NA MWATABU TAMARAWE

Bwana Bushiri Kaubanika akiwa na nyuso ya furaha baada ya kufunga pingu za maisha na Mwatabu Tamarawe arusi iliyofungwa Gongolamboto mwisho wa lami na kufuatiwa na tafrilija iliyofanyika Kigogo Dampo Dar es salaam bwana na bibi wote ni walimu.
Bwana Bushiri Kaubanika akiwa na nyuso ya furaha baada ya kufunga pingu za maisha na Mwatabu Tamarawe arusi iliyofungwa Gongolamboto mwisho wa lami na kufuatiwa na tafrilija iliyofanyika Kigogo Dampo Dar es salaam bwana na bibi wote ni walimu.
Bwana Bushiri Kaubanika akiwa na nyuso ya furaha baada ya kufunga pingu za maisha na Mwatabu Tamarawe arusi iliyofungwa Gongolamboto mwisho wa lami na kufuatiwa na tafrilija iliyofanyika Kigogo Dampo Dar es salaam bwana na bibi wote ni walimu.
Bwana Bushiri Kaubanika akiwa na nyuso ya furaha baada ya kufunga pingu za maisha na Mwatabu Tamarawe arusi iliyofungwa Gongolamboto mwisho wa lami na kufuatiwa na tafrilija iliyofanyika Kigogo Dampo Dar es salaam bwana na bibi wote ni walimu.
Bwana Bushiri Kaubanika akiwa na nyuso ya furaha baada ya kufunga pingu za maisha na Mwatabu Tamarawe arusi iliyofungwa Gongolamboto mwisho wa lami na kufuatiwa na tafrilija iliyofanyika Kigogo Dampo Dar es salaam bwana na bibi wote ni walimu.

Bwana Bushiri Kaubanika akiwa na nyuso ya furaha baada ya kufunga pingu za maisha na Mwatabu Tamarawe arusi iliyofungwa Gongolamboto mwisho wa lami na kufuatiwa na tafrilija iliyofanyika Kigogo Dampo Dar es salaam bwana na bibi wote ni walimu wa shule picha na www.burudan.blogspot.com

Friday, January 10, 2014

BURUDANI YA SKYLIGHT BAND IJUMAA YA KWANZA KWA MWAKA 2014 NDANI YA KIOTA CHA THAI VILAGE.

DSC_0009
Digna Mbepera akiwaimbia kwa hisia mashabiki wa Skylight Band Ijumaa ya kwanza kwa mwaka 2014 ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar huku akisindikizwa na Mary Lucos pamoja na Winnie.
DSC_0045
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 akifanya yake jukwaani huku akisindikizwa na Rappa Joniko Flower sambamba na Winnie.
DSC_0008
Aneth Kushaba AK47 akiimba na kucheza na mashabiki wa Skylight Band wanaokunwa na uimbaji wake.
DSC_0014
Njagalawe chimanyee baby........!!!Kutoka kushoto ni Hashim Donode, Winnie na Digna Mbepera wakitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band.
DSC_0061
Mashabiki wakiburudika na Skylight Band ndani ya kiota cha Thai Village Ijumaa ya kwanza tangu mwaka 2014 uanze.
DSC_0031
Kanyaga twende...kutoka kushoto ni Mary Lucos, Sony Masamba na Winnie wakicheza staili ya "Yachuma chuma".
DSC_0121
Ni mwendo wa mukanda ya chuma......!
DSC_0126
Hapo Je......Tiki titi titi......hii ni Gym tosha kila Ijumaa ndani ya Thai Village Masaki.
DSC_0062
Skylight Band na watu wastaarabu ndani ya kiota cha Thai Village.
DSC_0095
Hashim Donode akikamua jukwaani.
DSC_0100
Mzungu akionekana kuchizika na Skylight Band.
DSC_0130
Mary Lucos akiwapa raha za Pwani mashabiki wa Skylight Band.
DSC_0139
Wake kwa waume kwa raha zao wakizungusha mduara.
DSC_0147
Mh. Bundala kwa raha zake akijinafasi.....burudani mwanzo mwisho....
DSC_0051
Sam Mapenzi akipagawisha mashabiki wa Skylight Band....!
DSC_0170
Skelewu....Skelewu....Skeleleleeeee....!!
DSC_0172
Aneth Kushaba AK47 akicheza na mdau Anorld wa Skylight Band.
DSC_0157
Aneth Kushaba AK47 na Petit Man wakipata Ukodak.
DSC_0184
Mdau kutoka DStv na warembo wa ukweli ndani ya Thai Village.
DSC_0186
Mwanafamilia wa Skylight Band Victor Maginga akipata Ukodak na wadau.
DSC_0188
Mdau Alois Ngonyani na Swahiba wake.
DSC_0022
Mdau Cosmas Mtesigwa (kulia) na marafiki kabla ya kukwea pipa kuelekea Zambia aliamua kuja kula bata na Skylight Band.....Vitu kama hivi adimu nchi za watu...
DSC_0195
Wadau wakiendelea kupata Ukodak.
DSC_0178

MH. LOWASSA AKAGUA MIRADI YA MAJI JIMBONI KWAKE MONDULI.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (katikati) akiongozana na wadau mbali mbali wa maendeleo wakati ziara yake ya kukagua maendeleo ya Mradi wa ujenzi wa bwawa la maji katika kata ya Meserani kijiji cha Nalarami,jimbo la Monduli.Wa tatu kushoto ni Diwani wa kata hiyo,Edward Lenanuu.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisikiliza maelezo kutoka kwa kaimu mhandisi wa maji wa wilaya ya Monduli,Bw. Wasiwasi Mgala (kushoto) wakati alipotembelea Mradi wa ujenzi wa bwawa la maji katika kata ya Meserani kijiji cha Nalarami,jimbo la Monduli.Katikati mwenye shati jekundu ni mwenyekiti wa CCM Monduli,Ruben Kunayi.

Thursday, January 9, 2014

MADIWANI WA JIJI LA MWANZA WAMGOMEA MKURUGENZI WAO:BAJETI IMEJAA UBABAISHAJI,VIWANDA VYA SAMAKI VINALIPA LAKI 1 KAMA KODI KWA MWAKA ILEHALI VINAINGIZA MABILIONI.

Na PETER FABIAN
G.SENGO BLOG.

MADIWANI wa Jiji la Mwanza leo wamegomea kujadili Rasimu ya Bajeti ya mwaka 2014/2015 iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa jiji la Mwanza, kwa madai kuwa haijakidhi na ina ubabaishaji katika mpango mkakati wa makusanyo ya Kodi kupitia Vyanzo vyake vya ndani.

Rasimu hiyo liyowasilishwa na Mchumi Msaidizi Joseph  Kashushula kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji hilo ilionekana kuwakera sana waheshimiwa Madiwani wote bila kujali wanatoka vyama gani vya siasa na kuanza kuchangia hoja ambazo zimepelekea kutolewa azimio la kurudisha Kamati ya Fedha kufanyiwa marekebisha upya na kuja na majibu ya msingi kabla ya kuwasilishwa tena na kuanza kujadiliwa.

Akizungumza wakati wa kuendesha kikao hicho Meya wa Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula alisema kwamba kutokana na hoja za waheshimiwa Madiwani walizochangia na kuwepo mapungufu huku Mkurugenzi na timu yake ya wataalamu kukosa majibu ya kina kuhusiana na hoja za mpango mkakati za ukusanyaji mapato kuonyesha kukusanya bilioni 9 tu kupitia vyanzo vyake vya ndani.

Meya Mabula alisema kamwe hawako tayari kukaa na kupoteza muda wa kujadili Rasimu hiyo kutokana na mapungufu hayo yaliyojitokeza huku hoja za madiwani zikidai kuwa kupitia vyanzo vya mapato ya Halmashauri hiyo ya Jiji vilivyopo vinaweza kukusanya kiasi cha zaidi ya bilioni 13 huku hoja zingine zilizochangiwa ni fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kuwa kidogo.

“Mkurugenzi na timu yako tunaomba mrudi mkajipange upya kwa rasimu hii hatuko tayari kukaa na kujadili haiwezekani viwanda vilivyopo hapa Jijini vikawa vinalipa Kodi ya laki moja kwa mwaka wakati vinaingiza mabilioni ya fedha kwa mwaka hili halikubaliki na Bajeti hii siyo rafiki kwa mustakabali wa kuwatumikia wananchi wa Jiji hili na inaonyesha tumekuja hapa kufanya mchezo wa kuigiza” alisema

Aliongeza kuwa kufatia wajumbe ambao ni waheshimiwa madiwani kwa umoja wao na kwa masilahi ya wananchi ambao wanawawakilisha kuamua kuweka tofauti zao za kisiasa na kuungana kuikataa rasimu hii kujadiliwa kutokana na kutokidhi ni vyema mkajipanga kuanda na kurekebisha kasoro hizo ili kujadiliwa kuletwa na kuwasilishwa ili kuwapa mwanya wa kujadiliwa.

Meya Mabula aliahilisha kikao hicho kwa kumtaka Mkurugenzi Alfa Hassan Hida kuitisha kikao cha dharula cha Kamati ya Fedha (FINENCE) kesho asubuhi majira ya saa 3:00 na mchana majira ya 6:00 kuwe na kikao cha dharula kuipitia baada ya kufanyiwa marekebisho kwenye ukusanyaji wa mapato,kujiandaa kulipa madeni ya wakandarasi utekelezwaji wa miradi katika sekta za Afya, Elimu, Maji, Miundombinu ya Barabara kupitia fedha za Mapato ya ndani. mengineyo.

Kufatia hatua hiyo baadhi ya wananchi wamempongeza Meya Mabula,Wabunge na waheshimiwa Madiwani kwa kuungana pamoja na kuweka tofauti zao za kisiasa (Vyama vyao) ili kuhakikisha Bajeti watakayopitisha inakuwa suluhisho kwa wananchi wa Jiji hili na mwarobaini kwa wanohujumu mapato ya Halmashauri ya Jiji kupitia vyanzo vyake vya ndani.

“Huyu ndiye Meya, wananchi wa Jiji hili tunaona amekuwa ni mtu asiyetaka sifa na amekuwa mtu wa kuchukua maamuzi sahihi na kusikiliza kilio cha wananchi kwani hali ya miundombinu kwa sasa huko kwenye mitaa na kata inatisha, madeni ya malipo ya fidia ya maeneo yaliyochukuliwa na Jiji ni muda sasa na huduma za Jamii zinazorota, tunaomba Kamanda awabane kweli kweli” walisema.

OXFAM YAWEKEZA MAISHA PLUS MSHINDI ZAIDI YA MILIONI 25 KUSHINDANIWA: MWANZA YAANZA KUCHUKUWA FOMU

Mmoja wa wakurugenzi wa Maisha Plus Tv Kaka Bonda (wa kwanza kushoto) amesema kuwa mwaka uu kampuni yake imeamua kuetengeneza fomu na  kuzigawa bure bila malipoTanzania nzima ambapo kwa washiriki wa Maisha Plus ni wale wenye umri wa miaka 21 -  26 na kwa Mama Shujaa ni wale wenye umri wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea.

Mambo yote kesho katika viwanja vya wazi Buhongwa, mtu yoyote anaye jiamini anakaribishwa kushiriki haijalishi unaelimu gani suala ni jeh! una uwezo wa kushiriki shughuli za maendeleo na uzalishaji mali?
Katika mwendelezo wa Kampeni ya Grow unao lenga kumkwamua mwanamke kutoka katika lindi la umasikini, sanjari na kukabiliana na changamoto ya upungufuwa chakula inayolikabili taifa letu, Shirika la Kimataifa la Oxfam na wadau wake limeandaa shindano la Mama Shujaa wa Chakula ikiwa ni msimu wa Tatu litakalousiswa ndani ya kipindi cha kijamii cha Maisha Plus.

Kwa mujibu wa wa Meneja Kampeni ya Haki na Uchumi wa Oxfam Bi. Eluka Kibona amesema kuwa shirika lake liliamua kuwekeza mpango wake ndani ya kipindi cha Maisha Plus ili kuendesha kampeni yake kwa manufaa zaidi kutokana na ubunifu na elimu inayozalishwa ndani ya kipindi hicho ambayo inahitaji kupanuka zaidi kwa wawekezaji kuwekeza kwenye mchezo wa kipindi hicho cha manufaa kwa jamii.
Mkamiti Mgawe Afisa Uchumi na Uchochezi wa Oxfam amesema kuwa kwa mujibu wa tafiti zilizo fanywa zinaonyesha asilimia 60 ya wanawake Tanzania wananjihusisha na kilimo lakini ni asilimia 3 tu ya wanawake wanaomiliki ardhi, na zaidi ya asilimia 33 ya wanawake hufanyiwa ukatili wa jinsia.

Hivyo shindano la Mama shujaa linalenga kuwahamasisha, kuwawezesha na kuwasaidia wanawake na vijana katika sekta ya uzalishaji wa chakula. Hii ni kwasababu wanawake huzalisha zaidi ya asilimia 70 ya chakula chote kinachozalishwa nchini, ila kwa  bahati mbaya wanawake hao na watoto ndio wamekuwa waathirika wakubwa wa kwanza wa majanga ya njaa na utapiamlo. 
Khadija Liganga toka KIVULINI.
Naye Afisa Habari wa Kivulini Khadija Liganga amewahamasisha wadau wa Mwanza kujitokeza kwa wingi kesho katika viwanja vya Buhongwa jijini Mwanza kushuhudia yatakayojiri ikiwa ni pamoja na utoaji elimu ambapo mwisho wa siku fursa itakuwepo kwa watakao hitaji kushiriki kuchukua fomu zinazotolewa bure.
Wadau wa habari pamoja na waelimishaji kupitia sanaa nao walikuwepo kwenye mkutano wa utoaji taarifa.
Sekta muhimu habari.
Afisa Uchumi wa Uchochezi wa Oxfam Mkamiti Mgawe (katikati) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kushoto ni mmoja wa Wakurugenzi wa Maisha Plus Kaka Bonda na kulia ni meneja Kampeni ya Haki na Uchumi wa Oxfam Bi. Eluka Kibona.
Shughuli ikiendelea.
Point zikinaswa.
Wadau waliojitokeza leo kuchukuwa fomu mkoani Mwanza, wakijaza vielelezo muhimu kushiriki.