ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 25, 2018

VIONGOZI UPINZANI KONGO DR WALAANI PANGA LILILOKATA MAJINA YAO KUSHIRIKI UCHAGUZI UJAO.

Jean-Pierre Bemba, mmoja wa viongozi wa upinzani ambaye amezuiwa kugombea 
Viongozi wa vyama vya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wameijia juu Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo (CENI) kwa hatua yake ya kukata majina sita miongoni mwa majina ya waliojiandikisha kugombea kiti cha urais katika uchaguzi ujao nchini humo.
Kwa mujibu wa viongozi hao wa upinzani, panga hilo la kukata majina yao limesukumbwa na sababu za kisiasa tu na hivyo wametishia kwenda mahakamani kuiburuza Tume hiyo ya Uchaguzi (CENI) .
Miongoni mwa wapinzani mashuhuri ambao jinao lao limekumbwa na panga CENI, ni Jean-Pierre Bemba ambaye sasa hatoweza kushiriki kinyang'anyiro hicho.

UBALOZI WA INDIA WAFUNGUA FURSA ZA UWEKEZAJI MWANZA



NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella amesema kuwa bado milango ya fursa za uwekezaji iko wazi kwa wadau mbalimbali ndani na nje ya mkoa wake na nchi kwa ujumla hivyo ni vyema sasa kwa wafanyabiashara kutumia vyema mwanya huo kwaajili ya mapinduzi ya kimaendeleo.

Mhe. Mongella ametoa rai hiyo mwishoni mwa wiki wakati akifungua mkutano baina ya Balozi wa India nchini Tanzania na wafanyabiashara mkoani Mwanza kupitia taasisi ya wafanyabiashara wa kilimo na viwanda TCCIA uliofanyika katika ukumbi wa Rock City Mall Jijini hapa.

KIKWETE KUMUWAKILISHA RAIS JPM UAPISHO WA MNANGAGWA.


 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemtuma Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kumwakilisha katika sherehe za uapisho wa Rais mteule wa Jamuhuri ya Zimbabwe Mhe. Emmerson Dambudzo Mnangagwa zitakazofanyika jumapili tarehe 26 Agosti 2018 katika uwanja wa michezo wa Taifa mjini Harare.

MKOA WA MWANZA WAZINDUA MPANGO WA UUZAJI MATREKTA NA ZANA ZA KILIMO.


GSENGOtV
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella mnamo Agosti 16 mwaka 2018 amezindua programu ya uuzaji wa matrekta na zana za kilimo mkoani kwake, unaolenga kuboresha sekta ya kilimo na kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao mbalimbali.

WAZIRI UMMY AKABIDHI MADAWATI SHULE YA SEKONDARI TOLEDO TANGA ATOA NENO KWA WAZAZI NCHINI

 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga{CCM)  kulia akimkabidhi madawati 40 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Toledo ya Jijini Tanga Daudi Nchia ikiwa ni mkakati wake wa  kukabiliana na uhaba uliopo

 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga{CCM) kushoto akiwa amekaa kwenye moja ya madawati 40 aliyokabidhi kwa shule ya Sekondari Toledo Jijini Tanga
 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga{CCM) katika akiwa na Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Toledo Daudi Nchia mara baada ya kuwakabidhi madawati 40
 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga{CCM) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Toledo mara baada ya kuwakabidhi madawati 40


Na Mwandishi Wetu,Tanga.

WAZAZI kote nchini wametakiwa kuacha kulalamikia wadau wa elimu na badala yake wameshauriwa kushirikiana na walimu kukagua madaftari ya watoto wao kwa lengo la kuongeza ufaulu ili kupunguza mimba za utotoni zinazosababisha ndoto zao kushindwa kufikiwa.

Hayo yalisemwa NA  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati halfa ya kukabidhiano ya madawati na viti vyake 40 aliyoyatoa kwenye shule ya Sekondari Toledo ya Jijini Tanga.

Ummy ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chama cha Mapinduzi {CCM) mkoa wa Tanga alisema kimsingi wazazi wanapaswa kutambua kufanya hivyo kutawasaidia kuwawezesha vijana wao kuongeza ufaulu na hivyo kufanikiwa kuepukana na vishawishi ambavyo wanakabiliana navyo wakati wakiwa shuleni.

“Ndugu zangu wazazi na walezi lazima tutambue jukumu letu la kufuatilia maendeleo ya watoto wetu kwani hii ndio njia pekee inayoweza kuwasaidia kwa kushirikiana na walimu wao kwa lengo la kuwezesha kufikia ndoto zao”Alisema.

Naye ka upande wake Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa aliwataka wanafunzi kutumia fursa hiyo kuongeza jitihada kwenye kusoma ili azma ya serikali ya kuongeza ufaulu kwa shule zake iweze kufikiwa.

“Ndugu zangu wanafunzi mmepata madawati haya yatumieni vizuri kwenye matumizi yaliyokusudiwa kwa lengo la kuwawezesha kufikia malengo yenu kwa kuongeza ufaulu “Alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Sekondari Toledo Daudi Nchia alimshukuru Waziri Ummy kwa msaada huo na kuongeza kuwa bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa matundu ya vyoo vya wasichana .

Alisema kutokana na uhaba huo umesababisha wasichana na wavulana kushiriki katika huduma hiyo.

SAUTI:- SERIKALI YA MAREKANI KUINASUA WILAYA YA NJOMBE TOKA KWENYE KASI YA MAAMBUKIZI VVU.


GSENGOtV
Serikali ya marekani imeahidi kuendelea kushirikiana na jamhuri ya muungano wa Tanzania hususani mkoa wa Njombe katika kuendeleza jitihada za kupambana na kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi kutokana na mkoa wa Njombe kuendelea kuongoza kwa asilimia 11.6 nchini.

Akizungumza na mkuu wa mkoa wa Njombe CHRISTOPHER OLESENDEKA ofisini kwake Barozi wa Marekani nchini Tanzania INMI K PATTERSON baada ya kuwasili mkoani Njombe,anasema kutokana na ushirikiano wa mda mrefu baina ya serikali hizo mbili  hivyo serikali ya Marekani inaona nia ya kuongeza nguvu ili kutimiza adhma ya serikali ya Tanzania kufikia uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025

Friday, August 24, 2018

SERENGETI BOYS YAFA KIUME TAIFA.


Timu ya Uganda imefanikiwa kutinga fainali ya kufuzu Afcon u17 kwa kanda ya Africa Mashariki na kati baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Tanzania, Serengeti Boys magoli 3-1 Na sasa itacheza na Ethiopia katika fainali itakayochezwa Siku ya Jumapili August 26 saa 11:00 jioni katika dimba la Taifa Dar huku Tanzania itacheza mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu na Rwanda majira ya saa 8:00 mchana.

Tanzania tayari ana tiketi ya kushiriki michuano kama mwenyeji wa fainali za Afcon u17, 2019 zitakazofanyika Tanzania kuanzia May 12 hadi May 26 mwakani. Mshindi wa Ethiopia na Uganda atapata tiketi ya kushiriki fainali hizo kama mwakilishi kutoka Kanda ya Afrika Mashariki na Kati.

Timu 8 kutoka katika Kanda 7 za kisoka ndio zitashiriki michuano hiyo Tanzania kama mwenyeji, Cameroon nayo imefuzu kutoka kanda ya Kati, Angola nayo imefuzu kutoka kanda ya Kusini bado kanda 5 kuwajua wawakilishi ambao wataungana na timu hizo tatu kucheza fainali ya Afrika kwa chini ya umri wa miaka 17.

WENGER ATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA NA RAIS WEAH WA LIBERIA.

Rais wa Liberia George Weah amemtuza aliyekuwa meneja wa klabu ya Arsenal, Arsène Wenger na tuzo ya hadhi ya juu zaidi nchini Liberia kwenye sherehe iliyoandaliwa kwenye mji mkuu Monrovia.

Wenger alikuwa kocha wa kwanza wa Rais George Weah kwenye klabu ya Ulaya baada ya Wenger kumleta Monaco 1988.

Weah ndiye mwafrika wa kwanza kushinda tuzo la Fifa la mchezaji wa mwaka. Alistaafu kutoka soka mwaka 2003 na kuingia siasa.

Lakini ya hatua ya Wenger kutuzwa hatua hiyo imezua maoni tofauti nchini humo.

aadhi wanasema kuwa tuzo hiyo haistahili kupewa mtu binafsi kwa kile amemfanyia rais pekee.

Lakini tuzo hiyo si tuzo kuhusu uhusiano wa Rais na Wenger bali inatambua kile Wenger amechangia kwa michezo barani Afrika na kuwapa waafrika wengi fursa kwa mujibu wa waziri wa habari.


Ikulu.
Rais Weah amesema kuwa Wenger "alinitunza kama mtoto wake" wakati alijiunga na Monaco, akisema kuwa "kando na Mungu, anafikiri kuwa bila ya Wenger hakuna vile nigefanikiwa Ulaya".

SERIKALI WILAYANI ULANGA YASIFU JUHUDI ZINAZOFANYWA NA BODI YA KOROSHO NCHINI.

  Afisa Habari wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana akisistiza jambo kqwa Mkuu wa wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro Ngolo Malinya wakati wa ziara yao ya kuhamasisha wakulima umuhimu wa kuongeza tija ya kilimo hicho
  Afisa Habari wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana akisaini kitabu cha wageni ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ulanga mara baada ya kuwasili kulia kwake ni Mkuu wa wilaya hiyo Ngolo Malinya
 Mkuu wa wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro Ngolo Malinya akisistiza jambo
  Katibu Tawala wa wilaya ya Ulanga (DAS) Abraham Mwaikwila  akizungumza kuhusu namna walivyojipanga kuhimiza kilimo cha zao la Korosho wilayani humo
 Katibu Tawala wa wilaya ya Ulanga (DAS) Abraham Mwaikwila kulia akisisitiza jambo kwa Afisa Kilimo Bodi ya Korosho Tanzania Frank Mfutakamba mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake
 Afisa Habari wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana kushoto  akiagana na Katibu Tawala wa wilaya ya Ulanga (DAS) Abraham Mwaikwila mara baada ya kumaliza mazungumzo nae
 Afisa Habari wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana kulia akisistiza jambo wakati akitoa elimu kwa wakulima wa zao hilo kwenye kikundi cha  Igombiro wilayani Ulanga mkoani Morogoro
 Afisa Kilimo Bodi ya Korosho Tanzania Frank Mfutakamba  kulia akisisitiza jambo kwa wakulima hao kuhusu magonjwa hatari yanayolishambulia zao hilo wakati wa uzalishaji wake na namna ya kukabiliana nalo
 MKUU wa wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro Ngolo Malinya katika akiwa na Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana kulia kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Ulanga  (DAS) Abraham Mwaikwila akifuatiwa na  Afisa Kilimo Bodi ya Korosho Tanzania Frank Mfutakamba
Afisa Habari wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana kulia akionyeshwa kitu na mmoja wa wakulima wa zao la Korosho wa kikundi cha Igombiro wilayani Ulanga mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kuhamasisha umuhimu wa kulimo hicho

NA MWANDISHI WETU, ULANGA. 

SERIKALI wilayani Ulanga mkoani Morogoro imesifu jitihada kubwa zinazo fanywa na bodi ya Korosho Tanzania kwa kuwatembelea wakulima ili kuwahamasisha umuhimu wa kulima kilimo chenye tija ili kuongeza uzalishaji ikiwa ni mpango wa kuliendeleza zao hilo. 

Hayo yalibainishwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Ulanga (DAS) Abraham Mwaikwila wakati wakati wa ziara ya viongozi wa Bodi ya Korosho iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kilimo hicho kwa wakulima wilayani Ulanga ikiwemo upuliziaji wa dawa ili kuongeza uzalishaji. 

Viongozi wa bodi ya Korosho ambao walikuwa kwenye ziara hiyo ya uhama sishaji huo ni Afisa Habari wa Bodi ya Korosho Tanzania Bryson Mshana na Afisa Kilimo Bodi ya Korosho Tanzania Frank Mfutakamba ambao walikutana na wakulima wanaolima korosho wa kikundi cha Igombiro 

Alisema kwamba wilaya hiyo tokea miaka ya nyuma walikuwa wanalima korosho lakini baadae waliliacha kutokana na kutokuwa na soko la uhakika lakini kwa sasa ili kuhakikisha zao hilo linalimwa kwa tija mwaka jana walipewa ruzuku ya uzalishaji wa miche ya korosho laki tatu ambayo waliigawa kwa wakulima. 

“Sio hilo mikorosho ya zamani iliyokuwepo tulikuwa na Mkurugenzi aliyekuwa akiitwa Isabela Chiluba aliyetoka Tandahimba kwani baada ya kufika aliweza kuja na mwamko mzuri wa kufufua mikorosho ya zamani kwa mfano mwaka jana walipata pembejo na kupulizia mikorosho ya zamani jambo ambalo limefungua ukurasa mpya kwetu “Alisema. 

Alisema kutokana na hilo mwaka huu wanatarajia kuzalisha miche kwa wingi hivyo anaamini bodi ya korosho itakuwa na uhamasishaji mzuri na miche laki tatu iliyotolewa kwa hiyo mwaka huu itakuwa chachu ya wananchi kuhitaji miche utakuwa mkubwa sana. 

Hata hivyo aliiomba bodi ya Korosho kuweka utaratibu wa kuwapa miche ya korosho kutokana na kwamba asilimia kubwa ya mapato kwenye Halamshauri ya Ulanga yanatokana na mazao hivyo anaamini Mkurugezi na timu yake ya idara ya kilimo watajipanga kuhakikisha wanaenda kununua mbegu kwenye vituo vya naindelee ili waweze kupata miche iliyobora na kuwawezesha kuongeza uzalishaji wenye tija. 

Naye kwa upande wake, Mratibu wa zao la Korosho wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro Samweli Masaro alisema kutokana na kuwepo kwa uhamaishaji huo umewawezesha kuongeza uzalishaji kufikia tani 80. 

Ambapo awali ulikuwa kwa kiwango cha chini hali iliyowa ikiwalazimu kutilia mkazo uzalishaji wa zao hilo kwa kuhamasishaji wakulima kulima ikiwemo kutunza miti yao na kupiga dawa jambo ambalo kwa asilimia kubwa limesaidia kuweza kuwawezesha kupata tani hizo ambazo pia wanatarajia huenda zikaongezeka 

WAZANZIBARI SASA KUTAMBULIWA KIDIGITALI (E-ID CARD)



Baadhi ya Vituo vya Usajili vinavyokamilishwa kila kila wilaya ya Unguja na Pemba 
Mifumo mipya iliyofungwa ili kuhifadhi kumbukumbu kisasa (kidigitali).
Baadhi ya Vifaa vilivyoko ndani ya vituo vipya.
Baadhi ya Vifaa vilivyoko ndani ya vituo vipya .
Jengo jipya ambapo Ofisi kuu ya Wakala wa usajili wa matukio ya Kijamii Zanzibar 
Mambo Msiige jengo la mwanzo lililotunza kumbukumbu za Wazanzibar za maswala ya matukio ya kijamii 

Zaharan Nassor Mhifadhi Mkuu wa Nyaraka wa wakala wa usajili wa matukio ya kijamii Zanzibar akionyesha Nyaraka Kongwe zaidi yenye majina ya Uzazi kuanzia mwaka 1909 hadi 1911 
Mhifadhi akichambua Taarifa katika Ghala la Nyaraka Ofisi kuu ya Mamlaka ya Usajili matukio ya kijamii Zanzibar. 
Dr Hussein Khamis Shaaban, Mkurugenzi mtendandaji wa wakala wa usajili wa matukio ya kijamii akikagua Nyaraka za Kale za vizazi na vifo ambazo zinachakatwa kuwekwa katika mfumo wa Kidigitali
Nyaraka zenye kumbu kumbu za wazanzibari za Uzazi, Vifo, Talaka, Ndoa na na utambulisho tangu 1909
Msajili wa vizazi na vifo Wilaya ya Kati Mkoa wa kusini Unguja akichambua Taarifa za mwananchi ili kujaza vyeti mbali mbali vya Wazanzibar 
*Ni baada ya kuimarishwa kwa mifumo ya kuhifadhi taarifa kieletroniki.

WENGER ATUA KWA WEAH, KUPOKEA TUZO MAALUM.






Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger, yupo nchini Liberia kupokea tuzo maalumu ya heshima kutoka kwa Rais wa nchi hiyo, George Weah.

Wenger alimsajili Weah kama mchezaji mwaka 1988 wakati akifundisha Monaco.

SALAMU ZA RC MONGELLA KWENYE MAZISHI YA BIBI WA RC MAKONDA.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella leo Agosti 23, 2018 ameungana waombolezaji mbalimbali kushiriki mazishi ya Bi. Anna Makwega Manasse (81) ambaye ni bibi wa Mhe.Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa Dar es salaam.

Mazishi ya Bi. Manasse ambaye alifariki dunia juzi Agosti 21, 2018 akiwa katika hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu, yamefanyika katika makaburi ya nyumbani yaliyopo Kahangala wilayani Magu.
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella akitoa pole kwa wanafamilia

MWANDISHI MATHIAS CANAL ATUPA UKAPELA, WAZIRI TIZEBA AMPA OFA MAALUMU

Mwandishi Mathias Canal akionyesha cheti cha ndoa aliyoifunga Jumamosi tarehe 18 Agosti 2018 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Mabibo Farasi Jijini Dar es salaam na mkewe Bi Elizabeth Chagamba.
Mwandishi Mathias Canal na mkewe Bi Elizabeth Chagamba (walioketi) pamoja na watumishi wa Wizara ya Kilimo wakiongozwa na waziri wa wizara hiyo Mhe Dkt Charles Tizeba, Watumishi kutoka Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wakati wa hafla ya jioni baada ya ibada ya ndoa Takatifu tarehe 18 Agosti 2018 katika eneo la Urafiki Social Hall Ukumbi wa Nyangumi Jijini Dar es salaam.
Mwandishi Mathias Canal akivishwa Pete na mkewe Bi Elizabeth Chagamba wakati wa ibada ya ndoa Takatifu iliyofanyika katika kanisa la kiinjili la kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Mabibo Farasi jijini Dar es salaam tarehe 18 Agosti 2018.
Mwandishi Mathias Canal akimtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji J. Mtaturu wakati wa tafrija iliyofanyika eneo la Urafiki Social Hall ukumbi wa Nyangumi baada ya ibada ya ndoa Takatifu iliyofanyika katika kanisa la kiinjili la kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Mabibo Farasi jijini Dar es salaam tarehe 18 Agosti 2018.
Bwana harusi Mathias Canal na Bi harusi Elizabeth Chagamba wakicheza wimbo maalumu ulioimbwa na msanii wa midondoko ya (RnB) Elias Barnabas maarufu Barnaba Boy Classic wakati wa tafrija iliyofanyika eneo la Urafiki Social Hall ukumbi wa Nyangumi baada ya ibada ya ndoa Takatifu iliyofanyika katika kanisa la kiinjili la kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Mabibo Farasi jijini Dar es salaam tarehe 18 Agosti 2018.

Na Mwandishi Wetu, Wazohuru Blog

Mwandishi na mchambuzi wa Habari nchini Tanzania ambaye ni Afisa Habari Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA)-Wizara ya kilimo ameingia kwenye historia ya vijana wachache waliofanya maamuzi ya busara na tija katika mustakabali wa maisha mema katika jamii kwa kufunga ndoa Takatifu.

Ibada ya ndoa Takatifu ilifanyika siku ya jumamosi tarehe 18 Agosti 2018 kuanzia majira ya saa sita na nusu (6:30) mchana mpaka saa nane na nusu (8:30) mchana katika kanisa la Kiinjili La Kilutheli Tanzania-Usharika wa Mabibo Farasi Jijini Dar as salaam.

Mathias Canal amefunga ndoa na Binti mstaarabu, wenye nidhamu na busara huku akiwa mcha Mungu Bi Elizabeth Chagamba mzaliwa wa Tanga ambaye kihistoria tangu kufahamiana urafiki wao umedumu kwa takribani miaka sita mpaka kufikia maamuzi ya kufunga ndoa Takatifu.

Ibada hiyo ya ndoa Takatifu iliendeshwa na Mchungaji Remmya Chuma kutoka kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania Dayosisi ya Mashariki ya Pwani Usharika wa Kawe Jijini Dar es salaam ambapo aliwataka Bwana Harusi Mathias Canal na Bi Elizabeth Chagamba kuishi kwa kuzingatia misingi ya ndoa na agano Takatifu baina yao na Mungu kwani ndoa yao imeshuhudiwa na watu duniani lakini shahidi pekee mwenye maono zaidi ya ndoa hiyo ni Mungu mwenyewe.

Mchungaji Chuma aliwakumbusha waumini wengine katika ibada hiyo kumshukuru Mungu kwa kila hatua wanazopita huku akiwasihi waumini hususani vijana ambao hawajafunga ndoa Takatifu kuingia katika tendo hilo muhimu machoni pa wanadamu na Mungu wa Mbinguni. Na kuongeza kwa kunukuu Kitabu cha Mathayo 19:5 kisemacho, "Kwa sababu hiyo mtu atamwacha Baba na Mama yake ataambatana na Mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja"

Mara baada ya Ndoa Takatifu kati ya Afisa Habari NFRA Ndg Mathias Canal na Bi Elizabeth Chagamba kukamilika kanisani ilihudhuriwa na tafrija fupi iliyofanyika katika eneo la Urafiki Social Hall katika ukumbi wa Nyangumi ambapo hafla hiyo ilihudhuriwa na mamia ya wananchi huku viongozi mbalimbali wa Chama na serikali wakihudhuria.

Kwa upande wa Chama cha Mapinduzi ndoa hiyo ilihudhuriwa na Timu ya uenezi kutoka Chama Cha Mapinduzi Taifa, Mohammed Alliyan Kaimu Katibu wa Idara ya oganaizesheni na uhusiano wa kimataifa Umoja wa Vijana (UVCCM) Makao makuu pamoja na wasaidizi wa Mwenyekiti na Katibu Mkuu UVCCM Taifa.

Kwa upande wa serikali hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba (Mb) ambaye katika salamu alizozitoa kwa niaba ya Wizara yake alisema kuwa Ndoa ni muunganiko wa kiagano wa kudumu kati ya mwanaume mmoja na mwanamke mmoja wenye kuishi na kuwa mume na mke. Neno agano ni neno muhimu sana kwa sababu agano ni patano la milele ambaye shahidi yake ni Mungu mwenyewe wala si mwanadamu hivyo kuwataka sana ndoa hao kuwa waaminifu milele.

Aidha, alitaja umahiri katika utendaji unaofanywa na wasaidizi wake akiwemo Mathias Canal pamoja na mwenzake Innocent Masaka kuwa ni wadogo sana kwake kiumri lakini wamekuwa msaada mkubwa katika kutekeleza majukumu ya serikali yakiwemo na yale ya Chama cha Mapinduzi.

Katika hafla hiyo Mhe Dkt Tizeba alisema kuwa Fungate ni jambo muhimu baada ya ndoa Takatifu hivyo akatoa ofa maalumu kwa maharusi hao kwenda mapumzikoni Mjini Unguja-Zanzibar huku akisema kuwa gharama zote za siku tano atagharamia yeye. Pia Dkt Tizeba ametoa ofa ya mapumziko ya siku tano kwa Ndg Mathias Canal ambaye muda wake wa mapumziko ulikuwa umemalizika hivyo kuendelea na mapumziko ya siku tano.

Tayari Mathias Canal na Mkewe Bi Elizabeth Chagamba wamewasili Mjini Unguja-Zanzibar ambapo katika mapumziko hayo wamesafiri na wapambe 10 waliohudumu katika sherehe yao (Maids) ili kufurahi kwa pamoja katika mapumziko hayo.