NA MWANDISHI WETU, ULANGA.
SERIKALI wilayani Ulanga mkoani Morogoro imesifu jitihada kubwa zinazo fanywa na bodi ya Korosho Tanzania kwa kuwatembelea wakulima ili kuwahamasisha umuhimu wa kulima kilimo chenye tija ili kuongeza uzalishaji ikiwa ni mpango wa kuliendeleza zao hilo.
Hayo yalibainishwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Ulanga (DAS) Abraham Mwaikwila wakati wakati wa ziara ya viongozi wa Bodi ya Korosho iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kilimo hicho kwa wakulima wilayani Ulanga ikiwemo upuliziaji wa dawa ili kuongeza uzalishaji.
Viongozi wa bodi ya Korosho ambao walikuwa kwenye ziara hiyo ya uhama sishaji huo ni Afisa Habari wa Bodi ya Korosho Tanzania Bryson Mshana na Afisa Kilimo Bodi ya Korosho Tanzania Frank Mfutakamba ambao walikutana na wakulima wanaolima korosho wa kikundi cha Igombiro
Alisema kwamba wilaya hiyo tokea miaka ya nyuma walikuwa wanalima korosho lakini baadae waliliacha kutokana na kutokuwa na soko la uhakika lakini kwa sasa ili kuhakikisha zao hilo linalimwa kwa tija mwaka jana walipewa ruzuku ya uzalishaji wa miche ya korosho laki tatu ambayo waliigawa kwa wakulima.
“Sio hilo mikorosho ya zamani iliyokuwepo tulikuwa na Mkurugenzi aliyekuwa akiitwa Isabela Chiluba aliyetoka Tandahimba kwani baada ya kufika aliweza kuja na mwamko mzuri wa kufufua mikorosho ya zamani kwa mfano mwaka jana walipata pembejo na kupulizia mikorosho ya zamani jambo ambalo limefungua ukurasa mpya kwetu “Alisema.
Alisema kutokana na hilo mwaka huu wanatarajia kuzalisha miche kwa wingi hivyo anaamini bodi ya korosho itakuwa na uhamasishaji mzuri na miche laki tatu iliyotolewa kwa hiyo mwaka huu itakuwa chachu ya wananchi kuhitaji miche utakuwa mkubwa sana.
Hata hivyo aliiomba bodi ya Korosho kuweka utaratibu wa kuwapa miche ya korosho kutokana na kwamba asilimia kubwa ya mapato kwenye Halamshauri ya Ulanga yanatokana na mazao hivyo anaamini Mkurugezi na timu yake ya idara ya kilimo watajipanga kuhakikisha wanaenda kununua mbegu kwenye vituo vya naindelee ili waweze kupata miche iliyobora na kuwawezesha kuongeza uzalishaji wenye tija.
Naye kwa upande wake, Mratibu wa zao la Korosho wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro Samweli Masaro alisema kutokana na kuwepo kwa uhamaishaji huo umewawezesha kuongeza uzalishaji kufikia tani 80.
Ambapo awali ulikuwa kwa kiwango cha chini hali iliyowa ikiwalazimu kutilia mkazo uzalishaji wa zao hilo kwa kuhamasishaji wakulima kulima ikiwemo kutunza miti yao na kupiga dawa jambo ambalo kwa asilimia kubwa limesaidia kuweza kuwawezesha kupata tani hizo ambazo pia wanatarajia huenda zikaongezeka
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.