ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 26, 2012

STELLA AGUSTINO NDIYE MISS ILEMELA 2012-2013

Mshindi wa taji la miss Ilemela 2012 Stella Agustino (katikati) akiwa na mshindi wa pili Hapiness (kushoto) na mshindi wa tatu

Majaji miss Ilemela 2012.
Wadau katika pozi kushuhudia tukio...

Warembo walioingia kumi bora miss Ilemela 2012.
Sharowbarow President Bob junior akimalizaaaaa...
Flash na sehemu ya Gold Crest Hotel.

Mshiriki namba moja.

Mshiriki namba 2.

Mshiriki namba 3.

Mshiriki namba 9.

Mshiriki namba 4.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya toka jijini Mwanza Dogo Baraka ni sehemu ya burudani iliyowakonga wengi waliofika kushuhudia miss Ilemela akitunukiwa taji usiku wa tarehe 25/05/2012

Pichani huyu si mshiriki miss Ilemela 2012 bali ni sehemu ya Onyesho la mavazi ya Harusi toka Munira Classic.

Wadau wakichukuwa matukio.com hapa ni mwendo wa face book.

Onesho la mavazi ya harusi toka duka la mavazi ya harusi na sendof na urembo Munira Classic.

Mbunifu wa mavazi Munira akitambulishwa mbele ya umma uliojitokeza.

Mc wa tukio Mr. G. Sengo toka Clouds Fm Mwanza.Meza ya majaji chini ikitafakari muonekano wa kwanza kupitia open show ya Miss Ilemela 2012.

Ze pipooo.

Wadadaz wakipata flash kwa blog....

Ni moja kati ya burudani zilizokuwepo kwenye kinyang'anyiro cha kumsaka miss Ilemela 2012 anaitwa Anna kutoka nchini Namibia akicheza Belly Dance.
Hapa Chief Judge Muhksin Mambo toka Star Tv (nyuma ya mshiriki no 7) alipokuwa akitaja kumi bora.

Ze flawaz..

Kipaji toka moyoni mshiriki wa kinyang'anyiro miss Ilemela Stela akionyesha kipaji cha kucheza wimbo wa Fally Ipupa - Bakanja.

Mshiriki wa kinyang'anyiro cha Miss Ilemela  Hapiness akichora ndani ya kuonyesha vipaji.

Kipaji toka moyoni mshiriki Zaifath kipaji cha kuimba.

Afisa Promosheni wa Nyanza Bottling Co. LTD watengenezaji wa soda jamii ya Coca cola Mr.Rutta, akimkabidhi mshindi nafsi ya 3 cheki ya shilingi laki mbili.

Afisa Promosheni wa Nyanza Bottling Co. LTD watengenezaji wa soda jamii ya Coca cola Mr.Rutta, akimkabidhi mshindi wa nafsi ya pili Hapiness, cheki ya shilingi laki tatu.
Afisa Promosheni wa Nyanza Bottling Co. LTD watengenezaji wa soda jamii ya Coca cola Mr.Rutta, akimkabidhi Miss Ilemela 2012 Stella Agustino, cheki ya shilingi laki tano.

Thursday, May 24, 2012

MARAIS WASTAAFU NANE WA NCHI ZA AFRIKA WAKUTANA NCHINI AFRIKA KUSINI KWA SIKU TATU.
                                              Pichani shoto ni Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania,Mh Benjamini Mkapa akichangia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye mkutano wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika,mapema leo jioni,mkutano huo umefanyika kwenye moja ya kumbi ya   chuo  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini.Pichani kati ni Rais mstaafu Pedro Pires wa Cape Verde na mwisho ni Rais mstaafu wa Benin,Nicéphore Dieudonné Soglo.


                                                                  Pichani kulia ni Rais mstaafu wa Benin,Nicéphore Dieudonné Soglo akifafanua jambo kwa makini wakati wa mchakato wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika ulipokuwa umepamba moto jioni ya leo,katika mkutano uliofanyika kweny moja ya kumbi ya   chuo  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini mapema leo mchana,Pichani kati ni Rais mstaafu Pedro Pires wa Cape Verde na   Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania,Mh Benjamini Mkapa
                                                                              Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijili kwenye mkutano huo
                                                                           Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijili kwenye mkutano huo
                                                                                                                                                   Pichani juu na chini Mkutano wa kujadili   maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika ukiendelea ndani ya chuo  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini mapema leo mchana.

                                                                                                                                                   Baadhi ya Marais Wastaafu kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakiwa kwenye mkutano wa kujadili   maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.
                                                                                                                                                    Kutoka kushoto ni Balozi Charles Stith  ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania,ambaye pia ni Mratibu mkuu wa mkutano akifafanua jambo kwa wageni waalikwa mbalimbali waliofika kuhudhuria Mkutano huo mapema leo mchana.
                                                                                                                                           Kutoka kushoto ni Balozi Charles Stith  ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania,Rais Nicéphore Dieudonné Soglo wa Benin,Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar,Rais Ali Hassan Mwinyi wa Tanzania,Rais Thambo Mbeki wa Afrika Kusini,Rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria,Rais Pedro Pires wa Cape Verde, Rais Benjamin Mkapa wa Tanzania na Rais Rupiah Banda wa Zambia wakiwa katika picha ya pamoja mapema leo mchana kabla ya kuanza mkutano wa kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.
                                                                                             Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Tanzania,Mh Benjamini Mkapa akijadiliana jambo na Rais Nicéphore Dieudonné Soglo wa Benin walipokuwa wakiwasili kwenye viunga vya vya chuo  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini mapema leo kwa ajili ya kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.

Pichani  mbele ni Marais Wastaafu wa Tanzania,Ally Hassan Mwinyi na  Benjamin Mkapa sambamba  na  Marais wengine wakiwasili katika viwanja vya chuo  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini mapema leo kwa ajili ya kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.
                                                                                                    Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali kutoka nchini Tanzania,wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini mapema leo kwa ajili ya kuripoti mkutano wa kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.Shoto ni Yvonne Msemembo (ITV) ,Joseph Kulangwa (Tanzania Standard News Paper),Nestor Mapund,Absolom Kibanda (Free Media),Mzee Theophili Makunga (Mwananchi Communications), Muondosha Mfanga (The Guardian) pamoja na Deus Mjatta (ITV).
                                                                                                    Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali wakijadiliana jambo nje ya ukumbi,kabla ya kuanza kwa Mkutano huo,Shoto ni Absolom Kibanda (Free Media),Mzee Theophili Makunga (Mwananchi Communications),Joseph Kulangwa (Tanzania Standard News Paper), Muondosha Mfanga (The Guardian).
                                                                                      Baadhi ya wanafunzi kutoka vyo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja mapema leo kabla ya kuanza kwa mkutano wa kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika,ambao umewashirikisha Marais Wastaafu nane wa Afrika. 
========  ====== ========
Marais Wastaafu nane wa nchi za Afrika wakutana nchini Afrika Kusini.
Marais Wastaafu nane wa nchi za Afrika wamekutana leo jijini Johannesburg, Afrika Kusini na kufanya mkutano wa siku tatu ndani ya chuo kikuu cha Witwatersrand. Ajenda kuu ya mkutano huo ni kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.

Marais wastaafu hao waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria, Rais Ali Hassan Mwinyi wa Tanzania, Rais Nicéphore Dieudonné Soglo wa Benin, Rais Pedro Pires wa Cape Verde, Rais Benjamin Mkapa wa Tanzania, Rais Joaquim Chissano wa Msumbiji, Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar na Rais Rupiah Banda wa Zambia.

Aidha - mbali ya Marais hao waliohudhuria mkutano huo, pia ulihudhuriwa na  Wataalam mbalimbali wa nishati, viongozi wa umma na sekta binafsi na wanafunzi na kitivo kutoka vyuo vikuu 9 vya kimataifa kikiwemo chuo kikuuu mwenyeji cha Witwatersrand a.k.a Wits. Tanzania iliwakilishwa na wanafunzi watano na walimu wawili kutoka chuo kikuu cha Dar-es-Salaam.

Mratibu mkuu wa mkutano huo - Balozi Charles Stith  ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kujadiliana juu ya ufumbuzi wa mageuzi ya nishati katika nchi za Kiafrika, na kuhakikisha nchi za Afrika zinajiwakilisha vyema katika kukabiliana na changamoto mbalimbali katika suala zima la Nishati.

Balozi Stith alisema kuwa mkutano huo utaleta mshikamano wa pamoja kwa viongozi wa sekta ya nishati na wafadhili mbalimbali wa miradi mbalimbali, ili kuhakikisha nishati hiyo inatosheleza mahitaji ya Afrika kwa ujumla. Mkutano huo wa siku 3 utafikia tamati Mei 25.

MBUNGE WA ROMBO JOSEPH SELASINI APATA AJALI MBAYA WATATU WAFARIKI DUNIA

Mbunge wa Rombo, Mhe. Joseph Selasini amepata ajali mbaya sana wakati alipokuwa akiendesha gari lake mkoani Kilimanjaro, ambapo watu 3 kati ya watu 6 waliokuwemo kwenye gari hilo wamepoteza maisha na miili yao imechukuliwa na gari la polisi na kupelekwa hospitali ya KCMC Moshi kutoka Boma Ng'ombe.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Absalom Mwakyoma amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo akielezea zaidi amesema Ilikuwa ni saa 1:00 jioni maeneo ya Boma Ng'ombe ambapo Mh Joseph Selasini wakati akiendesha gari hilo akitokea Arusha, ghafla aliona mwendesha Pikipiki wakati akijaribu kumkwepa ndipo gari lake likapinduka.

Watu wengine akiwemo mbunge huyo na mkwe wake alifahamika kwa jina la Digna Kavishe waliojeruhiwa katika ajali hiyo, wako katika hospitali ya Boma Ng'ombe hali zao zinaendelea vizuri na muda mfupi nao watapelekwa katika hospitali ya KCMC kwa matibabu zaidi
Chanzo: Full Shangwe

TANZANIA MUAY-THAI ACADEMY OF COMBAT

WKF TANZANIA has new leader ship. Kuanzia 3-9 may 2012 NIMESHIRI KWA MARA YA PILI 2011 .IFMA .WMC. Terhan Iranian kwenye mashindano ya dunia. Muay-thai world competitions cup SPORT AND PEACE .tulikua nchi 51 akiwemo Tanzania.
Dar es salam Tanzania, with immediate effect we have a new WKF office in Tanzania. Our new WKF TANZANIA president is Mr. Emmanuel SHIJA. He is expert in Muay Thai and leader of “Tanzania Muay Thai academy” in Daressalam.

This is the biggest City in Tanzania, located on the Indian Ocean. Soon we will see the professional fighters of Tanzania in the World ranking. Mr. Shija confirmed also the participation of the team in the World Championship in Varazdin, Croatia in July.
Emmanuel SHIJA wa pili kutoka kushoto akiwa na wapiganaji wenzake kabla ya kupanda ulingoni katika mashindano ya Muay thai academy of combat yaliyokua yakifanyika nchini Iran hivi karibuni.

Emmanuel SHIJA akiwa na shabiki wake baada ya kupigana nchini irani hivi karibuni.
Na. Super Boxing Coach.

KESI YA UBUNGE JIMBO LA UBUNGO MNYIKA AIBUKA KIDEDEA

Kesi ya kupinga matokeo ya jimbo la Ubungo jijini Dar es salaam iliyokuwa ikimkabili mbunge wa jimbo hilo Peter Mnyika hatimaye imempa ushindi mbunge huyo.

Kesi hiyo namba 107 ya 2010, ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CCM, Hawa Ngh’umbi dhidi ya Mnyika ambaye  katika kesi hiyo alikuwa akitetewa na Wakili Edson Mbogoro, walidai kuwa kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu na kisheria katika ujumlishaji wa kura na utangazaji wa matokeo ambao umeathiri matokeo hayo.

Katika uchaguzi huo, uliofanyika Oktoba 31, 2010, Msimamizi wa Uchaguzi, Raphael Ndunguru alimtangaza Mnyika kuwa mshindi Novemba 2, 2010 baada ya kupata kura 66,742. Ngh’umbi alipata kura 50,544. Hata hivyo, Ngh'umbi hakuridhishwa na matokeo hayo akaamua kufungua kesi Mahakama Kuu kuyapinga, akimtumia Wakili Issa Maige.


Pia katika kesi hiyo imemalizika leo kwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kumpa ushindi bwana Mnyika, imemwamuru  mlalamikaji Hawa Ng'humbi kufidia gharama zote za uendeshaji kesi baada ya shauri lake kutupiliwa mbali.