Kesi hiyo namba 107 ya 2010, ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CCM, Hawa Ngh’umbi dhidi ya Mnyika ambaye katika kesi hiyo alikuwa akitetewa na Wakili Edson Mbogoro, walidai kuwa kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu na kisheria katika ujumlishaji wa kura na utangazaji wa matokeo ambao umeathiri matokeo hayo.
Katika uchaguzi huo, uliofanyika Oktoba 31, 2010, Msimamizi wa Uchaguzi, Raphael Ndunguru alimtangaza Mnyika kuwa mshindi Novemba 2, 2010 baada ya kupata kura 66,742. Ngh’umbi alipata kura 50,544. Hata hivyo, Ngh'umbi hakuridhishwa na matokeo hayo akaamua kufungua kesi Mahakama Kuu kuyapinga, akimtumia Wakili Issa Maige.
Pia katika kesi hiyo imemalizika leo kwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kumpa ushindi bwana Mnyika, imemwamuru mlalamikaji Hawa Ng'humbi kufidia gharama zote za uendeshaji kesi baada ya shauri lake kutupiliwa mbali.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.