VICTOR MASANGU, PWANI ... HABARI ..OCTOBA 27 /2025
SERIKALI Mkoa wa Pwani imesema kwamba imejiandaa vya kutosha hususan katika hali ya ulinzi na usalama katika kuelekea katika uchagzuo mkuu wa mwaka 2025 ambaop unatarajiwa kufanyika octoba 29 mwaka huu ambayo itakuwa ni siku ya jumatano ya wiki hii.
Hayo yamebaishwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge wakati akizunhgumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na maandalizi ya kuelekea katika uchagzuzi huo ambapo amewaahimiza wanananchi wote wenye sifa kujitokeza kwa wingi kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo.