ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, December 23, 2024

NONAFILTER MKOMBOZI WA MAJI SAFI NA SALAMA TANZANIA

 

NA. MWANDISHI WETU

Teknolojia ya kuchuja maji ya "NANOFILTER" imeendelea  kuimarisha jitihada za usafi wa mazingira, upatikanaji wa maji safi na salama ili kuendelea kuhudumia jamii kwa kuwapata maji safi na salama ya kunywa hususani wanafunzi waliopo shule za Msingi na Sekondari nchini.


Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu kwa kushirikiana  na shirika la ActionAid Tanzania (AATZ), imeratibu ziara ya kikazi ya maafisa kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa "TAMISEMI", Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu, Wizara ya Maji, Wizara ya Fedha,  wametembelea eneo la Ngongali TASS  (Tanzania Adventist Secondary School) iliyopo wilayani Arumeru Mkoani Arusha na makao makuu ya "NANOFILTER" Jijini Arusha, tarehe 22 Disemba, 2024.

Lengo la ziara hiyo ni kujifunza na kuongeza ufahamu juu ya uvumbuzi wa teknolojia hiyo ya "NANOFILTER" na  Matumizi yake.



Katika ziara hiyo wamepata fursa ya  kujionea teknolojia ya kuchuja maji ili kupata maji safi na salama ya kunywa, kupitia mvumbuzi wa teknolojia hiyo, Profesa Askwar Hilonga, kutoka Taasisi ya Nelson Mandela.


Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Profesa Askwar Hilonga amesema kuwa teknolojia ya kuchuja maji lengo lake kuu ni kukabiliana na magonjwa yatokanayo na bakteria waliopo kwenye maji na kemikali hatarishi katika maji ya kunywa.


Kwa upande wake mwakilishi kutoka shirika la ActionAid, Profesa Oskar Mkasa alipongeza na kumshukuru Profesa Askwar Hilonga kwa elimu aliyoitoa kwa washiriki wa ziara hiyo,  na jitihada aliyoitumia katika kuvumbua mashine hizo, na kusisitiza kuwa, lengo la ziara hiyo pamoja na kujifunza watahakikisha, teknolojia hiyo wanaiwezesha  kuzifikia  shule za msingi na sekondari elfu ishirini na Tina (29000) Tanzania Bara, shule elfu moja na mia mbili (1200) kwa upande wa Zanzibar, ili kuziwezesha kupata maji safi na salama.


KASESELA MBUNGE, DIWANI UKISHINDWA UCHAGUZI JILAUMU MWENYEWE

 

Mjumbe wa Halmshauri kuu ya chama cha Mapinduzi (CCM) taifa (MNEC) Richard Kasesela akisisitiza mambo mazuri aliyoyafanya Rais Dkt samia Suluhu Hassan kwenye kila jimbo na kata hapa nchini 

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Daud Yassin akikabidhi MNEC Salim Abri Asas tuzo ya mchango wake mkubwa ndani ya chama cha Mapinduzi mkoa wa Iringa 


Na Fredy Mgunda, Iringa.

Mjumbe wa Halmshauri kuu ya chama cha Mapinduzi (CCM) taifa (MNEC) Richard Kasesela amesema kuwa Mbunge au Diwani atakayeshindwa kutetea nafasi yake ajilaumu mwenyewe kwa kuwa Rais Dkt samia Suluhu Hassan ametekeleza mikubwa kwenye kila jimbo na kata kulingana na ila ya CCM ya 2020/2025.


Kasesela aliyasema hayo katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Iringa, ambapo alisisitiza kuwa kazi kubwa zilizofanywa na Rais Samia zinawapa urahisi viongozi waliopo kuendelea na nafasi zao, na iwapo watashindwa, ni wao wenyewe watakaojilaumu.


Katika hatua nyingine, alimpongeza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Salim Abri Asas, kwa mchango wake mkubwa ndani ya chama hicho, ambao umekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya chama hicho.


Aidha, alikipongeza chama hicho kwa ushindi wa asilimia 99.99 katika uchaguzi wa serikali za mitaa, akisisitiza kuwa CCM kimeshinda kwa haki na hiyo ndiyo sababu ya kutokuwepo malalamiko kutoka vyama vya upinzani.

ADEM FAFANYA KWELI YATOA MSAADA GEREZA LA KIGONGONI BAGAMOYO

 


NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO 


Katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuisaidia jamii   Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu-ADEM imeamua  kufanya ziara maalumu yenye lengo la  kutembelea wafungwa katika gereza la Kigongoni lilipo Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani na kutoa  misaada ya mahitaji ya msingi na vitu mbalimbali ambavyo vitawasaidia katika gereza hilo.

 Akizunngumza Katika ziara hiyo mkurugenzi wa taaluma wa ADEM Bugendi Joseph amesema  kwamba  wamepata  fursa ya kutembelea gereza hilo na kutoa mahitaji kama vile  miswaki, dawa za meno, viwembe, sabuni, unga na mchele  kwa kuzingatia mahitaji ya wafungwa.


Pia Bugendi amebainisha kwamba mbali na kutembelea gereza hilo pia  watumishi pamoja na wanafunzi wa ADEM wametembelea kituo cha kulelea watoto wanaotoka katika mazingira magumu cha  Amani Orphanage Center kilichopo katika Kata ya Zinga Wilayani Bagamoyo na kutoa msaada wa mahitaji  mbalimbali ikiwemo  vyakula, nguo, vifaa vya shule, na mahitaji mengine madogo madogo ya watoto wanaohudumiwa katika kituo hicho.


Aidha Mkurugenzi amesema  sambamba na kukabidhi msaada huo uongozi wa Adem ukaamua kuchangia  kiasi cha shilingi laki nane kwa ajili ya kuwasaidia katika  kuboresha mazingira ya nyumba yao wanayoishi hasa miundombinu ya umeme. 

Aidha, ziara hiyo pia imehusisha kutembelea Kaya zisizojiweza katika Kaya ya Kisutu, Bagamoyo ambazo zilibainishwa na Wenyeviti wa Mitaa katika Kata hiyo ambapo kaya zipatazo 13 zilisaidiwa mahitaji ya chakula na nguo.

Bugendi katika hatua nyingine amebainisha kwamba lengo la chuo hicho ni kuweka mikakati ya kuandaa wataalamu na viongozi mahiri ambao watakwenda kusaidia katika sekta ya elimu hapa nchini.


Naye Rais wa Serikali ya Wanafunzi-ASO Bw. Joshua Raphael  mara baada ya kukamilika kwa ziara hiyo amesema, wao kama wanachuo wa ADEM kwa kushirikiana na Menejimenti ya ADEM wanaona fahari kubwa kushirikiana na jamii inayowazunguka hasa kwa kuisaidia jamii katika mshitaji mbali mbali.


Adem imekuwa mstari wa mbele katika kufanya  Ziara kama hizo ambazo uwa zinafanyika  kila mwaka ili kurudisha huduma kwa jamii na mskundi mbali mbali  ikiratibiwa na Ofisi ya huduma saidizi za wanafunzi pamoja na Serikali ya Wanachuo wa ADEM-ASO.