ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 14, 2012

BUBU AFANYA KWELI EBSS MWANZA...



Kwa mara ya kwanza jiji la Mwanza limetia fora na limeweka historia ya kupata mshiriki mmoja aliyeingia kwenye shindano la Epiq Bongo Star Search akiwa na ulemavu wa sauti  (bubu-yaani asiyeweza kuongea kawaida)  hali iliyopelekea majaji wa mchuano huo kuvutiwa na mikogo yake iliyopelekea ushawishi uliowafanya waingie kingi kiasi cha kumpa nafasi ya kuingia hatua ya pili ya mchakato huo.. Hebu mshuhudie kupitia kideo na makamuzi ya hip hop pindi tu alipotoka kwenye usaili na kutajwa kwamba amesonga mbele.

TENGA AONGOZA MAELFU KATIKA MSIBA WA MWENYEKITI WA CHAMA SOKA MARA

Rais wa shirikisho la soka hapa Nchini (TFF) Leodiger Tenga akitoa salamu za shirikisho.
 Rais wa shirikisho la soka hapa Nchini (TFF) Leodiger Tenga ameongoza maelfu ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha soka Mkoani Mara (FAM) na mjumbe wa kamati ndogo ya mahesabu ya (TFF) Fabian Samo yaliyofanyika nyumbani kwake maeneo ya Nyakato katika Manispaa ya Musoma.

Makongoro Nyerere ambaye ni mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere.
Akitoa salamu kwa upande wa Serikali kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tuppa ambaye pia alikuwepo msibani hapo Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara Makongoro Nyerere alisema licha ya kujishughulisha na kupenda masuala ya michezo marehemu Fabian Samo alikuwa ni kiongozi mzuri katika masuala ya siasa na kiongozi mvumilivu tangu alipokuwa Diwani na makamo Mwenyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya Musoma kwa kipindi cha miaka 10.

Makongoro alisema ili kumuenzi kiukweli marehemu Fabian Samo ni kufuata yale yote mazuri aliyoyaacha kwa dhati na kuwa wawazi katika masuala ya uongozi kama ambavyo alikuwa akifanya kiongozi huyo.

Heshima za mwisho.
  Marehemu Fabian Samo alizaliwa mwaka 1944 katika kijiji cha Wegero Wilaya ya Musoma vijijini ameacha mjane,watoto 12 na wajukuu 17.

Michael Wambura mdau wa soka.
 Akizungumza kwa niaba ya wadau wa soka katika kutoa saramu za rambirambi,aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha soka zamani (FAT) Michael Wambura alisema pengo walilopata wadau wa soka kufuatia kifo cha Fabian Samo halitazibika kutokana na moyo aliokuwa nao katika kusimamia masuala ya mpira.

Wambura alisema ni wajibu wa kila mdau kuiga mazuri yote yaliyofanywa na Fabian Samo katika kusimamia haki na kuwa wawazi katika kusimamia ukweli ili kuweza kuendeleza soka la Mkoa wa Mara na Tanzania kwa ujumla.


Mhe. Nimrod Mkono Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.
 Viongozi wengine waliohudhulia mazishi hayo ni Waziri wa kazi na na ajira Gaudensia Kabaka, Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Nimrod Mkono, Mkuu wa wilaya ya Bunda Joshua Mirumbe na mstahiki Meya wa Manispaa ya Musoma Alex Kisulula.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Musoma mjini Mussa Matoroka akiweka shada la maua kwenye kaburi.

Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tuppa ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Mara akiweka shada la maua kwenye kaburi.


Na mwandishi wa blogu hii
Shomari Binda
Musoma


Akisoma salamu za rambirambi kutoka Shirikisho la soka hapa Nchini,Tenga alisema wamepata pengo kubwa kwa kuondokewea na kiongozi huyo kwa kile alichokieleza bado mchango na mawazo ya kiongozi huyo yalikuwa yakihitajika kutokana na uwezo wake mkubwa aliokuwa nao katika masuala ya mahesabu.

Alisema Samo alikuwa mwepesi wa kuhudhulia vikao pale alipokuwa akihitajika na alichangia kwa kiasi kikubwa kuhakikisha uwezo wake aliokuwa nao katika masuala ya mahesabu anayatoa katika shirikisho hilo na imepelekea kuwa na uangalizi mzuri katika kusimamia masuala ya fedha.

Tenga ameeleza kuwa uwezo mkubwa aliokuwa nao Fabian Samo ndio uliopelekea wadau wa soka katika Mkoa wa Mara kumchagua kwa vipindi viwili kukiongoza chama cha mpira wa miguu (FAM) na katika kipindi hicho kumekuwa na mabadiliko makubwa katika soka la Mkoa wa Mara.

Rais huyo wa TFF amewaomba wadau wa soka Mkoani Mara kufata yale yote mazuri aliyoyafanya marehemu Fabian Samo ili kupitia hayo soka la Mkoa wa Mara na Tanzania kwa ujumla liweze kundelea na kupanda na kuwaomba viongozi wengine katika Soka la Mkoa wa Mara kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba na kudai kuwa TFF ipo pamoja katika kipindi hiki cha msiba.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Fabian Samo mahali pema peponi.

EPIQ BONGO STAR SEARCH INAENDELEA MCHANA HUU NDANI YA CCM KIRUMBA.....VIPAJI KIBAO VIMEJITOKEZA!!

Majaji wa Epiq Bongo Star Search, kutoka kushoto ni Master J, Madam Ritha na Salama Jabir katika usaili wa Mwanza, ndani ya uwanja wa CCM Kirumba

Mmoja wa washiriki wa Epiq Bongo star search akisailiwa Mwanza

Mshiriki wa BSS Mwanza akisailiwa

Mablogist wanaongoza Mwanza wakiwajibika kuwapasha habari blogers katika usaili wa BSS Mwanza ndani ya uwanja wa CCM Kirumba, Kutoka kulia ni Mukhsin Mambo (Mc Stopper) wa thebigtopten.blogspot.com na G Sengo wa gsengo.blogspot.com

Judges wa Epiq Bongo Star Search, Kutoka kulia Salama, Ritha, Master Jay
Foleni ya Vipaji vya BSS ikijiandaa kusailiwa ndani ya uwanja wa CCM Kirumba
Umati uliojitokeza wengine wakisuburi usaili wengine wasindikizaji ndani ya uwanja wa CCM Kirumba
Hili ni eneo la kujiandikisha

Washiriki waliojitokeza leo uwanja wa CCM Kirumba mchakato wa EBSS.

Mmoja au kadhaa kati ya hawa kuitwaa nafasi...

Subiri mpango mzima utaonekana sebuleni kwako .. Wataalamu wakiwa kazini kuzichukuwa engo kutoka kulia ni Nickson (mchanganya picha), Alex (director) na mtaalamu wa sauti Said.

Mtangazaji wa Barmedaz Tv Steve Bugumba akifanya mahojiano ya live na moja wa washiriki EBSS Mwanza. 

Picha ya pamoko Aloyce Nyanda aka Van B (C) akiwa na majaji wa EBSS Master Jay na Salama

Caesar Daniel wa Clouds Tv na Oficial Presenter wa Epic Bongo Star Search 2012 akiwa na Yusuph Mussa ambaye ni Cordinator kutoka Barmedaz Tv Mwanza akishow love na kamera ya blog ya G. Sengo

Vijana mbalimbali waliojitokeza leo wakiwa kwenye foleni kwaajili ya kuingia chumhga cha usaili kwenye uwanja CCM Kirumba jijini Mwanza.

QUESTION CREW ndio kinara wa serengeti dance la fiesta 2012 mkoani tanga

Mmoja wa waratibu na jaji,Isakwisa Thomson akikabidhi kitita cha shilingi milioni moja kwa kundi kinara la Questions Crew kati ya saba yaliyojitokeza kushiriki shindano la Serengeti dance la Fiesta 2012,lililofanyika jioni ya leo ndani ya kiota cha mangoma cha Lakasachika mkoani Tanga.
Mmoja wa waratibu na jaji,Isakwisa Thomson akiwa na kitita cha fedha taslim sh milioni moja,kwa ajili ya kukabidhi kwa kundi la Questions Crew lililoibuka mshindi wa kwanza kati ya makundi saba yaliyojitokeza kushiriki shindano la Serengeti dance la Fiesta 2012,lililofanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Lakasachika mkoani Tanga.
Baadhi ya wacheza shoo wa kundi la Questions Crew wakizungumza machache mara baada ya kukabidhiwa kitita chao cha shilingi milioni moja
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti-Tanga wakikabidhi Kreti moja ya bia ya Serengeti ikiwa ni sehemu ya zawadi kwa kundi la Questions Crew mara baada ya kuibuka washindi wa Serengeti dance la Fiesta 2012 mkoani Tanga.
Watu mbalimbali wakifuatilia shindano hilo.
Kundi la Sweet Girls likionesha umahiri wake kucheza kwenye shindano la kulisaka kundi kinara la Serengeti dance la Fiesta 2012
Kundi la la Street Colour likionesha umahiri wa kucheza mbele ya sehemu ya wakazi wa jiji la Tanga waliojitokeza jioni ya leo kushuhudia shindano la Serengeti dance la Fiesta lililofanyika ndani ya ukumbi wa Lakasachika
Kundi la Questions Crew likicheza kouwania kitita cha milioni moja kilichotolewa na kampuni ya bia ya Serengeti sambamba na kreti moja ya bia.
Mdau Thomson akikata kiu yake safi kabisaa.
Palikuwa hapatoshi leo ndani ya ukumbi wa Lakasachika.
Macho mbeeeeele...
Pichani juu na chini Sehemu ya wakazi mbalimbali wa jiji la Tanga waliojitokeza kushuhudia shindano hilo lilovuta hisia za vijana wengi
Mmoja wa majaji wa shindano hilo B Dozen akifafanua jambo wakati wa kumsaka kinara wa mashindano hayo kwa mkoa wa Tanga.
Maujuzi na maufundi..


Mmoja wa majaji wa shindano hilo Isakwisa Thomson akifafanua jambo wakati wa kumsaka kinara wa mashindano hayo kwa mkoa wa Tanga.

Majaji wa shindano la Serengeti dance la fiesta 2012 wakijadiliana jambo wakati shindano likiendelea ndani ya ukumbi wa Lakasachika jioni ya leo,ambapo wakazi mbalimbali wa jiji la Tanga walijitokeza kwa wingi na kujionea vipaji

Friday, July 13, 2012

MAJAJI WA EBSS WATINGA STUDIO ZA RFR NA STAR TV


Majaji wa Bongo Star Search 2012, Master Jay, Madam Ritha na Salama Jabir wakiwa studio za RFA Ilemela jijini Mwanza hii leo.


Madam Ritha na Master Jay ndani ya Studio za RFA


Mtangazaji wa RFA Sam Davis Kiama aka 'Uncle Sam'

Madama Ritha na Master Jay

Madam Ritha na Salama Jabir

Master Jay, Madam Ritha na Salama Jabir

Madam Ritha, Kisali Simba wa Star TV na Salama Jabir

Jopo la Majaji wa BSS, Master Jay, Madam Ritha na Salama Jabir wakiwa studio za Star TV