Rais wa shirikisho la soka hapa Nchini (TFF) Leodiger Tenga akitoa salamu za shirikisho. |
Makongoro Nyerere ambaye ni mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere. |
Makongoro alisema ili kumuenzi kiukweli marehemu Fabian Samo ni kufuata yale yote mazuri aliyoyaacha kwa dhati na kuwa wawazi katika masuala ya uongozi kama ambavyo alikuwa akifanya kiongozi huyo.
Heshima za mwisho. |
Michael Wambura mdau wa soka. |
Wambura alisema ni wajibu wa kila mdau kuiga mazuri yote yaliyofanywa na Fabian Samo katika kusimamia haki na kuwa wawazi katika kusimamia ukweli ili kuweza kuendeleza soka la Mkoa wa Mara na Tanzania kwa ujumla.
Mhe. Nimrod Mkono Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini. |
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Musoma mjini Mussa Matoroka akiweka shada la maua kwenye kaburi. |
Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tuppa ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Mara akiweka shada la maua kwenye kaburi. |
Na mwandishi wa blogu hii
Shomari Binda
Musoma
Akisoma salamu za rambirambi kutoka Shirikisho
la soka hapa Nchini,Tenga alisema wamepata pengo kubwa kwa kuondokewea na
kiongozi huyo kwa kile alichokieleza bado mchango na mawazo ya kiongozi huyo
yalikuwa yakihitajika kutokana na uwezo wake mkubwa aliokuwa nao katika masuala
ya mahesabu.
Alisema Samo alikuwa mwepesi wa kuhudhulia vikao pale alipokuwa akihitajika na alichangia kwa kiasi kikubwa kuhakikisha uwezo wake aliokuwa nao katika masuala ya mahesabu anayatoa katika shirikisho hilo na imepelekea kuwa na uangalizi mzuri katika kusimamia masuala ya fedha.
Tenga ameeleza kuwa uwezo mkubwa aliokuwa nao Fabian Samo ndio uliopelekea wadau wa soka katika Mkoa wa Mara kumchagua kwa vipindi viwili kukiongoza chama cha mpira wa miguu (FAM) na katika kipindi hicho kumekuwa na mabadiliko makubwa katika soka la Mkoa wa Mara.
Rais huyo wa TFF amewaomba wadau wa soka Mkoani Mara kufata yale yote mazuri aliyoyafanya marehemu Fabian Samo ili kupitia hayo soka la Mkoa wa Mara na Tanzania kwa ujumla liweze kundelea na kupanda na kuwaomba viongozi wengine katika Soka la Mkoa wa Mara kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba na kudai kuwa TFF ipo pamoja katika kipindi hiki cha msiba.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Fabian Samo mahali pema peponi.

Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.