ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 21, 2017

MAELFU WAANDAMANA MJINI WASHINGTON KUPINGA URAIS WA DONALD TRUMP.


MAELFU ya wananchi wa Marekani wanaendelea kumiminika mjini Washington kupaza sauti zao wakieleza hasira na wasiwasi wao kuhusu urais wa Donald Trump, siku moja tu baada ya kuapishwa rasmi kuwa rais wa 45 wa Marekani.
Maandamano ya Wanawake mjini Washington ambayo watayarishaji wake wanasema yatawakutanisha pamoja malaki ya watu, yana lengo ya kuwazindua Wamarekani kuhusu haki za wanawake na haki nyingine za kiraia ambazo Wamarekani wengi wana wasiwasi kwamba zinatishiwa na rais mpya wa nchi hiyo.
Trump amewakasirisha watu wengi ndani na nje ya Marekani kwa kukariri matamshi yanayowashushia hadhi wanawake, Waislamu na wahamiaji wakati wa kampeni zake za urais.

Wamarekani waandamana dhidi ya Rais Donald Trump.
Maandamano ya Jumamosi ya Wanawake ambayo yalianza kwa wito uliotolewa na bibi wa Hawai katika mtandao wa kijamii wa Facebook baada ya ushindi wa Donald Trump mwezi Novemba mwaka uliopita, yanahesabiwa kuwa maandamano makubwa zaidi ya kisiasa kuwahi kushuhudiwa katika mji mkuu wa Marekani.
Wapinzani wa Rais Donald Trump wa Marekani walikuwa wakiendelea kumiminika mjini Washington kwa mabasi wakitokea katika miji na maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Richmond, Crystal Hoyt, anasema leo Wamarekani watashuhudia moja kati ya maandamano makubwa na muhimu zaidi ya kupigania uadilifu wa kijamii katika historia ya miaka 240 ya Marekani. Profesa Crystal Hoyt ameongea kuwa, Trump ametumia siasa za kuchochea hofu, ubaguzi wa kijinsia na chuki dhidi ya wageni na wahamiaji kwa ajili ya maslahi ya kisiasa.

Maandamano ya Washington.
Maandamano ya leo mjini Washington yanafanyika siku moja baada ya sherehe za jana za kuapishwa Rais mpya wa Marekani zilizoandamana na maandamano na ghasia ambazo ni kielelezo cha mgawanyiko mkubwa unaotawala jamii ya Marekani kutokana na siasa za kibaguzi za rais mpya wa nchi hiyo.
Polisi ya Washington imetangaza kuwa imewatia nguvuni waandamanaji wasiopungua 217 katika maandamano na machafuko ya jana.

WASANII MKOANI GEITA WAIOMBA SERIKALI KUWATAMBUA KATIKA SHUGHULI AMBAZO WANAZIFANYA.

Meza kuu ikiongozwa na mgeni rasimi ambaye ni afsa maendeleo wa halmashauri ya Mji ndugu,Maiga Majagi aliyevaa shati ya drafti katikakati.
Msanii wa nyimbo za asili katoka kata ya Bukoli akiburudisha wakati wa mashindano hayo.
Mwenyekiti wa chama cha wasanii Mkoani Geita,Rose Bonface (ROSE BONANZA) akitambulisha baadhi ya wageni waalikwa.
Moja kati ya majaji katika mashindano hayo,Bi Anithar Kagemulo akijitambulisha wakati wa mashindano hayo.
Kikundim cha uwimbaji kutoka wilayani Chato cha Mwagazege kikiimba katika mashindano hayo.
Mgeni rasimi ambaye ni afsa maendeleo ya jamii Ndugu Maiga Majagi akizungumza na wasanii huku akiwaasa kuendeleo kuwa na umoja na kushikamana ili kuendeleza sanaa katika Mkoa wa Geita.
Meza kuu ikimsikiliza mgeni rasimi wakati wa hotuba yake .
Majaji wakifatilia mashindano.


PICHA NA JOEL MADUKA

STORY NA MADUKAONLINE

GEITA:Chama cha wasanii Mkoani Geita,kimeiomba serikali Mkoani humo kuendelea kutoa ushirikiano katika Nyanja hiyo muhimu ikiwa ni pamoja na kusapoti kazi  ambazo zimekuwa zikifanywa  na wasanii.

Kauli hiyo imesemwa na mwenyekiti wa chama hicho Mkoani Humo Rose Bonface wakati wa ufunguzi wa mashindano ya kuwasaka wasanii wenye vipaji vya kuimba kuigiza na kuchekesha yaliyokuwa yanafanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Mji wa Geita.

Rose alisema kuwa Tasnia ya sanaa bado inachangamoto nyingi ikiwa ni pamojan na kushindwa kutambulika na kushikwa mkono  kwenye serikali kutokana na kwamba baadhi  viongozi wa kiserikali wanaona swala la wasanii limekaa kiunu jambo ambalo si kweli kwani  kazi ya sanaa ni sawa na shughuli zingine katika jamii.

“Sisi wasanii bado tunachangamoto kubwa sana katika serikali ingawa kwa sasa kuna wizara inayotutambua lakini bado kuna ugumu mwingi tu tukiangali kwenye serikali kuna viongozi ambao wanaona kuwa hatuna mchango wowote lakini sio kweli sisi tunauwezo wa kufikisha ujumbe kwa jamii na ikatuelewa zaidi kuliko vile ambavyo serikali imeendelea kutuchukulia”alisema Rose.

Kwa upande wake mwenyekiti wa waigizaji Mkoa wa Mwanza,Ramadhani  Masululi,amesema kuwa jambo ambalo limekuwa likisababisha sanaa au wasanii kuonekana ni wahuni ni kutokana na baadhi ya wasanii kuonekana kutokujieshimu na wengine kuingia kwenye sanaa bila ya kuwa na maono au mtazamo chanya katika sanaa.

“Sanaa sio uhuni kwanini wanasema uhuni waigizaji  wengine wameingia ni mamluki unakuta mwingine anaingia kwenye sanaa ni mlevi mvuta bangi na mwingine ni Malaya na hii ya wezekana kwasababu nikutokana na vigezo kutokuwa vigumu lakini sisi kama chama  cha wasanii hatuwezi kukubaliana na swala hili tutaakikisha wale wenyetabia za ajabu wanatupisha ili tuwe na wasanii ambao wananidhamu”alisema Ramadhani

Akimwakilisha Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Geita ambaye ndiye alikuwa mgeni rasimi kwenye uzinduzi huo,afisa maendeleo ya jamii wa halmashauri hiyo,Maiga Majagi,amewaasa wasanii kutumia umoja wao  kuleta mabadiliko kwa wanageita kwa kufanya kazi na kukitumia chama chao kwa kuwa tetea zaidi na kupata taarifa  mbali mbali za soko la kazi zao na pia amewataka  kupanga mikakati ya kushirikiana  na wadau wote  na kwamba jambo likiongelewa na wote linakuwa na nguvu kuliko kuzungumziwa na mtu mmoja.

NAIBU WAZIRI MASAUNI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI JIJINI MBEYA

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na maafisa wa Jeshi la Polisi alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kubaini mafanikio na changamoto za jeshi hilo. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisikiliza maelezo juu ya gari lililokamatwa likisafirisha wahamiaji haramu   kutoka kwa Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benjamini Kaizaga(aliyenyoosha mkono).Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benjamini Kaizaga, juu ya gari  lililokamatwa likisafirisha madawa ya kulevya.Wengine mstari wa mbele  ni   Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula(wapili kulia)  na  Naibu Kamishna wa Uhamiaji,Asumsio Achachaa .Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kulia), akifurahia jambo wakati alipotembelea makazi ya mbwa wanaotumika na Jeshi la Polisi katika masuala ya ulinzi na usalama.Baada ya Naibu Waziri ni Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya,Emmanuel Lukula. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipanda mti katika makazi ya mbwa wanaotumika katika masuala ya ulinzi na usalama na Jeshi la Polisi.Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

MRADI WA LVEMP2 SASA KUJA NA MBINU KUBWA ZA KUPAMBANA NA UCHAFUZI WA MAZINGIRA ZIWA VICTORIA.

NA ANNASTAZIA MAGINGA,
GSENGO BLOG 
Mwanza

KAMATI ya Bunge ya kudumu ya viwanda ,Biashara na Uwekezaji imewataka wataalamu wanaosimamia uhifadhi wa mazingira ziwa Victoria kwa awamu ya pili (LVEMPII) kuwa na mradi mkubwa utakao zuia uchafuzi katika ziwa hilo.

Hatua hiyo imekuja baada ya muwaslisha mradi ,mratibu wa LVEMPII Omary Myanza kueleza miradi inayotekelezwa na mradi huo katika kuondoa uchafuzi katika ziwa Victoria kupitia jamii.

Akizungumza kwenye kikao hicho Mwenyekiti wa kamati hiyo Dkt.Dalali Kafumu amesema kuwa mradi huo hauna mradi endelevu  utakaosaidia kukusanya na kuzuia uchafuzi na kulinda mazingira ya ziwa Victoria kwani iliyopo ni midogo midogo ambayo itakufa baada ya mradi kuisha muda wake.

“Kukiwa na mradi mkubwa utasaidia kwa sababu mradi huu unaisha Disemba 31mwaka huu na kama unaisha ina maana hata hii midogo midogo mnayowezesha wananchi pia itakufa kutokana na mradi utakuwa umekufa”amesema Kafumu.

Aidha awali akiwasilisha mradi huo mbele ya kamati hiyo mratibu Myanza amesema mradi wa LVEMP II umeanza  2009 sept na kutarajiwa kukamirika disemba 31 mwaka huu  huku ukiwa hadi sasa miradi 341 ikiwa imekwisha wanaufaisha wananchi.

“Miradi 203 imekamilika kwa 100%, 90 imekamirika zaidia ya 50% na 48% iko chini ya 50% kukamilika  miradi inayofadhiliwa na bank ya dunia kwa dolla milioni 42.5  za kimarekani na nchi yetu ilitoa dolla milioni 3  na kutekelezwa na nchi tano za Afrika mashariki”amesema Myanza.

MASHINDANO YA LIGI DARAJA LA NNE NGAZI YA WILAYA YA GEITA YAFUNGULIWA RASMI ,HUKU TIMU YA BOMANI FC IKIAMBULIA KICHAPO CHA MABAO MATATU KWA MAWILI KUTOKA KWA BUKOLI FC

Timu ya Bukoli FC wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo kuanza
Timu ya Bomani kutoka mjini Geita wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo kuanza.

Kaimu Mgeni Rasmi ambaye ni Diwani wa Bukoli  Faraji Seif  akikagua vikosi na kusalimiana na wachezaji wa timu zote mbili yaani Bukoli Fc na Bomani Mgeni Rasmi akiongozwa na kapteni wa timu ya Bukoli Fc akisalimiana na wachezaji wa timu hiyo kabla ya mchezo kuanza.

Mh,Faraji Seif ambaye ndiye mgeni rasimi kwenye uzinduzi wa ligi daraja la nne wilaya ya Geita akifatilia kwa makini mchezo uliokuwa ukiendelea uwanjani

Mlinda mlango wa timu ya Bomani akitoka nje baada ya kuwa amepata majeraha katika mchezo huo.

Mlinda mlango akiwa amebebwa .

Baadhi ya mashabiki wakiendelea kufatilia kwa umakini mechi ambayo ilikuwa inaendelea uwanjani.

Mashambulizi yakiendelea kwa kasi kubwa kwenye viwanja vya bukoli

Mwamuzi wa mchezo huo , Majeshi Mgema akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu ya Bomani.

PICHA NA JOEL MADUKA
STORY NA MADUKAONLINE.
Mashindano ya Soka Ligi daraja la nne (4) ngazi ya wilaya ya Geita yameanza kutimua Vumbi jana ambapo Mechi ya Ufunguzi ilikuwa kati ya Bukoli FC dhidi ya  Bomani FC na Mshindi ameibuka Bukoli kwa goli tatu(3)didi ya Bomani kutoka mjini Geita .

 Ilikiuwa siku ya  jana January 19,2017 majira ya jioni ambao Historia imeandikwa kwa mala ya kwanza baada ya miaka ishiriki ( 20)kupatikana kwa kituo cha ufunguzi wa Ligi daraja la nne ngazi ya wilaya.

Akifungua mashindano hayo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Geita Mwl,Herman Kapufi ambaye alitarajia kuwa mgeni rasmi Diwani wa Kata ya Bukoli Faraji Seif,aliwataka wachezaji kuwa na nidhamu ya hali ya juu katika kipindi chote cha ligi huku akiwataka mashabiki kuwa na nidhamu katika swala la ushangiliaji.

“Natambua kuwa michezo ni ajira ni vyema kutumia nafasi hii kwa kujituma kwa timu zote ambazo zitashiriki ligi hii na niwaombe sana wale ambao mtashindwa mkubali kushindwa maana mchezo ni dakika sitini(90) kwa hiyo hatutarajii kuona mnakuwa sio watu wa kuheshimiana jambo la msingi wasikilizeni walimu wenu nikiwa na maana makocha na pia muwe watu wa kujituma kwenye mazoezi naamini mkizingatia haya basi mtafanya vizuri timu zote”aliwasisitiza Seif

Katika mechi ya ufunguzi wenyeji Bukoli waliitandika    Boman FC mikwaju mitatu dhidi ya miwili katika kipindi cha pili .katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Majeshi Mgema.

Mabadiliko makubwa yalionekana katika kipindi cha pili ambapo timu zote zilionesha ushindani na kucheza kwa kukamiana ambapo kunako dakika ya hamsini(50) mchezaji Shukuru Mtesiga aliiandikia bao la kwanza Bukoli FC, na dakika ya  hamsini na saba (57) mchezaji mwenzake Marius Joseph akafunga goli la pili

Bomani FC wakapata goli la kwanza katika dakika ya sitini na saba ( 67 )kupitia kwa mchezaji wao Kasaba Sabu,na dakika ya sabini na saba (77)kwa mara nyingine Shukuru Mutesiga aliyeonekana kinara katika mchezo huo akaipatia ushindi timu ya Bukoli kwakuzamisha mpira kimiani na kuandika bao la  tatu(3). Goli la pili la Bomani lilipatikana kunako dakika ya themanini na mbili (82 )kupitia kwa mchezaji John Pastory.

MAGAZETI YA LEO:- TRUMP AAPISHWA,WATU 3 HUHITAJI VIUNGO BANDIA KILA SIKU, VIGOGO WATANO WA RUSHWA JELA MIAKA MITANO

Watu 3 huhitaji viungo bandia kila siku, Vigogo watano wa rushwa utakatishaji fedha jela miaka 5, Trump aapishwa, DC azuia shamba la Mbowe.  Askofu Sangu atoa machozi hadharani, Profesa Lipumba ahofia baa la njaa, Dkt Possi: Nmejiuzulu, Mtifuanao UVCCM Dodoma. Habarika na dondoo hizi za magazeti ya leo hapa; 

MO DEWJI ATANGAZWA KUWA MSHINDI WA TUZO YA AFRICAN LEADERSHIP MAGAZINE PERSON OF THE YEAR 2016


Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji ametangazwa na Jarida la African Leadership kuwa mshindi wa tuzo ya African Leadership Magazine Person of the year 2016 baada ya kuibuka mshindi katika kinyang’anyiro kilishohusisha watu nane.

MO Dewji ambaye ni Mtanzania anayejihusisha na biashara kupitia kampuni yake ya MeTL Group na kusaidia jamii kupitia Taasisi ya MO Dewji ameibuka mshindi kwa kupata asilimia 60.8 ya kura zote zilizopigwa akifuatiwa na Rais mstaafu wa Ghana, Dramani Mahama ambaye alipata asilimia 30.2.

Wengine waliowania tuzo hiyo ni Strive Masiyiwa, Chris Kirubi, Akinwumi Adesina, Cyril Ramaphosa, Atiku Abubakar na Aisha Mohammed.

Akizungumza kuhusu MO Dewji, Mjumbe wa Bodi ya Ushauri wa Jarida la African Leadership, Joe Beasley amemtaja MO Dewji kama mtu ambaye anaumuhimu mkubwa kutokana na dhamira yake ya kusaidia bara la Afrika kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa kutoa nafasi nyingi za kazi.

“Dhamira ya Dewji ni kutengeneza ajira jambo ambalo ni kiini cha tatizo kubwa linalokabili Afrika la ukosefu wa ajira … kupitia biashara zake amesaidia kupunguza ukosefu wa ajira, kupata utajiri na kutoa ajira kwa vijana ambao hawana ajira barani [Afrika],” alisema Beasley.

Mohammed Dewji anakuwa mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka 2016 ambapo kwa mwaka 2015 ilichukuliwa na Rais Mstaafu wa Nigeria, Goodluck Jonathan.

TRUMP AANZA KUFANYIA MABADILIKO SHERIA ZA OBAMA.

The inaugural parade passing by President Donald J. Trump at Lafayette Park, near the White House, on Friday.
U.S. President Donald Trump waves to supporters as he walks the parade route with his wife, Melania, after being sworn in on Friday.
Trump na mkewe wakitembea mjini Washington


Rais wa Marekani Donald Trump ameanza kutia saini maagizo ya rais, baadhi yake yakiwa ni ya kubadili yale yalioafikiwa na mtangulizi wake Barak Obama.

Muda mfupi baada ya kukagua gwaride la kuapishwa kwake, Bw Trump, alitia amri ya serikali, kupunguza mzigo wa kiuchumi kwa taifa, unaotokana na gharama za kufadhili bima ya matibabu ya bei nafuu inayofahamika kama Obamacare, ambayo Trump aliahidi kufanyia marekebisho.

693719551KE00014_Parade_Cel
A military band marches during the inaugural parade. Trump ni rais wa 45th wa The United States. (Joe Readle/Getty Images)

Trump pia ametia saini amri ya kuwaidhinisha mawaziri wake wapya wa Ulinzi na usalama wa kitaifa ambao uteuzi wao umepitishwa na bunge la seneti.


Utawala wa Trump pia umeaanza kufanyia marekebisho mtandao wa kijamii wa Ikulu ya White House kwa kuweka masuala yatakayopatiwa kipaumbele na uongozi huo mpya.

Friday, January 20, 2017

Dar Construction Trade Expo 2017

DAR CONSTRUCTION AND TRADE EXPO.
The construction industry is a sector of the economy that transforms various resources into constructed physical economic and social infrastructure necessary for socio-economic development.
It embraces the process by which the said physical infrastructure are planned, designed, procured, constructed or produced, altered, repaired, maintained and demolished.
dar construction expo.jpg

TIZAMA LIVE KINACHOENDELEA NCHINI MAREKANI KUELEKEA KUAPISHWA KWA TRUMP.

CNN Live Fox News Live Stream Now Today 24/7 - Donald Trump Inauguration News

MBWANA SAMATTA ALIPOFUNGUKA UTOFAUTI KATI YA TP MAZEMBE NA GENK.

Akihojiwa na mtangazaji wa BBC Swahili  Salim Kikeke, hapa Samatta anafunguka pia nini matamanio yake kwa zama zijazo katika soka lake. Jeh ni klabu ipi anayotamani kukiputa nayo Barani Ulaya?

Thursday, January 19, 2017

YANGA NA ASHANTI JUMAMOSI, SIMBA NA POLISI JUMAPILI KOMBE LA TFF.

RATIBA KAMILI 32 BORA ASFC
Januari 21, 2017
Alliance Vs Mbao (CCM Kirumba, Mwanza) 
Maji Maji Vs Mighty (Maji Maji, Songea) 
Yanga Vs Ashanti United (Uhuru, Dar es Salaam) 
Januari 22, 2017
Ruvu Shooting Vs Kiluvya United (Mabatini, Mlandizi) 
Toto Africans Vs Mwadui (CCM Kirumba, Mwanza) 
Simba SC Vs Polisi Dar (Uhuru, Dar es Salaam)
Mbeya Worriors Vs Prisons (Sokoine, Mbeya) 
Januari 23, 2017
Stand United Vs Polisi Mara (Karume, Musoma) 
Azam FC Vs Cosmopolitan (Azam Complex, Chamazi) 
Ndanda FC Vs Mlale JKT (Nangwanda Sijaona, Mtwara) 
Januari 24, 2016
Mtibwa Sugar Vs Polisi Moro (Jamhuri, Morogoro) 
Kurugenzi FC Vs JKT Ruvu (Mafinga, Iringa) 
Mbeya City Vs Kabela City (Sokoine, Mbeya) 
Madini Vs Panone (Sheikh Amri Abeid, Arusha) 
Januari 25, 2017
Singida United Vs Kagera Sugar (Namfua, Singida) 
African Lyon Vs Mshikamano (Uhuru, Dar es Salaam)

JPM AWAPANGIA VITUO MABALOZI WATANO.Rais John Magufuli

Dar es Salaam. Rais  John Magufuli, leo (Alhamisi) amefanya uteuzi wa mabalozi watano watakaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imesema mabalozi hao wataapishwa kesho (Ijumaa) Ikulu jijini hapa.
Mabalozi hao ni Emmanuel John Nchimbi ambaye ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Brazil, Mbelwa Brighton Kairuki ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania, China, George Kahema Madafa ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Rome , Italy.
Fatma Rajab ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Doha, Qatar, Profesa  Elizabeth Kiondo ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Uturuki,  James Alex Msekela ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Geneva, Umoja wa Mataifa.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Muhidin Mboweto kuwa balozi.
Tarehe ya kuapishwa na kituo cha kazi cha  Mboweto vitatangazwa baadaye.

PAKISTAN YAPINGA KUHAMISHWA UBALOZI WA MAREKANI KUTOKA TEL AVIV KWENDA QUDUS.Mwakilishi wa Kudumu wa Pakistan katika Umoja wa Mataifa amepinga hatua yoyote ya uhamishaji wa ubalozi wa Marekani kutoka Tel-Aviv, Israel kwenda Baytul-Muqaddas na kwamba, kitendo hicho ni ukiukaji wa wazi wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Maleeha Lodhi, ameyasema hayo katika kupinga matamshi ya rais mteule wa Marekani Donald Trump, ya kutaka kuhamishiwa ubalozi wa nchi hiyo kutoka mji mkuu wa utawala wa Kizayuni Tel Aviv kwenda Quds Tukufu na kuongeza kuwa, kupatikana taifa huru la Palestina kunadhaminiwa na mji mkuu wake kuwa Baytul-Muqaddas na si vinginevyo.

Ubalozi wa Marekani uliopo Tel Aviv unaokusudiwa kuhamishiwa Quds

Lodhi amesema kuwa, kwa zaidi ya nusu karne sasa, utawala wa Kizayuni ambao kwa kutoheshimu maazimio na sheria za Umoja wa Mataifa, umeendelea kuyakalia kwa mabavu maeneo ya Ukingo wa Mto Jordan sambamba na kuyafanya maisha ya raia asili wa Palestina kuwa magumu zaidi. Mwakilishi huyo wa Kudumu wa Pakistan katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, Baytul-Muqaddas ni moyo wa ulimwengu wa Kiislamu na kwamba, tukio lolote linalotokea Palestina na wakazi wake, litakuwa na taathira kwa eneo zima la Mashariki ya Kati na dunia kwa ujumla.


Baytul-Muqaddas inayokaliwa kwa mabavu hadi sasa.

Katika kampeni zake za urais, Donald Trump aliashiria kuwa kama angechaguliwa kuwa rais wa Marekani angetekeleza mpango huo, suala ambalo lilikabiliwa na radiamali nyingi kali kieneo na kimataifa.

GAMBIA YAVUNJA REKODI 'YAWA NA RAIS WAWILI NDANI YA MUHULA'


Rais mpya wa Gambia aapishwa; Jammeh ang'ang'ania madaraka.

Adama Barrow ameapishwa na kuwa Rais mpya wa Gambia huku Yahya Jammeh aliyetawala nchi hiyo kwa miaka 22 aking'ang'ania madaraka ya nchi.
Baadhi ya duru zinasema kuwa Barrow ameapishwa leo kuwa rais mpya na wanajeshi wa nchi za Afrika Magharibi wako tayari kuingilia kati. Sherehe za kuapishwa Adama Barrow zimefanyika nje ya nchi katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, mawaziri na viongozi mbalimbali wa serikali ya Rais Jammeh wameendelea kujiuzulu na hivyo kuzidi kumdhoofisha kiongozi huyo mwenye nia ya kung'ang'ania madaraka.
Makamu wa rais nchini Gambia Isatou Njie-Saidy amejiuzulu saa chache kabla ya muda wake wa kuongoza kutimia. Asidha Waziri wa Mazingira na Elimu ya Juu pia amejiuzulu, ikiwa ni msururu wa mawaziri kumtoroka Jammeh kufuatia hatua yake ya kukataa kujiuzulu baada ya zaidi ya miongo miwili ya utawala.
Adama Barrow, Rais mpya wa Gambia.
Wakati huo huo, majeshi ya mataifa ya magharibi mwa Afrika yanatarajiwa kuingia nchini Gambia leo ili kuhimiza uhamisho wa mamlaka. Baadhi ya ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa, vikosi vya Senegal tayari vimeingia nchini Gambia.
Katika upande mwingine Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitazamiwa kufanya mkutano wa dharura hii leo kuhusiana na mgogoro wa kisiasa na kunukia machafuko ya umwagikaji damu nchini Gambia.
Rais Yahya Jammeh ambaye alikuwa amekubali kushindwa na Adama Barrow katika uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi Desemba na hata kumpongeza mpinzani wake huyo, ghafla alibadilisha uamuzi na kuyakataa matokeo kwa madai kuwa zoezi la uchaguzi lilitawaliwa na dosari nyingi na sasa anataka uchaguzi wa rais ufanyike tena.