Timu ya Bukoli FC wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo kuanza |
Mgeni Rasmi akiongozwa na kapteni wa timu ya Bukoli Fc akisalimiana na wachezaji wa timu hiyo kabla ya mchezo kuanza.
PICHA NA JOEL MADUKA
STORY NA MADUKAONLINE.
Mashindano ya Soka Ligi daraja la nne (4) ngazi ya wilaya ya Geita yameanza kutimua Vumbi jana ambapo Mechi ya Ufunguzi ilikuwa kati ya Bukoli FC dhidi ya Bomani FC na Mshindi ameibuka Bukoli kwa goli tatu(3)didi ya Bomani kutoka mjini Geita .
Ilikiuwa siku ya jana January 19,2017 majira ya jioni ambao Historia imeandikwa kwa mala ya kwanza baada ya miaka ishiriki ( 20)kupatikana kwa kituo cha ufunguzi wa Ligi daraja la nne ngazi ya wilaya.
Akifungua mashindano hayo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Geita Mwl,Herman Kapufi ambaye alitarajia kuwa mgeni rasmi Diwani wa Kata ya Bukoli Faraji Seif,aliwataka wachezaji kuwa na nidhamu ya hali ya juu katika kipindi chote cha ligi huku akiwataka mashabiki kuwa na nidhamu katika swala la ushangiliaji.
“Natambua kuwa michezo ni ajira ni vyema kutumia nafasi hii kwa kujituma kwa timu zote ambazo zitashiriki ligi hii na niwaombe sana wale ambao mtashindwa mkubali kushindwa maana mchezo ni dakika sitini(90) kwa hiyo hatutarajii kuona mnakuwa sio watu wa kuheshimiana jambo la msingi wasikilizeni walimu wenu nikiwa na maana makocha na pia muwe watu wa kujituma kwenye mazoezi naamini mkizingatia haya basi mtafanya vizuri timu zote”aliwasisitiza Seif
Katika mechi ya ufunguzi wenyeji Bukoli waliitandika Boman FC mikwaju mitatu dhidi ya miwili katika kipindi cha pili .katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Majeshi Mgema.
Mabadiliko makubwa yalionekana katika kipindi cha pili ambapo timu zote zilionesha ushindani na kucheza kwa kukamiana ambapo kunako dakika ya hamsini(50) mchezaji Shukuru Mtesiga aliiandikia bao la kwanza Bukoli FC, na dakika ya hamsini na saba (57) mchezaji mwenzake Marius Joseph akafunga goli la pili
Bomani FC wakapata goli la kwanza katika dakika ya sitini na saba ( 67 )kupitia kwa mchezaji wao Kasaba Sabu,na dakika ya sabini na saba (77)kwa mara nyingine Shukuru Mutesiga aliyeonekana kinara katika mchezo huo akaipatia ushindi timu ya Bukoli kwakuzamisha mpira kimiani na kuandika bao la tatu(3). Goli la pili la Bomani lilipatikana kunako dakika ya themanini na mbili (82 )kupitia kwa mchezaji John Pastory.
|
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.