ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 5, 2019

MAFINGA ACADEMY KINARA WA MAGOLI WA ASAS SUPER LEAGUE 2019/2020 MZUNGUKO WA TATU WA NANE BORA

Mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwasalimia wa wachezaji wa timu ya IUO wakati wa mchezo katika yao dhidi ya Irole fc(PICHA KUTOKA MAKTABA)
Mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiongea wa wachezaji wa timu ya IUO wakati wa mchezo katika yao dhidi ya Irole fc(PICHA KUTOKA MAKTABA)

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Asas Super League 2019/2020 hatua nane bora imemaliza hatua ya mzunguko wa tatu kwa timu ya mafinga academy kuongoza kundi B na Isiman Fc kuongoza kundi A huku timu ya mafinga academy wakiongoza kwa kufunga magoli kumi.

Kufuatia kutamatika kwa mzunguko wa tatu wa Asas Super League 2019/2020 kundi Alinaongozwa na timu ya Isimani fc yenye alama saba na magoli ya kufunga matano huku ikiwa imefungwa goli moja tu katika michezo mitatu ya awali.

Kidamali fc na kalinga fc wanalinga alama kwa kila timu kwa kuwa na alama nne huku wakitofautiana kwa idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa huku Kidamali fc akiwa na magoli ya kufunga matano na wamefungwa magoli mawili tu na timu ya kalinga wakiwa wamefunga magoli mawili na kufungwa magoli manne.

Timu ya Young Stars wakiwa wanaburuza mkia kwenye kundi hilo wakiwa wana alama moja huku wakiwa wamefungwa jumla ya magoli sita katika michezo mitatu waliyocheza katika mzunguko wa kwanza wa Asas Super League 2019/2020

Kwa upande wa kundi B,timu ya Mafinga Academy wanaongoza kundi B wakiwa wamekusanya jumla ya alama tisa huku wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja huku wakiwa wamefunga jumla ya magoli kumi na kufungwa magoli mawili kwenye michezo mitatu ya awali ya kundi B.

Timu ya Mkimbizi fc,Nzihi fc na Irole Fc zote zimekusanya jumla ya alama mbili kwenye michezo mitatu huku wakiwa wametofautiana kwenye magoli ya kufunga na kufungwa,ukiangalia Mkimbizi Fc wamefunga magoli mawili na kufungwa magoli matatu,Nzihi fc wamefunga magoli mawili na kufungwa magoli manne na Irole Fc wamefunga magoli mawili na kufungwa magoli saba na ndio timu inayongoza kwa kufungwa magoli mengi kuliko timu yeyote ile kwenye hatua ya nane bora.

Asas Super League 2019/2020 itaendelea siku ya ijumaa tarehe sita mwenzi wa kumi na mbili kati Kidamali Fc na Isimani fc mchezo utachezwa katika uwanja wa Kidamali na ikumbukwe kuwa kwenye nmchezo wa awali timu ya Isimani ilishinda kwa goli moja bila.

CRDB YAKUTANA NA MAWAKALA WAKE MWANZA - 2020 KUJA NA MAPINDUZI MAPYA.


Benki ya CRDB imejipanga kuendelea kuwekeza zaidi katika huduma za kidigitali ili kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake, anasema Daniel Mbaga ambaye ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha Huduma Wakala CRDB.
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Huduma Wakala Daniel Mbaga akipiga darasa mawakala mkoa wa Mwanza katika mafunzo ya yaliyofanyika katika ukumbi mkubwa Rock City Mall jijini humo.
Sehemu ya kusanyiko hilo la mawakala mkoa wa Mwanza katika mafunzo ya yaliyofanyika katika ukumbi mkubwa Rock City Mall jijini humo.
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Huduma Wakala Daniel Mbaga akipiga darasa mawakala mkoa wa Mwanza katika mafunzo ya yaliyofanyika katika ukumbi mkubwa Rock City Mall jijini humo.
Licha ya Mafunzo hayo kulenga kuwaongezea Mawakala hao ufanisi katika utoaji huduma kwa wateja, pia yamelenga kuisaidia Serikali kutimiza azma yake ya kusambaza huduma nchini hasa maeneo ya vijijini ambako humuza ka kibenki zinahitajika kwaajili ya kusukuma harakati za maendeleo.
Kwa umakini Sehemu ya kusanyiko hilo la mawakala mkoa wa Mwanza katika mafunzo ya yaliyofanyika katika ukumbi mkubwa Rock City Mall jijini humo.
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Huduma Wakala Daniel Mbaga akipiga darasa mawakala mkoa wa Mwanza katika mafunzo ya yaliyofanyika katika ukumbi mkubwa Rock City Mall jijini humo.
"Leo tuko hapa kwaajili ya kuwapa mafunzo yatakayo waboresha kiutendaji kwakuwapa mbinu mbalimbali za kisasa, kumshawishi mteja kuzichangamkia huduma  zetu zenye manufaa" asema  Daniel Mbaga, Meneja Mwandamizi Kitengo cha Huduma Wakala
Engo moja wapo ya kusanyiko.
Darasa linaendelea.
Aidha Mawakala hawa wamefundishwa pia ni kwanini umakini unahitajika kwenye shughuli zao za utoaji huduma za kifedha, suala zima la kuhakikisha wanajikinga na dalili zote za utakatishaji fedha hususani pale linapojitokeza genge la watu lililopanga kuwaharibia mitaji yao.
Kwa kuwa Benki ya CRDB ndiyo Benki inayoongoza kuwa na mawakala wengi nchini, hivyo mafunzo hayo yamepangwa kwenye kalenda kuwa endelevu yakipangwa kuwafikia mawakala wote wa maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
Erick Willy ni Mkuu wa kitengo cha Huduma za CRDB Wakala (kushoto) akimkabidhi cheti ch ushindi nafasi ya pili Bi. Rose Josepha Mnangu.
Erick Willy ni Mkuu wa kitengo cha Huduma za CRDB Wakala (kushoto) akimkabidhi cheti cha ushindi nafasi ya tatu Alphrick FGeneral Supplies .
“Ningependa kuwakumbusha kuwa Sasa mteja wetu anaweza kufanya malipo akiwa ofisini kwake kwa njia ya mtandao wa intaneti akatuma pesa kwa wateja wake ambao pengine ingebidi awapelekee au waje pale, CRDB itaendelea kuboresha na tayari imesha fanikiwa kuongeza huduma nyingine bora ya malipo kwa njia ya mtandao ili kutengeneza fursa mbalimbali za kibiashara kwa wateja wetu”, alisema Erick Willy ni Mkuu wa kitengo cha Huduma za CRDB Wakala




Erick Willy ni Mkuu wa kitengo cha Huduma za CRDB Wakala (kushoto) akimkabidhi cheti cha ushindi nafasi ya nane Inocent Thobias.

Picha ya pamoja Meza kuu na Mawakala washindi.


Wednesday, December 4, 2019

MBNGE WA SINGIDA MASHARIKI AFUNGUA MASHINDANO YA MBUNGE KILIMO CUP.


Mashindano ya Mbunge Kilimo Cup yanayoshirikisha timu nane za jimbo la Singida Mashariki yameanza kutimua vumbi kwa timu ya Mawakala Fc kuwatandika vikali mahasimu wao Sokoni Fc bao mbili kwa bila.

Mashindano hayo yamefunguliwa na mbunge wa jimbo hilo Miraji Mtaturu katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Ikungi na kushirikisha viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilaya,viongozi wa serikali na madiwani wakiongozwa na mwenyekiti wa halmashauri ya Ikungi Ally Mwanga.

Akifungua mashindano hayo Mhe Mtaturu amewataka  wachezaji na wananchi kujiandaa vizuri kwenye msimu wa kilimo kwa kufuata kanuni bora za kilimo na kupanda mbegu zilizoshauriwa na wataalam ili kujitosheleza kwa chakula.

“Nawaahidi kuwa nitaendelea kufadhili mashindano kama haya ili kuwaweka vijana pamoja ikiwa ni kudumisha upendo,undugu na mshikamano,na kuunga mkono juhudi za serikali za kupambana na upatikanaji wa ajira kwa vile najua michezo ni ajira,”alisisitiza Mhe Mtaturu.

Ametoa rai kwa timu za wilaya ya Ikungi kuitikia wito wa kujisajili mapema ili kuwe na ligi ya wilaya itakayoendana na kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini(TFF) kila mwaka.

Awali akisoma taarifa ya mashindano kwa mgeni rasmi mratibu wa mashindano hayo Yassin Ntandu amesema wameamua kuandaa mashindano hayo ili kuwaweka vijana pamoja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri mhe Mwanga amempongeza sana mhe mbunge kwa kuwaandalia vijana ligi ya mpira ambayo itawasaidia kuwaepusha na makundi hatarishi na kuwahamasisha kufanya kazi.

“Nimevutiwa sana na utekelezaji wa majukumu anayofanya mbunge kwani toka alipokuwa mkuu wa wilaya alifanya mambo mengi ya kimaendeleo yanayostahili kuigwa,nimuahidi kama halmashauri kuunga mkono kwenye zawadi zitakazotolewa kwa washindi.

Nae Mwenyekiti wa CCM wilaya Mika Likapakapa amempongeza sana Mhe Mtaturu kwa namna anavyoitekeleza Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho kwenye sekta mbalimbali ikiwemo michezo kwa vitendo.

MWENYEKITI UVCCM ANG'OLEWA MADARAKANI KWA KUDANGANYA UMRI.


Aliyekua Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Mtwara, Aziz Mrope amevuliwa nafasi hiyo pamoja na kufutiwa uanachama wa umoja huo baada ya kubainika kuwa amedanganya umri.

Uamuzi wa kumvua madaraka  umetolewa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James baada ya mkutano wa umoja huo kupitisha maamuzi hayo  jijini Dodoma.

Bw.James akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza mkutano huo amesema kuwa uamuzi umefikiwa na  mkutano mkuu kujiridhisha kuwa Mrope alifanya udanganyifu kwenye umri.

” Kwa umoja wetu ambayo tumejadili katika Mkutano mkuu tumeridhia kwa pamoja kumfuta uanachama Bw.Mrope kwa udanganyifu na tumemuondoa katika nafasi yake ya uongozi aliyokuwa nayo, hivyo niuagize Mkoa wa Mtwara kuanza mara moja mchakato wa kujaza nafasi hiyo ambayo iko wazi,” Amesema Kheri.

Aidha alizungumzia ziara ya Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Bashiru Ally aliyoifanya visiwani Zanzibar  amesema kuwa ilikuwa ziara ya kuimarisha uhai wa Chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015 – 2020 Visiwani Zanzibar.

” Tumemsikia mzee mmoja anaitwa Maalim Seif anahoji uhalali wa Dk Bashiru, tumpe taarifa tu kuwa Katibu Mkuu ataendelea kufanya ziara hizo ambazo zina tija kwa Chama chetu na Serikali lakini pia akimaliza yeye na sisi vijana pamoja na Jumuiya za Wazazi na Wanawake tutafanya ziara zetu,” Amesema Kheri James.

Hata hivyo Bw.James amewapongeza viongozi wa Mikoa wa UVCCM na wanachama wao kwa kuhakikisha kuwa CCM inashinda kwa kishindo kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 24 mwaka huu.

Amewataka kuendelea kutangaza kazi kubwa inayofanywa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe Rais Dk John Magufuli ili kumtengenezea njia rahisi ya kupata kura nyingi katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.

”Sisi kama vijana moja ya majukumu yetu ni kuwa  mabalozi wa kazi nzuri inayofanywa na serikali yetu chini ya Mzalendo Dkt Magufuli, twendeni kazini tukatangaze yote yaliyofanywa na Serikali yetu ambayo ni ya Chama chetu.

STEVE NYERERE ASIMULIA MAAJABU YA BURIGI NA KISIWA CHA SAANANE ALIPOITWA NA MAMBA.



Mwishoni mwa wiki Mabalozi wa Uzalendo Kwanza Tanzania walitembelea hifadhi mbalimbali Kanda ya Ziwa ikiwemo Burigi Chato, Rubondo, Ibanda na kumalizia utalii wao kisiwa cha Saa Nane. Wakiwa wameambatana na waziri mwenye dhamana ya sekta husika, Waziri wa Mali Asili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na wasanii hao akiwemo maarufu wa wa maigizo na komedi Steve Nyerere amesimulia maajabu aliyokutana nayo.
Kisiwa cha Saanane (Saanane Island National Park) ni hifadhi ya taifa la Tanzania na ni hifadhi ndogo yenye eneo la kilomita za mraba 2.18, na iko umbali wa kilometa 2 kusini magharibi kutoka katikati ya jiji la Mwanza, katika Ghuba ya Ziwa Victoria nchini Tanzania. Hifadhi hii ilianzishwa kama bustani ya kwanza ya wanyama nchini Tanzania mwaka 1964 ikawa hifadhi kamili mwaka 2013. Lengo la kuanzishwa kwake ilikuwa kuhamasisha uhifadhi wa wanyama na kuelimisha jamii, pamoja na kutoa nafasi kwa wakazi wa Mwanza kupumzika.

Tuesday, December 3, 2019

MICHEPUKO KIKWAZO KWA WANAUME WENGI KUGWAYA KUPIMA UKIMWI


WAKATI vita dhidi ya mapambano ya ugonjwa wa Ukimwi ikipamba moto nchini, imebainika kuwa baadhi ya wanaume kuwa na uhusiano wa mapenzi na wanawake wengi ni moja ya sababu inayowafanya waogope kupima virusi vya Ukimwi.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (Nacopha), Leticia Kapela, alisema hayo jana, wakati wa maadhimisho ya kilele cha Siku ya ukimwi Duniani mkoani Mwanza.

Amesema kutokana na hali hiyo, wengi wao hujikuta wakisubiri wenzi wao wapime afya zao pindi wanapokuwa wajawazito, ambapo wakiona wako salama na wao huamini kuwa hawana maambuzi ya VVU.

Aidha Bi. Leticia ameongeza kuwa wanaume hao badala ya kupima afya zao, husubiri wake zao kupima afya wanapokuwa wajawazito.

PROF. NDALICHAKO AKERWA NA KUSUASUA KWA UJENZI WA CHUO CHA UALIMU


Na Ezekiel Mtonyole, Mbeya.

Kusuasua kwa ukamilishaji wa ujenzi wa baadhi ya miundombinu katika Chuo cha Ualimu Mpuguso, Mkoani Mbeya unaotekelezwa na mkandarasi Lukolo Construction Company umepelekea Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako kutoa agizo kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo kusimamia kwa karibu ukamilishaji wa kazi hiyo ili majengo hayo yaweze kutumiwa na walimu tarajali.

Waziri Ndalichako ametoa agizo hilo mara baada ya kukagua mradi huo na kukuta ukitekelezwa kwa hali isiyoridhisha na katika baadhi ya maeneo  kuwa chini ya kiwango.

Amesema mkandarasi huyo pamoja na kushindwa kukamilisha kazi yake kwa wakati  aliepewa muda zaidi ili kukamilisha kazi hiyo lakini bado hajakamilisha hivyo  kupelekea chuo kushindwa kutumia  miundo mbinu na Serikali kuchelewa  kufikia malengo yake ya uboreshaji na upanuzi wa Chuo hicho.

"Naelekeza mradi huu ukamilike ifikapo Desemba 30 tena kwa ubora kama ilivyopangwa  hivyo Katibu Mkuu afuatilie kwa karibu kazi hii  na makandarasi akishindwa kukamilisha mchukulie hatua," amesema Ndalichako.


Kiongozi huyo alisema kwa mujibu wa makubaliano mapya baada ya kurudishwa kazini ni kukamilisha kazi hiyo Desemba 30, 2019 lakini hata sasa haonekani kuwepo eneo la mradi na hakuna kinachoendelea.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa mbeya Albert Chalamila amemweleza waziri kuwa mkandarasi huyo asipokamilisha kazi hiyo kwa muda uliopangwa atachukuliwa hatua na kuwa kama Mkoa watafuatilia pia utekelezaji wake kwa karibu.

 Katika hatua nyingine  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya pia amemwomba waziri wa elimu kukipatia Chuo hicho  gari ili kusaidia katika huduma mbalimbali jambo ambalo Waziri aliridhia na kusema kuwa tayari  Wizara imenunua magari kwa ajili ya  vyuo vya ualimu ambavyo havina huduma hiyo.

Nae mkuu wa chuo cha ualimu Mpuguso Dorothy Mhaiki ameishukuru Serikali kwa namna inavyoboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika chuo hicho na kuomba kukarabati maeneo mengine yaliyobakia kwa kuwa bado kuna uhitaji ikiwa ni pamoja na kusaidia kupatikana watumishi wa kudumu Upande wa walinzi na wapishi ili kupunguza gharama ya uendeshaji.

Ukamilishaji wa ujenzi wa miundombinu katika Chuo cha Ualimu Mpuguso ni  sehemu ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi na ukarabati wa miundo mbinu katika Chuo hicho ambao umegharimu  kiasi cha sh bilioni 10 unaotekelezwa na serikali ya Tanzania na ile ya Canada.

Mradi huo umetekelezwa na kandarasi mbili Salem Construction Ltd ambao wamekalilisha kazi zao kwa ubora na majengo kuanza kutumika na Lukolo Construction Company ambao bado kazi yao haijakamilika.

Monday, December 2, 2019

'MAKUBWA' VIJANA WA KIUME WANAWAOMBA AKINAMAMA WAWALEE


 Mwenyekiti wa Baraza la watu wanaoishi na Ukimwi hapa nchini (NACOPHA), Leticia Kapela, amewataka vijana kujiepusha na ngono isiyo salama, sanjari na kuwaonya vijana wanaopenda kujihusisha kimapenzi na watu wazima hii ni kutokana na kuwepo kwa ongezeko kubwa la vijana wanaoishi na ugonjwa.

Hayo ameyabainisha Desemba 1, 2019, Jijini Mwanza, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani na kuwataka wanaume watu wazima, wanaowarubuni mabinti kuingia nao katika mahusiano ya kimapenzi waache tabia hiyo.

LUGOLA:HATUWAFUKUZI WAKIMBIZI

 Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kutoka Burundi, Pascal Barandagiye (kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), George   Okoth   Obbo wakibadilishana  mkataba unaohusu makubaliano ya pande hizo tatu katika kuhakikisha urejeshwaji  wa  wakimbizi  wa Burundi   wanaotaka   kurejea   nchini   kwao  kwa  hiari.  Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, Kangi  Lugola,  akisaini moja ya mkataba  unaohusu  makubaliano  katika  kuhakikisha  urejeshwaji  wa  wakimbizi  wa Burundi  wanaotaka  kurejea  nchini  kwao  kwa  hiari.Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi  wa  Idara ya Wakimbizi,Sudi Mwakibasi na Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma,Rashid Mchata. Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kutoka Burundi, Pascal Barandagiye, akisaini moja ya mkataba unaohusu makubaliano katika kuhakikisha urejeshwaji  wa  wakimbizi  wa Burundi  wanaotaka  kurejea  nchini  kwao  kwa  hiari. Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Kamishna Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), George  Okoth  Obbo, akizungumza wakati wa Kikao cha makubaliano katika kuhakikisha urejeshwaji  wa  wakimbizi  wa Burundi  wanaotaka  kurejea  nchini  kwao  kwa  hiari. Kulia ni Mwakilishi wa UNHCR nchini Tanzania,Chansa Kapaya.Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akizungumza wakati wa Kikao cha makubaliano katika kuhakikisha urejeshwaji  wa  wakimbizi  wa Burundi  wanaotaka  kurejea  nchini  kwao  kwa  hiari.Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Hatuwafukuzi Wakimbizi-Lugola
Na Abubakari Akida,MOHA
Serikali ya Tanzania imepinga tuhuma zinazoelekezwa kwake kwamba imekua ikiwafukuza wakimbizi kutoka nchini Burundi wanaoishi katika makazi na kambi mbalimbali katika mikoa ya Kigoma,Tabora na Katavi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Kangi Lugola katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam kikihusisha pande tatu;Serikali ya Tanzania,Serikali ya Burundi na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi(UNHCR),huku mkataba maalumu ukisainiwa na pande hizo tatu lengo ni kuwezesha urejeshwaji wa wakimbizi walioomba kurejea nchini kwao baada ya amani kurejea.
“Ni vyema tukaliweka hili wazi ili jumuiya za kimataifa na Mataifa mengine yajue kwamba tunaposema tunawarejesha wakimbizi wa Burundi sisi na Serikali ya Burundi tunachofanya ni kuhamasisha,kuhimiza wale ambao wako na hiari warudi Burundi,baada ya kugundua amani imerejea Burundi,sasa tunapofanya hivyo wenzetu wanatafasiri kwamba tunawafukuza wakimbizi,hiyo sio sahihi,serikali ya Tanzania na wananchi wake kwa ujumla wamekua wakipokea wakimbizi kutoka nchi mbalimbali na hatujaanza leo tumekua tukiwahifadhi na amani inaporejea wanaomba warejee katika nchi zao” alisema Lugola
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa Mambo ya Ndani kutoka nchini Burundi,Pascal Barandagiye amesemaBurundi sasa ina amani na wameona ipo haja ya raia wake warejee ili kuweza kuijenga nchi yao.
“Tunawahakikishia kwamba kama nchi tuna uwezo wa kupokea warundi 2000 kwa wiki na sisi tutahakikisha warundi wote wanarejea nyumbani,tutawafuata popote walipo,tunawahitaji warudi nyumbani ili tuje tujenge nchi yetu pamoja,” alisema Barandagiye
Kwa upande wa Kamishna Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi(UNHCR),George Okoth Obbo alisema wameshirikiana na nchi mbili za Tanzania na Burundi katika kuhakikisha yanakuwepo mazingira salama na yenye utu katika uendeshaji wa zoezi hilo huku akiwashukuru Watanzania kwa mwema wao wa kuendelea kuwapokea wakimbizi.
“Tanzania imekua nchi rafiki kwa wakimbizi,mawaziri wote wawili wamekubaliana suala la kurudi wa warundi nchini kwao,tuko hapa kuhakikisha zoezi hilo litaenda salama likizingatia ustawi wa pande zote tatu” alisema Okoth
Ni takribani mwezi mmoja umepita tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Magufuli kwenye ziara yake katika mkoa wa Katavi kuagiza pande zote zinazohusiana na masuala ya wakimbizi wakutane ili kuweza kujadili suala la warundi wanaojiandikisha kwa hiari kurudi nchini kwao,akiwaambia umefika wakati sasa wakurudi katika nchi zao kwenda kuzijenga   huku akiwaonya wakimbizi wanaoshiriki katika matukio ya uhalifu hapa nchini.

RIPOTI YA UCHUNGUZI DHIDI YA RAIS TRUMP KUWEKWA WAZI WIKI HII.

Ripoti ya uchunguzi inayolenga kumshitaki Rais Donald Trump wa Marekani, itawasilishwa leo kwa faragha mbele ya wabunge muhimu wakati wabunge wa chama cha Democratic wakizidi kuongeza shinikizo, licha ya azimio la Ikulu ya Marekani, white House kutoshiriki usikilizwaji wa kwanza mbele ya kamati ya mahakama.

Kamati ya usalama iliyo na wingi wa wajumbe wa chama cha Democratic imesema kwamba ripoti hiyo, iliyojumuishwa baada ya wiki mbili za ushahidi itajieleza yenyewe, katika kile mwenyekiti wa kamati hiyo Adam Schiff alichokiita makosa yaliyofanywa na rais juu ya Ukraine.

Ripoti hiyo inatayarishwa kwa ajili ya wabunge wa kamati kuitathimni kuelekea kura itakayopigwa kesho ya kuipeleka kwenye kamati ya mahakama.

Hapo jana ikulu ya White House iliwaeleza wabunge wa chama cha Democratic kwamba rais Trump na mawakili wake hawatoshiriki katika mchakato wa uchunguzi wiki hii wakielezea kuwa umekosa misingi ya haki

JIMBO KATOLIKI MOSHI LAMPATA ASKOFU.


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Ludovick Joseph Minde, ALCP/OSS kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Moshi, nchini Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Askofu Ludovick Joseph Minde alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki Kahama. Itakumbukwa kwamba, Askofu Minde alizaliwa tarehe 9 Desemba 1952 kwenye Parokia ya Kibosho, Jimbo Katoliki la Moshi.

Ni mtoto wa mzee Joseph Ndasika Minde na Mama Maria Joseph Mukure. Baada ya masomo yake Seminari Ndogo ya Mtakatifu James, Jimbo Katoliki la Moshi kunako mwaka 1979 alijiunga na Shirika la Mapadre wa Maisha ya Kitume na Kazi ya Roho Mtakatifu ALCP/OSS. Akaendelea na masomo yake ya falsafa Seminari kuu ya Kibosho na kuhitimisha masomo ya taalimungu kwenye Seminari kuu ya Segerea, Jimbo kuu la Dar es Salaam.

Tarehe 26 Juni 1986 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Mtakatifu Yohane Paulo II kunako tarehe 24 Aprili 2001 akamteuwa kuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Kahama na kuwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 5 Agosti 2001 na Kardinali Polycarp Pengo, Askofu mkuu mstaafu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, akisaidiana na Askofu Mathew Shija, Muasisi wa Jimbo Katoliki la Kahama pamoja na Hayati Askofu Mstaafu Amedeus Msarikie wa Jimbo Katoliki la Moshi. 

Itakumbukwa kwamba, Askofu Ludovick Joseph Minde, ALCP/OSS ni kati ya Mapadre watano walioteuliwa kwenda Roma kwa masomo zaidi baada ya hija ya kitume ya Mtakatifu Yohane Paulo II nchini Tanzania kunako mwaka 1990. Mtakatifu Yohane Paulo II alitaka kuimarisha malezi na makuzi ya majandokasisi kutoka Tanzania.

Tangu mwaka 1990 hadi mwaka 1995 alikuwa mjini Roma akijifunza Maandiko Matakatifu na hatimaye, akajipatia Shahada ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana, kilichoko mjini Roma. Ni kati ya wanafunzi waliofanya vizuri sana katika masomo yao kwa mwaka huo. 

Katika maisha na utume wake, amewahi kuwa Jaalimu wa Maandiko Matakatifu, Mlezi na Baba wa maisha ya kiroho, Seminari kuu ya Segerea, Jimbo kuu la Dar es Salaam. Itakumbukwa kwamba, Jimbo katoliki la Moshi limekuwa wazi baada ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 27 Desemba 2017 kumteua Askofu Isaac Amani Massawe wa Jimbo Katoliki Moshi, kuwa Askofu mkuu mpya wa Jimbo Kuu la Arusha, nchini Tanzania.

WANAMBEYA WAISHIO MWANZA WAFANYA HILI


Kikundi cha watu wanaotoka mikoa ya kusini ambao wanaishi jijini Mwanza maarufu kama MBEYA NI KWETU  mwishoni mwa wiki wamefanya harambee ya kukusanya fedha ambazo zitatumika kujenga chuo cha ufundi kitakachotoa elimu kwa vijana waliohitimu elimu ya msingi na wamekosa alama za ufaulu wa kuendelea na elimu ya sekondari.

Akisoma lisala kwa mgeni ramsi Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana  Dk Philis Nyimbi aliyemwakilisha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Tulia Akson Mwansasu, katibu wa kikundi hicho Paul Mwaiteleke amesema kikundi hicho kilichoanzishwa mwaka 2018, hadi kufikia sasa kina jumla ya wanachama 102 na fedha zilizopo benki kutokana na michango ni millioni 30,208,348/= 

Akiongoza harambee hiyo ambayo ilidhamiria kukusanya shilingi kiasi cha Shilingi milioni 20 na hatimaye kufanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni saba, Dk Nyimbi amewapongeza na kuwataka kuendelea na juhudi za kukusanya fedha ili kuweza kutimiza adhma waliyojiwekea.

Sunday, December 1, 2019

ARSENAL YAKALIWA KOONI NA NORWICH EPL, AUBAMEYANG ADUNGUA MBILI.


Klabu ya soka ya Arsenal imetoka sare na katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Norwich City katika mchezo wa ligi kuu Uingereza wakiwa na kocha wao mpya wa muda Freddie Ljungberg.

Katika mchezo huo ambao Arsenal walikuwa ugenini wametoka sare ya kufungana mabao 2-2.

Norwich ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 21 kupitia kwa Teemu Pukki lakini Arsenal walisawazisha dakika ya 29 kwa njia ya penalti kupitia kwa Pierre-Emerick Aubameyang.

Hata hivyo Norwich walipata bao dakika mbili za nyoogeza kipindi cha kwanza kupitia kwa Todd Cantwell, lakini Aubameyang alisawazisha tena dakika ya 57.

Kwa matokeo hayo sasa Arsenal inashika nafasi ya nane ikiwa na alama 19 wakati Liverpool ikiongoza ligi hiyo ikiwa na alama 40.

WAZIRI MHAGAMA AKAGUA MAANDALIZI SHEREHE ZA UHURU MWANZA.

Maandalizi ya maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru yamefikia hatua za kuridhisha huku Serikali ikieleza kuwa sherehe hiyo itapambwa na onesho maalum la Jeshi la Jadi la sungusungu kutoka Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameeleza itakuwa ni mara ya kwanza kwa jeshi hilo kuonesha namna wanavyofanya kazi za ulinzi katika maeneo yao ili kuendelea kuenzi nia ya Rais wa Awamu ya Tano Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ya kuilinda amani na utulivu uliopo nchini.


Waziri alieleza hayo mapema Novemba 30, 2019 alipotembelea na kukagua maandalzii ya onesho hilo yanayoendelea katika Kijiji cha Hunghumalwa Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.

“Hii itakuwa ni mara ya kwanza kuwa na onesho hili maalum ambalo linatukumbusha nia ya Mhe. Rais ya kuilinda amani iliyopo na kuhakikisha haichezewi kwa gharama yoyote na kuona namna tunavyojivunia jeshi hili lililoundwa katika misingi na maadili mema ya amani na utulivu,” alisema waziri Mhagama

Aliongezea kuwa, Jeshi hilo litajumuisha zaidi ya sungusungu 1300 watakaoshiriki kwa siku hiyo kwa kuongozwa na Manji wao pamoja na Mtemi wa Wilaya Mogan Shimbi.

Sambamba na hilo maandalizi mengine ikiwemo, uandaaji wa uwanja wa CCM Kilumba, mazoezi ya Majeshi (Gwaride), Usafi wa mazingira pamoja na vikundi vya burudani yanaendelea mkoani hapo.

“Maandalizi muhimu ikiwa ni pamoja na marekebisho ya miundombinu katika uwanja yanaendelea pamoja na maandalizi muhimu ikiwemo, kutoa mialiko, kuandaa  malazi kwa wageni, kuandaa vikundi vya ngoma za asili, kuandaa gwaride , kuandaa wanafunzi wa watakaoumba umbo la bendera, pamoja na nyimbo za kizazi kipya  na mahitaji mengine muhimu yapo katika hatua za kuridhisha,” alisema Waziri Mhagama.


Aidha, kutakuwa na vikundi vya burudani ikiwemo; ngoma za asili kutoka mkoa wa Mara (Ritungu) na mkoa wa Mwanza, wimbo maalum kutoka Zanzibar pamoja na kwaya ya AIC Mwanza na bendi ya Tanzania One Theatre (T.O.T) vitatumbuiza.

Alifafanua kuwa maonyesho hayo yatakayofanyika Desemba 9 yatajumuisha gwaride maalumu la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama nchini.

 “Watoto 3200 kutoka shule za msingi na sekondari za mkoa wa Mwanza wataonesha umbo la bendera ya Taifa letu,” alisema Waziri Mhagama

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella aliwasihi Watanzania kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kuendelea kuilinda amani iliyopo kwa kuzingatia kaulimbiu ya mwaka huu pamoja na kuendelea kuwa na uzalendo na kufanya kazi kwa bidiii kwa ajili ya kujiletea maendeleo.

Pia, aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo na kuendelea kujiandaa kwa bidii, usanifu na ubunifu wa kipekee katika kuiadhimisha siku hiyo muhimu.

“Ninamshukuru sana Mhe. Rais kwa kuelekeza maadhimisho haya kufanyika mkoani kwetu, niiwaase wananchi wa Mwanza kuitumia heshima tuliyopewa kwa kujitokeza kwa wingi katika siku hiyo ili kuunga mkono jituhada za Mhe. Rais wetu,” Alisisitiza Mongella.

Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri kwa mwaka huu (2019) kitaifa yatafanyika Mkoani Mwanza katika viwanja vya CCM Kilumba ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli na kupambwa na kauli mbiu inayosema “Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri; Uzalendo, Uwajibikaji na Ubunifu ni msingi wa Ujenzi wa Uchumi wa Tifa letu”.

WAZIRI MWAKYEMBE AMTUMIA RC TANGA SALAMU ZA RAMBIRAMBI -VIFO VYA MASHABIKI WA HASSAN MWAKINYO.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe, ametuma salamu za rambi rambi kwa mkuu wa mkoa wa Tanga, Martin Shigella kufuatia vifo vya watu wawili ambao ni mashabii wa bondia Hassan Mwakinyo.

Soma barua hiyo hapa chini.

WAZAZI WAWAPAKA UNGA WATOTO WA KIKE DARASA LA 3 KUWAVUTIA WANAUME.


Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini Yassin Ally ameeleza kuwa maambukizi mapya ya Virusi vya ukimwi kwa umri wa miaka 15-24 umeongezeka kwa kasi kutokana na wazazi jinsi wawaleavyo watoto wao pamoja na baadhi ya mikoa ikiwemo mkoa wa shinyanga wanafunzi wa wa kike kuanzia darasa la tatu wanapakwa unga ujulikanao kama 'Samba' ambao unadaiwa kuwavuta wanaume.

Jeh nao baadhi ya viongozi wa dini wanaojihusisha na vitendo viovu vya ukatili ambapo ni chanzo cha maambukizi nani wa kuwakemea?

A