ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, December 2, 2019

LUGOLA:HATUWAFUKUZI WAKIMBIZI

 Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kutoka Burundi, Pascal Barandagiye (kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), George   Okoth   Obbo wakibadilishana  mkataba unaohusu makubaliano ya pande hizo tatu katika kuhakikisha urejeshwaji  wa  wakimbizi  wa Burundi   wanaotaka   kurejea   nchini   kwao  kwa  hiari.  Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, Kangi  Lugola,  akisaini moja ya mkataba  unaohusu  makubaliano  katika  kuhakikisha  urejeshwaji  wa  wakimbizi  wa Burundi  wanaotaka  kurejea  nchini  kwao  kwa  hiari.Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi  wa  Idara ya Wakimbizi,Sudi Mwakibasi na Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma,Rashid Mchata. Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kutoka Burundi, Pascal Barandagiye, akisaini moja ya mkataba unaohusu makubaliano katika kuhakikisha urejeshwaji  wa  wakimbizi  wa Burundi  wanaotaka  kurejea  nchini  kwao  kwa  hiari. Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Kamishna Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), George  Okoth  Obbo, akizungumza wakati wa Kikao cha makubaliano katika kuhakikisha urejeshwaji  wa  wakimbizi  wa Burundi  wanaotaka  kurejea  nchini  kwao  kwa  hiari. Kulia ni Mwakilishi wa UNHCR nchini Tanzania,Chansa Kapaya.Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akizungumza wakati wa Kikao cha makubaliano katika kuhakikisha urejeshwaji  wa  wakimbizi  wa Burundi  wanaotaka  kurejea  nchini  kwao  kwa  hiari.Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Hatuwafukuzi Wakimbizi-Lugola
Na Abubakari Akida,MOHA
Serikali ya Tanzania imepinga tuhuma zinazoelekezwa kwake kwamba imekua ikiwafukuza wakimbizi kutoka nchini Burundi wanaoishi katika makazi na kambi mbalimbali katika mikoa ya Kigoma,Tabora na Katavi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Kangi Lugola katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam kikihusisha pande tatu;Serikali ya Tanzania,Serikali ya Burundi na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi(UNHCR),huku mkataba maalumu ukisainiwa na pande hizo tatu lengo ni kuwezesha urejeshwaji wa wakimbizi walioomba kurejea nchini kwao baada ya amani kurejea.
“Ni vyema tukaliweka hili wazi ili jumuiya za kimataifa na Mataifa mengine yajue kwamba tunaposema tunawarejesha wakimbizi wa Burundi sisi na Serikali ya Burundi tunachofanya ni kuhamasisha,kuhimiza wale ambao wako na hiari warudi Burundi,baada ya kugundua amani imerejea Burundi,sasa tunapofanya hivyo wenzetu wanatafasiri kwamba tunawafukuza wakimbizi,hiyo sio sahihi,serikali ya Tanzania na wananchi wake kwa ujumla wamekua wakipokea wakimbizi kutoka nchi mbalimbali na hatujaanza leo tumekua tukiwahifadhi na amani inaporejea wanaomba warejee katika nchi zao” alisema Lugola
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa Mambo ya Ndani kutoka nchini Burundi,Pascal Barandagiye amesemaBurundi sasa ina amani na wameona ipo haja ya raia wake warejee ili kuweza kuijenga nchi yao.
“Tunawahakikishia kwamba kama nchi tuna uwezo wa kupokea warundi 2000 kwa wiki na sisi tutahakikisha warundi wote wanarejea nyumbani,tutawafuata popote walipo,tunawahitaji warudi nyumbani ili tuje tujenge nchi yetu pamoja,” alisema Barandagiye
Kwa upande wa Kamishna Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi(UNHCR),George Okoth Obbo alisema wameshirikiana na nchi mbili za Tanzania na Burundi katika kuhakikisha yanakuwepo mazingira salama na yenye utu katika uendeshaji wa zoezi hilo huku akiwashukuru Watanzania kwa mwema wao wa kuendelea kuwapokea wakimbizi.
“Tanzania imekua nchi rafiki kwa wakimbizi,mawaziri wote wawili wamekubaliana suala la kurudi wa warundi nchini kwao,tuko hapa kuhakikisha zoezi hilo litaenda salama likizingatia ustawi wa pande zote tatu” alisema Okoth
Ni takribani mwezi mmoja umepita tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Magufuli kwenye ziara yake katika mkoa wa Katavi kuagiza pande zote zinazohusiana na masuala ya wakimbizi wakutane ili kuweza kujadili suala la warundi wanaojiandikisha kwa hiari kurudi nchini kwao,akiwaambia umefika wakati sasa wakurudi katika nchi zao kwenda kuzijenga   huku akiwaonya wakimbizi wanaoshiriki katika matukio ya uhalifu hapa nchini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.