ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 26, 2015

MAGAZETI DEC 26 AZAM TV.

Hapatoshi Kerry dhidi ya Julio uwanjani leo, Guardiola yupo tayari kutua Old Trafford, Wenger amtengea dau Chicharito. Fuatilia Magazeti ya michezo hapa.

WARAGHABISHI WAKOLEZA KASI YA MABADILIKO WILAYANI KISHAPU.

Watendaji wa Kituo cha Maendeleo cha Jamii ya Uchunga wilayani Kishapu  wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi mbele ya jengo la kituo hicho likiwa limekamilika kutokana na michango yao ya fedha na nguvu kazi. 


Na Krantz Mwantepele ,Kishapu 

Mabadiliko katika jamii yoyote kwa kiasi kikubwa huchangiwa na ongezeo la mahitaji ya binadamu katika mambo mbalimbali. Kwamba, kadri dunia inavyopitia mabadiliko, kadiri ile ile changamoto, mahitaji na huduma katika jamii husika huongezeka.

Ili kufikia malengo yanayotokana na misukumo na mageuzi yasiyokwepeka, binadamu amelazimika kubuni mikakati mbalimbali ya maendeleo. Si hivyo tu, mabadiliko haya yamemfungulia binadamu fursa ya uthubutu wa kujaribu mambo mbalimbali, siyo tu kwa faida yake, bali jamii nzima inayomzunguka.

"Sikutegemea kama siku moja katika maisha yangu nitapata wazo ambalo lingebadili na kushawishi watu kuchukua hatua kwa mustakabali wa jamii.”

Hiyo ni kauli ya mraghbishi Revocatus Richard ambaye pia, kitaaluma ni mwalimu katika shule ya msingi Uchunga. Richard alitoa kauli hiyo baada ya kupitia mafunzo ya uraghbishi na mwalimu mwenzake, Restusta Katobesi, ambao  baadaye kwa pamoja, walianzisha Kituo cha KIMAJU (Kituo cha Maendeleo cha Jamii ya Uchunga) kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji na wananchi. Na hilo ndiyo lilifanya achaguliwe kuwa Mkurugenzi wa kituo hicho.

Walimu hao walikuwa miongoni mwa waraghbishi 30 walioshiriki mafunzo ya uraghbishi yaliyotolewa mwezi Machi, mwaka 2012 wilayani Kishapu katika mkoa wa Shinyanga. Kutokana na faida na maarifa waliyoyapata kwenye mafunzo hayo, walimu hao waliamua kuunda umoja uliokuwa chachu ya kuanzishwa kituo hicho cha maendeleo.

Mwanazuoni Sarah Earl, aliwahi kusema:  "Maendeleo ni watu na mazingira yao. Kwamba, kusingekuwa na maana iwapo barabara, hospitali, shule na miradi mingine ya  maendeleo inayojengwa kwa ajili ya watu isingetumika."

Kwa mantiki hiyo, miradi yote ya maendeleo, ikiwamo Chukua Hatua ni kwa ajili ya ustawi wa maisha ya watu. Kwa kuwa kiini cha maendeleo ni watu. Shabaha kubwa ya mradi huu wa Chukua Hatua ni kuhakikisha  wananchi (waraghbishi) wanajielewa na kujitambua katika  kutimiza majukumu yao na kupata haki zao zikiwamo huduma bora za kijamii na kuhakikisha  wananufaika na rasilimali zao. Pia unawasaidia kuwawajibisha viongozi wao ili watimize majukumu yao ya kuhamasisha maendeleo na kutatua shida za wananchi.


Mraghbishi ni mwananchi anayeleta uhai mpya ndani ya jamii kwa kutambua matatizo na kupendekeza njia sahihi za kuyatatua.Katika kipindi cha miaka mitano ya mradi, zaidi ya waraghbishi 380 wameleta uhai katika jamii zao, hususani kwenye vijiji vya mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Arusha hasa katika wilaya ya Ngorongoro.


Tafsiri ya uhai huu ni pamoja na kuwachukulia hatua viongozi wabadhirifu, watendaji wabovu, kuandaa midahalo, kudai huduma bora za kijamii, kuibua na kufuatilia matatizo mbalimbali katika vijiji vyao kama ambavyo waraghbishaji Richard na Katobesi wamefanya.


Uraghbishi Kijiji cha Uchunga


Baada ya kupatiwa mafunzo ya uraghbishi, walimu hawa walirudi kijijini kwao wakiwa na jukumu moja la kutambua changamoto zinazoikabili jamii yao na kupendekeza nini kifanyike wakitumia nafasi na uwezo walio nao.

Kikubwa walichoangalia ni mustakabali wa mtoto wa Kijiji cha Uchunga, kwa maana ya nafasi ya mtoto, ikiwamo ya kufahamu huduma anazopata.Katika kufikiria sehemu ya kuanzia na ili kumpa mtoto wa kike nafasi katika jamii, hasa ya kuongoza, walianza na wanafunzi wa shule wanayofundisha, Uchunga.


“Nimepata bahati ya kuwa mwalimu mkuu msaidizi mara kadhaa na nimetumia fursa hiyo kuleta mabadiliko, nikianzia kubadilisha utaratibu wa kuchagua viongozi wa wanafunzi katika shule yetu," alisema Richard na kuongeza:

"Kwanza tulibadilisha wazo la Kaka Mkuu na badala yake tukasema tutakuwa na Kiranja Mkuu, ili kutoa fursa kwa wanafunzi wa kike kushika nafasi za uongozi wa wanafunzi."
Hadi sasa chaguzi mbili za kidemokrasia za kuchagua viongozi wa wanafunzi zimefanyika shuleni Uchunga Julai 2012 na Mei 2013.


Katika kuhakikisha wanaendeleza mawazo hayo, waraghbishi hao walikuja na wazo la kujenga kituo cha kujisomea. Walianza kuwatembelea wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Uchunga wanaoishi katika kijijini hapo.  


Baadhi ya wananchi na wajumbe wa Kituo cha Maendeleo cha Uchunga wakiwa mbele ya kituo kabla hakijaezekwa na mabati.


Ili kufikia malengo yao, waliomba ushirikiano, siyo tu kwa walengwa ambao ni wanafunzi, bali kutoka kada zingine ndani ya jamii.
Akielezea jinsi walivyoanza, mraghbishi Katobesi alisema:
“Tulikutana na wanafunzi na kuunda umoja wa kikundi wa Wanafunzi wa Sekondari Uchunga (UWASU).  Kikundi hiki kiliamsha hamasa kwa wanafunzi waliokukubali kujitolea kufanya kazi.”  
Na baadhi ya wanafunzi hao wametembelea shule nyingine na kuhamasisha wenzao kujitolea kusaidia kazi mbalimbali kama kuchota maji na kuokota mawe kwa ajili ya ujenzi wa  jengo la kituo hicho cha kujisomea.

Ndani ya jamii yoyote kuna mamlaka, hivyo ili malengo yao yatimie kuliwalazimu waraghbishaji hao kupata ruhusa kutoka kwa walimu na aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji wakati huo, Mahona Punguja.

“Baada ya kutoka kwenye mafunzo yao, walikuja kuzungumza na mimi kuhusiana na mambo waliyojifunza na jinsi watakavyoleta mabadiliko. Nilikubaliana nao na kuweka utaratibu wa kuwashirikisha wazazi kama wadau muhimu na makundi mengine maalumu,” alisema Punguja.
Makundi maalumu ni pamoja na watumishi wa uma, kwa maana ya walimu na mtendaji wa kijiji na kata, wazee maarufu, viongozi wa dini, vijana na wajumbe wa halmashauri ya serikali ya kijiji. Waraghbishi hawa kwa ushirikiano na uliokuwa uongozi wa serikali ya kijiji waliweza kukutana na makundi hayo ili kuwaelimisha kuhusu wazo la kituo cha kujisomea. Baada ya kila kundi kukutana na waraghbishi, uliitishwa mkutano wa pamoja wa kujadili jambo hilo na kamati  ikaundwa ya kusimamia mchakato mzima. Kamati hii ilichaguliwa kwa kila kundi kuwa na mwakilishi wake.
“Njia ya kwanza ilikuwa ni kukusanya fedha, kisha kuwaomba wananchi kuchangia nguvu zao. Kila mmoja kwa nafasi yake alijitolea. Wengine tulisomba mawe na kuchimba msingi.  Wanawake walileta vyakula kwa ajili ya mafundi ambao nao walijitolea pia utaalamu wao bure”, anaelezea Michael Butu, Mwenyekiti wa Kituo cha KIMAJU.

Wanajamii waliohamasika waliombwa kuchangia kila mmoja Shilingi 10,000 za Kitanzania, ingawa baadhi walitoa nusu ya mchango huo. Kila kitongoji kiliombwa kuchangia Shilingi 60,000. Michango hii ilikusanywa baada ya kuundwa kwa nguvu ya pamoja na wenyeviti wa vitongoji. Kati ya vitongoji vitatu, viwili vilikamilisha ahadi zao.
Harakati hizi ziliwezesha wanajamii kujenga kituo hadi ngazi ya linta, kabla ya mlezi wa kituo hicho, Charles  Dida kutoa shilingi 355,000 kama mkopo kwa ajili ya  kununua mabati na mbao.

“Nilipoona jengo letu linasuasua, niliamua kujitolea kufanikisha ujenzi. Niliamua kumshirikisha mke wangu, ambaye aliunga mkono uamuzi wangu kwa kujua mafanikio yatakayopatikana ni ya jamii nzima,” alisema Charles Dida.

Katika hili tumejifunza mahusiano yaliyopo baina ya baba na mama katika kufanya maamuzi ya pamoja. Ni tofauti na mfumo dume uliozoeleka katika jamiii ya kisukuma. Na mpaka sasa kituo kimeweza kulipa kiasi cha Shilingi 110,000 na hivyo bado kinadaiwa Shilingi 245,000.
Ili kuhakikisha kituo kinaendelea kutoa huduma kwa watoto wa Uchunga wajumbe wa kamati tendaji wanafanyakazi kwa kujitolea kwa kuwa wao kuwa sehemu ya jamii ya wananchi wa kijiji cha Uchunga.

“Nilihamasika baada ya kupendezwa na wazo la kuanzishwa kwa kituo hiki. Na siku nilipoombwa kuwa sehemu ya kuleta mafanikio, nilikubali mara moja na kushiriki mikutano na ratiba nyingine,” alifafanua katibu wa vijana, Bahati Juma.
Moja ya majukumu aliyokabidhiwa ni huhakikisha kituo kinafunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa 10 jioni. Kwa wastani, kituo kinahudumia wanafunzi 20 kwa siku.

Mbali na katibu huyo, watendaji wengine ni pamoja na mkurugenzi, katibu, mhasibu, na kamati tendaji chini ya mwenyekiti na mlezi wa Kituo. Nafasi hizi zote zina wasaidizi isipokuwa ya mkurugenzi na mlezi.

Uongozi huu ulipatikana kidemokrasia kwa kuchaguliwa kwenye mkutano mkuu wa kijiji. Baada ya kupata uongozi walitengeneza katiba na kukisajili kituo chao. Kwa mujibu wa katiba ya kituo hicho, uongozi unachaguliwa kila baada ya miaka mitatu.

“Waasisi wa kituo ndio waliopendekeza mfumo wa uongozi na baada ya hapo wakauwakilisha kwenye mkutano mkuu wa kijiji. Kwa hiyo walioweza walishiriki. Na kila mtu aliyeona anafaa kuwa sehemu ya uongozi wa kituo hicho alipendekeza jina lake ama la mwenzake. Baada ya majina hayo kupatikana ndipo yalipigiwa kura na kupata viongozi,” anafafanua mwenyekiti wa kituo, Michael Butu.

Tukiachilia suala la uongozi, kuna utaratibu maalumu wa kuendesha kituo hicho. Kuna vijana wanaohusika na kuhakikissha ofisi inafunguliwa ili kutoa huduma za kujisoma bure, ikiwa ni mkakati wa kuhamasisha watu na kukifahamu kituo.


Huduma za KIMAJU
Taasisi hii ya kijamii kwa kiasi kikubwa imelenga kwenye uzalishaji maarifa kwa kutoa huduma ya maktaba, ambayo wanafunzi wanaoishi kijiji cha Uchunga hutumia kusoma na kufanya kazi za nyumbani baada ya masomo shuleni.
Katika ziara za ufuatiliaji na uwezeshaji, wafanyakazi wa shirika mtendaji la TAMASHA katika mradi huo wa Chukua Hatua, walishauri kituo kupanua wigo wa huduma zake, kama anavyoelezea Afisa Mradi Winston Churchill.
“Tuliwashauri kuwalenga pia vijana walio nje ya shule ili kuwawezesha vijana wote kutumia kituo hicho vizuri kijijini hapo.”
Watu wazima pia wanatumia kituo hicho kujisomea magazeti, ambayo huwa ni ya siku nyingi na hii ndio sababu ya umuhimu wa kutafuta redio ili watu wasikilize taarifa za habari.
Hali hii imehamasisha wanafunzi wa shule za sekondari na msingi kuja kujisomea, kama anavyoelezea mwanafunzi wa darasa la saba Leticia Isaka kutoka Shule ya Msingi Uchunga,





“Kituo kinanisaidia kutambua mambo mbalimbali, kwa mfano kupitia mafunzo ya hapa, napata malezi bora ya kuniandaa niwe mwalimu au daktari. Lakini si hivyo tu, wakati wa mapumziko ya saa sita huwa tunakuja kujisomea hapa baada ya kupatiwa mazoezi na walimu shuleni,”

Pamoja na sababu nyingine, uwepo wa kituo hiki umechangia kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu katika shule ya sekondari ya kata ya Uchunga, ambapo mwaka 2013 jumla ya wanafunzi .... tu ndio waliofaulu katika ngazi ya ... , wakati mwaka uliofuata waliongezeka na kufikia kiasi cha ...
"Mbali na mafanikio haya, kituo kina changamoto kadhaa ikiwamo ukosefu wa meza, viti na makabati ya kuhifadhia vitabu," anasema mkurugenzi wa kituo, Richard na kuongeza:
“Haya mabenchi na meza tumeazima kanisani na tukimaliza tunarudisha sehemu husika. Hatuna vitabu vya mitaala kwa ajili ya wanafunzi wetu, ingawa eneo la kujisomea lipo vizuri, nishati ya umeme nayo ni shida.”

Kimsingi, wanajamii wa Uchunga kwa kushirikiana na waraghbishi na uongozi kwa kijiji wamefanikiwa kufikia malengo.

AJALI YAUA WA 4 NA KUJERUHI 105

**SATURDAY EXPRESS** Ajali mbaya ya kusikitisha imetokea jana 25/Dec2015 majira ya saa 12 asubuhi eneo la Soni Lushoto Tanga na watu wapatao 4 kufariki na majeruhi 105 baada ya lori walilokuwa wakisafiria Kutoka Korogwe kwenda Mugwashi wilayani Lushoto kuacha njia na kupinduka. Gari hilo aina ya Mitsubish Fuso lenye namba za usajili T 326 ADE lilipinduka baada ya dereva wa Gari hilo kushindwa kulimudu kutokana na mwendo kasi na likatumbukia kwenye korongo.... 
ZAIDI TAARIFA IFUATAYO.

WAZIRI ATEMA CHECHE.

Naibu waziri wa maliasili na utalii awataka maafisa wanayama pori kote nchini kuachia mifugo yote iliyokamatwa katika mapori mbalimbali mpaka hapo badae serikali itakapotoa maelekezo.

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI DAR ES SALAAM WANAWAKE 12 WAPATA WATOTO MKESHA WA KRISMAS

 Afisa Muuguzi Msaidizi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam Mwanne Satara  akimsaidia kumuelekeza Lulu Mohamed namna ya kumfunika nguo Mtoto aliyezaliwa usiku wa kuamkia Krismas Dar es Salaam ambapo akinamama 12 walipata watoto na Mmoja wa akinamama hao alipata mapacha 2 na  kufanya watoto wa kiume kufikia 6 na wakike 7, kati yao akinamama  waliofanyiwa upasuaji ni  akinamama 10 na kati ya hao  watoto njiti 2 na Hospitali ya Temeke akina mama waliojifungua hospitalini hapo kufikia idadi ya watoto 12, wakiume 4 na  wakike 8  (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa UJIJIRAHAA BLOG
Afisa Muuguzi wa Zamu wa Hospita ya Mkoa Amana Florensia Ndumbaro akizungumza na waandishi wa Habari  (pichani hawapo), Hospitali tumepokea idadi ya watoto waliozaliwa mkesha wa Krismas ni 33 kati yao 15 ni wakike na 18 ni wakiume na wote wapo katika hali nzuri na wananyonya vizuri pia mama zao wanaendelea vizuti

Friday, December 25, 2015

RAIS MAGUFULI ASHIRIKI MISA YA KRISMASI.

Rais Magufuli ashiriki katika misa ya kuadhimisha sikukuu ya Krismasi katika kanisa la Mt. Petro Oystabay jijini Dar Es Salaam.
Rais Magufuli ametuma salamu na heri ya sikukuu ya krismasi kwa Watanzania wote na kuwataka kufuata misingi ya dini na kudumisha upendo.

NAKUTAKIA KILA LA KHERI YA SIKUKUU YA CHRISTMASS NA MWAKA MPYAA


Na Krantz Mwantepele,

“Huku tupo tu tunahangaika na kilimo, tunalima kila mwaka, lakini ukweli ni kwamba kilimo chetu wala hakina faida basi tu bora siku ziende”

Lilikuwa ni jibu toka Alex Jonh maarufu kwa jina la “Mafuriko” mmoja wa wanaharakati na waraghbishi wa kijiji cha Lugunga, kilichopo wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita baada ya kuulizwa swali kuhusu maendeleo ya kijiji chao na mmoja wa waandishi wa habari za mitandao Ali Masoud maarufu kwa jina la Kipanya.

Kijiji hiki kina wakazi wanakadiriwa kuwa na wakazi 3,685 wengi wao wakiwa ni wakulima wadogo wadogo. Kilimo kinaajiri karibu 75% ya wakazi wa vijijini. Lakini ni ukweli pia, ni kilimo ambacho bado kinategemea jembe la mkono na mvua na hivyo kuathiri sekta hiyo kwa kiasi kikubwa. Tukiacha hiyo pia upatikanaji wa pembejeo kwa mifumo iliyomo kwenye sera ya kilimo, bado ni changamoto kubwa.

Waraghbishi wengi ni wakulima, ingawa wapo pia walimu, viongozi wa dini, wenyeviti wa vijiji, na watendaji wa kata lakini ukweli unabaki  kwamba wengi wao wanategemea kilimo. Changamoto wanazokutana nazo wakulima ndiyo sababu inayopelekea kilimo kutokuwa cha faida hali inayowakatisha tamaa na kusema bora liende.


Mraghbishi Alex John maarufu kwa jina Mafuriko akiongea na mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Herieth Makwetta alipotembelea kijijini hapo 



Akielezea masikitiko yake kuhusu hali yetu, mraghbishi Alex John ama Mafuriko anasema:

“Ndugu zangu sisi huku tumesahaulika kabisa, kilimo chetu tunacholima ni kilimo cha bora liende maana hatuna kabisa elimu yoyote hapa kijijini. Kila mtu analima na kupanda anavyojua maana tumeshazoea maisha ya hivi.”

Katika ufafanuzi wake Mafuriko ameendelea kusema kuwa kijiji chao kina ardhi yenye rutuba na inayokubali mazao mengi yakiwemo mahindi, maharage, mpunga na karanga lakini licha ya kuwa na ardhi nzuri kama hiyo bado kilimo hakina faida kwao.

Mchora Katuni Ali Masoud (mwenye miwani) akizungumza na waraghbishi na wananchi wa kijiji cha Lugunga

Lakini ni sababu gani inayowafanya wakose faida katika kilimo chao licha ya kuwa na ardhi nzuri inayokubali zaidi ya mazao ya aina tatu. Hapo ndipo waraghbishi walipoanza kuelezea changamoto wanazokabiliana nazo.

Akifafanua ukubwa wa tatizo linalowakabili wakulima wa kijiji hapo raia mwamilifu na mraghbishi Gabriel Jonathan anasema:

“Unajua ndugu mwaandishi hapa kijijini tatizo ni moja, asilimia kubwa ni wakulima na wakulima wengi hawana elimu. Unaona, wengi wao wameishia darasa la saba na wengine hawajasoma kabisa, hivyo hata kilimo chao wanalima ili mradi msimu upite hata akilima heka mbili akatoa gunia tano kwake anaona sawa.”

Ni kweli kilimo ni suala la kitaalamu na hivyo kuna uhitaji mkubwa wa ufahamu kwa mkulima, na hapo ndipo serikali inapomwajiri Afisa Kilimo. Ambaye kimsingi ndio mwenye jukumu hilo katika kuhakikisha anawatembelea wakulima na kuwasaidia kitaalamu ili waweze kuzalisha mazao mengi na yenye ubora.

Hali hii iliibua hamu ya kutaka kujua iwapo kijijini hapo yupo Afisa wa Kilimo ama Bwana Shamba kama anavyojulikana na wengi, katika hali ya kutokuridhishwa na kiwango cha huduma anachotoa mtaalamu huyo wa mashamba, mraghbishi Mafuriko alisema,

“Bwana Shamba yupo tena yupo sana lakini hana ushirikiano kabisa na wakulima wa Lugunga, kwanza hakai hapa kijijini. Pili wengine hawamjui kabisa yaani kwa wiki anaweza kuja mara mbili au msimuone mwezi mzima ila mshahara analipwa”

Akiongezea kuhusu upatikanaji wa Afisa huyo Yohana Julius alisema:

“Tunasikia anaishi Masumbwe na anapoishi hatujui ni mtaa gani na wala mimi simjui licha ya kwamba nakaa hapa katikati (Center) hata nikikutana naye bila kuambiwa simjui je mwananchi anayeishi Mahameni itakuwaje”

Mahameni ni kitongoji kilichopo pembeni ya kijiji cha Lugunga ambapo pia bwana Shamba wa kijiji hicho anatakiwa kufika katika kutimiza wajibu wake.

Mraghbishi Gabriel (wa kwanza kushoto) akiwa na wananchi wenzake wa kijiji cha Lugunga, wakisikiliza maswali toka kwa mwandishi


Umbali wa kutoka Masumbwe hadi Lugunga ni kilometa 17 hali inayodhihirisha kuwepo umbali mrefu kati ya anapoishi Afisa kilimo huyo Dickson Silvester na kituo chake cha kazi.

Kukaa tu na kulaumu hakusaidii sana hivyo ni jukumu la waraghbishi kujua nini wanachotakiwa kufanya,  

“Mimi naona hapa tuandamane mpaka ofisi ya Mkurugenzi, yeye ni mwajiri wake na inawezekana akawa hana hata taarifa ya nini kinafanyika huku, alisikika mmoja wa wananchi aliyetambulika kwa jina moja la Hassan.

Katika hatua nyingine wananchi hao wakapaza sauti kwa kumtaka afisa kilimo huyo kurudi kuishi kijijini na kuongeza kuwa kama alikubali kuja kufanya kazi na kupokea mshahara basi akubali kuishi katika kijiji hicho cha Lugunga kama wanavyoishi wananchi alioenda kuwatumikia.

Safari ya kujua ukweli wa kwanini afisa kilimo huyo haishi katika kituo chake cha kazi ilizidi kusonga mbele na ndipo mwandishi wa makala hii alipomtafuta kwa njia ya simu na kufanya naye mahojiano yaliyodumu kwa dakika kumi na tano.

Katika mahojiano hayo afisa kilimo huyo Dickosn Silvester alikiri kuwa yeye ndiye afisa kilimo wa kijiji cha Lugunga na kukanusha taarifa za kuwa haishi katika kituo chake cha kazi.

“Mimi ni afisa kilimo wa Lugunga kweli na ninaishi hapo hapo Lugunga Center aliyekwambia siishi hapo ni nani? Mana huo ni uzushi”, alisikika akisema Dickson kwa njia ya simu wakati akiongea na mwandishi wa makala hii.

Baada ya kupata majibu ambayo hayakuniridhisha kutoka kwa afisa kilimo huyo nilirudi Lugunga kwa njia ya simu na kumtafuta mwenyekiti wa kitongoji cha Lugunga Kati (Center) bwana Mashiba Dioniz ili kupata ukweli yalipo makazi ya afisa kilimo huyo.

“Mimi ndiye mwenyekiti wa kitongoji cha hapa Senta, kwakweli mwandishi huyo afisa kilimo hana makazi hapa mimi nazijua kaya zangu zote, Ila huwa namuona mara moja kwa wiki basi ila kusema anaishi hapa ni uongo kabisa.’ Alisema Bwana Mashiba mwenyekiti wa Lugunga.

Lakini waraghbishi hawa si tu wanajaribu kufuatilia upatikanaji wa huduma za ugani katika kijiji chao, ila wameendelea kutoa elimu kwa wanakajiji wengine wa kijiji hapo. Mfano mmoja ni migogoro baina ya wakulima wenyewe. Na kwa kuwa waraghbishi hawa hawaitishi mikutano ya vijiji mara nyingi wamekuwa wakitumia maeneo ya migogoro kama sehemu yao ya kutolea elimu.

Akifafanua hilo Felix Daudi, mraghbishi mwingine katika kijiji hicho anasema,
“Kuna kesi tunakutana nazo ambazo tunazitumia pia kutoa elimu. Moja ya kesi hizo ni zile na mtu kuacha mifugo yake bila uangalizi na mwishowe inaingia kwenye mashamba ya watu na kuanza kula mazao. Utakuta mtu hajui wapi akapeleke tatizo lake ama akishaikamata mifugo hiyo afanye nayo ni nini,”

Hivyo ni vizuri watendaji wa serikali wakashirikiana na waraghbishi na muda mwingine kuwapatia ujuzi mdogo mdogo. Hii itasaidia kufanikisha shabaha ya Maendeleo kwani pande zote watakuwa wanategemeana. Na si katika hali hii ambayo watu wanashutumiana.  Hivyo ni jukumu letu sote kucheza nafasi zetu katika kusukuma gurudumu la maendeleo.


                        Moja ya mashamba ya mpunga yaliyopo katika kijiji cha Lugunga



                       CHANZO ; MWANAHARAKATI MZALENDO BLOG 

Thursday, December 24, 2015

MSAKO KWA KAYA ZISIZO NA VYOO WAANZA JIJINI MWANZA.

Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Adam Mgoyi akitoa tamko kuhusu suala la ugonjwa wa kipindupindu na namna Halmashauri ya jiji hatua inazo chukua juu ya wale wote watakao endelea kuuza vyakula sehemu zisizo rasmi kuchukuliwa hatua kali. Pia Mkurugenzi amewataka wale ambao wanaishi kwenye nyumba ambazo hazina vyooo basi wajengee mara moja kwani msako unaanza na atakae bainika kuwa nyumba yake haina choo atashughulikiwa mara 1

RAIA WAAMINIFU WILAYANI KAHAMA WAKERWA NA UTORO.


Pichani nikiwa nazungumza na   Raia waamilifu kutoka kijiji cha Kilago  wilayani Kahama ambapo nilipata nafasi ya kujua mambo  mbalimbali ikwemo mchango wa uraghabishi  katika kijiji hicho katika sekta ya elimu 

Na Krantz Mwantepele , Kahama
Utoro ni tabia ya kuondoka au kutokufika mahali mara kwa mara bila ya kutoa taarifa. Tabia hii ipo kwenye maeneo ya makazini pamoja na shuleni. Katika baadhi ya kata za wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Tabia hii imekuwa kero kwa wanajamii wa kata za Nyandekwa na Kilago kwa kuwa inawarudisha nyuma kimaendeleo. Wakiwa kama sehemu ya wananchi wa kata hizo, waraghbishi wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watoto watoro wanahudhuria shuleni.

Ikiwa kama sehemu ya uraghbishi, kutambua changamoto zinazokabili jamii wanayoishi, waraghbishi walitambua kwamba hili ni tatizo na hivyo kuamua kulishughulikia.

“Nikiwa njiani kuelekea kwenye shughuli zangu, nikakuta watoto wamejibanza kwenye kichaka, na wengine walikuwa wakicheza mpira. Nikataka kujua kulikoni mbona hawapo shuleni, wakati ni muda wa masomo?”

Hili ni swali ambalo raia mwamilifu na mraghbishi Paul Izengo toka katika kijiji cha Nyandekwa kilichopo wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, alitaka kulipatia majibu yake. Udadisi huu ndio uliopelekea kwa yeye kuwasogelea watoto ambao kimsingi walitakiwa kuwa shuleni mda huo na kutaka kujua kulikoni.
Na jibu lilikuwa ni moja tu kwamba wametoroka shule na kwanini watoroke. Paul hakuishia tu kujiuliza maswali, alikwenda hatua moja mbele kwa kuwafuata watoto wale na kuwauliza,
“Nyinyi mnafanya nini hapa? Wakati huu ni muda wa kuwa darasani. Haya shuleni haraka, niliwakaripia, hao wakakimbia.”
Kukimbia wakati umeulizwa ni dalili ya kuogopa kutokana na kosa unalojua umefanya. Watoto wale walijua kwamba wamekosa, na kosa lilikuwa ni utoro shuleni. Hili si tatizo tu la kijiji cha Nyandekwa, hata Kilago pia ambapo baadhi ya wazazi wanatajwa kuwa chanzo cha tatizo hilo la utoro.
Akiwa kama raia mwamilifu na mraghbishi toka katika kijiji cha Kilago, wilayani Kahama Mathew Charles anasema:
“Wazazi ndio sababu ya utoro huu mashuleni, wanawapa watoto wao kazi muda ambao ni wa kwenda shule. HIvyo unapomwambia ukweli anachukia anaona kama vile unamwingilia maisha yake,”
Tabia hiyo ya baadhi wa wazazi kuunga mkono utoro wa watoto wao kwa visingizio vya kutaka kuwa huru na maisha, haviwatakatishi tamaa waraghbishi hao. Kwani hili ni jukumu lao katika kuhakikisha watoto wanapata haki zao.
Katika kusadia watoto hao wanarudi shuleni, waraghbishi kupitia mtandao wao wa wilaya ya Kahama, wamekuwa wakitoa elimu na kuwakishirikisha baadhi ya wazazi wa watoto hao kutambua umuhimu wa elimu na inapobidi kukamata watoto watoro na kuwapelekashule. Na baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwafuata na kuomba ushauri wanapoona mtoto ameanza kuwa na tabia ya utoro. Na mara nyingi wamekuwa wakiwashauri wazazi hawa kushirikiana na walimu ili kuweza kufuatilia maendeleo ya watoto wao. Akifafanua hilo Michael Mathew anasema:

“Kwa mfano katika kipindi cha mwezi wa 10 wazazi wawili wamekuja kuniomba niongee na watoto wao umuhimu wa kwenda shule. Na nafarijika kuona harakati zangu za uraghbishi zinatambuliwa kwenye kijiji change.


Raia Waamilifu, Mathew Charles (kushoto) wa kijiji cha Kilago na Alphonce Peter toka kijiji cha Ufala wilayani Kahama wakifurahia jambo walipkuwa wakijadili tatizo la utoro mashuleni

Tukiacha hili za wazazi kutowapeleka watoto wao shule kwa sababu mbalimbali, ambapo serikali imekuwa ikiwachulia hatua kali za kisheria wazazi hao, watoto wenyewe nao ni chanzo cha kingine cha utoro mashuleni. Wengine wanaaga wamekwenda shule lakini ukweli ni kwamba hawafiki shule na badala yake wanajificha wanapokujua hadi muda wa kurudi unapofika nao hurejea majumbani kana kwamba wanatoka shule.
Hivyo ni wajibu wa raia mwamilifu na aliye mraghbishi anapaswa kuhakikisha watoto wanapata haki yao hii ya msingi ya elimu. Na hivyo ikibidi hata kutumia nguvu, kama anavyosimulia Mathew Charles:
“Muda mwingine nawabeba kwa nguvu watoto hadi shuleni na kuwakabidhi kwa mwalimu. Nimeshafanya hivyo kwa watoto watano sasa. Tunajua kwamba wasiposoma sasa watakuwa mizigo kwenye jamii. Kuna siku watatukumbuka kwamba tulikuwa tunawasaidia,”
Ni dhahiri kwamba tatizo hili ni kubwa na si jukumu la walimu peke yao?
Nikiwa katika picha ya pamoja na waragahbishi na raia waamilifu wa kijiji cha Kilago wilayani Kahama siku za hivi karibuni 
Kila mwananchi pale alipo ana jukumu la kuhahakisha huduma bora za jamii zinapatikana kwa mustakabali wa maendeleo yao. Katika kufanikisha hili raia waamirifu ama waraghbishi toka katika vijiji vya kata ya Nyandekwa na Kilago wameonesha njia katika kuhakikisha wanafunzi watoro wanahudhuria shuleni.

Waraghbishi na Raia Waamilifu toka katika kijiji cha Nyandekwa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano wao hapo kijijini
                                                              
Akielezea jinsi alivyoamua kushughulikia tatizo hilo kijijini pao, Paul ambaye pia ni kiongozi wa waraghbishi wapya kutoka kijiji cha Nyandekwa anasema:

“Nililazimika kumpigia simu mwalimu mkuu na kuomba kuonana naye kwa lengo la kujadiliana naye kuhusu hili tatizo. Na pale ndipo nilipoweza kuelewa ukubwa wa tatizo la utoro. Hivyo nikakubaliana na mwalimu kuwa tutasaidiana katika kuhakikisha kwamba watoto watoro wanahudhuria shuleni.”
Kwa mujibu wa orodha aliyokabidhiwa mraghbishi Paul Izengo na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyandekwa, kuna wanafunzi 21 ambao wameripotiwa utoro kati ya 449 wa shule hiyo.
Kitendo hiki cha mraghbishi kuamua pasipo kulazimishwa na mtu kufuatilia suala la utoro wa wanafunzi katika shule yao ya msingi pale kijijini, ndicho ambacho raia mwamilifu anatakiwa kukifanya.
Raia mwamilifu ni yule ambaye anachukua hatua kwa kushirikiana na wanajamii wengine wa maeneo yake. Huyu ni yule anayetambua majukumu na haki zake kwa mujibu wa ibara ya 12 hadi 24 ya Katiba ya Muungano wa Tanzania. Huyu ni raia anayependa kuona mabadiliko chanya kwenye jamii yake. Huyu ni yule anayetenda pasipo kulazimishwa, bali kwa utashi na uelewa wake kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa. 
Katika kuhakikisha anaelewa vizuri chanzo cha tatizo hilo, ilimlazimu Paul kwenda kumtembelea mzazi ambaye mtoto wake yumo kwenye orodha wa watoro. Na huko alitaka kujua, nini hasa kinachosababisha tatizo hilo.
“Nilikwenda kwa mama mzazi wa mmoja wa wale watoto walioripotiwa kuwa watoro. Lengo langu nilitaka kujua nini hasa tatizo mpaka mtoto haendi shuleni. Ndipo nilipogundua kuna changamoto kubwa zaidi. Inahitajika elimu ya ziada kutolewa,” 
Mama mzazi huyo, alimweleza mraghbishi huyo kwamba michango kwa ajili ya kulipia mitihani ya watoto wake waliopo darasa la 4 na la 6 ni changamoto kubwa inayomkabili. Kushindwa huko kuwalipia watoto wake gharama hizo kumepelekea kwa watoto hao kurudihswa nyumbani.
Sababu nyingine anayoitaja mama huyo ni upungufu wa chakula hasa watoto wanapokwenda asubuhi na kurudi shule mchana. Hali hii inasababisha watoto wasiende shule na kujikita katika shughuli za kuzalisha kwa ajili ya familia.
Pamoja na changamoto hizo, bado raia huyu mwamilifu alimshauri mama huyo kwenda kuonana na mwalimu mkuu ili aangalie ni kwa jinsi gani anaweza kusaidiwa ili watoto wake wahudhurie shuleni.
Ushauri huu unatokana na ukweli kwamba mwalimu mkuu wa shule hiyo Ramadhani Masatu naye pia ni raia mwamilifu kwa nafasi yake. Uwamilifu huo unaelezewa na mraghbishi Elizabeth Ngayalina, toka kijiji cha Nyandekwa:
“Mwalimu mkuu ni muelewa na ndio maana amekubali kushirikiana nasi. Ametupatia kwanza idadi ya wanafunzi ambao ni watoro kwa kuwa anajua ni jukumu letu sote si la kwake na walimu wenzake”  
Nikiwa katika picha ya  pamoja na Waraghbishi na Raia Waamilifu toka katika kijiji cha Nyandekwa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano wao hapo kijijini

Kwa hakika raia hawa waamilifu toka katika vijiji vya Nyandekwa na Kilago wanahitaji kuungwa mkono na wadau wote wa maendeleo. Elimu ni haki ya msingi ya kila mtoto na ndio maana sera ya serikali ni kutoa bure elimu ya msingi na ile ya sekondari. Njia pekee ya kumkomboa mtoto ni kumpatia elimu ambayo ndio dira ya maendeleo ya kila nchi, kuwa na wasomi wengi kadri iwezekanavyo. 

                  CHANZO; MWANAHARAKATI MZALENDO 

BAJAJ AUTO COMPANY WAKISHIRIKIANA NA JEMBE FM WAMWAGA ZAWADI ZA SIKUKUU KWA BODABODA MWANZA

Zawadi ya flat screen TV kwa dereva wa bodaboda Mwanza katika Onyesho la Boxer BM 100 shughuli iliyoruka LIVE kupiti aJembe Fm toka viwanja vya Magomeni Kirumba.
Mafundi wa Bajaji Auto Company wakitoa service ya bure kwa madereva wa bodaboda Mwanza katika Onyesho la Boxer BM 100 viwanja vya Magomeni Kirumba.
Mara baada ya service....Sasa tayari kwa huduma.....
Mamia ya madereva walifika viwanjani hapa na pikipiki zao kupigwa service.
Service zikiendelea ...
Safiiiii....
Watangazaji wa Jembe Fm 93.7 wakifanya mazungumzo na baadhi ya madereva wa bodaboda Mwanza.
OB Van ya 93.7
Magomeni Kirumba.
Red Carpet ya Bajaj Auto Service ilikuwa hivi.
Bodaboda...
Ni mara chache sana kushuhudia wafanyabiashara wa usafiri huu wa bodaboda wakifanya ukaguzi kwa vyombo vyao vya usafiri lakini kupitia Bajaj Auto Company wameamua kuwaanzishia utaratibu huu ili iwe jadi kwa madereva hao.
Kazi inaendelea...
Ze vyomboz vya usafiri.
Mtangazaji wa Jembe Fm Bonz Akihusika kwa hewa 93.7
Pia kulikuwa na mauzo ya pikipiki aina ya Boxer ambapo licha ya majaribio kwa vyombo hivyo vya usafiri pia madereva wapya walipewa mafunzo ya udereva kwa vitendo viwanjani hapo.
Wadau wa Bajaj Auto Company wakijadiliana kuhusu huduma wanazozitoa.
Mtangazaji wa Jembe Fm Jacline Shuma akifanya mahojiano na Mkurugenzi wa Bajaj Auto Company Tawi la Mwanza.
Spare na Vipuli vilikuwepo eneo la huduma.
Uandikishaji pamoja na mauzo.
Hapa kazi tu!!.
Kazi kazini....na KAZI NA NGOMA.