ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 27, 2018

CHINA KUJENGA VIWANDA VITATU JIJINI MWANZA



GSENGOtV/ZEPHANIA MANDIA
KATIKA kuunga mkono juhudi za Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Sera ya Serikali ya viwanda, akiwa ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema wawekezaji hao kutoka China wako tayari kuwekeza jijini humo kwa kujenga viwanda vitatu vya aina tofauti ikiwa ni pamoja na viwanda vya kusindika na kuongezea thamani kwa bidhaa za chakula, viwanda vya kuunganisha magari na mitambo.

MONGELLA AWATEMBELEA WATOTO WALIOUNGANA BUGANDO MWANZA


GSENGOtV/ZEPHANIA MANDIA
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imezungumzia hali za watoto pacha waliozaliwa wameungana kwamba wamelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU).
Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo Julai 27 baada ya kumtembeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella kuwaona pacha hao wa kiume, Mkurugenzi Mkuu wa Bugando Dk Abel Makubi amesema watoto hao walizaliwa kwa njia ya upasuaji. 

Kwa mujibu wa Dk Makubi watoto hao waliozaliwa na Angelina Ramadhani (34) mkazi wa Nyakato jijini Mwanza, wameungana sehemu ya kifua na tumbo.


ABDUL NONDO AKAMATWA NA POLISI.


Taarifa ya kuifahamu ni kumhusu Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo ambapo inadaiwa amekamatwa tena na Polisi na kulala katika Kituo cha Polisi Chuo Kikuu DSM.

Taarifa iliyotolewa na TSNP inasema Nondo amekamatwa usiku jana July 26 majira ya saa tatu usiku akiwa chuoni hapo pamoja na baadhi ya wanafunzi wenzie.

MZIGO MPYA :- Flavour - Time to Party (Feat. Diamond Platnumz) [Official Video]



GSENGOtV
Flavour presents his latest video, "Time to Party", featuring Diamond Platnumz. Directed by Patrick Elis.

KUFICHULIWA MSAADA WA KIFEDHA WA MAREKANI KWA AL QAIDA NCHINI SUDAN

Kufichuliwa msaada wa kifedha wa Marekani kwa al Qaida nchini Sudan



Kituo kimoja cha utafiti nchini Marekani kimefichua kuwa serikali ya zamani ya nchi hiyo ilikuwa ikilifadhili kifedha tawi la kundi la kigaidi la al Qaida huko Sudan.
Kituo hicho cha utafiti kwa jina la Middle East Forum kimefichua na kueleza kuwa serikali ya Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama ilipasisha kiasi cha dola laki mbili kama msaada kwa moja ya matawi ya mtandao wa kigaidi wa al Qaida huko Sudan kwa jina la Taasisi ya Kiislamu ya Misaada. 
Msaada huo wa fedha uliidhinishwa huku Wizara ya Fedha ya Marekani ilikuwa ikifahamu kuwa tawi hilo lipo katika orodha ya makundi ya  yanayowafadhili kifedha magaidi. Pamoja na hayo yote, ushadhi mpya unaonyesha kuwa ofisi ya kudhibiti fedha za kigeni katika Wizara ya Fedha ya Marekani tarehe 7 Mei mwaka 2015 ilitoa kibali cha kupatiwa fedha kundi moja lenye mfungamano na mtandao wa al Qaida huko Sudan. Kundi hilo lilikuwa na nafasi katika kutoroka Usama bin Laden katika miaka baada ya matukio ya Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani. 
Usama bin Laden, aliyekuwa kinara wa mtandao wa kigaidi wa al Qaida 
Ripoti hii imetolewa huku hadi sasa kukiwa na ushahidi chungunzima unaoashiria misaada inayotolewa na Marekani kwa makundi ya kigaidi huko Iraq na Syria pia ikiwemo misaada kwa kundi la kigaidi la Daesh.

EXHIBITOR SPACE AT WATER TANZANIA SHOW 2018

WATER TANZANIA -DAR-01 1
 

BE AN EXHIBITOR

at

WATER TANZANIA SHOW 2018

Exhibit at Tanzania's and East Africa's BIGGEST business trade show, networking event & conference for Water technologies,Equipment and services.
Reach thousands of decision-makers shopping for products & services like yours!

Why Exhibit?

• Get hundreds of qualified leads in one day!
• Gain direct face-to-face contact with decision-makers!
• Reach a captive audience & generate NEW CUSTOMERS immediately!
• Make immediate on-the-spot sales!
• Introduce your company to new prospects!
• Reach a very large prospect pool within a short period of time!
• Brand your business!
• Direct access to your target market!
• Introduce new products and services!
• Conduct market research!
• Direct access to the press!
• Live product and service demonstrationsI
• Distribute product samples!
27th Sept -29th Sept Dare salaam, Julius nyerere International Convention Center JNICC

REGISTER ONLINE FOR FREE ENTRY

BOOKINGS OPEN NOW!!

For Booking and Inquiries:
sales@mikonospeakers.com
+255717109362
 
©2018 Mikono Speakers International | South Africa,Johannesburg,Bed Ford View S,Tanzania Office, Mikocheni ,Senga Road, Kilimanjaro Street,Plot No. 6,

ACT YAMCHUKULIA HATUA MGOMBEA WAO WA UDIWANI KATA YA ITULAHUMBA

GSENGOtV NJOMBE

Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoani Njombe Kimetangaza kuchukua hatua na Kumburuza Mahakamani Aliyekuwa Mgombea Wao wa Udiwani Katika Uchaguzi Mdogo wa madiwani Kata ya Itulahumba Wilayani Wanging'ombe Baada ya Kujitoa katika hatua za mwisho za kinyang'anyilo hicho cha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika AUGOST 12 mwaka huu.  


Mgombea Huyo wa udiwani Bwana Samwel Kihombo Awali Aliwekewa Pingamizi na Chama Tawala Lakini Akashinda Rufaa na Kuwa Mgombea Pekee Kwa Upande wa Vyama Vya Upinzani Baada ya Mgombea wa CHADEMA Kuondolewa Baada ya Kuwekewa Pingamizi na Chama Tawala.

HEAMEDA MEDICAL CLINIC ILIYOPO BUNJU B YATANGAZA KAMPENI YA KUPIMA AFYA KWA WANANCHI BURE


Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo nchini Dk.Hery Mwandolewa akiwa ofisini kwake Heameda Medical Clinc Bunju B jijini Dar es Salaam.
* Madaktari Bingwa nchini waungana na wezao kutoka India kuwahudumia wananchi,waombwa kujitokeza kwa wingi

Na Said Mwishehe, Glob ya Jamii

HEAMEDA Medical Clinic iliyopo Bunju B njia ya kuelekea Mabwepande imetangaza kambi ya uchunguzi wa afya ya magonjwa yasiyoambukiza kwa wananchi wote na kwamba hakutakuwa na gharama.

Akizungumza na Michuzi blog leo jijini Dar es Salaam Dk. Hery Mwandolela amesema wameaza kambi hiyo ya uchunguzi leo jijini Dar es Salaam kwa kupima wananchi mbalimbali waliojitokeza na kusisitiza upimaji huo ambao umeanza leo Julai 26 utaendelea hadi Julai 28 mwaka huu.

Amesema upimaji huo unafanywa na Madaktari bingwa wa hapa nchini kwa kushirikiana na madaktari bingwa kutoka nchini India na lengo kuu ni kuwawezesha wananchi kutambua afya zao mapema na iwapo watabainika kuwa na tatizo la kiafya waaze tiba mapema.

Amefafanua huduma zinazotolewa katika kambi hiyo ya uchunguzi ni pamoja na kupima magonjwa yasiyoambukizwa yakiwemo ya Moyo ,sukari,shinikizo la damu,Tenzi Dume, lehemu(cholestrol) nakiwango cha mafuta mwilini."Madaktari bingwa wa Heameda Medical Clinic kwa kushirikiana na madaktari bingwa wengine nchini pamoja na madaktari bingwa kutoka India tutatoa huduma hizo kwa kiwango cha hali ya juu.

Nakuongeza kuwa " hivyo tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi nakwamba huduma hii inafanyika kwa siku tatu ambapo tumeaza leo na tunaendelea kesho na keshokutwa na hakuna gharama yeyote ."amesema Dkt Mwandolela.Amesisitiza kwakutambua umuhimu wa afya yako wameamua kufanya kampeni hiyo ya kupima magonjwa hayo wakiamini ni fursa ya kila mwananchi kujitambua kiafya mapema..

Katika kampeni hiyo kwa siku ya leo ambayo ni ya kwaza idadi kubwa ya wananchi wamejitokeza lakini Dkt.Mwandolela anafafanua kwa idadi ya madaktari bingwa waliopo nivema wananchi wakaendelea kujitokeza kwani wote watahudumiwa kwakupata vipimo vya afya zao.

Muonekano wa sehemu ya mapokezi ndani ya Clinic hiyo
Muonekano wa moja ya chumba chenye vifaa mbalimbali kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa/matibabu
Muoneakano wa Clinic hiyo kwa nje

Thursday, July 26, 2018

FREEDOM HOUSE YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI WA MITANDAO YA KIJAMII

1
Clerance Kipobota kutoka Shirika la Freedom House ambaye amemwakilisha mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo akifungua semina ya (Alternative Media) kwa waandishi wa habari za Mitandao ya kijamii (Online Platform Reporters) inayofanyika kwenye Hoteli ya Flomi mjini Morogoro.

Shirika la Kimataifa la Freedom House linaendesha mafunzo kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii 'bloggers' kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu namna kuendesha vyombo vya habari mbadala.

Mafunzo hayo ya siku mbili ‘Julai 26 – 27,2018’ kuhusu Vyombo vya habari mbadala ‘Alternative Media’ yaliyoratibiwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) yanafanyika katika ukumbi wa Flomi Hotel mkoani Morogoro.

Awali akifungua mafunzo hayo,Mwakilishi wa Mkurugenzi wa shirika la Freedom House Clarence Kipobota alisema kupitia mafunzo hayo waendeshaji wa mitandao ya kijamii watajifunza mbinu mbalimbali kuhusu namna ya kuendesha mitandao yao.

“Tutajengeana uwezo na kujadili na kuunda jukwaa moja la waandishi ambao wanatumia Alternative Media”,alieleza.
4
Mwezeshaji wa semina hiyo Bw. Daniel Lema akitoa mada kwa waandishi wa habari katika semina inayofanyika katika hoteli ya Flomi mjini Morogoro.
kadam
Mwezeshaji John Kaoneka akitoa mada katika semina hiyo kuhusu mitandao ya kijamii.
2
5 6 7 10 11 12 13 14 15 16 17
Victor Maleko Afisa Mafunzo , Utafiti na Machapisho UTPC akiwa katika semina hiyo.
18
Picha mbalimbali zikionyesha washiriki wa semina hiyo
19
9
Waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua semina hiyo.
9

TUTEGEMEE NINI TOKA KWA MA-BLOGGERS WANAOKUTANA MJINI MOROGORO HII LEO



GSENGOtV


Taasisi ya Freedom House kupitia mradi wake wa Data Driven Advocacy imeandaa mafunzo kuhusu Altenative Media kwaajili ya waandishi wa habari unaofanyakazi kupitia mfumo wa mitandao shughuli inayofanyika mjini Morogoro.


Zaidi ya waandishi 25 wamekutana hapa.


Nini tutegemee toka kwao?



HASARA 5 ZA MITANDAO YA KIJAMII
Mitandao ya Kijamii imekua kwa kasi ya ajabu sana kuanzia mwaka 2006 mpaka leo tofauti ni kubwa sana. Kuanzia Facebook, twitter, Instagram mpaka Youtube zimekuwa kwa kasi ya ajabu na kukusanya mamilioni ya watumiaji.
Kila kitu kina faida na hasara pia naweza kusema kuwa mitandao ya kijamii ina athari kubwa sana katika jamii, pia imeweza kurahisisha mambo mengi sana katika jamii yetu inategemea na mtumiaji anayetumia.
Zifuatazo ni baadhi ya Hasara za kutumia mitandao ya kijamii:
1. Kuvunjika kwa Maadili yetu
Mitandao ya kijamii kama yalivyo maendeleo yoyote yameletwa na watu wa Magharibi, hivyo hasa kwa nchi zetu za Afrika zimeonja utandawazi wa hali ya juu ila sisi waafrika tuna mila na desturi zetu ambazo ziko tofauti na wazungu baadhi ya vitu vilivyoharibu maadili yetu ni ukiingia kwenye mtandao wowote wa kijamii utakutana na matusi yaliyopitiliza yaani lugha ambayo watu wanatumia utakimbia. Pia vijana kufuata wanayofanya wazungu na kujiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya, pombe, kupiga picha za uchi n.k.
2. Majanga Kama Vifo
Kupitia mitandao ya kijamii hasa facebook au Instagram watu wanakutana wanachat lakini hawajuani wanahis mtu unayeongea naye ni mtu mzuri kuja kuonana wengi wanaishia kuuliwa au kubakwa. Kuna stori niliisikia hapa hapa Tanzania msichana kakutana na mvulana facebook wakapendana ingawa hawajawahi kuonana siku wakasema wakutane Magomeni, yule msichana hakuonekana tena wamekuja kukuta maiti yake Bagamoyo.
3. Wizi na Utapeli
Kwa bahati mbaya mitandao ya kijamii inatumika vibaya sana tofauti na lengo au sababu zilizowekwa kuna watu wanatumia mitandao ya kijamii kuibia wengine yaani utapeli kwa kuuza vitu feki  na kadhalika.
4. Uzembe
Mitandao ya kijamii imesababisha uzembe na kujiendekeza kwa watu wengi hasa vijana wenye nguvu kabisa. Yaani hivi sasa kuna watu ambao watashinda kutoka asubuhi mpaka jioni kwenye facebook au instagram bila kufanya kazi yoyote yaani myu ataamka asubuhi kabla hata ya kufanya kiyu chochote aingie kwanza kwenye mitandao ya kijamii ndo asikie raha kitu ambacho hakileti maendelea yoyote.
5. Kuvunjika kwa Mahusiano 
Kwa kiasi kikubwa mitandao ya kijamii imepelekea kwa mahusiano mengi sana kuvunjika yaani watu wengi wanaitumia vibaya hii mitandao, zamani ilikuwa ili upate mchepuko basi ukakutane mtu mbali huko lakini siku hizi unakutana na mtu kwenye kiganja cha mkono wako hivyo imerahisisha zaidi watu kupata michepuko na kuvunjika kwa mahusiano mengi sana, hasa hawa wasichana wanaopiga picha za nusu uchi watu wanajikuta wanaharibu mahusiano
Ingawa Mitandao ya Kijamii ina faida nyingi hizi ni baadhi tu ya hasara za kuwepo kwa mitandao ya kijamii hasa kwa hizi nchi zetu za Afrika.

Je kuna hasara nyingine ambazo sijazitaja tafadhali funguka hapo chini na uongezee za kwako......
KAA TAYARI KWA KUZIJUA FAIDA.
Kutoka kushoto ni Exaud Mtei wa Habari 24 Blog akifuatiwa na Marco Maduhu wa Shinyanga News Blog.
Kutoka kushoto ni Given Mashishanga wa Global Tv Online, James Range, Midraj Ibrahim wa Mwananchi Comunications.

Kutoka kulia ni John Bukuku wa Full Shangwe Blog.
Kutoka kushoto Eliya Mbonea kutoka Mtanzania Digital,
Mbele pichani ni George Binagi wa BMG Habari
Kutoka kushoto ni Pamela Mollel wa Jamii Blog, Malunde Blog na Full Shangwe Blog.
'Muosha huoshwa'

KAMPUNI ZA HOWDEN BROKING NA B.R,PURI ZAJA NA MKAKATI WA KUSHIRIKIANA KIBIASHARA


David Howden, Afisa Mtendaji Mkuu wa Hyperion and Howden amesema (Pichani) “Hii ni hatua nzuri kwetu kwa kampuni ya Howden kuwa na mshirika wa kibiashara barani Africa na tunayo furaha kushirikiana kibiashara na kampuni ya B.R. Puri, ikiwa ni moja ya kampuni kubwa inayoongoza katika soko la Tanzania.  Mikakati yake mikubwa ya kibiashara inaenda sambamba na mikakati ya Howden na tuna imani kwa kuunganisha mikakati yetu ya kibiashara kupitia kampuni mpya ya Howden Puri tutaweza kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wa ndani na jumuiya za kimataifa nchini Tanzania, Afrika Mashariki na zaidi ya hapo.  Kupitia ushirikiano huu tunaona zipo fursa nyingi zinazotuwezesha kukua zaidi kibiashara”

Akiongelea ushirikiano huu wa kibiashara, Arun Puri, Mwenyekiti wa Howden Puri alisema “Kampuni ya BR Puri & Company, ilianzishwa na baba yangu kwenye miaka ya 1950, ikiwa ni moja ya kampuni ya kwanza nchini Tanzania kujishughulisha na biashara za uwakala wa bima. Naamini kwa kuunganisha ujuzi wetu na uzoefu mkubwa tulionao na utaalamu wa Howden wa kutoa huduma katika nchi nyingi duniani kutanufaisha wateja wetu tulio nao na watakaojiunga nasi.

Umesh Puri, Afisa Mtendaji Mkuu wa Howden Puri, aliongeza kusema “Tukiwa kampuni ya uwakala wa bima inayoangalia mbele hapa nchini Tanzania, lengo letu ni kubuni huduma mpya za bima zinazoendana na hali ya soko la Tanzania. Howden imechagua kushirikiana na kampuni ya Tanzania kibiashara ikiwa ni ya kwanza barani Afrika kutokana na jitihada nzuri zinazofanywa na wasimamiaji wa sekta ya bima kuiboresha zaidi sambamba na mazingira mazuri ya kufanyia biashara yaliyopo nchini kwa ujumla”.

*Biashara zake nchini kuendeshwa kwa jina la Howden Puri Insurance Brokers Limited

Kampuni ya kimataifa ya Howden, chini ya kampuni mama ya Hyperion Insurance Group imeingia katika ushirikiano wa kimkakati wa kukuza biashara na kampuni kongwe ya masuala ya bima nchini ya B.R. Puri & Company Limited, ambapo chini ya ushirikiano huo imeanzishwa kampuni itakayoendesha biashara zake nchini inayojulikana kwa jina la Howden Puri Insurance Brokers Limited.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 25.07.2018



Ungana na Zuhura Yunus na Dayo Yusuf kupata habari, maelezo, uchambuzi, maoni na michezo kutoka Idhaa ya Kiswahili ya BBC

RC MONGELLA AUNGANA NA WANANCHI KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA JIJINI MWANZA.

 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella ameshiriki zoezi la kufanya usafi maeneo ya soko la sabasaba kwa kushirikiana na wananchi, baadhi ya watumishi na wanajeshi wa Jeshi la Wananchi.

"Leo ni siku ya kuwakumbuka mashujaa wetu hivyo hatuna budi kuwaenzi kwa kushiriki shughuli za kijamii na wananchi,"alisema Mongella.


 Aidha Mhe.Mongella amesisitiza kuwa utaratibu wa usafi wa kila mwisho wa mwezi uko pale pale hivyo wananchi na watumishi wote waendelee na utaratibu huo ili kudumisha usafi katika maeneo yao majumbani na mahala pa kazi

Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo wamebainisha kuvutiwa na kitendo cha wanajeshi kufanya usafi katika eneo hilo ambalo lilikuwa limekithiri kwa uchafu.

Usafi wa mazingira ni njia ya kuendeleza afya kwa kuzuia  mawasiliano ya binadamu na athari za taka.  Athari hizo zinaweza kuhusu mwili, mikrobiolojia, biolojia au kemikali vikolezo vya ugonjwa.

Taka ambazo zinaweza kusababisha matatizo ya afya ni kinyesi cha binadamu na wanyama, taka ngumu, maji machafu, taka za viwandani, na taka za kilimo.

Usafi kama njia ya kuzuia maradhi unaweza kutumika kwa ufumbuzi handisi (kama majitaka na tiba ya maji machafu), teknolojia rahisi kama vyoo, au matendo ya usafi binafsi (kama uoshaji wa mikono kwa sabuni).

Usafi wa mazingira kama unavyoelezwa kwa ujumla na Shirika la Afya Duniani (kwa Kiingereza World Health Organisation, kifupi WHO), unahusu utoaji wa vifaa na huduma ya usalama wa mkojo na kinyesi cha binadamu.

Upungufu wa usafi wa mazingira ni sababu kuu ya maradhi duniani kote. 

Uboreshaji wa mazingira una manufaa makubwa kwa afya ya wote katika kaya na katika jamii.

Usafi wa mazingira unahusu pia udumishaji wa ratiba ya usafi, kwa njia ya huduma kama vile ukusanyaji wa taka na maji machafu.

USAJILI MBAO FC MOTO UPAMBIRE.

 Golikipa Hashim mussa Ametia wino kujiunga na Mbao Fc kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Majimaji Fc ya Songea.
 Mshambuliaji Evaristigus Bernard Mujwahuki amesaini mkataba wamiaka miwili kujiunga na Mbao Fc akitokea Mwadui Fc ya Shinyanga.

Evaristigus amejiunga moja kwa moja kambini, jijini Mwanza na wachezaji wengine kuendelea na program za koca katika kujiandaa na msimu ujao wa ligi.
 Aliwahi kuzichezea Kagera Sugar, Stand United, Simba Sc, Singida United na Toto Africans katika nyakati tofauti anamudu kucheza kama kiungo wa pembeni au mshambuliaji, tayari kajiunga rasmi na Mbao Fc.
Mshambuliaji Rajesh Kotecha ameongeza mkataba wa mwaka mmoja na Mbao Fc kwaajili ya msimu ujao wa ligi chini ya kocha Amri Said

Wednesday, July 25, 2018

MAKAMU WA RAIS AHITIMISHA ZIARA MKOANI SONGWE NA KUSISITIZA USHIRIKIANO

MAELEZO YA PICHA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan mapema leo akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Songwe (walioko mstari wa nyuma) kabla hajaondoka kuelekea Mkoa wa Mbeya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amehitimisha ziara ya siku tano Mkoani Songwe mapema leo na kusisitiza ushirikiano baina ya uongozi ili kuharakisha maendeleo.
Mhe Samia Suluhu Hassan amesema akiwa ziarani katika wilaya za Momba, Mbozi na Ileje amebaini kuwa Mkoa wa Songwe umebarikiwa kuwa na rasilimali na utajiri mkubwa kinachotakiwa ni viongozi kushirikiana katika kuwatumikia wananchi.
“Nimefurahishwa na kaulimbiu yenu ya maendeleo yataletwa na sisi wenyewe kwa ushindani na ushirikiano, bila ushirikiano hakuna maendeleo, kauli mbiu hii sasa ionekane kwa vitendo”, amesisitiza.
Ameongeza kwa kuwataka watendaji na viongozi wote wapende kuwatembelea wananchi kuanzia ngazi za vijiji ili waweze kuwahudumia vizuri na sio kukaa ofisini.
Mhe Samia Suluhu Hassan ameongeza kwa kuzitaka halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya kuwakopesha wanawake na vijana na kubuni miradi mikubwa itayaowaunganisha wajasiriamali wanawake na vijana kutengeneza viwanda ili kuondokana na umasikini.
Amesema mpango wa mkoa wa kuanzisha vituo vya maendeleo vya kata utawezekana na kuwanufaisha wananchi endapo watendapo watajitoa kwa dhati kuufanikisha na mpango huu utaiwezesha Songwe kupaa kiuchumi.
Aidha Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Mkoa wa Songwe kuendelea kutunza mazingira kwa kupanda miti na wale walioko mipakani kuendelea kutunza amani.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa ameshukuru Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kufanya ziara mkoani Songwe kuahidi kuwa maelekezo na maagizo aliyoyatoa atayasimamia yatekelezwe.

ZANTEL YAINGIA MAKUBALIANO NA MABENKI 9 KUWEZESHA EZYPESA KUFANYA MIAMALA YA KIBENKI

 Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Khamis Baucha mkutano na waandishi wa habari  (hawapo pichani) mjini Zanzibar kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Meneja wa Huduma za wateja wa NMB, Salim Kimweri, Mkuu wa Kitengo cha masoko, Abdalla Jabir wa benki ya watu wa Zanzibar na Mkuu wa masoko na mawasiliano wa Zantel, Sakyi Opoku (kulia). Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Zanzibar.
 Baadhi ya waandishi wa habari wa habari na wageni waalikwa wakifuatilia matukio.
Picha ya pamoja ya Maofisa wa Zantel na baadhi ya wafanyakazi wa mabenki  mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Zanzibar.

Kampuni ya mawasiliano ya Zantel imeingia makubaliano na mabenki tisa nchini kuwawezesha watumiaji wa huduma yake ya fedha ya Ezypesa, kufanya miamala ya kibenki kupitia simu zao za mikononi wakiwa mahali popote nchini Tanzania.

Mabenki hayo ni; Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ya Zanzibar, NBC, NMB, Barclays, Amana Bank, Equity Bank, Access Bank, Exim Bank na BOA.

Hatua hii ni mapinduzi makubwa kwa matumizi ya teknolojia kurahisisha huduma za kifedha nchini, hivyo Zantel imejipanga kuhakikisha wateja wake hawaachwi nyuma katika mapinduzi haya na imejipanga kuhakikisha wateja wake wanafanya miamala yao ya kibenki kirahisi na kw usalama.

Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Zanzibar, Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa (Baucha) alisema kampuni ya Zantel kwa muda mrefu imekuwa ikifanyia kazi suala hili la kushirikiana na mabenki ili kuhakikisha huduma ya Ezypesa inaenda sambamba na maendeleo ya kiteknolojia ya kufanya miamala kwa njia ya simu na kimtandao.

“Katika mchakato wa kushirikiana na mabenki kutoa huduma za kifedha, mwanzoni tulianza kushirikiana na Benki ya Watu wa Zanzibar pekee lakini baadaye tukaona kuna umuhimu kuingia makubaliano na mabenki mengine 8 ili kuwawezesha wateja wetu kufanya miamala ya kifedha kwa urahisi na bila mipaka,” alisema Baucha.

Baucha alisema Zantel, imejipanga kuleta mapinduzi ya teknolojia kupitia simu za mkononi kuwarahishia maisha wateja wake ambapo mbali na huduma za kibenki, watumiaji wa Ezypesa vilevile wanaweza kufanya malipo kwa taasisi mbalimbali za serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na serikali ya Muungano wakati wowote.

“Ili kufanya malipo ya kiserikali mteja ataingia kwenye menu ya Ezypesa kwa kubonyeza *150*02#, halafu atachagua namba 8 itakayomuweza kuchagua kati ya Zan e-pay (kwa malipo ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar) au UnionGov e-epay (kwa Tanzania bara),” alisema Baucha.

Baadhi ya malipo ya kiserikali yanayoweza kufanyika kupitia EzyPesa ni faini zinazotozwa na Polisi, malipo ya tozo za uhamiaji na malipo kwenye Wizara mbalimbali kwa mujibu wa sheria za nchi.

Akiongea kwa niaba ya taasisi za fedha zilizoingia makubaliano na Zantel,Bw. Salim Kimweri,ambaye ni Meneja wa Huduma za wateja wa NMB, alipongeza ushirikiano huo  na kuongeza kuwa utawarahishia wananchi huduma za kibenki na kuleta mapinduzi ya huduma za kifedha nchini.

Katika mkakati wa kuboresha huduma zake nchini, hivi karibuni Zantel iliwekeza katika kuimarisha mtandao wake wa huduma za mawasiliano ya intaneti nchini na kuzindua kampeni ya “Tunaliamsha Kivingine” inayowezesha wateja wake kupata intaneti yenye kasi kubwa na kwa gharama nafuu.