ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 26, 2018

RC MONGELLA AUNGANA NA WANANCHI KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA JIJINI MWANZA.

 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella ameshiriki zoezi la kufanya usafi maeneo ya soko la sabasaba kwa kushirikiana na wananchi, baadhi ya watumishi na wanajeshi wa Jeshi la Wananchi.

"Leo ni siku ya kuwakumbuka mashujaa wetu hivyo hatuna budi kuwaenzi kwa kushiriki shughuli za kijamii na wananchi,"alisema Mongella.


 Aidha Mhe.Mongella amesisitiza kuwa utaratibu wa usafi wa kila mwisho wa mwezi uko pale pale hivyo wananchi na watumishi wote waendelee na utaratibu huo ili kudumisha usafi katika maeneo yao majumbani na mahala pa kazi

Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo wamebainisha kuvutiwa na kitendo cha wanajeshi kufanya usafi katika eneo hilo ambalo lilikuwa limekithiri kwa uchafu.

Usafi wa mazingira ni njia ya kuendeleza afya kwa kuzuia  mawasiliano ya binadamu na athari za taka.  Athari hizo zinaweza kuhusu mwili, mikrobiolojia, biolojia au kemikali vikolezo vya ugonjwa.

Taka ambazo zinaweza kusababisha matatizo ya afya ni kinyesi cha binadamu na wanyama, taka ngumu, maji machafu, taka za viwandani, na taka za kilimo.

Usafi kama njia ya kuzuia maradhi unaweza kutumika kwa ufumbuzi handisi (kama majitaka na tiba ya maji machafu), teknolojia rahisi kama vyoo, au matendo ya usafi binafsi (kama uoshaji wa mikono kwa sabuni).

Usafi wa mazingira kama unavyoelezwa kwa ujumla na Shirika la Afya Duniani (kwa Kiingereza World Health Organisation, kifupi WHO), unahusu utoaji wa vifaa na huduma ya usalama wa mkojo na kinyesi cha binadamu.

Upungufu wa usafi wa mazingira ni sababu kuu ya maradhi duniani kote. 

Uboreshaji wa mazingira una manufaa makubwa kwa afya ya wote katika kaya na katika jamii.

Usafi wa mazingira unahusu pia udumishaji wa ratiba ya usafi, kwa njia ya huduma kama vile ukusanyaji wa taka na maji machafu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.