ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 6, 2025

MISUNGWI YAPANIA KUONGOZA 'KURA ZA SAMIA KITAIFA NA MAFIGA MATATU' - YAFUNGUA KAMPENI KWA KISHIND0

 NA ALBERT G. SENGO/MISUNGWI

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza Michael Masanja Lushinge (SMART) amedhuru katika viwanja vya Misasi Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kwa ajili ya uzinduzi wa Mikutano ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2025 kiwilaya na kutumia nafasi hiyo kuwanadi mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, mgombea ubunge kupitia tiketi ya CCM jimbo la Misungwi Silvery Luboja Salvatory pamoja na madiwani wote wa kata 27 za jimbo la Misungwi.

Friday, September 5, 2025

BRELA YAWASHA TAA NYEKUNDU EPUKA VISHOKA FIKA BANDA LAO RASMI MAONESHO YA AFRIKA MASHARIKI MWANZA

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Ni Maonesho ya 20 ya Biashara Afrika Mashariki yanayoendelea katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza, na zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya kufungwa rasmi, mwanahabari wetu George Kivumbi amezungumza na Afisa Habari kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bi. Christina Njovu, ambaye anaeleza fursa lukuki na faida zinazopatikana kwenye banda lao. Fuatilia..."

Thursday, September 4, 2025

DKT. BITEKO AMWAKILISHA RAIS SAMIA MAZISHI YA HAYATI ASKOFU SHAO

 



📌 Awataka Watanzania kuacha alama katika utumishi wao

📌 Asema Serikali iko pamoja na wafiwa katika kipindi hiki cha majonzi
📌 Askofu Malasusa ataka waumini kumshuhudia Kristo kwa vitendo


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ibada ya mazishi ya Askofu Mstaafu Dkt. Martin Fatael Shao aliyefariki Dunia Agosti 25, mwaka huu.

Akizungumza katika ibada ya mazishi Septemba 4, 2025 yaliyofanyika katika kijiji cha Lole, Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro Dkt. Biteko amesema Hayati Askofu Shao wakati wa uhai wake alifanya mambo mengi mazuri ya kukumbukwa hata baada ya kifo chake.

“ Mzee wetu, Hayati Askofu Shao ameanza kazi za kanisa akiwa kijana na amefanya kazi kubwa ambayo kila mmoja anaishuhudia leo, ameacha alama inayotokana na kazi aliyoifanya, amesema

“Mheshimiwa Rais amenituma niwaletee salamu zake za pole nyingi sana Wanafamilia, Viongozi wote wa Kanisa KKKT pamoja na ndugu jamaa na marafiki wote kwa na msiba” amesema

Amesema Serikali itakumbuka mchango wa Askofu Shao ambaye ametumikia Kanisa katika maisha yake tangu ujana wake na hata baada ya kustaafu ameendelea kuwa mshauri.

Amewahimiza waombolezaji kuendelea kuwa karibu na kushirikiana na wafiwa  katika kipindi hiki cha majonzi huku akiwahakikishia kuwa Serikali iko pamoja nao hasa katika kipindi hiki cha majonzi.

Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT, Dkt. Alex Malasusa amewataka waumini kutumia msiba huu kumshukuru Mungu kwa ajili ya mtu kama hayati Askofu Shao ambaye alikuwa kielelezo cha maisha bora kwa wanadamu.

Ameongeza kuwa Hayati Askofu Shao akikuwa mnyenyekevu na msikivu hali ambayo amesema imeanza kutoweka miongoni mwa wanajamii

“wanyenyekevu kama Dkt. Shao wameanza kuwa hadimu katika jamii na Viongozi waliomtengeneza Hayati Dkt. Shao walifaulu sana… amefanya mambo mengi ndani na nje ya usharika” amesema Askofu Dkt. Malasusa.

Amefafanua kuwa Askofu Shao enzi za uhai wake akifanya kazi kubwa ya
uinjiliahaji ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kwa umahiri mkubwa.

“ Tusizoee misiba, kila msiba utupe nafasi ya kutafakari maisha yetu,” amesema Askofu Malasusa.


Ibada ya mazishi imehudhuriwa na maelfu ya waombolezaji na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro, Nurdin Babu na Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CHAUMMA, Salum Mwalimu.


Wednesday, September 3, 2025

BEI YA MAFUTA MWEZI SEPTEMBA YASHUKA.


Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za mafuta zinazotumika kuanzia leo Septemba 3, 2025, zikionesha kupungua kwa kwa shilingi 36 kwa bei ya petroli na shilingi 23 kwa bei ya dizeli kwa mafuta yaliyopokelewa bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara mtawalia.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dk. James Andilile, bei ya petroli katika soko la dunia imepungua kwa asilimia 0.2 %, dizeli kwa   5.5 % na mafuta ya taa kwa 3.5%. Vilevile, kwa bei za mwezi Septemba, 2025, wastani wa gharama za kubadilisha fedha za kigeni umepungua kwa 3.96%.

Gharama za kuagiza mafuta katika Bandari ya Dar es salaam zimeongezeka kwa wastani wa 20.73% kwa mafuta ya petroli, 7.75% kwa mafuta ya dizeli na 2.62% kwa mafuta ya taa; katika Bandari ya Mtwara hakuna mabadiliko, na kwa Bandari ya Tanga zimepungua kwa 12.66% kwa mafuta ya petroli na 12.66% kwa mafuta ya dizeli.

Aidha, wafanyabiashara wanakumbushwa kuuza mafuta kwa bei zilizoidhinishwa na EWURA na yeyote atakayekiuka agizo hili atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Tuesday, September 2, 2025

MBIO ZA KUKINADI CHAMA CHA MAPINDUZI MKOANI GEITA ZAANZA KWA KISHINDO



📌 Majimbo 7 kati ya 9 yapita bila kupingwa

📌 Kata 92 kati ya 122 zapita bila kupingwa

📌 Maelfu wakusanyika kusikiliza Ilani ya CCM 2025-2030

📌 Dkt. Biteko awasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kumpigia kura Dkt. Samia Suluhu Hassan

📌 Asisitiza mshikamano kabla na baada ya uchaguzi

Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Geita leo Septemba 2, 2025 kimezindua kwa kishindo kampeni za kuinadi Ilani ya CCM 2025-2030 kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ambapo imeelezwa kuwa mpaka sasa tayari Majimbo 7 kati ya 9 ya Ubunge yamepita bila kupingwa huku kata 92 kati ya 122 zikipita bila kupingwa.


Mgeni rasmi katika uzinduzi huo uliofanyika katika Kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe, Mkoani Geita ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa huo, Nicholaus Kasendamila amesema Chama cha Mapinduzi kinaingia kwenye kampeni kikiwa na mtaji mkubwa wa uadilifu, uaminifu, uchapakazi na busara ya mgombea Urais wa kwa tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan.



Amesema kupitia kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, CCM inazo sababu za kuomba ridhaa ya wananchi kuendelea kuongoza nchi akisema kuwa amefanya maendeleo mengi ikiwemo uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam ambayo ni lango kubwa la biashara kwaTanzania na nchi jirani, amejenga daraja refu la Busisi, amekamilisha ujenzi wa Bwawa la Julius Nyerere (MW 2,115) na reli ya kisasa imeshaanza kufanya kazi.

Kasendamila amesema kuwa katika Mkoa wa Geita, Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025 imetekelezwa kwa mafanikio ambapo ameeleza kuwa shule mpya za msingi 151 zimejengwa, Shule za sekondari mpya 118 zimejengwa, zimejengwa hospitali mbili za rufaa, hospitali za wilaya mpya 4 na vituo vya afya 17 vipya vimejengwa.

Ameongeza kuwa, kupitia Ilani ya CCM 2020-2025, zahanati 69 zimejengwa, leseni za madini 7600 zimetolewa kwa wachimbaji wadogo na kuhusu umeme, kabla ya kuingia kwa Serikali ya Awamu ya Sita kulikuwa na vijiji 362 tu vyenye umeme lakini sasa vijiji vyote 486 mkoani Geita vina umeme.

Kuhusu miundombinu ya Barabara amesema Barabara za lami na changarawe zimeendelea kujengwa mkoani Geita ili kurahisisha usafiri wa wananchi.


Ametaja vipaumbele vya CCM katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi kuwa ni pamoja na kuongeza fursa za wananchi kujiimarisha kiuchumi, kuendeleza sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, madini, umeme n.k 

Mwenyekiti huyo wa CCM, ameomba wananchi waipigie kura CCM kwani kura zao zitafanyiwa kazi kupitia maendeleo.


Akizungumza kwa niaba ya Wagombea nafasi ya Ubunge mkoani Geita, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ambaye ni Mbunge Mteule wa Jimbo la Bukombe, amewashukuru wananchi  kwa kujitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa kampeni akieleza kuwa ni  ishara ya Wananchi kukipenda Chama cha Mapinduzi na kuridhika na kazi zinazofanywa na Dkt. Samia suluhu Hassan.

Amesema uchaguzi wa mwaka huu utapeleka salaam ndani ya nchi na kimataifa kuhusu uwepo wa demokrasia nchini hivyo amewaasa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura akiahidi kuwa maendeleo wanayoyaona sasa ni rasharasha tu kwani maendeleo makubwa zaidi yanakuja.


Amesema Mkoa wa Geita unazidi kukua ambapo kwa sasa umekuwa ni moja ya mikoa mitano yenye uchumi mkubwa nchini ni mkoa namba moja kwa kuzalisha dhahabu, umekuwa ni mkoa kiungo kwa maeneo mengine nchini na watu wake ni wachapakazi hivyo  watampigia kura Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kupata maendeleo zaidi.

Kuelekea uchaguzi Mkuu 2025, Dkt. Bitelo amesisitiza kuwa uchaguzi huo uunganishe wananchi badala ya kutenganisha, kuwe na kampeni za kistaarab na Chama cha Mapinduzi kuendelea kufanya kazi kwa umoja.
"Uchaguzi huu ni kwa ajili ya maendeleo yetu, tunataka barabara bora, umeme, afya, mitaji ya biashara, tusiuchukulie  poa uchaguzi huu kwani maana kubwa kwenye maisha yetu," Amesisitiza Dkt.Biteko 

Akizungumzia maendeleo mbalimbali yaliyofanywa katika Jimbo la Bukombe, Dkt. Biteko amesema, chini ya uongozi wa Dkt.Samia Suluhu Hassan Bukombe sasa kunajengwa Chuo cha VETA ambacho kitawezesha vijana kupata ujuzi wa aina mbalimbali pia Chuo cha Uhasibu Arusha kimeanzisha tawi wilayani Bukombe.

Ameongeza kuwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan amezigusa sekta zote kimaendeleo akitolea mfano Shule za msingi sasa zimefikia 104,  shule za sekondari zimefikia 25 na shule za sekondari kidato cha tano na sita zimefikia 5 huku umeme ukifika kwenye vijiji vyote.

Ameongeza kuwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewezesha ujenzi wa kituo kikubwa cha kuzalisha umeme wa jua wa megawati 5 wilayani Bukombe, kikiwa ni cha pili kwa ukubwa ukiacha kituo cha namna hiyo kilichopo Kigoma pia anajenga barabara ya lami kutoka Ushirombo hadi Katoro.

Katika hatua nyingine Dkt. Biteko amewaasa wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea mgombea mwenza wa Kiti cha Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye anatarajiwa kuanza ziara mkoani Geita tarehe 5 Septemba 2025.

Awali, Katibu wa CCM Mkoa wa Geita, Alexandarina Katabi amesema Mkoa wa Geita una mtaji wa wapiga kura waliojiandikisha takriban 1,532,408 huku Wanaccm waliojiandikisha wakiwa ni 524,000 ikiwa ni mtaji wa nusu ya wananchi waliojiandikisha.

Amesema katika Mkoa wa Geita, Majimbo yanayogombewa ni 9  na kata ni 122.

Ameongeza kuwa katika Majimbo hayo 9 majimbo 7 tayari yamepita bila kupingwa na katika kata 122 tayari kata 92 zimepita  bila kupingwa na zilizobaki ndizo zenye wapinzani.