|
Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akiwa anachangia hoja. |
NA VICTOR MASANGU, UTETE RUFIJI
MBUNGE wa jimbo la Rufiji Mkoani Pwani Mohamed Mchengerwa ameahidi kulivalia njuga suala la migogoro ya ardhi inayotokana na jamii ya wafugaji na wakulima ambao wamekuwa wakigombania maeneo ya mashamba na kusababisha kutokea kwa mapigano ambayo wakati mwingine yanapelekea uvunjifu wa amani.
Kuwepo kwa hali hiyo ya migogoro ya ardhi kwa wakulima na wafugaji katika halmashauri ya Rufiji kunatokana na baadhi ya wafugaji kuamua kuvunja sheria na taratibu zilizowekwa na kwenda kulisha mifugo yao katika maeneo yaliyotengwa maalumu kwa ajili ya shughuli mbali mbali za kilimo.
Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa wa viongozi katika halmashauri hiyo mpya ya ya rufiji, ambapo alisema mesema hawezi kuwavulilia wale wote ambao wataonekana wanakwenda kinyume cha sheria za nchi, na kuhakikisha kila mfugaji na mkulima anatengewa maeneo yao rasmi kwa ajili ya kufanyia shughuli zao lengo ikiwani kuepukana na migogoro na mapigano ambayo yamekuwa yakijitokeza kutokana na kugombania ardhi.
Aliongeza kwamba nia yake kubwa ni kuhakikisha naweka mikakati kabambe ambayo itaweza kuwawasaidia wananchi wake wakiwemo wafugaji na wakulima kwa kushirikina na viongozi wa halmashauri katika kuwatenge maeneo yao maalumu ambayo yataweza kusaidia kuepukana na migogoro hiyo ya ardhi.
“Mimi kama mbunge wa jimbo hili la rufiji ninatambua kuwepo kwa changamoto kubwa na mogogoro katika ya wakulima na wafigaji, laki I dhamora yangu kubwa nataka nione wanachi wangu wa jimbo la rufiji wanakaa kwa amani bila ya kuwepo kwa mapigano yoyote kwa hiyo ili nitalivalia njuga na kuhakikisha kwamba sula la amani na utulivu linakuwepo,”alisema Mchengerwa.
Aidha alisema kwamba anatambua wananchi wa jimbo lake wanategemea sana shughuli za kilimo hivyo kwa sasa wameshaweka utaratibu wa kutenga maeneo ya wafugaji ili wasiweze kuingia katika mashamba ya wakulima na kupelekea vurugu z amara kwa mara kitu amabcho sio kizuri na kinarudisha nyuma maendeleo.
Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Saidina Malenda mara baada ya kushindakatika uchaguzi huo alisema atahakikisha nasharikina bega kwa began a viongozi wenzake kwa lengo la kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi wa Rufiji.
Malenda aliongeza kuwa anawashukuru madiwani wenzake kwa kuweza kumchagua kuwaongoza na kubainisha kwamba atafanya kazi bidii zote na kwa kushirikina katika mambo mbali mbali ya kimaendeleo bila ya kuwa na ubaguzi wa aina yoyote wa itikadi ya vyama ili kuweza kuwatumikia wananchi katika huduma mbali mbali wanazozihitaji.
Katika uchaguzi huo wa halmashauri mpya ya Wilaya ya Rufiji,uliofanyika utete nafasi ya Mwenyekiti ilikwenda kwa Saidani Malenda ambaye alipata kura 11 kati ya kura 19 zilizopigwa, ambapo nafasi ya Makamu mwenyekiti ilikwenda kwa Hawa Mtopa ambaye aliyepata kura 10 katika ya kura 19 zilizopigwa.